











Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
Baada ya miaka,miezi,wiki na siku hatimaye yamebaki masaa machache tu kabla filimbi ya kwanza kupulizwa kuashiria kuanza kwa kivumbi cha kuwania ubingwa wa dunia wa soka.Ni wakati wa World Cup 2010.Kwa mara ya kwanza kabisa kindumbwendubwe hicho kipo barani mwetu,Afrika.
Wataalamu na watabiri mbalimbali wa soka wameshaanza kazi zao.Wacheza kamari nao hawapo nyuma.Kuna kulia na kucheka.Mfalme wa soka ulimwenguni,Pele,ametoa utabiri wake.Anasema anaziona Brazil na Spain zikiumana katika fainali.Lakini anasema pia angependa sana kuona timu ya Afrika ikifika fainali.
Mchezo wa fungua dimba hapo baadaye ni kati ya wenyeji Afrika Kusini na Mexico(South Africa Vs Mexico).Historia inaonyesha kwamba hakuna timu wenyeji iliyowahi kupoteza au kufungwa katika mchezo wa fungua dimba.Je South Africa wataendeleza historia hiyo?
Mchezo wa kesho unafanyikia katika uwanja ujulikanao kama Soccer City(pichani) uliopo jijini Johannesburg.Ulianza kujengwa mwaka 1986 na kufunguliwa rasmi mwaka 1987 na una uwezo wa kuchukua watu 94,000 ukitoa watu wa habari na VIP.Uwanja huo upo maeneo ya Soweto(chanzo cha jina ni South West Town.Ni uwanja wenye historia kemkem.Hapo ndipo utakapofanyika pia mchezo wa fainali tarehe 11 Julai.
Wakati homa ya Kombe la Dunia ikiwa ndio inazidi kupaa,ulimwengu unasubiri kwa hamu kitu kimoja.Je,Rais mstaafu wa nchi hiyo,Nelson Mandela “Madiba”,ataweza kuhudhuria japo mchezo huu wa ufunguzi?Mimi binafsi ningefurahi sana kumuona Mzee huyo akihudhuria japo mchezo huo wa ufunguzi kwani mchango wake katika kuzileta fainali hizo barani Afrika ni mkubwa sana.Bila shaka utakumbuka kwamba,alipotoka jela mwaka 1990,hapo hapo katika uwanja wa Soccer City ndipo alipowahutubia watu wake kwa mara ya kwanza baada ya miaka 27.
Baadhi ya wageni wengine maarufu na viongozi wanaotarajiwa kuhudhuria ufunguzi wa fainali hizo ni pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban-Ki-Moon, Rais wa Mexico,Felipe Calderon,Makamu wa Rais wa Marekani,Joe Biden, na Mwenyeji wao,Jacob Zuma.Lakini waliotia fora zaidi ni majirani zetu Kenya ambao watawakilishwa na viongozi wao wote wa juu kabisa Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga(sijui nchi wamemuachia nani).
Kivutio kingine kinatarajiwa kuwa mwimbaji maarufu wa muziki wa R&B kutoka nchini Marekani,R.Kelly,ambaye anatarajiwa kuimba wimbo wake wa “Sign of Victory” ambao ni anthem maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Kombe la Dunia.Ataimba kwa kushirikiana na Soweto Spiritual Singers. Wasanii wengine wanaotarajiwa kushiriki ufunguzi huo ni pamoja na Hugh Masekela, Femi Kuti na bendi ya Osibisa kutoka nchini Ghana.
Mpira utakaotumika ni Jabulani.Ingawa umelalamikiwa na makipa kadhaa(akiwemo Muharami Mohammed wa Taifa Stars) kwamba haufai na unawapa shida,FIFA wamesisitiza kwamba ndio utakaotumika.Jabulani ni neno la kiZulu linalomaanisha “kuleta furaha kwa kila mtu”.
Ratiba kamili ya Fainali hizi unaweza kuipata kupitia mtandao wa FIFA kwa kubonyeza hapa.Pia jamaa wa SoccerNet.com wana ratiba nzuri zikiwa na masaa ya hapo ulipo(local time).Kama hukufanikiwa kuliona tamasha la ufunguzi (2010 FIFA Official World Cup Kick Off Concert) bonyeza hapa.Jamaa wa Vevo bado wanalionyesha kwa kulirudia kila mara.It is Time For Africa.Viva Africa!!
Baada ya mchezo wa fungua dimba, Ufaransa(mabingwa wa dunia mwaka 1998) watakipiga na
Katika hali ambayo bado sijaielewa,jana jioni nilikuwa nikijaribu kutengeneza orodha ya wanamuziki au miziki 100 maarufu ama kwa lugha nyingine, iliyotamba sana barani Afrika(Africa’s 100 Top Hit Songs). Nilichoamua kukifanya ni kujaribu kwenda(kwa kutumia mtandao) nchi moja mpaka nyingine huku nikijaribu kuchunguza kama nchi hiyo ina mwanamuziki au muziki ambao ulitokea kutamba zaidi barani Afrika.
Zoezi hilo bado naendelea nalo.Kwa hakika ni zoezi gumu hususani ukizingatia jinsi bara la Afrika lilivyosheheni vipaji na wasanii wa kiwango cha kimataifa.Nani aingie katika Top 100 na nani abakie nje.Mashabiki wake hawatonilalamikia kwanini nimemuweka pembeni mtu wao?Mawazo kama hayo yalitawala.
Wakati naendelea na zoezi hilo,nikawa pia napitiwa na huzuni kila nilipokuwa nasoma na huku nikisikiliza muziki kutoka kwa mwanamuziki fulani ambaye alishaiga dunia.Wapo wengi ila nazikumbuka hisia zangu nilipoyapitia majina kama Mbaraka Mwaruka Mwinshehe(Tanzania),Franco(DRC Congo),Madilu System(DRC Congo),Brenda Fassie(Afrika Kusini),Miriam Makeba(Afrika Kusini),Lucky Dube(Afrika Kusini),Fella Kuti(Nigeria) na kadhalika na kadhalika.
Nilipofika Gabon,jina ambalo bila shaka sote tunakubaliana kwamba ni vigumu(kama sio kashfa kabisa) kuliacha katika orodha ni jina la Oliver N’goma. Ni jana hiyo nilipojikuta nikisikiliza nyimbo kadhaa za Oliver N’goma kama vile Lusa,Bane,Betty,Nge’ Adia,Icole nk.Nikakumbuka sana jinsi nyimbo zake, zilivyotokea kuwa nyimbo ambazo haziwezi kukosa kunako shughuli mbalimbali hususani harusi hapa Bongo.Kwangu mimi Oliver alikuwa ni mfalme wa aina yake katika Zouk barani Afrika.
Unaweza kupata picha ya jinsi nilivyopata mshtuko na masikitiko kuamka asubuhi na kusikia kwamba Oliver N’goma amefariki dunia! Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari, Oliver N’goma au Noli kama alivyojulikana huko kwao Gabon, amefariki kwa ugonjwa wa figo (kidney failure) akiwa hospitalini alikokuwa amelazwa.
Oliver alizaliwa tarehe 23 March mwaka 1959 katika mji unaoitwa Mayumba uliopo Kusini Magharibi mwa Gabon. Alizaliwa katika familia ambayo haikuwa ngeni katika masuala ya muziki. Baba yake alikuwa mpiga kinanda cha mdomo(harmonica) maarufu.Mwanzoni mwa maisha yake alipenda sana kuwa mpiga picha.Baadaye aliikacha taaluma hiyo na kuendelea na muziki kitu ambacho kilikuwa kwenye damu.
Mwishoni mwa miaka ya 80 ndipo alipotoa albamu yake iliyobeba jina Bane ambayo ndio ilikuwa chanzo cha umaarufu na mafanikio makubwa katika safari yake ya muziki.Rest In Peace Oliver N’goma.
Sijui wewe mwenzangu. Ukiniuliza mimi,mojawapo ya mambo ambayo najivunia sana kuwa nayo kama mtanzania ni suala zima la nchi yetu kuwa nchi ambayo imejaa wastaarabu na waungwana. Tunapingana kistaarabu. Tusipokubaliana katika mambo fulani fulani,tunaambiana kwa heshima. Tukishindwa kabisa kuelewana,tunapiga kura.Waache maadui zetu waifananishe hali hiyo na uzembe au ujinga.Shauri yao. Matunda yake tunayaona.
Ninachotaka kusema kinaweza kisiwe mfano hai au mfano muafaka zaidi.Pamoja nahayo naomba nikiseme. Ni kwamba nimependa uungawana,u-tanzania,uanamichezo na ustaarabu ulioonyeshwa na watanzania wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete kabla na hata baada ya mchezo wa soka kati ya timu yetu ya taifa(Taifa Stars) na Brazil. Hata yule jamaa aliyekimbilia uwanjani kumkumbatia mchezaji maarufu wa Brazil,Kaka,naamini alifanya vile kwa kuzidiwa tu na “mapenzi” na mchezo na mchezaji mwenyewe.
Pamoja na kufungwa jumla ya mabao 5-1, hatukukasirika. Tuliichukulia hali hiyo kama sehemu ya mchezo na nafasi ya kujifunza(hata kama matokeo siku za mbeleni yataonyesha kwamba hatukujifunza chochote,nafasi tumepata).Isitoshe,asiyekubali kushindwa,si….Kama unavyoona pichani, Rais wetu Jakaya Kikwete anaonekana akimkabidhi zawadi ya kinyago mchezaji timu ya taifa ya Brazil Kaka mara baada ya mchezo wao na Taifa Stars. Wametufunga lakini na zawadi za ukumbusho tumewapa.Kama sisi sio waungwana na wastaarabu,nani basi?
Bila shaka wa-Brazil hawa watakumbuka uungwana huu.I hope they remember this genuineand honesty hospitality. Hapo sijazungumzia tabasamu la Meneja Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni ya Bia ya Serengeti ambao ndiyo wadhamini wakuu wa Taifa Stars,pembeni. Ni tabasamu la kweli,lisilo na kinyongo cha kuchabangwa 5-1.After all,ulikuwa mchezo wa kirafiki.Tungekuwa tunashindania Kombe la Dunia,ah tungewafunga hawa! Au unasemaje?
Miss Chang'ombe Geneviva Emmanuel akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Upendo Urasa kulia na mshindi wa tatu Anna Daud mara baada ya washindi kutangazwa katika shindano la Miss Chang'ombe liliofanyika kweny viwanja vya TCC Sigara Jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo.
Katika shindano hilo lililokuwa la kuvutia kutokana na viwango vya warembo walishiriki kwenye shindano hilo, mashabiki wengi waliinuka na kushangilia kwa nguvu mara baada ya washindi hao kutangazwa huku wakisikika kuwapongeza majaji kwa kazi nzuri kwani walidai kuwa majaji wametenda haki na hawa warembo wamejibu vizuri maswali yao, lakini pia mwaka huu chang'ombe wana wawakilishi wazuri kwenye Miss Temeke hata Miss Vodacom Tanzania Pia.
Katika onyesho
Hawa ni Tano bora kuanzia kulia ni Geneviva Emmanuel, Anna Daud, Upendo Urasa, Emaculata Njuu na Jaquiline Benson.
Mh we acha tu! yaani ni burudani kwa kwenda mbele.
wanenguaji wa bendi ya FM Academia wakishambulia jukwaa.
Warembo wakaingia kwa shoo kabambe