Oct 31, 2010

HAYA NI MATUKIO YA ASUBUHI KATIKA VITUO VYA KUPIGIA KURA WILAYANI TEMEKE, KINONDONI NA ILALA

Askari akiwatawanya wananchi waliokuwa wamejikusanya katika kituo cha shule ya msingi ya Madenge kata ya 14 Wilayani Temeke jijini Dar es salaam, watu hao walitii amri na kuondoka katika eneo hilo, haya ni matukio mbalimbali yaliyojiri katika baadhi ya vituo vya kupigia kura katika wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke tutaendelea kukuletea matukio kadiri hali itakavyokuwa
Hapa ni Shule ya Msingi Kijitonyama watu wakiwa wamejipanga tayari kwa kupiga kura mara baada ya kuona majina yao ubaoni.
Watu wakiangalia majina yao kwenye ubao ili kupiga kura katika kitu cha kupigia kura Shule ya Msingi Kijitonyama Wilayani Kinondoni hali ni tulivu kabisa.
Hapa ni Buguruni katika wilya ya Ilala ambapo waangalizi wa kimataifa wameonekana wakifuatilia mwenendo wa uchaguzi huo kwa kurekodi mambo mbalimbali yanayoendelea katika kituo hicho watu walikuwa ni wengi wakiendelea na zoezi la kupiga kura.
Hapa ni kitu cha Temeke kata ya 14 katika Shule ya msingi Madenge ambapo askari walionekana wakitawanya kikundi kidogo cha watu waliokuwa wamesimama karibu na kituo hicho.
Hiki ni kituo cha Temeke kata ya 14 jijini Dar es salaam na watu wako katika foleini kwa ajili ya kupiga kura hali ni shwari kabisa.
Hiki ni kituo cha Temeke Mwisho kilikuwa ni kitupu Kwani idadi ya wapiga kura ilikuwa ni kidogo lakini wasimamizi wa kituo hicho wamesema watu wanakuja kidogokidogo.
Wapiga kura wakiangalia majina yao kabla ya kupiga kura Mtoni Sifa.
Askari Polisi kutoka kituoa cha Kirwa Road wakipanga mikakati ya kuweka usalama wakati wote wa zoezi la kupiga kura katika kituo cha Mtoni Sifa asubuhi leo.
Wananchi wakiwa wamejipanga katika mstari kwa ajili ya kupiga kura katika kituo cha Mtoni Sifa Wilayani Temeke jijini Dar es salaam hali ni tulivu kabisa.
(kwa msaada wa blog jirani-fullshangwe)

CCM yahitimisha Kampeni zake


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM,Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jangwani leo kwa ajili ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal akiwahutubia wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi waliofurika katika viwanja vya Jangwani,jijini Dar leo wakati wa hafla ya kufunga mikutano ya kampeni za chama hicho.
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na mgombea mwenza wake Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati akishuka jukwaani baada ya kumaliza kutoa salamu kwa wanaCCM kwenye hafla ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM, iliyofanyika kwenye viwanja wa Jangwani jioni hii.
Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Rais Mstaaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa na rais Mstaafu wa awamu ya pili,Mh. Ali Hassan Mwinyi wakati alipomaliza kutoa salamu zake kwa wapenzi na wanachama wa CCM waliofurika leo katika viweanja vya Jangwani jijini Dar wakati wa hafla ya kufunga mikutano ya kampeni.
Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri kuu kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Asha Baraka, wakati akiingia kwenye viwanja vya Jangwani leo.
Sehemu ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa wamefurika katika viwanja Jangwani kuhudhulia hafla hiyo ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM iliyofanyika jioni hii.

Oct 30, 2010

FRIENDS OF JAKAYA KIKWETE WAWATAKA WATANZANIA KUMPA KURA JAKAYA KIKWETE!

Mwenyekiti wa Friends Of Jakaya Kikwete kutoka nchi za nje Haruna Mbeyu kutoka London Uingerea na Katibu wa Taasisi hiyo Zainab Janguo kutoka Marekani wakionyesha tuzo maalum waliyoitoa kwa Dk. Jakaya Kikwete kutokana na utendaji kazi wake wakati walipofanya mkutano na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam. Friends Of Jakaya Kikwete wamewataka watanzania kumpigia kura Dk.Jakaya Kikwete ili aendelee kuijenga Tanzania katika miaka mitano ijayo.
Haruna Mbey Kulia na Zainab Janguo wakionyesha pia cheti cha kumtambua Dk. Jakaya Kikwete kwa uttendaji wake.
Mmoja wa wajumbe wa taasisi hiyo Baraka akiongea katika mkutano huo.
Bw. Mickey John Amos akiongea na waandishi wa habari katika mkutano huo.
Waandishi wa habari mbalimbali wakiendelea na kazi yao katika mkutano huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam.

SUPER COACH SYLLESAID MZIRAY HE IS NO MORE

HABARI ZIMEINGIA ASUBUHI HII ZINASEMA SUPER COACH SYLLESAID MZIRAY AMEFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA LEO KATIKA HOSPITALI YA AGA KHAN JIJINI DAR ALIKOKUWA AMELAZWA AKISUMBULIWA N MALARIA. HABARI ZA MIPANGO YA MAZISHI ZITAFUATA MARA TU BAADA YA KUPATIKANA.
COACH MZIRAY , ALIYEKUWA MWAJIRIWA WA CHUO KIKUUU HURIA KAMA MHADHIRI, ATAKUMBUKWA KWA UMAHIRI KATIKA UFUNDISHAJI SOKA KATIKA VILABU MBALIMBALI HADI TIMU YA TAIFA ILIYOSHINDA UBINGWA WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI. ALIFUNDISHA PIA PILSNER, SIMBA, YANGA, PAN AFRICAN NA KABLA YA MAUTI KUMKUTA ALIKUWA MWALIMU WA VIUNGO NA SAIKOLOJIA WA KLABU YA SIMBA. TUNAUNGANA NA WATANZANIA WOTE KUOMBOLEZA MSIBA HUU MZITO AMBAO NI PIGO KWA TASNIA YA MICHEZO NCHINI UKIZINGATIA KUWA TUNA MAKOCHA WACHACHE WALIOSOMEA FANI HIYO NA KUBOBEA.
MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU
MAHALA PEMA PEPONI
- AMIN

DR JAKAYA ALIPOHUBIRI AMANI NA KUONYA WATANZANIA WANAOHUBIRI NA KUKUMBATIA UDINI!!

Jakaya Kikwete akiongea katika mkutano wake na waandishi usiku wa kuamkia leo ukumbi wa Anatouglou jijini Dar ambapo alihojiwa maswali mbalimbali juu ya mustakabali wa nchi endapo atachaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu nyingine Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unafanyika Kesho Oktoba 31 nchini kote. Katika mahojiano hayo RaisDr. Jakaya Kikwete amewatahadhalisha watanzania kufanya maamuzi pasipo kuhubiri wala kuzingatia udini kwani kuzungumzia udini ni hatari na ni jambo litakaloigawa nchi kwa kiwango kikubwa na hakuna wa kutuokoa kwani hatuna pa kukimbilia kwakuwa nchi hii ni yetu hivyo tunatakiwa kuilinda na kuiheshimu ili tuishi kwa amani (Picha na Ankal Issa Michuzi)
Jakaya Kikwete na mgombea mwenza Dr Mohamed Gharib Bilali wakiondoka ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar baada ya kuongea na waandishi wa habari usiku wa kuamkia leo.
Wahudhuriaji wakimsikiliza JK kwenye mkutano wake na waandishi wa habari katika ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar usiku usiku wa kuamkia leo
Wahudhuriaji wakimsikiliza Jakaya Kikwete kwenye mkutano wake na waandishi wa habari katika ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar usiku usiku wa kuamkia leo
Wahudhuriaji wakimsikiliza Jakaya Kikwete kwenye mkutano wake na waandishi wa habari katika ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Salva Rweyemamu akimuamkia Dk. Mohamed Ghalib Bilali kabla ya kuanza kwa mkutano wa Jakaya Kikwete na waandishi usiku wa kuamkia leo ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar
Jakaya Kikwete akiwashukuru watangazaji wa TV mbalimbali waliokuwa wakimhoji kwenye mkutano na waandishi usiku huo kwenye ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar
Jakaya Kikwete akisalimiana na waandishi na wageni waalikwa kwenye mkutano wake na waandishi ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar
Hassan Mhelela wa BBC London akimhoji mgombea mwenza wa urais Tanzania bara Dk. Mohamed Gharib Bilal baada ya mkutano wa JK na waandishi usiku wa kuamkia leo ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar
Hassan Mhelela wa BBC London akimhoji Makamu Mwenyekiti wa CCM Mh. Pius Msekwa baada ya mkutano wa JK na waandishi wa habari
Fundi mitambo mkuu wa Clouds TV Mehboub al Hadad akiwa kazini ambapo kituo hicho kiliungana na vingine kurusha mkutano wa JK na waandishi live
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali wakimsikiliza JK akijibu maswali usiku wa kuamkia loe katika ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar

Oct 29, 2010

KATIBU MTENDAJI WA BARAZA LA UWEZESHAJI (NEEC)AAGWA RASMI

Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bw. Emmanuel Kija Kamba akizungumza katika sherehe ya kumuaga Eliseta Kwayu (katikati)Katibu Mtendaji wa Baraza hilo aliyestaafu na kumkaribisha Katibu Mtendaji mpya Bw Anaclet Kashuliza katika hafla iliyofanyika kwenye Hoteli ya Paradise City jijini Dar es salaam jana jioni (kulia) ni mama Freita Kwayu.
Katibu Mtendaji Mpya wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Anaclet Kushuliza akizungumza na Bodi ya wakurugenzi wa baraza hilo pamoja na wafanyakazi wakati wa kumuaga katibu mtendaji aliyestaafu Bw Eliseta Kwayu aliyekaa (kushoto) katikati ni mke wa Mzee Eliseta Kwayu mama Freita Kwayu.
Bw. Eliseta Kwayu akiiaga Bodi ya Baraza hilo pamoja na wafanyakazi na katika hafla iliyofanyika kwenye Hoteli ya Paradise City jijini Dar es salaam kulia ni mwenyekiti wa Baraza hilo Bw. Emmanuel Kija Kamba na kushoto ni mama Freita Kwayu.
Wfanyakazi wa baraza hilo walikuwepo katika kumuaga kiongozi wao wa zamani na kumkaribisha kiongozi mpya.
Viongozi waandamizi wa Baraza hilo kutoka kulia ni Mjumbe wa bodi Charles Singili, Ally Laay Mkurugenzi wa Fedha na Utawala na mwisho ni Joyce Chonjo Mkurugenzi Uwezeshaji.
Katibu Mtendaji mpya wa Baraza hilo Anaclet Kashuliza kulia akigonganisha glasi ya mvinyo na Mjumbe wa baraza Bw. Peter Noni kama kutakiana kheri katika hafla hiyo katikati ni katibu Mtendaji wa zamani Eliseta Kwayu.
Wafanyakazi na viongozi wa Baraza hilowakigonganisha glasi kama ishara ya kutakiana kheri
Wafanyakazi wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NEEC wakimkabidhi zawadi ya (Laptop) Kompyuta ndogo Katibu Mtendaji wa zamani wa baraza hilo Eliseta Kwayu na Mkewe walipomuaga Bw. Eliseta amestaafu utumishi wa umma.
Wafanyakazi wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NEEC wakimkabidhi zawadi ya Katibu Mtendaji mpya wa baraza hilo Anaclet Kashuliza wakati walipomkaribisha na kumuaga Katibu Mtendaji wa zamani Bw. Eliseta amestaafu utumishi wa umma.
Hapa sasa wafanayakazi hao ilikuwa ni full kucheza tu
Mambo ni burudani tu kwa kwenda mbele si ndiyo eeeeeeeeeeeeeeeeh!

Safari Lager yatangaza kukamilisha mipango yote ya kuipeleka timu ya taifa ya Pool katika mashindano ya dunia,nchini ufaransa


Meneja wa Bia ya Safari lager,Fimbo Buttalah (kati) akizungumza mbele ya vyombo vya habari katika mkutano uliofanyika leo,wakati wa kutangazwa kwa timu ya Taifa ya Pool itakayoshiriki mashindano ya kimataifa huko nchini Ufaransa mapema mwezi ujao.Kushoto ni Mwenyekiti wa Pool Taifa,Isack Togocho na kulia ni Katibu mkuu Pool Taifa,Amos Kafwinga.
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Pool,Dennis Lungu,akitangaza kikosi chake chenye wachezaji saba ambao wataondoka nchini tarehe 6,Novemba kuelekea nchini Ufaransa kushiriki mashindano ya Kimataifa.wachezaji waliopo katika kikosi hicho ni Godfrey Muhando (nahodha),Omary Akida,Mohamed Iddy,Issa Mkindi,Felix Atanas pamoja na Vaileth Mrema (mshichana pekee katika timu hiyo).katikati ni Mwenyekiti wa Pool Taifa,Isack Togocho na kulia ni Meneja wa bia ya Safari Lager ambao ndio wadhamini wakuu wa timu hii ya Pool,Fimbo Buttalah.
Baadhi wa wachezaji wa timu ya Taifa ya Pool wakiwa katika picha ya pamoja na mdhamini wao pamoja na viongozi wa timu.

****** ****** ******

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza kukamilisha mipango yote ya kuipeleka timu ya taifa ya Pool katika mashindano ya dunia yatakayofanyika katika jiji la Paris, nchini Ufaransa mwezi Novemba.

Akitangaza kukamilika kwa maandalizi ya safari hiyo muhimu kwa timu yetu ya Taifa ya Pool, meneja wa Bia ya Safari Lager, Fimbo Butallah alisema; “timu yetu ya Taifa imekuwa ikionesha mafanikio makubwa na kupanda kwa kiwango cha mchezo mwaka hadi mwaka.

Nafasi hii ya kushiriki mashindano ya Dunia imetokana na matokeo mazuri ambayo timu yetu ilionesha katika mashindano ya Afrika yaliyofanyika mwaka jana nchini Afrika ya Kusini na kuibuka namba tano, hivyo kupata nafasi ya kuwa moja ya nchi zitakazowakilisha bara la Afrika katika mashindano hayo makubwa”

Bia ya Safari Lager inaungana na watanzania wote katika kufurahia matokeo na mafanikio haya mazuri ya timu yetu ya Taifa, na hii ndio sababu kubwa iliyopelekea tuhakikishe kuwa safari hii ya kwenda Paris inafanikiwa. Pia tunaahidi kuendelea kuudhamini mchezo huu wa Pool na kuuendeleza ili tutimize ahadi zetu, ambazo ni kuufanya mchezo huu kuwa ajira ya kutegemewa kwa vijana na pia kulitangaza Taifa letu kote ulimwenguni kupitia ushiriki wa mashindano kama haya ya kimataifa.

Nachukua nafasi hii pia kuipongeza kampuni ya Integrated Communication kwa ufanisi mkubwa wanaouonesha katika kuendesha mashindano yetu ya mchezo wa Pool, kampuni hii imetusaidia sana sisi wadhamini na chama cha pool kuhakikisha tunafikia malengo yetu.

Akizungumzia Safari hiyo, Katibu wa Chama cha Pool Taifa Amos Kafwinga alisema “timu itaondoka tarehe 6 Novemba na kuwasili Paris tarehe 7, itaelekea katika mji wa LIMOGES, ambako mashindano hayo yatafanyika na timu inategemea kurudi tarehe 15. Mashindano haya yanashirikisha jumla ya nchi 32 toka katika mabara matano, na bara la Afrika linawakilishwa na timu tano ikiwemo Tanzania.

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa Isaac Togocho alitoa shukrani nyingi kwa Safari Lager kwa jinsi wanavyoendeleza mchezo huu wa Pool hapa nchini, hususani kufanikisha safari hii muhimu zaidi kwa timu yetu na Taifa kwa ujumla, pia alisisitiza suala zima la nidhamu kwa vijana na ujumbe wote unaoelekea Ufaransa ili kulitangaza jina la nchi yetu vizuri na kuleta sifa hapa nyumbani.

Oct 28, 2010

RETURN OF PNC

Anajulikana kama PNC jamaa ambaye ilipata kusumbua sana kwenye gemu ya muziki wa kizazi kipya kabla ya kukaa kimya muda mrefu na sasa anarejea tena kwa nguvu kubwa zaidi akiwa na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la TUZUNGUMZE.
PNC na mchizi wake SHOW ME LAV wakisikiliza ngoma ya PNC- TUZUNGUMZWE iliyokuwa inatambulishwa via 106.5fm Mlimani Radio na mkali toka pande hizo JIWE4EVER aka MWANAKIJIJI.



THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA