Jan 11, 2011

LIVERPOOL YAMTAJA STEVE CLARKE KUWA KOCHA MKUU…!!!

Kocha Steve Clarke.

Klabu ya Liverpool ya Uingereza imemtaja aliyekuwa kocha msaidizi wa timu za Chelsea na West Ham Steve Clarke kama kocha wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Uteuzi wa Clarke mwenye umri wa miaka 47 unakuwa ni mabadiliko makubwa ya kwanza tangu meneja mpya Kenny Dalgish kuchukua madaraka kutoka kwa bosi wa zamani Roy Hodson siku ya jumamosi.

Meneja mpya wa klabu hiyo Kenny Dalgish amesema Steve ni nyongeza muhimu katika timu hiyo na kuwa amefurahishwa na hatua ya kuweza kumchukua.

Clarke alikuwa meneja msaidizi wa klabu ya Chelsea chini ya uongozi wa Jose Mourinho.

THIERY HENRY AREJEA KUFANYA MAZOEZI NA ARSENAL…!!!

Thierry Henry.

Nahodha wa zamani ya klabu ya soka ya Uingereza ya Arsenal Thiery Henry ameanza kufanya mazoezi na klabu hiyo ya kaskazini mwa jiji la London akijiweka fiti kipindi cha mapumziko ya ligi kuu ya soka ya Marekani MLS anakocheza.

Mshambiliaji huyo raia wa Ufaransa anayechezea klabu ya New York Red Bulls inayoshiriki ligi ya MLS, amerejea katika viwanja vya mazoezi vya klabu ya Arsenal.

Hendry bado anabakia kuwa kipenzi cha mashabiki wa Gunners baada ya kuweka rekodi ya kufunga mabao 226 katika mechi 370 alizocheza kati ya mwaka 1999 na mwaka 2007.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 aliondka arsenal na kujiunga na timu ya baecelona ya Hispania msimu wa kiangazi mwaka 2007 kabla ya kusajiliwa na New York Red Bulls mwezi Julai mwaka jana.

TAIFA STARS KUTUPA KARATA YA TATU LEO…!!!

Kikosi cha timu ya Taifa Stars.

Timu ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo inaingia uwanjani kumenyana majirani zake timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’, ikiwania nafasi ya kusonga mbele kuingia hatua ya nusu fainali katika michuano ya Nile basin.

Ili iweze kusonga mbele Taifa Stars inahitaji ushindi wa angalao goli mbili na wakati huo huo ikiomba Mungu wenyeji Misri waifunge timu ya Burundi. Hata hivyo Misri tayari imeshajihakikishia nafasi ya kucheza nusu fainali.

Kocha mkuu wa ‘Taifa Stars’ Jan Poulsen amesema vijana wake wanaari na uwezo wa kuifunga ‘The Cranes’, japokuwa amekiri kuwa mchezo huo utakuwa mgumu.

Katika mechi yake ya kwanza Stars ilifungwa bao 5 – 1 na Misri huku katika mechi ya pili ilikwenda sare ya bao 1 – 1 na Burundi.

RONALDINHO AJIUNGA NA KLABU YA FLAMENGO…!!!

Ronaldinho

Mashambuliaji wa timu ya Brazil Ronaldinho amejunga na klabu ya Flamengo yenye makazi yake mjini Rio de Janeiro na kumaliza matumaini kuwa huenda klabu ya Blackburn ingemsajili kutoka AC Milan.

Ronaldinho mwenye umri wa miaka 30 aliyejiunga na AC Milan akitokea Barcelona mwaka 2008, pia alikuwa akihusishwa na klabu nyingine za Brazil za Gremio na Palmeras.

Nayo klabu ya Rovers ambayo inawamiliki wapya ilikuwa imempa ofa ya paundi milioni 20 kwa mkataba wa miaka mitatu.

MESSI ANYAKUA FIFA BALLON D’OR AWARD…!!!

Na.MO BLOG TEAM

Mshambuliaji mahiri wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona ya Hispania Lionel Messi ameshinda tuzo ya Fifa ballon d’Or katika hafla iliyofanyika Zurich.

Messi mwenye umri wa miaka 23 ameshinda tuzo za Mchezaji Bora wa Mwaka wa Fifa na Ballon d’Or, akiwashinda wachezaji wenzake katika klabu hiyo Andres Iniesta na Xavi.

Messi aliyeshinda tozo mbili tofauti mwaka jana amesema ameshangazwa na ushindi huo, lakini amefurashwa kuwa pamoja na marafiki zake.

Kocha Jose Mourinho aliyeshinda unpredecent Treble akiwa na Inter Milan mwaka 2010, ametajwa kuwa Kocha wa Mwaka.

ALBAM SITA ZA T.H.T KUZINDULIWA LEO


THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA