Sep 29, 2010

WANAMUZIKI WA FERRE GOLA WAWASILI JIJINI DAR TAYARI KWA MAKAMUZI, FERRE KUTUA KESHO SAA TANO!!

Mwimbaji na rapa wa Mwanamuziki Ferre Gola kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo anayejulikana kama (Shikitu) akihojiwa na wanahabari kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu J.K,Nyerere, hata hivyo Kiongozi wao mwanamuziki Ferre Gola anatarajiwa kuwasili kesho saa tano za asubuhi na anatarajia kufanya onyesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee siku ya Ijumaa akishirikiana na bendi ya Mashujaa inayoongozwa na Mwanamuziki Jado Field Force
Mwanamuziki mpiga gitaa la Sollo kutoka kundi la Ferre Gola anayejulikana kama Chally Sollo akihojiwa na vyombo vya habari kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere mara baada ya kuwasili kwa ajili ya onyesho lao linalotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee keshokutwa Ijumaa.
Mnenguaji wa bendi ya Mashujaa Frola Bamboocha akipozi kwa picha huku akiwa amevaa bango kubwa linaloonyesha picha za mwanamuziki Ferre Gola na wanamuziki wake kwenye uwanja wa ndege wa J.K.Nyerere usiku huu.
Wanamuziki wa Bendi ya Mashujaa wakiongozwa na kiongozi wa bendi hiyo Jado Field Force katika kutia hamasa ya ujio wa mwanamuziki Ferre Gola (Shetani) mbele ya Camera ya Clouds Televisheni wakati walipokuwa wakimsubiri mwanamuziki huyo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu J.K.Nrerere usiku huu, hata hivyo mwanamuziki huyo atawasili kesho saa tano za asubuhi na waliotangulia ni wanamuziki wake.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AHUTUBIA BARAZA LA UMOJA WA MATAIFA!!

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Mjini New York alikomwakilisha Rais Jakaya Kikwete Septemba 27, 2010.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Aiowa nchini Marekani wakti alipotembelea Chuo hicho Septemba 25, 2010.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe baada ya kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Mjini New York Rais Jakaya Kikwete Septemba 27, 2010. Katikati ni mkewe Tunu.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana huku akipiga picha na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon kabla ya mazungumzo yao kwenye Ofisi za Umoja huo jijiniNew York Septemba 27, 2010. Mheshimiwa Pinda alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye umoja wa Mataifa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kushoto) wakiwa katika Mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mtaifa Ban Ki Moon (watatu kulia ) na Nibu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Dr. Asha Rose Migiro (wanne kulia) kwenye Ofisi za Umoja huo Mjini New York Septemba 27, 2010.

MISS PROGRESS INTERNATIONAL JULIETH WILLY AREJEA NYUMBANI NA MAFANIKIO MAKUBWA!!

Miss Progress International Juliet Willy akipozi kwa picha mara alipowasili akitokea nchini Italia alikoshiriki shindano la urembo katika taji hilo na kufanikiwa kutwaa taji hilo la Dunia ambalo ndiyo kwanza limeanzishwa mwaka huu, hivyo kuwatoa kimasomaso watanzania katika nyanja ya Urembo. Juliet amekwa mrembo wa kwanza Tanzania kutwaa taji la dunia katika masuala ya urembo na warembo wengi wameshiriki katika mashindano tofauti tofauti ya dunia lakini bado hawajafanikiwa kufikia katika kutwaa taji la dunia.
Rosemary Momburi Mama mzazi wa Miss Progress International Juliet Willy akimkabidhi ua kama ishara ya kumkaribisha nyumbani Tanzania mara baada ya kufanya vyema na kutwaa taji la dunia linalojulikana kama Miss Progress International.
Miss Progress International Juliet Willy katikati akipungia mashabiki ndugu na jamaa waliokuja kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dar es salaam mara baada ya kuwasili akitokea nchini Italia, kulia ni Caroline Sanga Mwandaaji wa Mashindano hayo Tanzania na kushoto ni Rosemary Momburi mama mzazi wa Juliet Willy.

TBL yazindua mashindano ya mitumbwi leo jijini dar


Meneja wa bia ya Balimi Extra,Fimbo Butallah akiongea na waandishi wa habari namna masindano ya mitumbwi yatakavyofanyika katika mikoa ya Mwanza,Kigoma,Mara,Kagera pamoja na Ukerewe katika mkutano na waandishi hao ulifanyika leo makao makuu ya kampuni ya bia Tanzania (TBL).Kushoto ni Meneja msaidizi wa bia hiyo,Edith Bebwa.
Meneja wa bia ya Balimi,Fimbo Butallah (pili shoto),Meneja msaidizi wa bia ya Balimi,Edith Bebwa (shoto) wakiwa na wadau wa Inter grated mara baada ya mkutano huo.
Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo leo.

****** ******* ********

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager leo imezindua rasmi mashindano ya mitumbwi kwa mwaka 2010.

Mashindano hayo ya kupiga kasia, ambayo yatashirikisha mikoa ya Kigoma, Mwanza, Mara, Kagera na visiwa vya Ukerewe, yametokea kuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa Kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kufuatia mashabiki na wapenzi wa mchezo huo kuongezeka mwaka hadi mwaka.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Fimbo Butallah alisema, Ni zaidi ya miaka mitano sasa, bia ya Balimi imekuwa ikiendesha mashindano haya katika kanda ya Ziwa na mkoani Kigoma, kwa kipindi chote hiki tumefanikiwa kuleta changamoto katika upigaji makasia, kwa kuwapa fursa wapiga makasia kutumia mitumbwi yao katika michezo na kujipatia kipato cha ziada kupitia zawadi nono zinazotolewa lakini pia kuleta burudani kwa wakazi wanaozunguka ziwa Victoria na lile la Tanganyika.

Mashindano haya ya mitumbwi ya Balimi sasa yamekuwa na umaarufu mkubwa na kuongoza kwa mashabiki katika kanda ya ziwa. Kama ilivyo kawaida, mashindano haya yatatanguliwa na burudani mbalimbali za uhamasishaji, zikifuatiwa na mpambano katika hatua ya mwanzo kabla ya fainali kuu itakayofanyikia Jijini Mwanza tarehe 4 Decemba.

Katika hatua za awali mashindano yataanzia Kituo cha Kigoma tarehe 9 Octoba, Kagera 23 Octoba, Mwanza 13 Novemba, Mara na Ukerewe 27 Octoba. Pia ninapenda kuwajulisha washiriki kuwa zawadi za mwaka huu zimeboreshwa zaidi, ukilinganisha na miaka ya nyuma. Hivyo washiriki waongeze mazoezi ili kujihakikishia ushindi katika maeneo yao, pia timu mbili za wanaume na moja ya wanawake zitakazoshika nafasi za juu katika ngazi ya awali ndizo zitakazoingia katika fainali kuu itakayofanyika Jijini Mwanza.

Akizitaja zawadi watakazopata washindi katika ngazi za awali na fainali, Meneja Msaidizi wa Bia ya Balimi Edith Bebwa alisema; Katika ngazi za mikoa zawadi zitakuwa kama ifuatavyo: Ngazi ya Mikoa Fainali Kuu Wanaume Wanawake Wanaume Wanawake

Mshindi wa kwanza 700,000 500,000 2,500,000 2,000,000
Mshindi wa Pili 550,000 400,000 2,000,000 1,500,000
Mshindi wa Tatu 350,000 250,000 1,500,000 750,000
Mashindi wa Nne 300,000 200,000 750,000 500,000
5 hadi 10 - Kila timu 200,000 100,000 400,000 200,000

Tuna imani kubwa kuwa zawadi hizi zitaongeza chachu ya ushindani kwa washiriki na hivyo kuleta burudani ya aina yake kwa mashabiki.

Tunawaomba wakazi wa kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kujitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano haya ya aina yake.

Sep 28, 2010

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO MAREKANI!!

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kisalimiana na Sister Davita Lumanzi wa Shirika la Wafrancisco wakati alipozungumza na watanzania waishio Marekani kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania, kwenye Umoja wa Maifa New York ,Septemba 26,2010. Sister Davita Msomi wa fani ya Utawala katika Hospitali na anafanya kazi nchini Marekani.(Picha na Ofisi ya Wziri MKuu)
.Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya watanzania waishio Marekani kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, New York, Septemba 26, 2010
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tuni Pinda akisalimiana na Meja Ibuge wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokutana na watanzania Waishio Marekani kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, New York Septemba 26, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mzee, Omar Juma Mwilima katika Mkutano wake na Watanzania waishio Marekani kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Matifa, New York, Septemba 26, 2010. Mzee Mwilima wa Mbezi, Dar es salaam,yuko Malekani kwa mwaliko wa wanae wanoishi huko. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

JAKAYA KIKWETE ALI POISISIMUA SHINYANGA

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Kikwete akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Shinyanga jana jioni (Picha na Freddy Maro na Muhidin Michuzi)
Jakaya Kikwete mara baada ya kutua kwa helikopta nje ya uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga leo Jumatatu na kuamua kutembea kwa miguu hadi uwanjani
Mwanachama Mkongwe wa CCM Bi.Fatma Ndugulile akimuonesha Mwenyekiti wa CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete kadi yake ya uanachama na risiti za malipo ya mwanachama tangu mwaka 1977 wakati Bibi huyo alipokutana na Mgombea huyo wa Urais kwa kupitia CCM mjini Shinyanga jana jioni. Dr.Kikwete alimsifu Bibi huyo kwa uaminifu wake kwa CCM na umahiri wake wa kutunza risiti zake za malipo.
Ze original Comedy wakiburudisha uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga jana Jumatatu
Kinamama waliokuwa wakimsubiri kwa hamu JK katika uwanja wa Kambarage mjini shinyanga wakirukaruka kwa furaha mara helikopta ya JK ilipokuwa ikitua nje ya uwanja huo.
Helikopta iliyombemba JK ikitua nje ya uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga leo Jumatatu

Dk Siame akaidi kuvunja kambi za wana CCM Mbozi

Na Richard Mwaikenda, Mbozi.
MGOMBEA ubunge Jimbo la Mbozi Magharibi, Dk. Lukas Siame,ametakiwa kuvunja makambi na kuwaomba radhi wananchi aliowakosea wakati wa mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ili kujenga umoja na mshikamano utakaokifanya chama kishinde kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 31,mwaka huu.
Alishinikizwa kufanya hivyo na uongozi wa CCM Wilaya ya Mbozi na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano wa ndani wa kuweka mikakati ya kukipatia chama hicho ushindi wa kishindo uliofanyika juzi mjini hapa.
Ililazimika kumwambia hivyo, baada ya kubaini kuendelea kuwepo kwa makundi katika baadhi ya Tarafa jimboni humo,hali ambayo inaweza kuhatarisha chama hicho kukosa baadhi kura muhimu zinazohitajika kukipatia chama hicho ushindi wa kimbunga.
Jambo linginne lilowashitua ni kitendo cha mgombea huyo, kutamka wazi katika mkutano huo, kuwa yupo tayari kukosa kura za watu wasiokubali kuvunja makundi na kuungana naye katika kampeni na kwamba ana uhakikia kupata kura kwa watu wengine wanaomkubali.
"Naamini makundi yaliyojitokeza wakati wa kura za maoni tulizimaliza, na endapo kama kuna kundi halikubali kuvunja makundi , basi mimi niko tayari kuzikosa kura zao,lakini tutazipata kwa wengine wanaoniunga mkono,"alisema Dk. Siame..
Akihutubia katika mkutano huo, uliohudhuriwa pia na Mgombea ubunge jimbo la Mbozi Mashariki kupitia chama hicho, Godfrey Zambi, Mgeni rasmi, Ridhiwani alielezea kuwa si dhambi wakati wa kipindi cha mchakato wa uchaguzi wa kura za maoni kuibuka makundi, na kudai kwamba hiyo ni demokrasia ndani ya CCM, lakini makundi hayo yanatakiwa kuvunjwa mara moja anapotangazwa mshindi.
"Si dhambi wakati wa kipindi cha uchaguzi, kuwepo mgawanyiko maana hiyo ndio demokrasia ndani ya CCM,kwani si lazima unayempenda wewe basi kila mtu ampende,lakini utake usitake mwana CCM atakayeshinda katika mchakato huo na ambaye uongozi wa juu utamjadili na kurudisha jina lake,basi huyo ni wetu wote inatakiwa tumpiganie ashinde," alisema Ridhiwani.
"Kipindi cha kura ya maoni kilishapita, kinachotakiwa sasa ni wanaCCM kuwa na umoja pamoja na mshikamano utakaotuwezesha kukipatia chama chetu ushindi wa kishindo usioelezeka,"alisema Ridhiwani huku akishangiliwa. .
Ridhiwani, alikemea kitendo cha wapambe kuendelea kuwadhihaki wenzao waliokuwa kwenye kambi iliyoshindwa, na kuwataka waache mara moja tabia hiyo kwani haimsaidii mgombea,mwananchi na hata chama chenyewe.
"Wagombea na wapambe acheni kuwadhihaki na kuwakejeli wenzenu walioshindwa, tabia hiyo siyo nzuri, inawafanya wakichukie chama, tusahau yaliyotokea, tujirekebishe tulipokosea, tujenge umoja kwani kidole kimoja hakivunji chawa,"aliwaasa Ridhiwani.
Naye Mgombea ubunge Jimbo la Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi, alitamba kuwa kwa jinsi anavyoendesha kampeni zake ni dhahiri CCM jimboni humo itapata ushindi si chini ya asilimia 90,kwa vile katika kampeni amewashirikisha watu bila kujali anatoka kundi gani na kwamba hana kundi bali alilobakia nalo ni kundi moja tu la CCM.
Pia, Mwenyekiti wa UVCCM, Wilaya ya Mbozi,Jobu Kabinja, alisisitiza kauli zilizotolewa na baadhi ya viongozi kwa kumtaka Dk. Siame asiendelee na tabia ya kuzikataa kura za watu wasiotaka kuvunja makundi, kwa vile kura hizo wanazihitaji.
Naye Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo,Aloyce Mdaravuma, aliungana na viongozi wenzie, kwa kusema kuwa, wataungana na Dk. Siame kwenye kampeni kwa kuziomba kura kwa unyenyekevu hata kwa kulala chini mpaka kieleweke.
"Tutaingia kiume kwenye kampeni kwa kuzisaka kura katika Kata,vitongoji na nyumba kwa nyumba, hatutaki hata kura moja ipotee, kwani kura siyo zako ni za CCM,"alimazia kusema Mdaravuma.

Oiko Credit yakopesha Bil 2.1/- kwa YWCA Moshi na Saccos ya Wazalendo ili kuiwezesha jamii


Meneja wa Oiko Credit Tanzania Deus Manyenye (Kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya bilioni 1.6/- Mwenyekiti wa Saccos ya Wazalendo, Mbonea Maghimbi (kulia) fedha ambazo ni mkopo ili kusaidia kuwawezesha watu wa hali ya chini, Wakati wa hafla hiyo Oiko pia ilikabidhi hundi hundi yenye thamani ya milioni 500/- kwa YWCA Moshi kwa ajili ya ukarabati wa jengo la chama hicho lililokaa muda mrefu bila kufanyiwa matengenezo.
Meneja wa mradi wa ukarabati wa jengo la YWCA Moshi, Elimringi Maringo akimuongoza Meneja wa Oiko Credit Tanzania, Deus Manyenye kuangalia hali ya ujenzi inavyoendelea mara baada ya kukabidhi hundi yenye thamani ya milioni 500/- kwa YWCA Moshi, fedha ambazo zimetolewa kwa mkopo kwa ajili ya ukarabati wa jengo la chama hicho lililokaa muda mrefu bila kufanyiwa matengenezo. Waliongozana nae ni makamu mwenyekiti wa chama hicho Vicky Lyimo.
Meneja wa Oiko Credit Tanzania Deus Manyenye akizungumza na Mwenyekiti wa Saccos ya Wazalendo, Mbonea Maghimbi (kulia), makamu mwenyekiti wa chama hicho Vicky Lyimo (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa YWCA Moshi, Valentine Mwinga kuhusiana na aina ya mikopo wanayotoa mara baada ya hafla kukabidhi hundi zenye thamani ya bilioni 2.1/- kwa YWCA Moshi na Saccos ya Wazalendo zote za mjini humo.


Na Mwandishi Wetu, Moshi

KAMPUNI ya OIKO Credit inayojishughulisha na ukopeshaji fedha kwa taasisi mbalimbali duniani zikiwemo benki, imezikopesha jumla ya shilingi bilioni 2.1/- YWCA Moshi na Saccos ya Wazalendo ili zitumike kuiwezesha jamii ya watu wa kipato cha chini.

Fedha hizo zinazotumika kwa ajili ya ukarabati wa jengo la makao makuu ya YWCA Moshi na uwezeshaji jamii ili ijiendeleze kimaisha kupitia Wazalendo ni muendelezo wa mikopo kutoka kampuni hiyo iliyoitoa katika kipindi cha mwaka huu kwa taasisi 12 nchini unaofikia jumla ya bilioni 8.2/-

Akizungumza jana mjini hapa wakati wa hafla ya kukabidhi hundi Meneja wa Oiko Credit Tanzania Deus Manyeye alisema kuwa lengo la kampuni yake ni kuwekeza kwenye taasisi za fedha zilizolenga kuiendeleza jamii ya kipato cha chini duniani.

Akifafanua Manyeye alibainisha kwamba licha ya kupokea maombi mengi lakini wamehakikisha fedha wanazotoa zinaelekezwa kwenda kusaidia miradi ya uzalishaji inayolenga watu wa hali duni wanaopigania kujikwamua kutoka kwenye umaskini.

“Tulichunguza na kubaini kwamba YWCA Moshi na Wazalendo Saccos wamekidhi vigezo vya kupewa mikopo kwani walikuwa na nia ya dhati ya kuikomboa jamii ya chini kutoka kwenye umaskini unaoikabili. Tayari fedha zimeshaanza kutumika kama mnavyoona ukarabati wa jengo hili unavyoendelea,” alisema Manyeye.

Aidha kwa kuwa idadi ya watu Tanzania ni kubwa kuliko ile ya Kenya na Uganda taasisi hiyo imepanga kuziwezesha kwa kuzikopesha zaidi asasi na wadau wa nchini ili waweze kuhudumia kundi kubwa la watu kuliko ilivyo sasa ambapo nchi hizo zimekuwa zikipata fungu kubwa la fedha.

Kwa upande wake Katibu wa YWCA, Frida Mbowe alisema kwamba kwa kuwa manispaa hiyo inajiandaa kuwa hadhi ya jiji mkopo huo wa milioni 500/- utawawezesha kukarabati jengo kuwa lenye muundo wa kisasa utakaotoa mvuto kwa wawekezaji kupangisha na kufungua ofisi mbalimbali.

Naye Mbonea Maghimbi ambaye ni mwenyekiti wa Wazalendo aliishukuru Oiko Credit kuwakopesha bilioni 1.6/- na kusema watazitumia kama ilivyokusudiwa kwa kuwawezesha watu wa kipato cha chini kuweza kuinua hali yao kimaisha.

“Mbali na hilo pia tumepanga kuzitumia fedha hizo kutoa elimu kwa jamii inayotuzunguka umuhimu wa kujenga utamaduni wa kuhifadhi ama kujiunga na Saccos ya Wazalendo na faida mbalimbali watakazonufaika nazo mara watakapotimiza vigezo,” alisema Maghimbi.

Tangu Oiko Credit yenye makao makuu yake nchini Uholanzi ilipoanzishwa nchini mwaka 2006 imejiongezea wateja kutoka sekta mbalimbali ikiwemo benki, SME’s, Saccos, Makanisa na kuwekeza kutoka milioni 260/- hadi kufikia bilioni 16 Juni mwaka huu kutoka wateja wawili hadi 21

dr. bilal aendelea na ziara za kampeni mkoani iringa



Mgombea Mwenza wa urais wa kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, Dk. William Mgimwa, wakati alipofika katika jimbo hilo kufanya mkutano wa kampeni na kumnadi mgombea huyo leo.


Mgombea Mwenza wa Urais akiwaangalia wasanii wa Sarakasi wa Kikundi cha Kijiji cha Mabaoni Wilaya ya Mufindi, wakati alipokuwa akiwasili Kijijini hapo leo kufanya mkutano wa kampeni.


Wananchi wa Kijiji cha Mabaoni Kata ya Makungu Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa, wakimsikiliza mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni leo.

HOSPITALI YA REGENCY KUJENGA KITUO KIPYA CHA AFYA


Daktari Bingwa wa tiba za Mifupa, viuongo na upasuaji kutoka India Kaushal Mishra akizungumza na waandishi wa habari juu ya namna atakavyofanya kazi kwa kushirikiana na madaktari wa Hospitali ya Regeny.
Mwenyekiti wa Hospitali ya Regency Dr. Rajni Kanabar (kulia) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya uimarishaji na utoaji wa huduma za magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya mifupa na viungo, moyo, figo na magonjwa ya mfumo wa njia ya mkojo kwa kushirikiana na mataktari bingwa kutoka nchini India leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni meneja wa mifumo ya komyuta ya hospitali hiyo Jingne Oza.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Na Mwandishi Wetu.

UONGOZI wa Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam ,umesema unajenga kituo kikubwa cha afya kwa ajili ya kutoa huduma za afya chenye thamani ya dola za Marekani milioni 15 ili kupunguza gharama za wagonjwa wanaotibiwa nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa hospitali hiyo, Dk. Rajni Kanabar wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu ushirikiano wao wa kutoa tiba mbalimbali na kundi la madaktari bingwa kutoka India (Forts – Hospital Health Care Limited).

“Tumepata eneo jingine kwa ajili ya ujenzi wa kituo kikubwa katika eneo lililojirani na hospitali yetu, ambapo tunajenga mahabara ya kisasa na vyumba vya upasuaji viwili, sehemu ya huduma ya dharura na uongozi. Hivyo tumeshaanza ujenzi huo lengo ni kupunguza gharama kwa Watanzania kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya tiba mbalimbali,”

alisema.

Dk. Kanabar alisema ujenzi huuo untarajia kuchuku kipindi cha miaka miwili.

Akizungumzia kuhusu ushirikiano wa madaktari hao kutoka India, Dk. Kanabar alisema watakuwepo hapa nchini kwa kipindi cha miezi mitatu kwa ajili ya kutoa tiba na ushauri kwa wagonjwa ikiwemo kutoa mafunzo kwa madaktari wa hapa nchini, hata hivyo aliongeza baada ya muda huo kumalizika watakuja wengine.

Alisema uzinduzi rasmi wa ushirikiano huo, utazinduliwa Oktoba 16, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Madaktari hao, ni Dk. Rajesh KR. Pandit ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya moyo na Dk. Avinash Ingnatuius mtaalamu wa magonjwa ya figo ambao waliwataka Watanzania kufika hospitalini mapema ili kufanya matibabu kuwa rahisi badala ya kusubiri hadi wazidiwe.

Wengine ni Dk. Kushaul Mishra ambaye ni mtaalamu wa mifupa na viungo alisema wamefurahishwa kuja Tanzania. ambapo lengo lao ni kutoa ujuzi kwa madaktari waliopo nchini hususan namna ya kufanya upasuaji mgumu na Dk. Aman Gupta mtalaamu wa magonjwa yanatokana na mfumo wa njia ya haja ndogo.

Madaktari hao watatoa tiba hizo kwa gharama nafuu na kufanya upasuaji mdogo.

“Tutatumia kifaa kidogo kwa ajili ya kugundua matatizo ya mfumo wa haja ndogo ambacho hakiko Tanzania,” alisema Dk Gupta.

Hopitali ya Regency imetoa ufadhili kwa watoto zaidi ya 1,000 kwaa ajili ya upasuaji wa moyo kwa gharama ya dola za Marekani 1,650 hadi 2000

taasisi ya superbrands yaingia Tanzania


Mkurugenzi wa mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba na Mkurugenzi wa masoko Ephraim Mafuru wakionyesha cheti cha kudhibitishwa ubora wa kampuni na bidhaa zinazokubalika kwa wateja wa simu za mkononi afrika mashariki mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Mkurugenzi wa superbrands Jawad Jaffer(hayupo pichani)
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Clouds Media Group Bw. Joseph Kusaga akitoa shukrani mara baada ya kukabidhiwa cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi
Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Breweries Limited Bw. Ajay Mehta akishukuru mara baada ya kukabidhiwa Cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi.
Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi Cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Breweries Limited Bw. Ajay Mehta.
Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Clouds Media Group Bw. Joseph Kusaga ambaye aliambatana na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Clouds Media Group Bw. Ruge Mtahaba.
Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi Cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinazotambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru katikati ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi. Mwamvita Makamba.
Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi Cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi Mkurugenzi wa Msaidizi wa Kampuni ya Azam Bw. Yusuph Kamau katikati ni Meneja Biashara wa kampuni hiyo ya Azam Bw. Daniel Hill aliyembatana nae.
Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi Cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi Mkurugenzi wa Kampuni ya Chemi&Cotex Industies LTD, Bw. Lakshmi Narayan, Katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Chemi&Cotex Industries LTD, Bw. Riyan Dewji. (Picha kwa hisani ya www.michuzijr.blogspot.com).

Sep 27, 2010

mbio za mashua bahari ya hindi zawa kivutio




Baadhi ya washiriki wa mbio za mashua za Vodacom Tanzacat wakishindana katika ufukwe wa bahari ya hindi yacht club ambapo zaidi ya boti 60 zilishindana na zaidi ya nchi kumi zilishiriki katika mashindano hayo ya kimataifa mashindano hayo yamefanyika kwa siku nne mfululizo.
Mwenyekiti wa Club ya Yacht Jim Bell(kushoto) akimkabidhi kombe mshindi wa mbio za mashua za Vodacom Tanzacat Blaine Dodds(kulia)wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza ,Peter Blaine

ridhiwani kikwete ndani ya chunya mkoani mbeya


Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa,Ridhiwani Kikwete,akivishwa skafu alpowasili leo asubuhi katika Jimbo la Lupa, Chunya kuendeleza kampeni za ushindi wa kishindo kwa CCM.Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa,Ridhiwani Kikwete, akiwatambulisha kwa wananchi, mgombea ubunge jimbo la Lupa, Victor Mwambalaswa kulia na mgombea Udiwani Kata ya Mbegani,Bosco Mwanginde leo asubuhi katika jimbo la Lupa,Chunya.Baadhi ya wakazi wa Kata ya Mbugani, Chunya wakisikiliza wakati Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa,Ridhiwani Kikwete,akihutubia mkutano wa Kampeni uliofanyika katika Kata hiyo, Jimbo la Lupa, Chunya.

Sep 26, 2010

Wateja wa Vodacom sasa kuchati bure kwa Intaneti

· Ni kwa Face Book na nyinginezo

Dar es Salaam, 26 Septemba, 2010. Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, imezindua huduma mpya ya Intaneti ambayo itawawezesha wateja wake kuchati kwa intaneti bure.

Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi Mwamvita Makamba alisema jana kwamba wateja wa Vodacom sasa wanaweza kuchati bure kwenye tovuti za Face Book, the Grid na Vodamail.

Alisema Vodacom Tanzania inatoa huduma hiyo kwa lengo la kuwawezesha wateja wake kupata muda wa kuchati zaidi.

Alifafanua kwamba hayo yote yatawezekana kwa kutumia mtandao wa 3G ambao una kasi na nguvu kubwa.

“Tunapenda wateja wetu watumie mtandao wetu kwa kuwasiliana bure na hivyo kukata kiu yao ya mawasiliano”.

Alitoa wito kwa wateja wa Vodacom na Watanzania kwa ujumla kutumia huduma hiyo ya mtandao wa Intaneti.

Aliwaomba Watanzania kujiunga na Vodacom ili kupata huduma hiyo bure na hivyo kuwasiliana zaidi.

Alisema huduma hiyo itapatikana kwa simu za mkononi na pia kwa Laptop zilizounganishwa na USB Moderm.

Tangu kuanzishwa kwake miaka kumi iliyopita Vodacom imekuwa ikizindua huduma mpya kila mara kwa lengo la kurahisha huduma za mawasiliano kwa wateja wake.

Hivi sasa kampuni hiyo inawateja zaidi ya milioni saba ambao wanaunganishwa na huduma mbalimbali zenye lengo la kuboresha maisha yao, baadhi ya huduma hizo ni kama M-Pesa, ambayo ni njia ya haraka na uhakika ya utumaji wa pesa hapa nchini.

Vodacom ndiyo wa kwanza kuanzisha huduma hiyo hapa nchini.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA