Nov 29, 2010

MATUKIO YALIJITOKEZA KATIKA VIWANJA VYA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA MAWIZIRI NA MANAIBU…!!!

Waziri wa Nsihati na Madini Mh. William Ngeleja akiwa amekaa kwenye nafasi maalum zilizotengwa kwa ajili ya mawaziri na manaibu waziri akiwa anasubira kuapishwa katika sherehe zilizofanyika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam

Waziri wa fedha Mh Mustafa Mkullo akisalimiana na kupongezana na Mh. Jumanne Maghembe Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika kabla ya kuapishwa katika Viwanja vya Ikulu.

Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Ofisi ya Waziri Mkuu Mh. Maria Nagu akifurahi jambo na Waziri wa Ulinzi Dk. Hussein Mwinyi katika viwanja vya Ikulu.

Waziri wa Mambmo ya nje na Ushirkiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe (kushoto) katika picha ya pamoja na Mh. Lazaro Nyalandu (kulia) Naibu Waziri wa Viwanja na Biashara ambaye ni mbunge wa Singida Kaskazini

Waheshimiwa wakijadiliana jambo kabla ya kuapishwa katika viwanja vya Ikulu.

Mh. Benard Membe akisalimiana na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mh.Shamsi Vuai Nahodha katika viwanja vya Ikulu

Waziri wa Ujenzi Mh. John Pombe Magufuli akitafakari jambo kabla ya kuanza kwa sherehe za kuapishwa kwa Mawaziri pamoja na manaibu waziri katika viwanja vya Ikulu

Waziri wa mawasiliano na uratibu Ofisi ya Rais Mh. Stephen Wassira akisalimiana na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Anna Tibaijuka

Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Baraza lake Jipya baada ya shughuli za kuapisha Mawaziri na Manaibu wake.

Mh. John Magufuli pamoja Mh. Anna Tibaijuka wakirudi sehemu zao walizopangiwa baada ya kupiga picha ya pamoja na Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe hizo.

Mh. Rais akiwa na Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wakirejea kwenye katika sehemu maalum ambayo iliandaliwa kwa ajili ya hafla za kuapishwa Mawaziri na manaibu Waziri baada ya kupiga picha ya pamoja

Mtangazaji wa ITV na Radio One Nambari 9 mgongoni Maulid Baraka wa Kitenge akimdokeza jambo Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam

Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete mwenye mapenzi na watoto akisalimia mtoto aliyekuwa amebebwa na mama yake katika viwanja vya Ikulu ilipofanyika hafla ya Kuapisha Mawaziri na Manaibu.

“HAYA NDIO NITAANZA NAYO KWA HARI ZAIDI NGUVU ZAIDI NA KASI ZAIDI” – WAZIRI MAGUFULI

Waziri wa Ujenzi Mh. John Pombe Magufuli

************************

Dk Magufuli alitaja mambo hayo kuwa, ni mvutano ndani ya Wakala wa barabara (Tanroads) kufuatia ajira tete ya Ofisa Mtendaji Mkuu, rushwa katika kandarasi, ujenzi wa daraja la Kigamboni, barabara ya Mandela, tatizo la msongamano wa Dar es Salaam na mpango wa ujenzi wa barabara za juu (Flyovers), malipo ya nyumba za serikali, usimamizi wa barabara na kupiga vita makundi na majungu kwenye wizara.

Wakati akiya bainisha hayo pia aliingilia sakata la ajira ya Mrema huku akimshangaa kwa kutoa matangazo ya ajira za Mameneja wote wa mikoa wa Tanroads na wakuu wa idara nyeti makao makuu, bila kile
alichokiita idhini ya bodi. Bila kusita, Waziri Magufuli alimtaka Mrema kusimamisha ajira hizo na kuwaandikia barua mameneja waliopo kuendelea na kazi zao kama kawaida, isipokuwa nafasi moja iliyowazi ya meneja wa Mkoa wa Dodoma. “Nimesoma katika gazeti moja wiki hii, umetangaza nafasi za kazi…kuna utaratibu kwa kazi zozote zinapotangazwa, hivyo waandikie vyombo vyahabari kuwa umefuta nafasi hizo,” alisema Dk Magufuli na kuongeza
umetangaza nafasi hizo baada ya kuona nawe unaondoka, fanya kazi hata kama hiyo nafasi imetangazwa na fanya kama vile hutaondoka kesho na unaishi miaka 100.”

Waziri huyo alielezea kushangazwa kwake pia na ripoti ya Mrema, aliyotoa hivi karibuni ya utendaji Tanroads na kuweka bayana kuwa, ilikuwa na upungufu kwani haikuwa na sahihi ya aliyekuwa waziri wa
kipindi hicho, Dk Shukuru Kawambwa, wala Katibu Mkuu wa wizara hiyoi, Omari Chambo.

Dk Magufuli ambaye anaonekana kuwa mkali, jasiri na mwenye msimamo katika kazi, alionya watendaji wote kwa ujumla akiwaambia: “Majungu yaishe kwa kuwa hayatatujenga na tena mmekuwa mkila rushwa kwa sasa
tunawaambia, tutategesha hata hela za mapolisi nawaombeni muache rushwa kwa wakandarasi.” Swala la pili, Dk Magufuli alisema kipindi cha miaka mitatu cha uongozi wake, atahakikisha barabara za juu zimeanza kujengwa kuondokana na msongamano wa magari Dar es Salaam.

Kuhusu ujenzi wa barabara ya Mandela, alitaka taarifa ya mwelekeo wa ujenzi wake ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia jana.

Dk Magufuli kwa msisitizo alisema: “Tumekuja kufanya kazi, wananchi wamechoka kuona ubabaishaji huo, na kuanzia ni barabara ya Mandela, nataka taarifa ya ujenzi ndani ya mwezi mmoja, kwa maana mkandarasi
sijui ni rafiki yenu au ni ndugu yenu kwani, hata kituo cha kazi hayupo sasa nataka ripoti yake alipofikia.”

Alisema hakuna haja ya kuwasumbua askari wa usalama barabarani kuongoza msongamano wa magari, huku wakazi wa jiji wakilia na kulalamikia kero hiyo wakati nchi imesheheni wahandisi wa kutosha.

Dk Magufuli alisema kama maghorofa yanaweza kujengwa kipindi kifupi, iweje ishindikane kwa barabara za juu. “Hata barabara za juu zinawezekana, hivyo kazi ya matrafiki ibakie kukaa na kutulindia nguzo zetu na kukamata magari yanayofanya makosa,” aliweka wazi.

Alimpa changamoto Chambo, akimtaka kuhakikisha fedha zinapatikana kutoka Wizara ya Fedha kuharakisha ujenzi wa miradi kwani, hawakwenda wizarani hapo kucheza. Kuhusu tabia ya baadhi ya wakandarasi wa nje kuzorotesha miradi, alisema tabia ya wakandarasi hao kushindwa kufanya kazi na kugeuza
eneo hilo kupata faida, imefikia ukingoni na hivi sasa hawatakiwi, wafukuzwe na kung’anyanywa vibali ili wasifanye kazi eneo lote la Afrika Mashariki.

Dk Magufuli alisema lazima kuhakikisha kila mkuu wa idara anawajibu kuwasimamia wakandarasi wa eneo lake na wakishindwa, hatasita kuchukua hatua ikiwemo ya kuwafukuza kazi.

Alionya: “Sisi pia tutakuwa na kazi tutavamia maeneo na tukikuta mmeshindwa kufanya kazi tutafukuza mkandarasi na wewe ukifuata, hatutacheka na mtu tumekuja kufanya kazi maana barabara nyingi zilizochini ya Tanroads ndizo zenye matatizo, hivyo lazima malengo yatimizwe kipindi cha miaka mitatu.”

Aliweka bayana kwamba, hataki kuwa mnafiki ndio maana ameamua kueleza ukweli na kama huko nyuma kulikuwa na makundi yanatakiwa kumalizwa kila mmoja linatakiwa lianze kubadilika. Kuhusu mradi sugu wa ujenzi wa daraja la Kigamboni, Dk Magufuli alionyesha kushangaza kuona ujenzi unasuasua na kutaka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuweka bayana kama hauwezi, atahakikisha linajengwa kwa fedha za serikali kwa kuomba kutoka Benki Kuu (BoT).

Kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege Songwe, alisema Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Prosper Tesha, anapaswa kuhakikisha na kusimamia kukamilika kwa uwanja huo uliopo mkoani Mbeya kutokana na mkandarasi kuchukua muda mrefu.

“Lazima usimamie ukweli ni suala la kujiuliza kwanini ule uwanja haukamiliki na hauishi, inawezekana mnawabembeleza nini hao wakandarasi? naomba usimwogope mtu, fanya kazi hata siku ukifa amini
utakwenda kuwa mkurugenzi mkuu wa viwanja vya ndege mbinguni,” alisema.

Alitaka watendaji kujituma na kurudisha heshima ya wizara hiyo, kuachana na majungu ya kupigana vita, wenyewe kwa wenyewe jambo lililosababisha kila mmoja kuwa na kundi lake.

Alisema ni vema kuhakikisha wale waliokopeshwa nyumba wanalipa madeni na wakishindwa kufanya hivyo, wafikishwe mahakamani ikiwamo kunyang’anywa nyumba hizo kwa kuwa wanasheria wapo, watakaosimamia
shughuli hiyo.

Dk Magufuli alikwenda mbali zaidi akitangaza kufanya mbinu za uchunguzi, kubaini utekelezaji sheria akisema: “Magari yanazidisha uzito, ipo siku nitafanya msako wa kushtukiza kwa magari yanayozidisha uzito… nitaingia katika lori moja na kupanda halafu nitajibadilisha kwa kuvaa miwani na kofia ili nikamate wale wafanya kazi wenu wa mizani maana wanachukua rushwa sana.”

MH.WAZIRI HAWA GHASIA ARIPOTI KAZINI LEO TAREHE 29/11/2010…!!!

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Hawa Ghasia akilakiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. George Yambesi (kulia) na Mkutugenzi wa Utawala na rasilimali watu Bw. Aloyce Msigwa (kushoto) mara baada kuwasili kuanza majukumu yake leo jijini Dar es Salaam

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Hawa Ghasia (kulia) akikaribishwa kwa furaha na wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Menejementi ya Utumishi wa Umma mara baada ya kuwasili Ofisni kwake leo jijini Dar es Salaam

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Hawa akizungumza na viongozi na baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo mara baada ya kuwasili Ofisini kwake mapema asubuhi ya leo. Pamoja na mambo mengine amewataka wafanye kazi kwa bidii ili kuimarisha Utendaji katika Sekta ya Umma nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Umma Bi. Hawa Ghasia akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili ofisini leo (Picha na Aron Msigwa- MAELEZO)

Nov 26, 2010

Kipenga Chalenji chapulizwa leo Vumbi la Chalenji kuanza kutimka leo



Beki wa Kilimanjaro Stars,Shadrack Nsajigwa akichuana na mshambuliaji wa timu hiyo,salum Machaku katika mazoezi ya timu hiyo jana jijini Dar es salaam.


PAZIA la michuano ya Kombe la Chalenji inafunguliwa leo jijini Dar es Salaam na kushirikisha timu 12 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati na nyingine zilizoalikwa mahususi kuiongezea ladha michuano hiyo.

Michuano hiyo ya wiki mbili, mshindi wake ataibuka na dola 30,000 (karibu Shilingi 42 milioni) ambazo zimetolewa na wadhamini, Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL, ikishirikiana na ile ya Serengeti (SBL).

Timu hizo zimegawanywa katika makundi matatu, ambako Kundi A linaundwa na wenyeji Kilimanjaro Stars, Chipolopolo ya Zambia, Intamba ya Burundi na Somalia, ambayo haijawasili.

Kundi B linajumuhisha Amavubi ya Rwanda, wageni waalikwa, Ivory Coast, Sudan na Zanzibar Heroes wakati Kundi C linazo, Uganda Cranes, Harambee Stars ya Kenya, Flames ya Malawi na Ethiopia.

Kulingana na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), ambao ndio waandaaji wakishirikiana na shirikisho la soka nchini (TFF), wameeleza kuwa maandalizi yamekamilika.

Kilimanjaro Stars leo watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Chipolopolo ya Zambia baada ya mchezo wa kwanza wa ufunguzi utakaoanza saa nane mchana utakazozikutanisha Somalia na Burundi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholous Musonye alisema maandalizi yamekamilika na timu zote, isipokuwa Somalia tayari zilikuwa zimewasili nchini kusubiri kuanza kwa michuano hiyo.

Alisema mashindano haya kwa sasa yamezidi kuboreshwa na kuongezwa ladha kwani timu mwalikwa zimekuwa nyingi tofauti na miaka ya nyuma hali inayoonyesha kuonekana kutanuka kwa michuano hiyo mwaka huu.

Ufunguzi wa michuano hiyo utaanza saa 8:00 mchana kwa mchezo kati ya Burundi na Somalia ambao utafanyika kabla ule wa wenyeji, Kilimanjaro Stars dhidi ya Zambia.

Michezo hiyo itatanguliwa na sherehe za ufunguzi ambapo timu zote 12 zitaingia kwa maandamano maalum na kufunguliwa rasmi kwa mashindano hayo.

Kwa upande wa kikosi cha Kilimanjaro Stars chini ya kocha wake Jan Poulsen kiko kamili tayari kwa mchezo wao wa kwanza dhidi ya Chipolopolo huku wakitamba kuwa watahakikisha wanaanza vyema kuipeperusha bendera ya nchi na kulibakiza kombe hilo hapa nyumbani.

Huo utakuwa mtihani wa kwanza kwa kocha huyo (Poulsen) katika mashindano hayo makubwa baada ya kukabidhiwa mikoba na Marcio Maximo mapema mwaka huu.

Kibarua hicho kitanoga endapo ataanza vyema kazi yake kwa kuipa ushindi Kilimanjaro Stars katika michuano hiyo.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Mwananchi, Poulsen alisema wamejiandaa vyema katika mashindano hayo na anategemea vijana wake wataanza kazi yao kama alivyowaagiza kwa kuanza na ushindi katika mchezo wa leo hivyo ni matumaini yake watakua katika nafasi nzuri ya kulitwaa kombe hilo.

Baadhi wa wachezaji wa kikosi cha Kilimanjaro Stars ambacho jana kilikuwa kikifanya maandalizi yake ya mwisho kimetamba kuwa kitahakikisha kinatoa dozi kwa wapinzani wao mara wanapokutana ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kufika katika hatua ya fainali.

Nahodha wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa alisema wamejiandaa kupigana hadi tone la mwisho katika mashindano hayo ili kuiletea sura mpya ya maendeleo Tanzania katika soka na kuhakikisha inabakiza kombe hilo hapa nyumbani.

Kocha wa Zambia, Dario Boneti amesema hatishwi na ugeni dhidi ya wapinzani wao katika mchezo huo wa kufungua pazia hilo bali anaamini ndio ataanza kurusha karata yake na kuhakikisha anashinda ili kuiwezesha kusonga mbele.

Wakati huohuo, Sweetbert Lukonge anaripoti kuwa huenda ratiba ya michuano ya Chalenje ambayo inaanza leo ikabadilishwa kufuatia kuwepo kwa wasiwasi juu ya ushiriki Somalia katika michuano hiyo.

Timu hiyo ambayo ilitarajiwa kuingia nchini jana tayari kwa kushuka uwanjani leo jioni katika mchezo wa pili wa ufunguzi wa michunao hiyo dhidi ya Burundi sasa inatarajiwa kuwasili nchini leo.

Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Msonye alisema kuwa kutoka na hali hiyo kamati ya mashindano ya baraza hilo ingekutana jana jioni kwa lengo la kuhakikisha mechi ya pili ya ufunguzi inakuwepo kama ilivyopangwa hata kama Somalia isiposhiriki.

"Mpaka sasa karibu timu zote zimewasili nchini tayari kwa michuano hiyo isipokuwa Somalia na Ethiopia.

"Lakini, pamoja hayo tuna wasiwasi juu ya ushiriki wa Somalia kwani kwa taarifa zilizotufikia timu hiyo ambayo ilikuwa iwasili leo,jana, sasa itawasili kesho,leo.

"Kutokana na hali hiyo tutakutana baadaye ili kuangalia ni jinsi gani ya kufanya ili mechi ya pili iweze kuwepo, " alisema Musonye

chanzo mwananchi

Pinda apokewa kwa bango UDSM





WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jana walimkaribisha chuoni kwao Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa bango lililoandikwa "Mtoto wa Mkulima, Tunalala Nje", kilio kilichomsukumu mtendaji huyo mkuu wa serikali kuahidi kukichangia Sh10 milioni kila mwaka kwenye ujenzi wa malazi yao hadi ukomo wa uongozi wake.

Wanafunzi hao wanalazimika kupanga kwenye hosteli na nyumba zilizo nje ya chuo hicho kikongwe kutokana na tatizo kubwa la upungufu wa malazi. Hata wale wanaolala chuoni hapo, hulazimika kujazana wengi kwenye chumba kimoja tofauti na zamani wakati chumba kimoja kilikuwa kikitumiwa na wanafunzi wawili tu.

Kutokana na upungufu huo, wanafunzi hutumia muda mwingi kwenye safari za kati ya chuoni na maeneo wanayoishi.

Hali hiyo ndio iliwasukumu waamue kumfikishia ujumbe mtendaji huyo mkuu wa serikali jana kwenye Ukumbi wa Nkurumah wakati Pinda alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya UDSM ambayo yamepangwa kufanyika Oktoba mwakani.

Iwapo Pinda atamaliza miaka mitano ya uongozi akiwa Waziri Mkuu atakuwa amechangia jumla ya Sh50 milioni katika jitihada za kukiwezesha chuo hicho kikongwe nchini kutatua tatizo la malazi kwa wanafunzi.

Katika tukio hilo la kwanza la aina yake kumkuta Pinda tangu alipoteuliwa tena kuwa waziri mkuu na kuapishwa wiki iliyopita, wanafunzi waliokuwa wameketi kwa utulivu sehemu ya juu ya Ukumbi wa Nkrumah walibandika bango hilo lililokuwa na maandishi hayo makubwa.

Pinda pamoja na baadhi viongozi waliokuwa meza kuu, walionekana kulisoma bango hilo lililoonyesha kilio cha wanafunzi hao kukosa maeneo ya kulala eneo la chuo na kulazimika kuishi nje ya chuo ambapo gharama za maisha ni kubwa.

Alipoanza kutoa hotuba yake, Pinda alianza kwa kulizungumzia bango hilo huku akieleza kuwa ujumbe walioukusudia wanafunzi hao umefika.

“Nilipokuwa nimeketi (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard) Membe aliniandikia ujumbe kwenye karatasi akaniambia 'umeona massage (ujumbe) yako?', nikamwambia 'niliiona toka zamani,'” alisema.

“(Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza) Mukandala naye akaniambia akihoji: 'Hawa wanafunzi sijui walipenya vipi na hili bango'.

"Nikamwambia 'itakuwa wametumia kaujanja kadogo tu kwa kulikunja likawa kama madaftari, kwa hiyo mtu akabeba kama kitabu anachoenda kujisomea', lakini pamoja na mwandiko na bango lao baya baya, nasema massage imefika.”

Kutoka na hali hiyo, Pinda alitoa ahadi ya kuchangia Sh10 milioni kila mwaka mpaka pale muda wa uongozi wake utakapomalizika.

Hata hivyo, baada ya kutoa ahadi hiyo Pinda alimtaka Membe naye kutoa ahadi yake na waziri huyo wa mambo ya nje akaahidi kutoa Sh5 milioni kila mwaka mpaka pale muda wa uongozi wa Pinda utakapomalizika.

“Natumaini utanikubalia ili na mimi niende nikawabane mawaziri, manaibu, makatibu wakuu na mabalozi wote waliosoma hapa ili nao watoe michango yao na ikiwezekana kiwango kiwe ni hiki hiki (Sh5 milioni kila mwaka),” alisema Membe.

Baada ya kauli hiyo ya Membe, Waziri Mkuu Pinda aliahidi kuwabana mawaziri na manaibu wote ili kuweza kuchangia chuo hicho.

“Desemba saba nitakutana nao, nitawabana mpaka watoe michango yao... nyie wakuu wa wilaya na mikoa zamu yenu inakuja,” alisema Pinda.

Hata hivyo, alimtaka Profesa Mukandala kuweka mpango madhubuti wa kutafuta watu mbalimbali waliosoma kwenye chuo hicho ili watoe michango ya kumaliza matatizo yanayokikabili chuo hicho.

chanzo - mwananchi

Poliosi wazuia mikutano ya Chadema nchi nzima




IGP Said Mwema

HALI bado si shwari baina ya Jeshi la Polisi na Chadema baada ya chombo hicho cha dola kukizuia chama hicho kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima "hadi hapo hali itakapotengemaa".

Lakini hakuna ofisa wa jeshi hilo aliyekuwa tayari kutoa maelezo bayana kuhusu amri ya kuzuia maandamano ya Chadema kwa kisingizio hicho, huku kila mmoja akirumshia mpira mwenzake na mwishoni kutaka aulizwe Waziri Mkuu au mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, ambaye hata hivyo hakupatikana.

Chadema iliweka rekodi ya kutwaa majimbo mengi ya Tanzania Bara kwenye uchaguzi mkuu na katika baadhi ya majimbo ilishindwa kwa tofauti ya kura chache na kusababisha kuibuka kwa vurugu zilizotokana na wananchi kudai matokeo yatangazwe mapema.

Baada ya kufanya uchunguzi kwenye majimbo kadhaa, Mwananchi imebaini kuwa wabunge na wagombea ubunge wa Chadema wamekuwa wakitaka kufanya mikutano ya hadhara kwa malengo tofauti, lakini wamejikuta wakizuiwa na jeshi hilo ambalo jukumu lake ni kutoa ulinzi kwenye mikutano ya hadhara.

Kamanda Clodwig Mtweve, ambaye hukaimu shughuli za IGP Mwema, alikiri kuwepo kwa agizo la kukizuia chama hicho kuendesha mikutano ya hadhara.

Kamishna Mtweve, ambaye anahusika na utawala na rasilimali, alisema:

"Maombi ya Chadema ambayo tumeyapokea yanaambatana na maandamano na wanasema ni maandamano ya kuhitimishwa kwa sherehe za mikutano ya hadhara ya kupongezana kwa ushindi.

"Sasa sisi tumeyakataa na kama ni sherehe za kupongezana tunasema zifanyike ukumbini. Na hii si kwa Chadema tu, bali hata kwa chama tawala."

Kamishna Mtweve alisema Chadema wanaruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara isiyoambatana na maandamano na kwamba amri ya kutoruhusiwa kwa maandamano haina muda maalum na inaendelea kuwepo hadi polisi watakapoamua vinginevyo.

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa alikitaka chama hicho kuwasilisha malalamiko hayo kwake kama kweli kimezuiwa kuendesha mikutano ya hadhara.

Awali kabla ya kuwasiliana na Kamishna Tweve, kamanda wa Kanda ya Dar es salaam, Suleiman Kova alisema: “Malalamiko ya Chadema ni ya nchi nzima. Mimi siwezi kuropoka chochote; kama unataka, ongea na Waziri Mkuu au Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema.”

IGP Mwema ndiye aliyemuelekeza mwandishi afuatilie suala hilo kwa Kamishna Tweve.

Mapema katika hatua za kutaka kuthibitisha taarifa hizo, Mwananchi iliwasiliana na msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso lakini akampa kazi nyingine mwandishi wetu.

“Wasiliana na makamanda wa majimbo yote yaliyotoa taarifa hizo kwa sababu wao ndio wahusika na wasemaji wakuu," alisema Senso.

Baadhi ya mikoa iliyoripotiwa kuwepo na matukio ya kuzuiwa kwa mikutano ya Chadema ni pamoja na Jimbo la Segerea mkoani Dar es Salaam, Mpanda (Katavi), Babati (Manyara), Arusha, Mbeya na Musoma mkoani Mara.

Makamu mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi amelalamikia kitendo cha jeshi hilo wilayani Mpanda kuzuia mkutano wa hadhara na maandamano yaliyopangwa kufanyika kesho jimboni humo.

Arfi, ambaye alishinda katika uchaguzi uliofanyika Novemba 14 baada ya kuahirishwa kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza kwenye majimbo saba wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, alisema kuwa wananchi wake waliandaa mkutano wa hadhara na kupeleka taarifa polisi, lakini walinyimwa ruhusa ya kufanya hivyo.

“Nikiwa najiandaa kwenda kwenye mkutano jimboni kwangu, nimepata faksi inayoonyesha barua ya Jeshi la Polisi inayokataza kuwepo kwa maandamano na mkutano huo,” alisema Arfi.

Barua hiyo yenye kumbukumbu namba MPA/S04/ Vol 2/93 imeleeza sababu ya kukatazwa kwa mkutano huo ni kuwepo kwa taarifa za baadhi ya vyama visivyo na mapenzi mema na Chadema kuashiria kuvunja amani.

“Pamoja na barua hii nakujulisha kuwa kutokana na taarifa tulizonazo, baadhi ya vyama vya siasa havina nia njema na zoezi hilo. Kwa sababu hiyo si ruksa kuandamana wala kufanya mikutano ya hadhara kwa sasa,” inasema barua hiyo ya polisi.

Arfi alisema kuwa amejaribu kuwasiliana bila ya mafanikio na kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa anayesimamia pia mkoa wa Rukwa.

Kwa upande mwingine, Arfi alisema wamebaini kuwa hali hiyo imetokea pia katika maeneo yote ambayo chama hicho kilipanga kufanya mikutano.

Aliyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na Jimbo la Tarime, Arusha, Segerea na Mbeya.

“Huu ni mkakati umewekwa ili kutukwamisha Chadema. Kama kuna hali ya hatari, mbona rais hajatangaza kuwepo kwa hali hiyo,” alihoji Arfi akirejea sheria inayomruhusu amiri jeshi mkuu tu kuwa ndiye mwenye uwezo wa kutangaza hali ya hatari ambayo huzuia mikusanyiko ya aina yoyote ile.

Alisema kwa hali hiyo serikali haiwatendei haki kwa kuwa imewazuia kufanya shughuli za siasa na kwamba watakutana kama chama ili kutoa tamko.

Kamanda polisi wa Ilala, Faustine Shilogile alikiri kuwepo na maelekezo ya kuzuia mikutano hiyo, akiweka bayana kuwa agizo hilo limetoka Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

“Agizo hilo tumelipokea kutoka ofisi zetu za Kanda Maalumu ya Dar es Salaam," alisema Shilogile na kuongeza: "Sababu za agizo hilo mimi sizijui ila nimeagizwa kufanya hivyo.”

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Rukwa, Isunto Mantage alisema hajapata taarifa zozote kuhusu hali mbaya ya usalama kwenye Wilaya ya Mpanda ambako mbunge Arfi alizuiwa kufanya mkutano wa hadhara.

"Hiyo barua kwenda kwa mbunge sijaiona, pengine ningeiona ningeweza kusema chochote... nipe muda niwasiliane na huko Mpanda ili niweze kufahamu kinachoendelea halafu nitakujulisha," alisema Kamanda Mantage.

Hata hivyo, alisema jana asingeweza kufanya mawasiliano na polisi wa Mpanda kutokana na kuwa kwenye ziara vijijini ambako kuna matatizo ya mawasiliano.

Kutoka mkoani Mwanza taarifa zinasema kuwa polisi imezuia maandamamo ya uzinduzi wa maadhimisho ya "Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Wanawake Majumbani" ikidaiwa ni kutokana na waandaaji wake kumualika mbunge mpya wa Jimbo la Nyamagana kwa tiketi ya Chadema, Ezekiel Wenje kuwa mgeni rasmi.

Mratibu wa maadhimisho hayo kutoka Shirika la Kutetea Haki za Wanawake (Kivulini), Yusta Ntibashima aliliambia gazeti hili jana kuwa polisi imezuia maandamano hayo kutokana na kuhofia watu kuwa wengi kwa sababu ya mgeni huyo rasmi.

Alisema kufanyika kwa maandamano hayo kungeweza kuwa na athari kubwa kwa uchaguzi mdogo wa udiwani ambao umepangwa kufanyika kesho katika kata mbili za Mkuyuni na Mirongo, hivyo kuwaomba waandaaji kufanya maandamano yao baada ya uchaguzi.

“Tukiwa katika kikao cha pamoja, Kamanda Sirro alisema jeshi lake haliwezi kutoa kibali cha maandamano kwa kuhofia watu watakuwa wengi na hivyo kusababisha kuzuka kwa vurugu kama zile za uchaguzi mkuu wakati watu walipochoma ofisi za CCM,” alieleza Ntibashima akimkariri kamanda wa polisi mkoa.

Kamanda huyo alisema jeshi lake lilipaswa kupewa taarifa wiki moja kabla ili liandae askari wa kutuliza wengi wa kutosha kila aneo ili kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani na kuepuka maafa.

Hata hivyo, habari kutoka ndani ya jeshi hilo zimeeleza kuwa, sababu za kuzuia maandamano ni kuhofia lawama ambazo zingeibuka kutokana na mgeni rasmi wa shughuli hiyo kuwa mbunge wa Chadema.

“Kama mgeni rasmi angekuwa kiongozi mwingine na siyo mbunge wa Chadema, basi maandamano hayo yangeruhusiwa, lakini CCM walitushutumu sana baada ya uchaguzi kuwa tulishindwa kulikomboa Jimbo la Nyamagana na tulikuwa tukiwaacha vijana kutamba na kufanya wanavyotaka... naona ameogopa kulaumiwa tena kamanda,” alieleza mmoja wa maofisa wa polisi ambaye hakutaka kutaja jina lake gazetini.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Kamanda Sirro alisema amezuia maandamano hayo kutokana na kutokuwa na muda wa kutosha baada ya waandaaji kuchelewa kutoa taarifa.

Kuhusu taarifa kuwa agizo hilo linahusiana na uchaguzi, Sirro alisema: “Kwa sasa nipo nje ya Mwanza; nitarejea Jumatatu, naomba unitafute... nitafafanua ni kwa nini tumezuia.”

Mkurugenzi wa Kivulini, Maimuna Kanyamala alisema uamuzi wao wa kumualika Wenje kuwa mgeni rasmi ni utaratibu wa kawaida na kwamba kila mara wanapokuwa na maadhimisho hayo hualika viongozi mbalimbali.
Alisema wakati majimbo ya Nyamagana na Ilemela yakiwa chini ya wabunge wa CCM, walikuwa wakiwaalika wabunge hao wa chama tawala na hawakukutana na vikwazo.

“Mgeni rasmi huchaguliwa katika kikao cha maandalizi ya maadhimisho. Lengo la kuwa na mgeni rasmi ni kupata kiongozi ambaye kwa uwezo wake anahusika na utungaji sera ama mabadiliko," alisema.

Akizungumza na gazeti hili, Wenje alisema polisi wanaingilia mambo bila ya kujua kwa kuwa maandamano hayo si ya kisiasa na hayana uhusiano na Kata ya Nyamagana kwa kuwa uchaguzi unafanyika kwenye Kata ya Mkuyuni na Mirongo.

“Nadhani Jeshi la Polisi linaitafsiri vibaya sheria. Mimi ni mbunge kama wale wa CCM, sasa siwezi kuzuiwa kuendelea na shughuli zangu kama mbunge kwa sababu ya kisingizio cha uchaguzi. Haya ni maandamano ya wanaharakati na siyo maandamano ya Chadema, polisi wanapaswa kuelewa hilo,” alisema Wenje.

Mkurugenzi wa mambo ya katiba na Bunge wa Chadema, John Mrema alisema chama chake kimeshtushwa na hatua ya polisi kuzuia mikutano ya chama hicho na kwamba kesho watatoa tamko.
"Wametuzuia nchi nzima; tayari tumekusanya ushahidi mwingi kutoka maeneo mbalimbali," alisema Mrema.

"Tunashangaa kwani vyama vya siasa vinakosa kazi baada ya uchaguzi? inakuwaje wametuzuia kufanya mikutano yetu, uchaguzi umekwisha, nchi ina amani na utulivu wa kutosha, hakuna vurugu, lakini wao wanasema wametuzuia kwa sababu ya taarifa za kipelelezi wakidai eti hali ni tete. Hii ni hofu isiyo na msingi."

chanzo - mwananchi

UAM yaungana CECAFA kupiga vita malaria michezoni


Meneja wa kampeni ya Tuungane Kutokomeza Malaria,David Kyne akizungumza katika Mkutano Mkuu wa CECAFA katika hoteli ya Paradise jijini Dar es Salaam.Rais wa CECAFA na TFF Leodgar Tenga (wapili kushoto) akiwa na Danny Jordan mwenyekiti wa kamati ya FIFA World Cup South Africa (wa kwanza kushoto), afisa wa CECAFA pamoja na Afisa Mtetezi wa UAM,Anna-McCartney Melstad wakifuatilia mkutano huo uliofanyika mchana wa huu katika hoteli ya Paradise City,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar.

**** ***** **********
Leo tarehe 26 Novemba 2010 hapa Dar es Salaam, katika mkutano wa waandishi wa habari kufungua mashindano ya Tusker Challenge yanayo anza kesho, washiriki na wadau wa kampeni ya “Tuungane Kutokomeza Malaria” - United Against Malaria (UAM) wameungana na wandaaji wa mashindano kumulika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Eneo hili la Afrika watu wapatao Milioni 38.9 huugua Malaria miongoni mwao wakiwa watoto.

Zaidi ya watu 209,000 hufariki kila mwaka ikiwa ni karibu robo ya vifo vyote vya malaria vinavyotokea barani Afrika. Malaria ni ugonjwa unao zuilika na kutibika ilihali kila sekunde 45 mtoto mmoja hufariki kwa Malaria na kusababisha hadithi za huzuni na umasikini.

Rais wa shirikisho la mpira la CECAFA Ndugu Leodegar Tenga alisema,” Mchezo wa mpira wa miguu unataka jamii yenye afya ili uendelee na kukua. Wanahitajika makocha, wachezaji, wasimamizi, marefa na hasa mashabiki wenye afya. Bila watu wenye afya hatuwezi kuendeleza soka. Jamii yenye Malaria haina afya, ndio maana tunaunga mkono juhudi za kutokomeza malaria zinazofanywa na kampeni ya United Against Malaria”

Timu 12 za Afrika Mashariki na Kati pamoja na washiriki wageni kutoka Malawi, Zambia na Ivory Coast zimekusanyika hapa Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano ya CECAFA, uongozi wa juu wa CECAFA umetangaza kushiriki kikamilifu katika kampeni za kutokomeza Malaria na kuhakikisha wanatumia mbinu zote za kuzuia wachezaji kupata Malaria ikiwa ni ahadi yake ya kujiunga na kampeni ya UAM.

“UAM imepata ushirikiano wa hali ya juu kutoka CECAFA, hii inadhihirisha dhamira yao ya kushiriki katika vita dhidi ya Malaria.” kasema David Kyne, Meneja wa kampeni ya UAM. Mashirikisho ya soka, timu za mataifa na wachezaji watatumia umaarufu wao katika michezo kuelimisha jamii zao dhidi ya umuhimu wa matumizi ya njia zote zinazoshauriwa na wataalamu za kujikinga au kutibu Malaria kama vile vyandarua, kupima na kutumia dawa endapo wataambukizwa malaria.

Ili kuthibitisha jitihada za sekta binafsi kuunga mkono kampeni ya UAM, mdhamini wa mashindano ya CECAFA atashawishi makampuni mengine yajiunge na kampeni na kusisitiza umuhimu wa wafanyakazi na wateja wao kuwa salama kwa kutumia kinga ama tiba dhidi ya Malaria.

“Kama wadhamini wa CECAFA Tusker Challenge Cup 2010 tunaungana na kampeni ya United Against Malaria kwa kuhakikisha wafanyakazi wetu wanapata kinga na tiba dhidi ya Malaria kwa muda wote.” Alisema Caroline Ndugu, Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweries Limited. Aliongeza ”Leo hii tuna ahidi kununua vyandarua vyenye dawa ya kuzuia mbu wa Malaria kwa wafanyakazi wetu wote hapa Tanzania”

Njia mbalimbali za kufikisha ujumbe wa malaria kwa jamii ambazo zitatumika muda wote wa mashindano ni pamoja na matangazo yatakayorusha katika vyombo vya habari kama redio, runinga na mtandao wa internet, mabango yenye ujumbe wakati wa kila mechi na nguo za mazoezi ya awali kwa timu kabla ya mechi pamoja na ujumbe kwenye programu ya mashindano.

Nov 24, 2010

Kikwete atangaza baraza la mawaziri

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ametangaza baraza lake jipya la mawaziri kukamilisha uundaji wa serikali tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.

Kikwete amewaacha mawaziri kadhaa wa zamani na kuteua sura mpya kama vile Profesa Anna Tibaijuka.

Rais Kikwete alitaja serikali yake mbele ya waandishi wa habari katika shughuli iliyofanyika Ikulu mjini Dar Es Salaam, akibainisha kuwa hakuna mabadiliko makubwa katika idadi ya wizara, zipo jumla ya wizara 26.

Sura mpya kadhaa zimetajwa ikiwa ni pamoja na Profesa Anna Tibaijuka atakayesimamia wizara ya ardhi na makazi.Profesa Tibaijuka alikuwa mkurugunzi mkuu wa shirika la makazi la Umoja wa Mataifa kabla ya kujiuzulu na kwenda kugombania ubunge jimbo la Muleba Kusini.

Waziri aliyetajwa kinyume na maelezo ya wachambuzi wengi wa kisiasa ni Samuel Sitta, baada ya kuondolewa kiti cha spika wa bunge la Muungano, sasa anakuwa Waziri wa maswala ya Afrika Mashariki.

Mawaziri wengi wa serikali iliyopitwa wamerejeshwa tena katika majukumu waliyokuwa nayo awali kama vile Bernard Membe atakayeendelea kusimamia mambo ya nje.Mustapha Mkullo anarudi kuongoza wizara ya fedha.

Marekebisho kadhaa ameyataja Rais Kikwete katika uundaji wa baraza lake kuwa idara ya vijana imeondolewa kutoka wizara ya kazi na kuhamishiwa wizara ya habari na michezo.

Wanasiasa kadhaa waliokuwa katika serikali iliyopita wameachwa, baadhi yao ni wasomi maarufu kama Profesa Peter Msola aliyekuwa Sayansi na Teknolojia, Profesa Juma Kapuya aliyekuwa Kazi na Profesa David Mwakyusa aliyekuwa afya, mwingine ni kada wa chama kama John Chiligati aliyeachwa wizara ya ardhi.

Waziri hao wataapishwa siku ya Jumamosi katika viwanja vya Ikulu ya Dar Es Salaam.

Orodha kamili ya mawaziri na manaibu waziri hii hapa chini.

Namba

Ofisi/Wizara

Waziri

Naibu Waziri

1.

Ofisi ya Rais

1. Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais – Utawala Bora

Mathias Chikawe

2. Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu

Stephen Wassira


2.

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma

Hawa Ghasia


3.

Ofisi ya Makamu wa Rais

1. Muungano

Samia Suluhu

2. Mazingira

Dr. Terezya Luoga Hovisa


4.

Ofisi ya Waziri Mkuu

1. Sera, Uratibu na Bunge

William Lukuvi

2.Uwekezaji na Uwezeshaji

Dr. Mary Nagu


5.

Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

George Mkuchika

1.Aggrey Mwanri

2. Kassim Majaliwa

6.

Wizara ya Fedha

Mustapha Mkulo

1. Gregory Teu

2. Pereira Ame Silima

7.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Shamsi Vuai Nahodha

Khamis Kagasheki

8.

Wizara ya Katiba na Sheria

Celina Kombani


9.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Bernard Membe

Mahadhi Juma Mahadhi

10.

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Dr. Hussein Mwinyi


11.

Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

Dr. Mathayo David Mathayo

Benedict Ole Nangoro

12.

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Charles Kitwanga

13.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Prof. Anna Tibaijuka

Goodluck Ole Madeye

14.

Wizara ya Maliasili na Utalii

Ezekiel Maige


15.

Wizara ya Nishati na Madini

William Ngeleja

Adam Kigoma Malima

16.

Wizara ya Ujenzi

Dr. John Magufuli

Dr. Harrison Mwakyembe

17.

Wizara ya Uchukuzi

Omari Nundu

Athumani Mfutakamba

18.

Wizara ya Viwanda na Biashara

Dr. Cyril Chami

Lazaro Nyalandu

19.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Dr. Shukuru Kawambwa

Philipo Mulugo

20.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

Dr. Haji Hussein Mpanda

Dr. Lucy Nkya

21.

Wizara ya Kazi na Ajira

Gaudensia Kabaka

Makongoro Mahanga

22.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

Sophia Simba

Umi Ali Mwalimu

23.

Wizara ya Habari, Vijana na Michezo

Emmanuel Nchimbi

Dr. Fenella Mukangara

24.

Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Samuel Sitta

Dr. Abdallah Juma Abdallah

25.

Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika

Prof. Jumanne Maghembe

Christopher Chiza

26.

Wizara ya Maji

Prof. Mark Mwandosya

Eng. Gerson Lwinge

Nov 22, 2010

ZAIN AFRIKA SASA KUITWA AIRTEL

Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za mkononi ya Zain Tanzania, mapema leo imezindua jina jipya ambapo sasa itajulikana kwa kwa Jina la Airtel. Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, majira ya saa nne asubuhi na kuhudhuriwa na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali nchini. Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Sam Elangalloor alisema kuwa, wameamua kuzindua chapa yake ya kimataifa ili kuunganisha shughuli zake kwa wateja barani Afrika ambapo wateja wake wote wataweze kufaidi viwango sawa. Pichani: Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Sam Elangalloor (katikati), akiwa ameshikilia Logo mpya tayari kwa uzinduzi huo Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Miradi na Maendeleo Afrika, Steve Torode na mwisho ni Mkurugenzi wa
Masoko wa Airtel Tanzania, Cheikh Sarr.

Wakurugenzi Airtel Tanzania wakisikiliza maswali kutoka kwa wanahabari.

Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Cheikh Sarr akifafanua jambo katika uzinduzi huo.

Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sam Elangalloor akielezea utaratibu mzima wa zoezi hilo.

eneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Mutta Mganyinzi wa (pili kushoto) akifuatilia mchakato huo na wandishi wa habari waliohudhuria katika uzinduzi huo.

aadhi ya Wanahabari wa vyombo mbalimbali nchini wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo.


Logo mpya ya Airtel

kwa msaada wa global publisher

MAHOJIANO MAALUM NA MBUNGE WA MBEYA MJINI (CHADEMA) MHESHIMIWA JOSEPH MBILINYI (MR. SUGU)…!!!

Mheshimiwa Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, awali ya yote mimi nikiwa mwakilishi wa Blog ya Mohammed Dewji, Mo blog, ninachukua nafasi hii kukupa pongezi kwa kuaminiwa na wananchi wa jimbo lako, Hongera sana.

MO BLOG : Unawezaje kuizungumzia safari yako ya siasa mpaka hapa ulipofikia katika hatua ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini?

MH SUGU: Kwanza ninachukua nafasi hii kuwashukuru wapiga kura wa Jimbo langu la Mbeya Mjini kwa kuniamini na kunichagua kwa kura nyingi kama ulivyosikia, lakini pia kazi hii ya uchaguzi kwangu na kwa wananchi wa Mbeya mjini imeandika Historia mpya, ambayo hakuna anayeweza kuivuruga.

Nikushukuru pia kwa kunipongeza kwa hatua hiyo, lakini pili ninaomba kukueleza kwamba hatua hii, sio siasa kwangu, bali ni harakati ya miaka 15 il.iyopita kupitia muziki, ambapo walizungumza na kulalamikia mambo kadhaa kuhusu Taifa yalizungumzwa.

Kimsingi ni kuwa tumeamua kuhamisha jukwaa la madai ya msingi kutoka katika muziki mpaka kwenye siasa, ambayo harakati zake zinaonekana kukubalika na kutekelezwa, na chombo hicho ni Bunge, hivyo jukwaa limehamia rasmi Bungeni.

Awali mambo yale ya muziki yalionekana kuwa ya kihuni tuliyazungumza kwenye majukwaa ya muziki, na waliopaswa kuyatekeleza hawakuchukua hatua kwa kuamini ni kama madai ya wahuni, lakini kwa sasa wajue kwamba mambo hayo ni rasmi katika chombo cha kutunga sheria, kwa maana tutayazungumza na kutaka hatua za kuchukuliwa kulingana na mahitaji ya jamii, kwani kwa pamoja hatukuzungumza mambo ya vijana ni malalamiko na mahitaji ya jamii kuhusu maendeleo.

MO BLOG: Mheshimiwa Mbilinyi, unaweza kuweka bayana hili wazo la kugombea Ubunge katika Jimbo la Mbeya, ulilipata lini na uamuzi kamili uliamua kuuchukua lini?

MH SUGU: Kuna mtu ndani ya CHADEMA ambaye hivi sasa naye ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo anaitwa John Mnyika, huyu alinishauri kuingia katika siasa akiamini kwamba ninao uwezo mkubwa wa kufanya siasa, na aliamua kunishawishi kufanya hivyo mwaka 2005, lakini kwa kipindi hicho sikuwa na utayari wa kuanza kufanya siasa, japo Mnyika aliamini kwamba ninaweza.

Mnyika pia katika kipindi hicho alinitaka kuwania Ubunge katika Jimbo la Ubungo na kwamba yeye binafsi anaweza kujitoa ili kuniachia nafasi hiyo, ili aweze kufanya kazi kama Meneja wa Kampeni zangu, kuhakikisha Jimbo hilo linachukuliwa na Chadema, na alifanya hivyo kwa nia njema akiamini kwamba uwezo wangu katika jukwaa la muziki inaweza kuwa lulu kwenye siasa.

Kwa hali hiyo, mwaka 2005 nilikataa kabisa kuwania nafasi hiyo Ubungo, na hivyo Mnyika aliamua kuchukua fomu na kukabiliana na Mgombea wa CCM wakati huo Mzee Charles Keenja, na ni hakika kwamba Mnyika alishinda uchaguzi ule kwani mimi binafsi nilikuwa mfuatiliaji wa karibu wa uchaguzi huo.

Mwaka 2010 Wananchi wa mjji wa Mbeya walinihitaji na kunitaka kwenda kugombea Ubunge katika Jimbo hilo la mjini, wakiamini kuwa mimi ni mtoto wa nyumbani na kwamba mazingira ya wazi yalikuwa yakiniihitaji kufanya hivyo bila makosa.

MO BLOG: Jimbo la Mbeya lilikuwa na ushindani mkubwa, ulifanya au uliwaambia nini wana-Mbeya mpaka wakaamua kukupa wewe ridhaa hiyo ya uwakilishi Bungeni na tena ukiwa bado kijana kabisa?

MH SUGU: Hakuna kitu cha ajabu sana, bali niliwaambia ukweli , niliwataka kuachana na siasa za ukabila, na nilifanya hivyo nikiamini kwamba hilo ni muhimu kwa ajili ya kuibua mawazo mazuri na mapya kwa jamii ya wana MBEYA.

Nilitumia nafasi hiyo kuipeperusha bendera ya CHADEMA kulihubiri vizuri kabisa suala hilo na kutokana na hali hiyo, tulifanya kazi ya kuwaeleza matatizo ya kijamii yanayoikabili Mbeya na jamii kwa ujumla.

MO BLOG: Mheshimiwa Mbilinyi, ni Changamoto zipi ulikumbana nazo toka kampeni zinaanza mpaka siku ya kutangazwa wewe kuwa ni mshindi kwa matokeo ya kura zilizopigwa na wananchi?

MH SUGU: Ni kutokana na maelezo yangu ya hapo juu, hali ya kusema ukweli na wananchi walinikubali mimi kuwa kwa maelezo yangu na hoja nilizozitoa majukwaani na sera wakasema nafaa kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini kupitia CHADEMA na kuachana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mgombea wake, Benson Mpesya, ambaye katika miaka yake 10 ya uwakilishi wananchi ameweza kuwagawa na kusababisha majeraha ya makabila kisiasa.

Mgombea wa CCM Mpesya hakuweza kuhimili vishindo vya CHADEMA kwa hoja kwani kwa namna moja ama nyingine baada ya kuona maji yanamfika shingoni na kila kona anayopita jina linalotajwa kuwa mbunge ni la kwangu, aliamua kushiriki kikamilifu kuendesha siasa za maji taka.

Katika uongozi wake wa jimbo hilo Mpesya aliwagawa wananchi kwa mitazamo ya ukabila na, huku akitumia muda mwingi katika kampeni kunitukana mimi majukwaani kwamba mimi ni muhuni, akiamini kuwa Jimbo la Mbeya lenye changamoto za wasomi wengi haliwezi kusimamiwa na Mwanamuziki.

MO BLOG: Kulikuwa na hisia kwamba matokeo ya sehemu mbalimbali yangeweza kuchakachuliwa ili kumwezesha mgombea wa CCM kupata ushindi, je kwa upande wako uliwahi kupata hofu ya aina hiyo, na kwamba mshindi akatangazwa aliyeshindwa badala ya aliyeshinda?

MH SUGU: Kwanza hilo lisingewezekana, kwani mimi sikuweza kulala kwa masaa 27 mpaka matokeo yanatangazwa, lakini pia maamuzi ya kushinikiza yalikuwa yakifanywa na wananchi, kila mtu alikuwa mfuatiliaji wa matokeo, na kwamba mawakala wetu wote walifanya kazi kwa uaminifu wa hali ya juu.

Uaminifu wa mawakala hao, ulisaidia sana kunihakikishia Ushindi na kwamba katika muda mfupi, tulikuwa tunajua kwamba tayari tumeshinda na kwamba tulihitaji hatua za kutangazwa kwa matokeo hayo kutoka kwa Msimamizi ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya.

Ningependa pia kukuhakikishia kwamba wasingeweza kuchakachua matokeo kwani wananchi walijiandaa kwa lolote, na hasa kwamba walitarajia ushindi utakuwa wangu na waliahidi kuzilinda kura kwa nguvu zote, na kwa hali hiyo USHINDI WANGU ULIKUWA WAZI MNO.

MO BLOG: Sasa ndio umeingia Bungeni, wananchi wa Mbeya wategemee nini kutoka kwako?

MH SUGU: Wategemee kile walichotarajia, na pengine kingine zaidi ya hilo,watarajie kazi nzuri kulingana na yale tuliyokuwa tukihubiri majukwaani, kwani huu ni muda muafaka kwa ajili ya kazi hiyo na kulingana na matakwa na mahitaji yao, hatutafanya kitu bila kusikiliza wananchi wanahitaji kipi kiwe cha kwanza na kipi kiwe cha mwisho.

Uongozi bora ni kusikiliza wapiga kura, na ukiona kiongozi asiye na nafasi ya kupata maelezo ama mawazo ya wapigakura wake, basi huyo ni dikteta, na hatua hiyo kwangu kwa aina hiyo yeyote haitawezekana na nitaendelea kujifunza kutoka kwa watu wengine ndani ya CHADEMA na nje ya chama changu.

MO BLOG: Nini ambacho unapanga kukifanya katika miaka miwili ya kwanza ya uongozi wako kama Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini?

MH SUGU: Asilimia 90 (90%) ya Jiji la Mbeya halina barabara za maana na za lami, hivyo katika kampeni moja ya mambo ya msingi ambayo niliyapa nafasi ya kwanza ni kutaka Mbeya ibadilike taswira yake na kuwa na barabara za lami, na kwamba kukosekana kwa hali hiyo kunapunguza hadhi ya Mbeya kuwa Jiji halisi.

Pia nimehitaji kufuatilia na kuboresha mfumo wa Afya kwa wananchi, kwani nikiwa huko nimesikia kwamba hivi sasa kumuona Daktari ni lazima mwananchi awe na Sh 15,000, hivyo nikiwa Mbunge sasa nimetarajia kuitisha vikao kwa ajili ya kujadili hali hiyo na kukubaliana hatua za kuchukua.

Mfumo wa Elimu, kuwa na shule za Sekondari, zenye maktaba na maabara pamopja na kutambulisha masomo ya Teknolojia ya Kompyuta kwa wanafunzi wa shule za Sekondari na Vyuo kwa nia ya kuwaandaa na mazingira ya ajira kwa vijana, kwani hali hiyo inachangia kuwakosesha vijana wengi sifa za kupata kazi .

Vijana wasiojua matumizi ya kompyuta wamekuwa katika mazingira magumu kupata kazi kwenye maeneo mengi ya wawekezaji nchini, kutokana na kigezo cha kuwa na ufahamu ama ujuzi wa matumizi ya kompyuta, na kutokana na hali hiyo ninatarajia kufanya mazungumzo na shirika moja la kimataifa linaloshughulikia ukuzaji wa masomo ya teknolijia ya kompyuta kwa nchi za Afrika.

Shirika hilo limefanikiwa kufanyakazi zake kwa nchi za Ghana na Kenya, ambapo program yao ni kutoka kompyuta ya mkononi moja kwa mtoto mmoja, One Laptop for One Child, mpango ambao umeonekana kufanikiwa na kuwaondolea adha vijana wa nchi hizo na changamoto za ajira kwa kigezo cha kujua matumizi ya kompyuta.

Lakini pia katika sekta ya Afya, kabla hatujaanza kazi rasmi tayari serikali Norway, imetoa vitanda 200 kwa ajili ya Hospitali ya Wazazi Mbeya META.

MO BLOG: Katika suala la Elimu, Mbeya ni Jiji hivi sasa, lakini hakuna Chuo Kikuu, je huwezi kushawishi wadau na wahisani wakafanyakazi ya kujenga Chuo Kikuu kimoja au kubadili kimojawapo kilichopo kuwa Chuo Kikuu?

MH SUGU: Mbeya ni kweli haina Chuo Kikuu, na hili ni moja kati ya changamoto za Ubunge wangu wa miaka mitano Mbeya, lakini kuna matawi ya Vyuo kama MZUMBE, Chuo cha TECU, Taasisi ya Sayansi na Teknolojia (Mbeya Institute of Science and Technology) MIST ambacho ninatarajia kwa kushirikiana na wadau tutahimiza jamii kuwa kiwe Chuo Kikuu cha Umma Mbeya.

MO BLOG: Ukiwa kama msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya, wasanii watarajie nini kutoka kwako?

MH SUGU: Bunge ni chombo cha kutunga sheria na wasanii sasa watarajie ubora wa maisha yao, yaani kama vitani watambue kwamba bataliani sasa inaingia katika Jiji na utamu wa vita ama mtu kutangazwa mshindi ni dhahiri kabisa, na kwa hali hiyo muziki tumefanya kwa nia ya kukemea madhambi kwa watu, lakini sasa tutahitaji hatua za kuchukua badala ya kukemea tu.

MO BLOG: Suala ambalo umewahi kuzungumzia kuhusu kuhujumiwa kwa wazo lako la Mradi wa Maralia Haikubaliki, utalishughulikiaje katika kipindi hiki ambacho tayari umechaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini?

MH SUGU: Suala la Maralia kwanza nataka kuweka wazi, na kuhakikisha hilo sio wazi ni kazi iliyokuwa tayari na mimi nimenyang’anywa kazi ikiwa tayari na mikataba yote ikiwa tayari, kwa haki suala hilo bado bichi na halijaisha hata kidogo, na katika suala hili nataka kusimamia usemi wa Rais Jakaya Kikwete kwamba KWENYE VITA VYA HAKI USHINDI NI LAZIMA, na kwa hali hiyo nataka kuonyesha jamii kwamba malalamiko yangu ni ukweli na sitanii hata kidogo.

Na kutokana na hali hiyo, kipimo kwamba ninaweza kufanyakazi kama Mbunge kwa mafanikio na kukidhi kiu ya wananchi walionichagua ni pamoja na kutetea haki zangu binafsi, na hili la MALARIA HAIKUBALIKI, litakuwa miongoni mwa mambo ya msingi.

Nitalifuatilia mpaka kieleweke ili jamii ijue kwamba nilikuwa na lalamikia haki na sio suala la uongo.

MO BLOG: Katika baadhi ya nyimbo zako, umekuwa ukipigia sana kelele suala la wasanii kuibiwa kazi zao, sasa ukiwa mmoja wa watunga sheria utawasaidieaje wasanii waweze kufaidika na jasho la kazi zao?

MH SUGU: Nilipoanza harakati za Muziki wa Bongo Fleva, hakuna aliyetambua kwamba leo hii hali ingeweza kuwa kama ilivyo, wapo watu ambao walitucheka na kusema ni uhuni, kuna wazazi waliozuia hata watoto wao kushirikiana nasi kwa kudai kwamba wataharibika.

Lakini kidogo kidogo mpaka sasa, muziki huu umeendelea kupata heshima na sasa umeonekana kupata njia rasmi ya vijana wengi kupata maendeleo, yao binafsi kwa maana ya ajira na hatimaye maendeleo ya jamii kwa ujumla.

Na kwa hakika kilichoonekana kuwa hakipendwi sasa ni rasmi kinapendwa na jamii na kukubalika, hivyo ninatarajia kutengeneza historia kama hiyo ndani ya Bunge kwa kudai na kupigania haki za wasanii, kwani maisha ya wasanii kwa Tanzania ni sawa na daraja kwa mawakala, Ulaya wanamuziki wanapata zaidi kuliko wakala, lakini Tanzania ni tofauti, kwani mawakala wanapata zaidi kuliko wasanii.

Kwa niaba ya MO BLOG

40 KUUNDA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anatarajiwa kutangaza baraza la mawaziri hivi karibuni.
BARAZA jipya la mawaziri linalotarajiwa kutangazwa wiki hii na Rais Jakaya Kikwete linatarajiwa kuwa na mawaziri kati ya 40 na 45, kati yao 23 wakiwa ni mawaziri kamili.Kwa maana hiyo, baraza hilo litakuwa na wizara 23 tu, Mwananchi imedokezwa.

Habari ambazo Mwananchin imezipata zinaeleza kuwa katika baraza hilo jipya, ambalo litakuwa la tatu kwa Rais Kikwete tangu alipoingia Ikulu mwaka 2005, waliokuwa manaibu waziri watano katika baraza lililopita, watapandishwa na kuwa mawaziri kamili.

Vyanzo vyetu vya kuaminika vimeeleza kuwa idadi ya mawaziri wanawake itaongezeka kulinganishwa na baraza lililopita na kwamba uteuzi umezingatia umri, uzoefu pamoja na uwiano wa mikoa.

Pamoja na kuwepo kwa sura mpya, idadi kubwa ya waliotajwa katika baraza hilo ni wanasiasa wakongwe ambao wengi wao walikuwamo katika baraza lililopita.

Chanzo chetu kimeeleza kuwa Rais Kikwete amekataa kuwapa nafasi ya uwaziri wabunge waliopata ushindi kwa kura chache katika uchaguzi mkuu uliopita.

Miongoni mwa wabunge waliokuwa manaibu kwenye baraza lililopita ni Emmanuel Nchimbi (Songea Mjini) ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Adamu Malima (Mkuranga) aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini na Christopher Chiza (Buyungu) ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji.

Wengine ni Dk David Mathayo (Same Magharibi) aliyekuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Ushirika pamoja na Balozi Khamis Kagasheki (Bukoba Mjini) aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani.

Habari hizo zinasema kuwa Wizara ya Fedha na Uchumi itaendelea kuwa na manaibu waziri wawili kama ilivyokuwa katika ngwe ya kwanza ya miaka mitano ya serikali ya Rais Kikwete.

Mbali na wabunge 27 waliotajwa na gazeti hili jana wengine ambao wametajwa kuwemo kwenye serikali mpya ya Rais Kikwete ni Muhammed Seif Khatibu kutoka Jimbo la Uzini ambaye alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Stephen Wasira(Bunda) aliyekuwa Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, na Hawa Ghasia (Mtwara Vijijini) aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma.

Wengine ni Mustapha Mkulo (Kilosa) aliyekuwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Mathias Chikawe (Nachingwea) aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria pamoja na Aggrey Mwanri (Siha) aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, (Tamisemi).

Wengine ni Bernard Membe (Mtama) ambaye katika serikali iliyopita alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa na Emmanuel Nchimbi (Songea Mjini) ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Mawaziri wengine waliokuwa katika Serikali iliyopita wanaotajwa kurejeshwa katika kipindi hiki cha mwisho cha utawala wa Kikwete ni Ezikeil Maige (Msalala) ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, William Ngeleja (Sengerema) aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, na Celina Kombani (Ulanga Mashariki) ambaye alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi),

Wengine ni Profesa Juma Kapuya (Urambo Magharibi), aliyekuwa Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, Profesa Mark Mwandosya (Rungwe Mashariki), ambaye alikuwa Waziri Maji na Umwagiliaji, Dk Hussein Mwinyi (Kwahani), aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Shukuru Kawambwa (Bagamoyo), aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na John Magufuli (Chato) ambaye alikuwa Waziri wa Maendeleo Mifugo na Uvuvi.

Wabunge wanaotajwa kuingia katika baraza la mawaziri kwa mara ya kwanza ni Anna Tibaijuka (Muleba Kusini), Samuel Sitta (Urambo Mashariki) na ambaye alikuwa spika wa Bunge la Tisa, Dk Harrison Mwakyembe (Kyela), Anne Kilango (Same Mashariki).

Wengine ni Januari Makamba (Bumbuli) ambaye alikuwa msaidizi wa rais katika awamu ya kwanza ya utawala wa Rais Kikwete, Salehe Pamba (Pangani), Steven Masele (Shinyanga Mjini), Gerson Lwenge (Njombe Magharibi) na Nyambari Nyangwine (Tarime).

Wengine ni Shamsi Vuai Nahodha (mbunge kuteuliwa) na alikuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Angela Mkwizu (Viti Maalum) na Amos Makala (Mvomelo) ambaye ni Mweka Hazina wa CCM, Said Bwanamdogo (Chalinze), Lazaro Nyarandu (Singinda Kaskazini) na Zakia Meghji (wa kuteuliwa).

Chanzo hicho kimebainisha kuwa Rais Kikwete amedhamiria kuunda baraza dogo la mawaziri litakalo kuwa na tija ikilinganishwa na alilounda wakati akiingia madarakani mwaka 2005, ambalo lilikuwa na mawaziri wapatao 60 na ambalo alilivunja Februari 2008 baada ya Edward Lowassa kujiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu.

Lowassa alijiuzulu kutokana na kashfa ya zabuni tata ya ufuaji umeme wa dharura iliyotolewa kwa kampuni ya Richmond.

Hata hivyo, baraza jipya aliloliunda baadaye chini ya Waziri Mkuu mpya, Mizengo Pinda lilikuwa na mawaziri 27 na manaibu mawaziri 21.

Kati ya mawaziri ambao hawatarajiwi kurejea kwenye baraza jipya ni wale walioanguka katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM na wengine waliangushwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu.

Akilihutubia Bunge Alhamisi iliyopita, Kikwete alidokeza kuunda serikali itakayokuwa na watu waadilifu, makini na wachapakazi hodari.

Pia alisema ataunda serikali ya watu wachache ambao wataondoa urasimu watakaokuwa karibu na wananchi na kushirikiana vizuri na wabunge wote bila kujali vyama vya siasa wanavyotoka.


CHANZO: MWANANCHI

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA