Oct 9, 2011

NUMBER 1 FAN AMENITENGA NA NUMBER 1 LOVE.

Yawezekana ukadhani ni story tu ndo zimemfanya benard paul aka ben pol mkali wa DOM ambaye anasumbua sana kwenye medani ya muziki wa kizazi kipya aka Bongo flava na albam yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la MABOMA ikiwa na maana NYUMBANI yenye ngoma kali kama NIKIKUPATA ngoma ambayo ilimpatia tunzo ya wimbo bora wa rnb na kuwapiga chini wakali wengine ambao alikuwa nao katika category moja kama vile diamond,barnaba na wengineo,pia kuna ngoma kama MAUMIVU na MABOMA iliyobeba jina la albam husika.
Ben pol ambaye game ya muziki aliaza kitambo ila akafanikiwa kutusua baada ya kuwa chini ya lebo ya music lab iliyo chini ya mkali wa touches huyu si mwingine bali ni duke touchez na ngoma ambayo ilimtambulisha uzuri kwenye game ya music wa kizazi kipya ni ngoma ya NIKIKUPATA ingawa kabla ya hapo alishiriki katika kuweka nakshi kwenye ngoma ya NIKKI MBISHI iliyojulikana kama PLAY BOY na baada ya kusikika ndipo akaibuka na NIKIKUPATA.


Pol ambaye amehitimu kidato cha sita mwaka 2009 na kwa sasa mpango wake ni kujiendeleza zaidi kielimu ameweka wazi kuwa mdundo wake mpya unaokwenda kwa jina la NUMBER 1FAN ni skendo ya kweli iliyomtokea yeye mwenyewe na kusababisha upande wake wa pili wa maisha kukumbwa na misuko suko kiasi cha Yule ambaye alikuwa akitamani kumpata na baada ya kumpata akampenda b’se kila mmoja anahisia nahii kitu mapenzi so dizaini nae akawa amezama kwa manzii ambaye aliamini they will be together for the rest of their life kumbe ilikuwa kinyume na alivyofikiri kwani baada ya kukutana na number 1 fan ambaye alikuwa akipenda kusikiza ngoma zake na kufikia hatua ya kumtaka amfundishe kuimba akatoswa na mpenzi wake .

‘’Unajua mimi ni tofauti na wasanii wengine,najitahidi sana kukutana na fanz wangu kwa namna yoyote ambayo naweza kiasi nikipata tym kidogo huwa naitumia kucheck wit ma fanz na kubadirishana nao mawazo,if ur ma fan n u have any means of contact me just do it n i will be able to reach u,kama ni facebook,twitter,ama u have ma number just dial on me n i will have fun together wit u’’

‘’Ila ki ukweli number one fan amebadiri mwelekeo wa maisha yangu kwa kukosa kile ambacho kila siku nilikuwa natamani kukipata yaani true love from the one i use to love n still i have feelings of love to ma x ila sina jinsi tena and all its bse of my number one fan inaniuma sana’’


So wat is goin on wit ya number one fan?’’kaka huezi amini hakuna chochote kinachoendelea kati yangu na my number one fan dat y nikaamua kuandika hii ngoma katika kufikisha ujumbe wangu kwa Yule ambaye alikuwa mpenzi wangu na hata yeye( number 1 fan) nilimwambia na anajua kuwa yeye ndo cauz ya mimi kuachwa na nimpendae.’’



Kwa sasa ben po ni moja kati ya wakali ambao wanajuvunia kuwapo katika nyumba ya vipaji tht na kamwe hajutii uwepo wake kwenye nyumba hiyo yenye wakalikama vile barnabas classic,amin,ditto,beker,davy d,mwasiti,linnah,recho,Beatrice na wengine kibao ambao huzaliwa kila kukicha.

Oct 8, 2011

Nchi za Afrika-Asia zaungana juu ya kusomesha wanawake


Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akihutubia Mkutano wa Afrika-Asia 2011 leo ambapo amesisitiza elimu yenye maadili ndiyo njia pekee ya kumkomboa mwanamke pamoja na jamii kwa ujumla. Mkutano huo umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Wanawake cha Sookmyung nchini Korea Kusini ambacho kimetiza miaka mia moja na tano tangu kianzishwe 1906.
Picha ya pamoja ya Viongozi wa ngazi ya juu kutoka Afrika na Asia waliohudhuria mkutano huo
Baadaye Spika Makinda alipata wasaa wa kukutana na vyombo vya habari na kufafanua umuhimu wa kuwa na vyuo vikuu vya wanawake. Hapa anaongena Avivang Tv ya Korea
Salma Dinya ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. John Dodoma ambaye alialikwa kwenye mkutano huo kuiwakilisha Tanzania kama kiongozi kijana. Hapa anatoa mada kwa wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Asia na Afrika kuhusu Tanzania.
Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Korea katika Vyuo Vikuu mbalimbali walifika kumsiliza spika wao
Spika wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwa na mwenyeji wake Dkt Han, Rais wa Chuo Kikuu cha wanawake cha Sookmyung, Korea
Wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali Asia na Afrika wakimsikiliza Bi. Salma Dinya
kwa hisani ya fullshangwe.blogspot.com

BALOZI MUTINDA MUTISO AFUNGUA MASHINDANO YA KENYA AIRWAYS GOLF SAFARI


Balozi wa Kenya nchini Tanzania Matiso Mutinda akipiga mpira wa Gofu wakati alipozindua Mashindano ya Kenya Airways Golf Safari kwenye viwanja vya Gymkana jijini Dar es salaam leo huku Meneja mkazi wa Kenya Airways Lucy Malu wa tatu kutoka kulia akishuhudia, mashindano haya yanafanyika nchi zaote za Afrika ambazo kampuni hiyo ina matawi, na mwakani washindi wote kutoka nchi 35 za Afrika watakutana pamoja mwakani na kushindana Nairobi nchini Kenya, ambapo mshindi wa kila nchi wa shindano hilo atagharamiwa kila kitu ikiwa ni pamoja na malazi kwenda kwenye mashindano hayo makubwa nchini Kenya.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mutindo Mutiso kulia akizungumza na Lucy Malu Meneja mkazi wa kampuni ya Kenya Airways wakati wa uzinfuzi wa mashindano ya Kenya Airways Golf Safari.
Meneja mkzi wa Kampuni ya ndege ya Kenya Airways Lucy Malu akiwa katika picha ya pamoja na Mchezaji wa gofu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Aerengeti Breweriers SBL wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya Gofu yanayoitwa Kenya Airways Safari Golf yanayozinduliwa leo katika viwanja vya Gymkana jijini Dar es salaam.
Mchezaji wa gofu Mustafa Jacks akipiga mpira wakati wa mashindano hayo yanayoendelea kwenye viwanja vya Gymkana.
Mchezaji K. Mbaya raiwa wa Kenya akipiga mpira katika mzunguko wa kwanza wa mchezo huo.
Victor Joseph akipiga mpira.
Mwanadada Halima Mussa ni mmoja wa washiriki katika mashindano hayo ya Kenya Airways Golf Safari.
Meneja mkazi wa Kampuni ya ndege ya Kenya Airways Lucy Malu katikati na Mchezaji wa gofu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Serengeti Breweriers (SBL) wa pili kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakzi wa Kenya Airways.
Wafanyakzi wa kampuni ya Blackberry Enterprises wakiwa katika picha ya pamoja.
kwa hisani ya fullshangwe blogspot

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA