May 26, 2010

Nyerere to be declared saint at Namugongo

FORMER Tanzanian president Julius Kambarage Nyerere will be declared saint on June 1, as part of the celebrations to mark this year’s Martyrs’ Day.

Heads of states of African countries and Nyerere’s widow Maria Gabriel Magige will attend.

Last year, President Yoweri Museveni supported the campaign to have Nyerere recognised as a saint.
The campaign began in January 2006, when Rome accepted the request from Bishop Musoma of Northern Tanzania Diocese.

Meanwhile, preparations for the celebrations are in high gear. Fr. Dennis Ssebuggwawo, the shrine rector, said the programme at the Catholic Shrine will begin with a nine-day Novena (reciting of prayers) from May 26 to June 2.

Ssebuggwawo said Moroto diocese will host this year’s celebrations under the theme “I am with you always, yes to the end of the time (Mathew 28:20)”.

Twenty-two Uganda martyrs were murdered at the Catholic shrines between 1885 and 1886.

May 18, 2010

KAKA MICHUZI KUMILIKI TOVUTI TOKA KWENYE BLOG(hongera kaka one more step ahead)




Blog ya Muhidini Issa Michuzi ipo mbioni kuhama.Hivi punde itakuwa tovuti kamili inayojitegemea na hivyo kuondoka katika ulingo wa .blogspot.com.Ufuatao ni ujumbe kutoka kwake Issa Michuzi.
Asalaam Aleikhum, Bwana Asifiwe, Tumsifu Bwana, Shalom, Namaste, konnichiwa, Nihao, olá…..
Kwa heshima na taadhima nawaamkia wadau wote popote mlipo ulimwenguni. Salamu nilizotoa hapo juu naomba ifahamike kuwa hizo nilizozimudu ni kama kielelezo kwamba nia ni kumuamkua kila mmoja kwa nafasi yake popote alipo. Mie sijambo na naendelea na Libeneke kama kawaida.
Waama, baada ya salamu, napenda kuwafahamisha kwamba Globu ya Jamii hivi karibuni itaingia kwenye awamu mpya ya dot com, ikiwa katika jitihada za kuboresha Libeneke zaidi.
Imechukua muda kuchukua hatua hii kutokana na mazoea kwani toka September 8, 2005 hadi leo si kidogo ati. Hivyo mabadiliko kama yapo inabidi yafanywe kwa uangalifu wa hali ya juu ili kutoleta usumbufu wa aina yoyote kwa wadau wa Globu ya Jamii ambao kwangu ndiyo waajiri wangu wakuu.
Naam, wakati wowote kuanzia sasa libeneke la issamichuzi.blogspot.com litaingia katika awamu ya www.imichuzi.com. unakaribishwa kujaribu na kutoa maoni yako.

SOME OF JIWE'S FRIENDZ ON FB


(shost huyu anaitwa aneth kashuba duu ana matalent kibao aisee)(

shost anaitwaJudy Premier Ruhumbika moja katii ya marafiki zangu wa facebook)

May 15, 2010

NDO TUZO ZETU HIZI JAMANI

kill music awards zimepata wenyewe na mkali wangu Khalid Ally alikuwepo eneo la tukio na akanimegea mastory yote na pics za kutosha toka eneo la tukio.

(bwana misosi akipokea tuzo ya ragga)







May 14, 2010

SAKATA LA TID NA HASHEEM

Zipo habari kuhusu celebrities wetu ambazo huwa nikizisikia kinachonijia kwanza ni masikitiko.Huwa nasikitika ninapoona kwamba watu fulani ambao ni role-models kwa vijana wetu,wanakuwa wanafanya mambo ambayo sio tu yanawavunjia heshima wao wenyewe,bali pia yanaporomosha maadili ya kiungwana na kiutu.

Bila shaka mpaka hivi sasa umeshasikia habari za mcheza kikapu Hasheem Thabeet kumpiga au kupigana na mwanamuziki nyota TID wikiendi iliyopita pale Club Bilicanas jijini Dar. Baada ya vita ya mikono na mateke,vita sasa imebakia kuwa ya maneno.
Kila mmoja, Hasheem na mwenzie TID amekuwa akitoa maelezo tofauti tofauti kuhusu kilichojiri pale Bilicanas.Kwa mujibu wa Gazeti la Amani(la Global Publisherz), Hasheem anasema alichokozwa kupita kiasi na TID. Na TID anasema,kupitia blog yake,kwamba hajui kwanini Hasheem aliamua kumtenda alivyomtenda.TID haweki wazi sana kilichotokea.Anachosema yeye ni kama vile Hasheem aliamua tu kumfanyia “ubabe” na kumdunda.

Katika vita ya maneno,wakati mwingine ni vigumu kupata ukweli.Ukweli halisi wanao Hasheem na TID. Cha msingi kilichopo mbele ni kwamba kwa kuonyeshana ubabe au ego zenu mbele ya kadamnasi,nyote mmekosea. Kama ulichokozwa Hasheem you could have handled it differently. Verbal violence doesn’t have to end with physical violence. Na TID,kama maelezo aliyoyatoa Hasheem katika gazeti la Amani ni ya kweli,tabia ya kupenda kununua ugomvi,haikujengi bali inakubomoa na kukushushia heshima.
Hasheem maliza likizo yako urudi Marekani kuendeleza mchezo wako.You are a role model to many youngsters.Be one.TID zingatia kazi yako muhimu ya kuburudisha,kuelimisha na kuonya jamii kupitia muziki wako.Pamoja.

KILL SI NDO LEO SASA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Kama we ni mdau wa muziki wa hapa nyumbani tanzania basi ni wasaa wako wa kucheki na kill muzic award bse ndo kama zinafanyika hii leo pale diamond jubilee then tuone nani ataibuka kinara walau kwa kuzikomba japo tuzo mbili,huku akishuhudiwa na mkali wa dancehall toka pande za kingston jamaica jamaa anajulikana kama SEAN KINGSTON.

May 10, 2010

KILICHOJIRI KILL TAIFA CUP KITUO CHA IRINGA


Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufanyika kwa droo ya mashindano ya Kili Taifa Cup katika ukumbi wa mikutano wa TFF ,wengine ni Salim Madadi (kulia) na Iddy Mshangama wote ni Maafisa wa TFF.

Wakati mkoa wa kimichezo wa Kinondoni na mkoa wa Iringa ikie ndelea kufanya vema katika mashindano ya Kili Taifa Cup 2010 katika kituo cha Iringa ,timu ya Pinda Boys timu ya mkoa wa Rukwa ikiendelea kuwa kichwa cha Mwendawazimu katika mashindano hayo baada ya kukubali kichapo cha goli 4-0 dhidi ya Kinondoni leo huku Mbeya ikiambulia kipigo cha goli 1-0 dhidi ya Iringa.

wakati huo huo udhamini wa Kili Taifa Cup Iringa umelalamikiwa baada ya leo kushindwa kutoa fedha za mfungaji bora kama ilivyotangazwa wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo juzi jumamosi.

YALIYOJIRI BAADA YA UCHAGUZI MKUU UK


Jambo moja nililojifunza kutoka kwa hawa wenzetu wa nchi zilizoendelea ni kile kinachoelezeka vizuri kwa kimombo kama not settling for less.Yaani,kwa tafsiri isiyo rasmi,ni kutokubali kuridhishwa na pungufu ya matarajio kamili.Kama ni mwanasiasa na wananachi wanaona 'unawazingua' basi usitarajie kuwa wataendelea 'kukulea'.Kama ni kwenye soka,wenye timu hawatarajii pungufu ya ushindi.
Baada ya matokeo yasiyoridhisha kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Alhamisi iliyopita,tayari 'bundi' mbaya ameshaanza kukiandama chama cha Labour.Baadhi ya wanasiasa ndani ya chama hicho wamejitokeza hadharani kutaka Gordon Brown atoswe kwa madai kuwa yeye ndio hasa chanzo cha matokeo mabaya kwenye uchaguzi huo ambapo Labour iliambulia nafasi ya pili nyuma ya chama cha wahafidhina (Conservative Party).
Japo hadi sasa Brown hajatamka kama ataachia ngazi uongozi wa chama hicho lakini dalili ni kwamba presha ikiendelea kuongezeka hatokuwa na jinsi zaidi ya kujiuzulu.Hapa sizungumzii u-waziri mkuu bali hali ya mambo ndani ya chama cha Labour.
Kukurejesha nyuma kidogo,Labour imekuwa na makundi mawili 'yasiyoiva' kwa kitambo kirefu sasa.Kwa upande mmoja ni wale wanaofahamika kama Blairites,ambao wanamhusudu Waziri Mkuu wa zamani Tony Blair,na kwa upande mwingine ni Brownites,ambao wanamhusudu Gordon Brown.Inasemekana kuwepo kwa makundi hayo kumechangia kwa kiasi flani matokeo mabaya ya chama hicho katika uchaguzi uliopita.Inadaiwa kwamba mmoja ya watu wenye nguvu kubwa ndani ya Labour,Lord Mandelson,alitumia kampeni za Brown na Labour kumuimarisha David Miliband,'Waziri' wa Mambo ya Nje wa Uingereza na chaguo la Blairites kumrithi Brown.Inaelezwa kwamba wakati Labour wanazindua kampeni zao kwa ajili ya uchaguzi huo,Mandelson (maarufu kama Malaika wa Giza-Angel of Darkness-ndani ya Labour)alifanikisha safari ya Miliband kwenda Marekani kwa mazungumzo na Rais Obama,fursa ambayo wachambuzi wa siasa wanaamini ingemwezesha Brown kuonekana kama kiongozi mwenye nguvu katika siasa za kimataifa.
Inadaiwa pia kuwa kampeni ya Brown iligeuzwa na Mandelson kuwa 'makao makuu ya Miliband' kwa maana kuwa ilikuwa ikitumika kwa namna flani kumpromoti mwanasiasa huyo (Miliband) ambaye bado ana ukaribu mkubwa na Blair.Hata meya wa zamani wa jiji la London,Ken Livingstone ameligusia hilo katika makala yake aliyoandika kwenye gazeti moja la Daily Mail.
Kwa sasa,harakati zinazoendelea chini chini ndani ya Labour ni za kumrithi Brown.Yani imekuwa kama ndugu za mgonjwa wanapoanza kugombania urithi kabla mgonjwa huyo hajaaaga dunia.Alosema siasa ni mchezo mchafu hakukosea.Baadhi ya majina yanayohusishwa na mpambano huo ni pamoja na akina Miliband,yaani David na mdogo wake Ed,ambaye ni waziri wa mazingira,Ed Ball- 'waziri' wa elimu na 'waziri' wa mambo ya ndani Alan Johnson.
Na akina Miliband wanazua mvutano ambao unavuka anga za siasa kwa vile wakati David ni Blairite,mdogo wake ni Brownite.Inaelezwa kuwa tayari Ed ameshamfahamisha mama yao kuwa anadhamiria kupambana na kaka yake kwenye kinyang'anyiro cha kuiongoza Labour.Hata hivyo,inaelezwa pia kuwa bado yuko njia panda kwa vile kwa upande mmoja Brownites wenzie wanamwona kama chaguo mwafaka kwa nafasi hiyo,lakini kwa upande mwingine 'damu ni nzito kuliko maji' na anatafakari kama pengine itakuwa jambo la busara kumsapoti kaka yake.
Tukiachana na mvutano huo wa kifamilia,'vita' kubwa inatarajiwa kuwa kati ya kaka yake (David) na (Ed) Balls.Wakati David anasifika kwa upeo na akili ya hali ya juu (ni Mwingireza mwenye asili ya Kiyahudi huyu) na ufahamu wake wa siasa za kimataifa hasa kutokana na wadhifa alionao sasa,Balls ana sapoti kubwa kwenye vyama vya wafanyakazi ambavyo kimsingi vina nguvu ya kutosha kwenye chama cha Labour.Kadhalika,wakati David anaonekana kama mtu wa 'tabaka la juu' Balls yuko karibu zaidi na wana-Labour wa ngazi za chini.
Tukiweka kando kidogo matatizo yaliyo ndani ya Labour kwa sasa,huko kwa wahafidhina nako mambo si shwari sana.Kuna wanaomuona mgombea wa chama hicho,David Cameron, kama amewaangushwa kwa kushindwa kwake kupata ushindi wa jumla (overall majority).Upinzani wa chini chini dhidi ya Camron haukuanza kwenye uchaguzi huu tu bali tangu alipoweka bayana dhamira yake ya kukibadilisha chama cha Conservative kutoka mwonekano wake kama 'chama kibaya' (nasty party) kwenda chama chenye kujumuisha makundi mbalimbali katika jamii.Kabla ya harakati za Cameron,chama hicho kimekuwa kikitafsiriwa kama 'cha Waingereza Weupe wa tabaka la juu' na kinachokumbatia zaidi mabwanyenye kuliko watu wa kawaida.
Cameron amefanikiwa kwa kiasi flani kubadili taswira hiyo japo si sana.Katika uchaguzi uliopita alihamasisha uteuzi wa baadhi ya wagombea kutoka makundi ambayo kimsingi 'hayamo kwenye akili za chama hicho' kwa mfano wagombea kutoka jamii ndogo za wasio weupe (ethnic minority),shoga na mabinti kadhaa.Japo baadhi ya wagombea hao wameshinda,wengi wao wamefanya vibaya na tayari baadhi ya wahafidhina wanamlaumu Cameron kwa uamuzi huo wa 'kuwapigia debe wageni wa tamaduni za chama hicho'.
Jingine linalomwandama Cameron ni mchango wa kundi dogo la washauri wake wanaofahamika kama 'wana-Eton wa zamani' (ex-Etonian),yaani marafiki zake wa karibu aliosoma nao katika shule ya Eton yenye hadhi ya juu kabisa na chaguo la 'wateule wachache' kwa hapa.Hao ni pamoja na Kansela ('waziri wa fedha') kivuli George Osborne na mwanamikakati anayesifika kwa akili nyingi Oliver Letwin (ambaye pia ni 'waziri' kivuli).Wengine wanaotuhumiwa 'kumshika akili' Cameron ni pamoja na kiongozi wa zamani wa Conservative,William Hague,na Mkurugenzi wa Mawasiliano,Andy Coulson (ambaye kabla ya kuchukua wadhifa huo alikuwa mhariri wa gazeti maarufu kwa udaku la News of The World).Coulson anafahamika kwa uwezo wake katika 'kutengeneza fitna,majungu na kummaliza mtu' (maeneo yanayolipa umaarufu News of the World).
Washauri hao wa Cameron wanatuhumiwa 'kumshauri vibaya' mgombea hasa katika wazo la 'jamii kubwa' (Big Society) ambalo inaelezwa kuwa liliasisiwa na Letwin.Wakosoaji wanadai kuwa wazo hilo halikueleweka kwa wapiga kura na wengine wanakwenda mbali zaidi na kulieleza kama 'wazo muflisi'.Vilevile,inaelezwa kuwa Lord Ashcroft,'kibopa' aliyemwaga fedha nyingi kwa minajili ya Conservative kushinda uchaguzi huo,hajaridhishwa na matokeo ya uchaguzi huo,sambamba na 'kushindwa' kwa Cameron kusimama kidete kumtetea mhafidhina huyo tajiri (Ashcroft) alipoandamwa na skandali ya 'hadhi ya raia asiyelipa kodi kutokana na ukazi wake nje ya nchi' (non-domicile status).Lord Ashcroft anaamini kuwa suala hilo limechangia kupunguza kura za chama chao na anaamini kuwa Cameron angeweza kumtetea vizuri zaidi ya alivyofanya.Kadhalika,tajiri huyo anadaiwa kutopendezwa na wazo la Cameron kushiriki midahalo ya uchaguzi kwenye runinga,ambapo anaona kuwa ilisaidia kumuimarisha mgombea wa chama cha Waliberali (Liberal Democrats) Nick Clegg na hivyo 'kula' kura za Conservatives.






SASA HII NDO TEXT YA SIMBA ZEE

Mfalme wa Rhymes, Suleiman Msindi ‘Afande Sele’, wiki iliyopita ‘aliisapraiz’ Showbiz ya Ijumaa baada ya kuidondoshea SMS kali kuhusu Bongo Fleva. Unaweza kuisoma hapo chini;
“Hivi sasa kila mtu anajidai anaijua Bongo Fleva kuliko hata wajuzi na wazoefu wa game hili, Bongo Flava inakua upande wa uimbaji lakini marapa wapya hakuna anayeishika jamii. Wengi wana mashairi dhaifu sana na idea ni za kitoto.
“Wengi wanabebwa na ma-Dj wenye maslahi nao. Kuna Ma-Dj wanawaumiza makusudi wakongwe hata kazi zao za ukweli wanazibana wakidhani wanaua wakongwe kumbe wanaliua game zima. Wanakata nguzo kuu ambazo ni mashairi na ujumbe bora toka kwa wakongwe ambao wanatambua haki zao.
“Walionyonywa ni wengi, wanaharakati wa ukweli! Sasa jamii inapaswa kuamka na kudai kile cha ukweli na si kuamini kila wanachokisema ma-Dj walioanza kazi juzi wakati game imetolewa mbali tena kwa machozi, jasho na damu.
“Watu wanapaswa kujua kwamba Watanzania ni walewale na si wajinga kama baadhi ya Ma-Dj na watangazaji wanavyofikiri kuwa kila wanachotaka wao basi Wabongo wataamini. Leo hii kuna artists wanapewa promo kila siku kwa kulazimisha lakini bado ukija huku mtaani watu bado hawawajui kwakuwa mchango wao katika game haufanani na sifa wanzopewa.
“Shabiki wa Afande, Prof. Jay, Daz Nundaz ndiyo huyo huyo atakayemkubali na artist mpya anayetoka vyema katika game, sasa kama kutoka kwa wasanii wapya dhaifu ndiyo kunasababisha kuwaua wakongwe wa ukweli, basi mashabiki hawatoendelea kuamini game na matokeo yake hadhi ya muziki inashuka.
“Katika jamii, kitendo cha watangazaji fulani na ma-Dj kutowapa nafasi waasisi, basi na jamii haitokubali au kumtambua msanii mchanga anayekuzwa kwa uongo na ufisadi unaofanywa na ma-Dj pamoja na mameneja uchwara wanaoshinda wakihonga na kuleta fitina ya wasanii na watangazaji, lakini ukweli unatashinda.”



KUNA UKWELI JUU YA HAYA WAYASEMAYO WAKONGWE?????

Kwa wadau wafuatiliaji, watakuwa wanaunyaka ukweli kwamba big names on Bongo Hip Hop industry, Godfrey Tumain ‘Dudubaya’ na Suleiman Msindi ‘Afande Sele’ wapo kwenye vita ya maneno na wale ambao wanadai ni wanyonyaji.
Guys hao wanawagonga fatuma some DJ’s ambao wanadai ni wanyonyaji wasio na aibu, kwamba miaka nenda rudi, zao ni kuishi kimjini mjini kupitia migongo ya wanamuziki ambao wanahenyeka kutoka kimaisha bila mafanikio.
Dudu, ameachia CD ambayo ndani yake anawasaga ile mbaya wote ambao wanaishi kwa kudandia jasho la wasanii, DJ’s ambao wanadaiwa kuweka utaratibu no money no your song on air. Kwa upande wa Sele, yeye analaani kitendo cha DJ’s na some presenters kuwawekea kauzibe wasanii wenye misimamo, kuwabania nyimbo zao na kuwapa chati underground ambao hawauziki, hawana vipaji na hawalipi. Kwa kifupi ni kwamba Sele na Dudu wana hoja moja, ila uwasilishaji ni tofauti.
Ngumi Jiwe yeye ameamua kuingia studio na kuingiza vocal kwa lengo la kuwapaka anaowadisi, wakati Mzungu wa Roho yeye anafunua mambo kwa SMS.

Tunajenga hoja kwa staili hii; Bila shaka Sele na Dudu wana hoja za msingi lakini pengine haziwezi kuwa na maana yoyote ikiwa kilio chao kitabaki kujadiliwa kama pointi za kujadili vijiweni. Ni muda wa mabadiliko, wasanii ni lazima wawe pamoja ikiwa wanataka kufanikisha harakati zao.

Kinachosemwa na Sele au Dudu ndiyo kile ambacho kipo kwa wengi lakini wapo kimya kwa sababu ya kusumbuliwa na nidhamu ya woga. Ni vizuri kushirikiana ili kupata mafanikio ambayo kila msanii anayakata. Unyonyaji ni mwingi. Kukataa dhuluma ni hatua namba moja ya kuelekea kwenye malisho mema. Hatahivyo, kumbuka; Akili za kuambiwa changanya na zako

Van Persie - I like the look of Chamakh



Robin Van Persie has only watched Marouane Chamakh on television - but he likes what he has seen.
The Moroccan striker has been strongly linked with a move to Arsenal when his contract with Bordeaux expires this summer and Arsène Wenger admitted last week that he was "confident" a deal will be done.
Chamakh could link up with Van Persie at Emirates Stadium and the Dutch forward is excited at the prospect.
"[I know him] just from TV," said Van Persie.
"He looks good, he looks quite strong in the air, he scores lots of goals with his head and he looks quite confident on the ball.
"Hopefully it [the deal] goes through. I think it is good for all of us and that is why I am happy to see him coming here."



kama kawa wabongo kwa show za kiingilio miguu yako huwa nyomi braaaa


(umati wa wapenda dezo)
Jana pande za coco beach GRAND MALTA ilikuwa inazinduliwa rasmi kwa wanywaji wa vinywaji visivyo na kilevi,nilikuwa miungoni mwa watu waliojumuika pande zile ila ilikuwa ni kwa ajili ya kusimamia na kuhakikisha kipindi cha mchizi wangu wa ukweli KHALID ALLY aka TAZ ambaye nagonga naye muzigo hapa MLIMANI MEDIA ila ye akiwa upande wa TV na pindi lake la ukweli la LADHA BOMBA BONGO BULLETS linakwenda poa ile ila mia aisee.

(flowers wakioneshana uwezo wa kuzungusha uno)
        Nilichoshuhudia ni kwamba wabongo ni watu wa kupenda sana vya dezo though wanapenda sana kuparty,labda ni kutokana na ugumu wa maisha dat wahy wamekuwa hivyo ila kama maisha yangekuwa bora kweli kwa kila mtanzania basi tungekuwa tunalipa kiingilio kwenda kumuona lady jay dee na machozi bendii live kila anapopiga mzigo na siyo kusubiri mpaka kwenye show za bure.

(chege na temba wakipagawisha fanz wao)

ukiondoa hilo wakali wa muziki huu wa kizazi kipya kama vile MARLAW na WANAUME TMK wakiongozwa na jamaa ambao kwa sasa wako juu sana MH TEMBA na CHEGE walikonga vilivyo nyoyo za mashabiki lukuki waliokuwapo maeneo hayo kiasi kila ngoma iliyoimbwa ilikuwa ni shangwe kwa kila mmoja.
(marlaw kabla ya kusababisha picha zote kwa msaada wa global publisher)

JK apishe Ikulu - Mbowe

ZINGATIA:HABARI HII IMETOKA KWENYE GAZETI LA TANZANIA   DAIMA.

MWENYEKITI WA Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amemtaka Rais Jakaya Kikwete aondoke Ikulu kwa vile ameshindwa kuwalipa wafanyakazi mshahara wa kima cha chini sh 315,000.

Akizungumza mjini hapa jana, wakati akihutubia mamia ya wakazi wa Kijiji cha Wasso, alisema kitendo kilichofanywa na Rais Kikwete kimeonyesha wazi jinsi alivyokosa uzalendo kwa watu wake.
“Ninamshangaa Rais Kikwete anaendelea kufanya nini Ikulu wakati ameshindwa hata kuwalipa wafanyakazi kima cha chini cha sh 315,000 wanachodai,” alisema Mbowe.
Alisema umefika wakati wa Rais Kikwete kuondoka kwa vile amepoteza sifa zote za urais kwa kufikia hatua ya kushindwa hata kuwalipa mishahara Watanzania wanaovuja jasho lao kwa uchungu wakilitumikia taifa.
“Rais Kikwete ameshindwa kulipa mshahara wa sh 315,000, ajiuzulu na aondoke Ikulu mara moja…hana tena hata sifa moja ya kuwa rais wa nchi hii. Amekataa kulipa fedha ambayo serikali yake inayo ili yeye na wenzake waendelee kuila,” alisema Mbowe.
Alisema kama CHADEMA ikifanikiwa kushika hatma ya kuiongoza nchi, itaweza kuwalipa wafanyakazi mshahara wa kima chini hata ukiwa sh 400,000.
Katika hatua nyingine, chama hicho kimefanikiwa kuiteka Tarafa ya Loliondo, wilayani hapa kwa kuvuna mamia ya wanachama.
Kutokana na hali hiyo, Mbowe aliitangaza rasmi wilaya hiyo kuwa ngome mpya ya CHADEMA.
Mbowe akiambatana na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, aliwasili wilayani hapa juzi na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa wakazi wa Kata ya Arashi na wale wa mji mdogo wa Wasso.
Alisema amefika wilayani hapa kuwaunganisha wananchi wa Ngorongoro na kuwatia ujasiri utakaomaliza manyanyaso na dhuluma wanayofanyiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Nafurahi kufika Wasso, nafurahi kufika Loliondo….ni mara yangu ya kwanza. Sijaja kuwagombanisha wala kuwatenganisha katika vyama, nimekuja kuwaunganisha.
“Msikubali vyama vya siasa vilivyoundwa na binadamu viwatenganishe na kuwasahaulisha shida zenu za pamoja…nimekuja kuwaunganisha kupigania haki na utajiri wenu mliopewa na Mungu. Nawashukuru kwa mapokezi makubwa,” alisema Mbowe.
Alisema CHADEMA ikiingia Ikulu itahakikisha inamwondoa ndani ya siku tatu Mwarabu wa Kampuni ya Uwindaji ya OBC, iliyomilikishwa eneo kubwa la ardhi iliyokuwa ikitegemewa na wakazi wengi wa Loliondo kwa shughuli za kilimo na malisho ya mifugo yao.
Mbowe alisema inashangaza na kusikitisha kuwa tangu mwaka 1979, wilaya hiyo bado haina umeme wala maji ya bomba licha ya kuwa ni chanzo kikubwa cha mapato ya serikali.
“Kwa kupewa eneo kubwa la ardhi, kazi pekee aliyowafanyia Mwarabu ni kuwachimbia kisima kimoja cha maji. Hii ina akili kweli? Yaani wameuza ardhi yenu kwa kuchimbiwa kisima cha maji…hivi kweli serikali haina uwezo wa kuchimba kisima? Hadi leo hamna umeme, hamna maji ya bomba.
“CCM inajali swala, tembo, simba, chui kuliko Wamasai. Inawatimua ninyi na kumweka Mwarabu ili awaletee pesa…inajali pesa kuliko utu wa mwanadamu. Ni ajabu kuendelea kuongozwa na chama hiki. Mkisikia CHADEMA imeshinda urais, hesabuni siku tatu tu, huyu Mwarabu tutakuwa tumeshamtimua,” alisema Mbowe.
Alifafanua kuwa mbali na matumizi mabaya ya fedha za umma, maisha ya wakazi wa Ngorongoro yamekuwa magumu kwa sababu ya kodi kubwa ya ongezeko la thamani (VAT) wanayotozwa wanaponunua bidhaa na huduma mbalimbali.
Mkutano huo pia ulihudhuhuriwa na mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Mkoa wa Morogoro, Suzan Kiwanga pamoja na Mratibu wa Vijana CHADEMA Mkoa wa Arusha, Ephata Nanyaro.
Zaidi ya wakazi 400 wa Wasso na 220 wa Arashi walijiunga na CHADEMA juzi katika mikutano hiyo.

LIPUMBA AUNGURUMA

BARAZA Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi (CUF), limetoa wito kwa Watanzania kuichukulia hali ya kupanda kwa gharama za maisha kama changamoto ya kufanya mabadiliko makubwa ya uongozi nchini kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka huu vinginevyo maisha bora waliyoahidiwa yatakuwa ndoto za alinacha.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema baraza hilo limesikitishwa na ukosefu wa vipaumbele wa Rais Jakaya Kikwete na Serikali yake katika kupanga mikakati na mbinu bora za kukabiliana na hali mbaya ya uchumi na umaskini wa Watanzania kwa kutumia fedha nyingi kuwa mwenyeji na kuendesha Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) kwa Afrika badala ya kuandaa Mkutano wa Kujadili Namna ya Kuinua Uchumi wa Tanzania (Tanzania Economic Forum) kwanza.

Prof. Lipumba aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati akitoa maazimio ya kikao cha baraza hilo, akisema kuwa ikiwa wataamua kuendelea kutawaliwa na 'utawala wa kifisadi' wa Chama cha Mapinduzi (CCM), suala la maisha bora kwa kila Mtanzania litaendelea kuwa ndoto za alinacha.
Profesa Lipumba alisema kuwa kupanda kwa maisha kumesababishwa na kutowajibika kwa Serikali ya CCM na kuwepo kwa ombwe kubwa la uongozi lililopo nchini, hivyo kusababisha kupanda kwa bei za bidhaa na mahitaji ya lazima ya kila siku ya wananchi.
"Huu ni mfano halisi wa kupanda kwa bei tangu mwaka 2005 hadi mwaka huu, sembe imepanda kutoka sh. 250/= kwa kilo hadi kufikia kati ya sh 600/= na 1,000/= mwaka 2010, sukari 560/= hadi sh. 1,600/= na 2,000/= kwa kilo, mafuta ya kupikia kutoka sh. 750/= kwa lita mpaka sh. 2,000/= na 2,500/=, mbolea kutoka sh. 8,000/= kwa mfuko wa kilo 50 mpaka 30,000/= na 45,000/= kwa sasa na vivyo hivyo kwa bidhaa nyingi nyinginezo," alisema Profesa Lipumba
Aliitaka serikali kuacha kutoa ahadi hewa zisizotekelezeka mfano kuongeza ajira kwa wananchi, huku akitoa takwimu za Benki ya Dunia kuwa zinaonesha kuwa katika kila watu 100 wanaoajirika Tanzania, 89 wana ajira za mashaka na wasiwasi.
Alisema takwimu zinazotolewa na serikali ni za kupika, ambazo huonesha kuongezeka kwa ajira katika sekta zisizokuwa rasmi, ikiwa na maana ya ajira za kubahatisha na kukata tamaa, kama zile za kuokota chupa za maji za plastiki na uuzaji wa karanga barabarani, ambazo haziwezi kuwaondoa Watanzania katika lindi la umaskini.
"Kushindwa kwa serikali kuwa na mipango thabiti na madhubuti ya kiuchumi kumesababisha kuongezeka kwa hali ya umaskini wa wananchi kutoka watu milioni 11.4 mwaka 2001 hadi kufikia milioni 12.9 mwaka 2007 na kumevunja kabisa matumaini ya wananchi kujikomboa kiuchumi na kujiletea maendeleo chini ya utawala wa CCM," alisema Profesa Lipumba.
Alisema Watanzania wanatakiwa kutambua kuwa hatua za Rais Kikwete za kujishughulisha na masuala ya kimataifa na safari zake za nje za mara kwa mara hakuisaidii nchi na badala yake anazitumia kama njia ya kukwepa kushughulikia matatizo ya msingi ya ndani ya nchi.
Kwa upande wa mgogoro wa serikali na wafanyakazi Profesa Lipumba alisema, wanaunga mkono madai ya msingi yaliyotolewa na wafanyakazi kupitia Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), wanaotaka kuboreshewa mishahara yao pamoja na maslahi yao kwa ujumla.
Alisema wamesikitishwa na kauli za vitisho, aibu na kufitinisha wafanyakazi na wananchi kwa serikali kutoa habari na taarifa zisizo na ukweli kamili ili kuwapaka matope viongozi wa TUCTA.
"Mheshimiwa Rais amepewa dhamana kubwa na wananchi kuwaongoza na kuwatatulia matatizo yao pale yanapojitokeza. Kwa kitendo chake cha kukurupuka na kusikiliza upande mmoja tu wa watendaji wa serikali bila ya kuwasikiliza TUCTA na kisha kuwahukumu hadharani, Rais hakuwatendea haki Watanzania hasa ikizingatiwa dhamana kubwa waliyompa," alisema Profesa Lipumba na kuongeza kuwa
"Rais hakuwatendea haki Watanzania hasa ikizingatiwa dhamana kubwa waliyompa, Baraza Kuu linaamini ingekuwa ni vyema kama angeliwaita viongozi wa TUCTA kuwasikiliza na kushauriana nao hatua muafaka za kufuatwa katika kushughulikia suala hili kabla ya kuwahukumu hadharani."

Alisisitiza kuwa haikuwa busara kwa Rais Kikwete kutumia 'jukwaa la wazee wa CCM wa vijiweni,' ambao wengi wao si wafanyakazi, kuelezea matatizo ya wafanyakazi na kudai kuwa amejidhalilisha na kudhihirisha tena kuwepo kwa ombwe kubwa la uongozi katika serikali anayoiongoza.
Aidha, alisema baraza hilo limelaani vitisho alivyovitoa rais kwa wafanyakazi nchini na kudai kuwa vinatakiwa kulaaniwa na wapenda amani na haki ili kuinusuru nchi na machafuko.

liongeza kuwa vitisho na kashfa walizofanyiwa wafanyakazi zinatakiwa kuchukuliwa kama changamoto na wanancho wote kwa ujumla, ili kuweka nguvu zaidi za kudai haki zao, pia wasichoke, wasiogope na wasitishwe wala kurudi nyuma katika kutekeleza dhamira zao za kupigania haki nchini.



HATIMAYE RAGE KINARA UCHAGUZI MKUU SIMBA


Katika kuhakikisha kuwa club ya simba inaongozwa na watu wanaoujua mpira hasa wa kibongo bongo club hiyo imepata viongozi wapya ambapo katika upande wa mwenyekiti nafasi hiyo muhimu imetwaliwa na aliyewahi kuwa mchezaji wa timu hiyo miaka ya nyuma,katibu mkuu wa iliyokuwa FAT na huyu si mwingine bali ni ISMAIL ADEN RAGE baada ya kumgalagaza aliyekuwa mpinzani wake na katibu mkuu wa zamani wa club hiyo HASSAN HASANOL-MPIGANAJI kwa tofauti ya kura za kutosha.

(HASSANOL na RAGE wakiteta kabla ya matokeo)
katika nafasi ya makamu mwenyekiti wa club hiyo ya msimbazi imekwenda kwa mwanachama mwandamizi wa kundi maarufu la FRIENDS OF SIMBA ambalo kwa kiasi kikubwa limeshikilia mafanikio ya club hiyo kwa siku za hivi karibuni na huyu si mwengine bali GODFREY NYANGE KABURU,ambaye alitoa ahadi kem kem za kuifanya simba kuwa moja ya club bora zaidi katika ukanda huu wa afrika ya mashariki.

(Godfrey Nyange akipongezwa)
ama katika upande wa wajumbe ambao watu sita walikuwa wanatakiwa kuunda kundi la wajumbe wa kamati ya utendaji wa club hiyo,nafasi hizo zimekwenda kwa JOSEPH ITAN'GARE maarufu kama Mzee KINES huku wajumbe wengine wakiwa ni IBRAHIM MASOUD maarufu kama MAESTRO,SAIDI PAMBA,TEDDY MKWABI,DAMIANI MANEMBE NA FRANCIS WAYA.

(Maestro akimwaga sera)
Hongera wekundu wa masimbazi kwa kufanya uchaguzi usio na kelele na pia pongezi kwa viongozi wote waliopewa jukumu la kuifanya simba kuwa bora zaidi.kumbukeni ahadi mlizo zitoa kwa mashabiki na hakikisheni kuwa simba inakuwa bora kweli.

May 9, 2010

HATIMAYE YAMETIMIA ENGLAND


Ni kama ilikwisha bainika kwamba matajiri wa london club ya chelsea itautwaa uchampion wa ligi kuu ya uingereza,hiyo imejidhihirisha hii leo mara baada ya kuikamua ama kuipa kipigo cha mbwa mwizi timu ya wigan athletics kwa jumla ya magoli manane kwa bila huku ushindi wa mashetani wekundu wa magoli manne bila toka kwa stock city ukiwa hauna maana yoyote kwao na kuwaacha matajiri hao wa jiji la london kutawazwa kuwa machampion wapya wa ligi kuu ya england


BINGWA WA UINGEREZA KUPATIKANA BAADA YA MASAA MATATU TOKA SASA


(man u wakishangilia ubingwa,je hii leo itakuwa kama hivi?)
Ni kama masaa matatu yamesalia kabla ya ligi kuu ya england kufungwa rasmi hii leo kwa timu zote ishirini kushuka dimbani hii leo huku bingwa akitarajiwa kujulikana hii leo,bingwa wa uingereza anatarajiwa kuwa aidha manchester united ama chelsea ambapo matokeo ya mwisho ndiyo hasa yatakayo toa bingwa kwa kuzingatia timu hizo mbili zilizo katika nafasi ya kuutwa uchampion wa england kutofautiana kwa point moja.
             katika hali nyingine club ya arsenal maarufu kama gunnerz wako katika pressuer kubla ya kuipoteza nafasi ya tatu endapo itapoteza mechi yake ya leo dhidi ya fulham huku timu ya tottenhum ikishinda mechi yake ya leo basi itakuwa na pointi 73 moja zaidi ya arsenal endapo itapoteza.yote kwa yote tusubiri na tuone kama hayo yatatimia,globu yako ya jamii itakufahamisha baada ya matokeo ya mwisho katika michezo itakayopigwa masaa matatu toka sasa.
(chelsea wakijiandaa kuiua wigan ili watawazwe kuwa mabingwa)

May 8, 2010

YA JAKAYA NA TUCTA

Hatimaye Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliamua kuhutubia Taifa mwisho wa mwezi wa Aprili kwa kutumia mtindo tofauti na mazoea. Hapa alibadili hadhira, badala ya kuhutubia Taifa, Raisi Jakaya Kikwete aliamua kuwahutubia wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam. Wengi wao walionekana ni wanachama wa CCM kwa mavazi yao hali ambayo sidhani kama iliwakilisha taswira ya utaifa kwa mtu yeyote makini.
Raisi wa nchi anapoamua kubadili hadhira, ni wazi anazo sababu za msingi na ndio hapa binafsi nadhani ukakazi unakoanzia kwa kuzingatia yote aliyoyasema katika hotuba ile huku akishangiliwa kwa kelele na makofi lukuki. Ushangiliaji huu wa kishabiki hata katika mambo ya msingi kabisa unatia shaka dhamira ya dhati ya raisi pamoja na watu wake wa karibu kwa ustawi wa Taifa letu. Ninasema hivi kwa maono yangu kwani kuna kila sababu ya kufikiri kwa kina ambayo imenifanya niione hotuba ile kama lengo lake kuu ilikuwa ni kuwajibu TUKTA dhidi ya azma yao ya kuwahamasisha wafanyakazi kugoma.
Moja ya wasiwasi wangu kuhusu dhamira ya kiongozi wetu mkuu ni ile hali iliyojitokeza kwa yeye kutumia muda mrefu kuponda na kukebehi madai ya TUKTA kutaka kima cha chini kiwe ni shilingi laki tatu. Binafsi kwa serikali yetu ninayoifahamu ni kweli haiwezi kulipa kiwango hicho kamwe lakini naamini inaweze kulipa kiwango cha juu zaidi ingawa chini ya hapo kama kima cha chini. Raisi hawatendei haki TUKTA kwa kuwaponda ilihali wamejaribu kumuamsha kutoka lindi la udhaifu wa serikali yake katika kukusanya kodi. Naamini kama kweli nchi hii kodi itakusanywa kwa dhati ni wazi serikali yetu ina uwezo wa kulipa wafanyakazi wake kwa mujibu madai ya TUKTA.
Serikali yetu haikusanyi kodi kuendana na rasilimali na biashara zilizopo; serikali yetu inasamehe sana kodi, mtu makini arejee taarifa ya CAG iliyotolewa hivi majuzi, angalia misamaha ya kodi inavyoathiri mapato ya serikali yetu. Raisi anapotuambia kuwa mapato ya serikali ni madogo sana nashindwa kumuelewa kabisa. Angalia viongozi wa ngazi za juu wanavyoikwangua hazina ya nchi yetu kupitia wabunge, mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa na wilaya kwa malipo lukuki ya posho mbalimbali ambazo hazilipwi kodi lakini mfanyakazi wan chi hii anakatwa kodi katika kila apatacho. Hapa nadhani Raisi wa Jamhuri angekuwa anapaona na ana dhamira ya dhati ya kupagusa ili kuleta haki na usawa wa kugawana keki ya Taifa basi asingelithubutu kung’aka kama alivyokuwa katika hotuba yake.
Raisi ameonesha kung’ang’ania sana mambo madogo katika kutia nguvu hoja yake na akaacha mambo makubwa ambayo ndiyo msingi wa wafanyakazi wa nchi hii kudai haki yao. Kwa mfano, sidhani kama ni sahihi sana kwa raisi kuongelea kuwa TUKTA inadai kima cha chini cha laki tatu kwa wafanyakazi wa majumbani (house girls) au kwenye mabaa (bar maids). Hivi kwa kazi wafanyakazi hawa wazifanyazo, ina maana hawastahili kulipwa malipo stahili kuliko wanayolipwa sasa? Sioni mantiki kama mtu ni tajiri, anakwenda kijijini anamchukua mtoto wa masikini ambaye ameshindwa kupelekwa shule alafu anakuja kumfanyisha kazi kwa kipato ambacho si haki kibinadamu. Hapa raisi ameonekana kuwatetea sana matajiri; kwake wenye viwanda kwa mfano alionekana kusisitiza kiwanda cha Maji, hapa nachukulia mtu kama Mengi, eti ukimlazimisha alipe kima cha chini cha juu hatapata faida. Inatia shaka inawezekana raisi ana ubia na watengeneza maji mpaka anajua faida yao, kwani mie naamini biashara ya Maji kwa sasa ina faida kubwa sana.
Raisi ameonekana kutowajali wafanyakazi wa Tanzania kabisa kwa kuwatisha eti kama mtu hataki kazi aache kuna wengine watajiunga. Hapa imeonesha jinsi gani raisi kama mwajiri mkuu asivyojua kabisa misingi ya utawala wa wafanyakazi. Ukiwa kama meneja mkuu, Raisi hapaswi kutumia kauli kama ile kwani moja kwa moja raisi analazimisha kuwa na wafanyakazi wa umma wanaofanya kazi bila msukumo chanya, waliokatishwa tamaa, wanafanya kazi bora liende. Ni katika mfumo huo, sitegemei maendeleo ya kweli kufikiwa katika kipindi tunaongozwa na sera za vitisho na kutojali. Ina maana raisi wetu haelewi madhara ya kisaikolojia watakayoyapata wafanyakazi ambao kwa ukweli wanafanya kazi kwa vipato vidogo sana lakini wanaona serikali yao ikisema haina fedha huku ikiruhusu mabilioni ya fedha kuliwa na vijikundi vidogovidogo vya mafisadi kupitia kashfa kama “Richmond, Meremeta, IPTL, mikataba ya Rites na vijimambo vingi ambavyo kamwe watanzania wamebaki gizani huku fedha zikipotea alafu watu wanaambiwa hatuna uwezo wa kulipa mnachotaka.
Raisi alizungumza jambo zuri sana kuwa kama serikali italipa kwa mujibu wa madai ya TUKTA, basi ina maana wafanyakazi 355,000 wa serikali watakuwa wanawanyonya wananchi wapatao milioni 39. Raisi anafikiri ukilipa wafanyakazi hao aliowataja basi inaishia hapo, kiuchumi hapa kuna “domino effect”, naamini kwa idadi ya wafanyakazi wa serikali wanategemewa sana na watu wengi. Malipo yao yanakwenda mpaka kwa watoto, wajukuu na hata wazee wa wafanyakazi hawa. Hapa naona raisi alighafilika kidogo lakini hapaswi kubeza idadi ya wafanyakazi eti ni ndogo. Kama kweli ana dhamira ya kuondoa unyonyaji basi asitumie wafanyakazi wa serikali bali atumie kundi dogo tu ambalo ndilo msingi wa unyonyaji hapa nchini. Nitaeleza:
Kundi hili ambalo naamini linatumia fedha nyingi sana ambayo kama ikidhibitiwa kwa utaratibu mzuri unaojali haki sawa katika jamii ya kitanzania ni kundi la wateule wachache wa nyadhifa mbalimbali za kitaifa pamoja na wawakilishi wa wananchi. Hapa naongelea wabunge takriban mia tatu na ushehe, nina hakika hawa ni mzigo kwa Taifa letu. Wengi wao hawana chochote wanachochangia bungeni ni kupiga usingizi, ama kukaa kimya na kila siku kujichukuliwa posho ambazo nadhani hazikatwi kodi. Nina wasiwasi hata kama mbunge hajahudhuria kikao bado analipwa. Siamini katika kipindi tunaelekea katika uchaguzi ni vyema wabunge wanaomaliza muda wao wakalipwa mafedha lukuki ya Mfuko wa Jimbo (CDF) kama si matumizi mabaya? Busara ingekuwa kuwasubiri wachaguliwa wapya, je kwa nini tusiamini kuwa hii itakuwa fedha ya uchaguzi? Bado tena mbunge huyuhuyu atalipwa mafao yake ya miaka mitano, mamilioni ya shilingi ambayo yanazidi kabisa mafao ya mfanyakazi wa serikali aliyeitumikia nchi hii kwa miaka zaidi ya thelathini. Hivi Mheshimiwa Raisi anajua vipaumbele vyetu halisi ni vipi?
Orodha ya wanyonyaji ni ndefu ikijumuisha waheshimiwa mbalimbali wa ngazi za kitaifa, wizara, mikoa hadi wilayani. Mtindo ni mmoja tu, kazi kidogo mapato ni makubwa tena bila kodi. Kama kweli Raisi angelikuwa ni muungwana basi angelijadili hili tuone mtizamo wake badala ya kutuletea mambo madogo kama ya “mahouse girls na mabar maids”. Nasema hivi nikitambua kuwa kama hili tabaka la viongozi ambalo ni mzigo kwa hazina yetu “parasitic class” kama litaangaliwa na serikali basi angalau itasaidia kuwezesha serikali kuwalipa wafanyakazi wake mshahara wenye heshima na utu. Hapa lazima niseme wazi kuwa sidhani kama mshahara wa laki tatu na kumi na tano ndio ulipwe kwani hata mie nadhani kwa maisha ya Kitanzania hii inaweza chochea mfumoko wa bei kama wa Zimbabwe. Naamimi panahitajika kiasi zaidi ya kinacholipwa kwa sasa.
Hapa lazima nimkumbushe Raisi kuwa alijisahau na hili angelizungumzia basi wafanyakazi wangeliridhika. Hakuwa na haja ya vitisho kwani mwisho wake Raisi anakuwa ndio chanzo cha tabaka la wafanyakazi wa umma ambao hawana tija kwani wanafanya bila kupenda wakifanyacho. Kwa maana nyingine, Raisi kupitia hotuba yake amedhoofisha ari ya wafanyakazi wake.
Nilipokuwa ninamsikiliza mheshimiwa Raisi JK, nilijikuta nikitafuta nakala ya magazeti ya nyuma ambayo iligusa ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) ya mwaka 2009 nakwambia nilijiuliza hivi raisi anapoongea na wananchi kweli anakuwa anatafakari mapungufu ya serikali yake katika kuhakikisha fedha za serikali zinatunzwa na kutumiwa vizuri ambapo kwa kiasi fulani ingesaidia kuboresha maslahi ya wafanyakazi? Kwa mfano ripoti hiyo inaonesha kuwa kwa mwaka 2009, serikali kupitia TRA ilitoa misamaha ya kodi shilingi 752.4 bilioni. Hii ni sawa na asilimia 18% ya mapato ya serikali yalisamehewa. Hapo hapo taarifa inaonesha kuwa TRA ilishindwa kukusanya kodi kwa kutimiza lengo kwa shilingi bilioni 426.4. Hapa ni wazi uwezo wa kukusanya kodi una walakini na ukiongeza na misamaha kuna kama takriban shilingi Bilioni moja inaachwa tu kupotea. Kwa ufupi taarifa hiyo naweza nikainyumbulisha kama ifuatavyo:
i) Matumizi ya hovyo kununua magari: 4 bilioni.

ii) Upotevu wa fedha katika manunuzi (procurements):12.9 bilioni

iii) Fedha zilizotumika nje ya bajeti iliyokusudiwa: 67. 4 bilioni

Ukitazama mashirika ya umma ndio hatari pia:

i) Bodi ya mikopo Elimu ya Juu (HESLB) imegeuka kuwa chombo cha kutoa zawadi kwa watanzania. Kwa mfano, taarifa inaonesha kuwa kutoka 1994 – 2004/05, imekopesha wanafunzi 113,240 lakini haijaweza kufuatilia fedha zake kwa wengi ni wachache sana wameanza ama wamerudisha mikopo. Bodi imetumia shilingi 51.1 bilioni ambazo kinadharia zinakuwa kama zawadi kwa walengwa, hakuna ufuatiliaji.

ii) Kuna hili la wafanyakazi hewa ambapo kutokana na udhaifu katika usimamizi wa malipo, shilingi bilioni 3 zilipotea mwaka 2009.
Kwa mtizamo wa haraka, kuna kama shilingi 890.8 bilioni, karibu Trilioni moja zimepotea katika kipindi cha mwa ka wa 2009. Kwa mantiki hii, nilipomsikiliza rais akilalama kama vile serikali yake ni masikini sana, ripoti ilinijia nikajiuliza labda ingelikuwa vyema kwa raisi kuwapa picha halisi ya changamoto zinazoikabili serikali yake na angeliwaomba wafanyakazi wajitoe mhanga ili kuepusha upotevu wa mapato ili serikali iboreshe makusanyo ndipo TUKTA ifikirie suala la kuomba maslahi. Badala ya kuwalaumu akina Mgaya, angeliwaomba wamsaidie kuwafunda wafanyakazi juu ya kujali kazi zao kwani upotevu mkubwa wa mafedha hayo au kutofikiwa kwa lengo la makusanyo ni matokeo ya wafanyakazi kuzembea majukumu yao. Ndio maana naamini kabisa raisi Kikwete pamoja na hotuba yake ndefu bado hakuwa na mantiki kabisa siku ile. Ile si hotuba ya Kitaifa, kama ni kwa wazee tu basi ilikuwa muafaka lakini kwa wafanyakazi ambao wengi wao wana akili na wanaona mapungufu kibao serikalini, rais hakututendea haki wafanyakazi.
Pamoja na mapungufu yote ya hotuba ile ya Raisi, lakini lazima nikiri kuwa, ni wajibu wa kiongozi wa serikali kama raisi kuhakikisha nchi haikumbani na migomo. Serikali haina budi kuwazoesha watu wake na masuala ya migomo kama njia ya kutatua matatizo yao. Katika kutimiza hili, raisi amefanikiwa kwani naamini kabisa hakuna mtu atakayegoma kama TUKTA wataendelea kuitisha mgomo mwingine baada ya kusitisha huu wa sasa. Hakuna mtanzania ambaye yuko tayari kufukuzwa kazi au kuandamana akumbane na rungu la dola. Kufanikiwa huko kuepusha mgomo ni ushindi kwa raisi lakini tija na weledi miongoni mwa wafanyakazi vitabakia vikishuka badala ya kuboreka.
Mwisho nimalizie kwa kusema tu kuwa Raisi alipoamua kuzungumza na wazee labda kwa kuwa wote wale enzi zao zimepita labda aliamua aongee katika lugha watakayoilewa ndio maana akaamua kujadili hoja kwa kutumia dhana nyepesi ambazo kimsingi hazikuwa madai makuu ya TUKTA. Naamini kama niliwasikiliza vizuri viongozi wa TUKTA, yapo mambo matatu ya msingi ambayo sikuona Raisi akiyagusa. Mambo hayo ni: Kodi kubwa kwa Makato ya Mishahara, Mishahara midogo sana, Mazingira bora ya Kazi. Hebu fikiria, kuna wafanyakazi lukuki wa serikali wanalazimika kufanya kazi zaidi ya muda wa saa za kazi lakini hawalipwi stahili zao kwa mujibu wa utaratibu.
Na ndipo hapa pamenifanya nijiulize: “Hivi kweli, Raisi wetu anajua athari za kisaikolojia za kauli zake hasi dhidi ya wafanyakazi na viongozi wake katika kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye mafanikio kutoka kwa wafanyakazi wake? Naachia hapa lakini niseme tu hii ni “ Food for Thought”.

MKUTANO WA UCHUMI ULIVYOFUNGWA BONGO

Mkutano wa uchumi Duniani kuhusu Bara la Afrika umemalizika rasmi hii leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambapo washiriki wengi wametoa rai ya kuamka kifikra na kuanza utekelezaji wa mawazo yao kivitendo.

Raisi wa Tanzania Jakaya Kikwete aliyehitimisha Mkutano huo amesema Bara la Afrika limekuwa likizalisha vitu lisivyovitumia na kutumia vile vinavyozalishwa kutoka nje, na kuita juhudi zaidi kufanyika ili kuondoa hali hiyo ili Bara hili liweze kujitegemea.
Awali wachangiaji wengi walio viongozi wa nchi za Bara hili, walitoa rai ya kuinua kilimo cha Bara la afrika ambacho ndicho kazi kuu ya Waafrika na kwamba wengi ni wakulima wadogowadogo.
Ili kulikomboa Bara la Afrika ni lazima kukikomboa kilimo wamesema washiriki, na hivyo juhudu, ujuzi na maarifa yatumike zaidi katika kubuni njia muafaka za kuimarisha kilimo hiki ili kuleta tija kwa wahusika.
Mkutano huu ulioanza katikati ya wiki Jumatano iliyopita, umekamilisha siku tatu za majadiliano na kubadilishana uzoefu ikiwa sambamba kuahidi kuweka mikakati thabiti ya kutekeleza uzoefu walioupata kutoka kwa wadau mbalimbali.



UCHAGUZI MKUU WA SIMBA KAMA KAWA

Pamoja na kujitahidi kuuzuia uchaguzi mkuu wa club ya simba bado mahakama kuu imeweza kutengua maamuzi ya mahakama ya kisutu na kutoa maamuzi ya kuutaka uongozi wa simba kupitia kamati yake ya uchaguzi kuendelea na harakati zake za uchaguzi utakao fanyika siku ya jumapili kama kwawaida.
(baadhi ya viongozi wa simba katika picha)
              Nikiwa kama mdau wa mpira wa miguu nchini nampongeza jaji aliyetoa maagizo hayo na naamini kuwa jaji huyo ni mwanamichezo kwa kuutaka uongozi wa simba kuendelea na uchaguzi basi wale wenye vitabia vya kukimbilia mahakamani wataula wa chuya.

Blogger Buzz: Blogger integrates with Amazon Associates

Blogger Buzz: Blogger integrates with Amazon Associates

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA