
Blog ya Muhidini Issa Michuzi ipo mbioni kuhama.Hivi punde itakuwa tovuti kamili inayojitegemea na hivyo kuondoka katika ulingo wa .blogspot.com.Ufuatao ni ujumbe kutoka kwake Issa Michuzi.
Asalaam Aleikhum, Bwana Asifiwe, Tumsifu Bwana, Shalom, Namaste, konnichiwa, Nihao, olá…..
Kwa heshima na taadhima nawaamkia wadau wote popote mlipo ulimwenguni. Salamu nilizotoa hapo juu naomba ifahamike kuwa hizo nilizozimudu ni kama kielelezo kwamba nia ni kumuamkua kila mmoja kwa nafasi yake popote alipo. Mie sijambo na naendelea na Libeneke kama kawaida.
Waama, baada ya salamu, napenda kuwafahamisha kwamba Globu ya Jamii hivi karibuni itaingia kwenye awamu mpya ya dot com, ikiwa katika jitihada za kuboresha Libeneke zaidi.
Imechukua muda kuchukua hatua hii kutokana na mazoea kwani toka September 8, 2005 hadi leo si kidogo ati. Hivyo mabadiliko kama yapo inabidi yafanywe kwa uangalifu wa hali ya juu ili kutoleta usumbufu wa aina yoyote kwa wadau wa Globu ya Jamii ambao kwangu ndiyo waajiri wangu wakuu.
Naam, wakati wowote kuanzia sasa libeneke la issamichuzi.blogspot.com litaingia katika awamu ya www.imichuzi.com. unakaribishwa kujaribu na kutoa maoni yako.
No comments:
Post a Comment