Dec 31, 2011

HALI HALISI YA MACHINGA COMPLEX

nilitegemea kukuta maneno kama haya''KARIBU BUSINESS PARK aka MACHINGA COMPLEX''Lakini matokeo yake nakutana na matangazo ya biashara na wafanyabiashara wenyewe wameridhika na hili ashee inakera sana.
kweli katika hili mamlaka husika siwezi kuzisamehe hakikika
sijaona nchi ya kijinga yenye viongozi wasiofikiri kwa makini kama tanzania kuanzia viongozi mpaka wasanii wao hakika inakera sana

Pipo zimeingia chaka pamoja na kuchukua vizimba katika jengo la machinga complex na kuacha vumbi zienee kila kona ya jengo
sio kwamba watu hawapendi kuwapo hapa ila hawajawezeshwa kuwapo hapa kwa maana ya miundombinu ya kumfanya mtanzania wa kawaida kufika hapa kama stendi ya daladala kukiwa na magari ya mbagala 2 kituo kimejaa unategemea nini?
sioni umuhimu wa hili jengo kwa kweli.
ni vumbi kila kona hasa floor ya tatu na ya pili asee

utasema banda la kufugia kuku ashee

jongo zima huezi amini hata wafanyabiashara 50 waliokatika shughuli za kila siku za kibiashara hawawezi fika huu ni mfano dhahili kuwa bora pesa zilizojenga jengo hili tungefanyia kitu kingine tofauti.
mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
vijana wa mlimani tv wakiwa kwa kazi ili kusanua nini kinachoendelea kwenye jengo la machinga complex na hata meneja wa soko hilo bi THERESIA amekiri kuwa MLIMANI TV imewapa support sana katika kulitangaza soko lao
kwa siku huezi amini nikikuambia kuwa wanaoweza kupanda kwenye jengo hilo hawawezi kuvuka watu 30 hasa kwa kuzingatia kuwa bidhaa nyingi zinazopatikana kwenye jengo hilo hata pale mchikichini na karume hata mwenge zapatikana kwa wingi sana
hakuna cha muhimu katika vibanda vya kufugia kuku vilivyopo katika jengo hili maana hakuna cha muhimu kwa weli
sasa unashangaa nini huu ndo uhalisia wa soko la MACHINGA COMPLEX.

Dec 23, 2011

TAMKO LA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO JUU YA MAFULIKO

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SALAAM ZA RAMBIRAMBI NA POLE KWA WANAFAMILIA NA WANANCHI KUHUSIANA NA JANGA LA MAFURIKO YALIYOKUMBA JIJI LA DAR ES SALAAM, MBEYA NA DODOMA .

Usiku wa kuamkia tarehe 20.12.2011 Maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, Mbeya na Dodoma yamekumbwa na maafa makubwa ya mafuriko ambayo yamesababishwa na mvua kubwa ambazo zimeendelea kunyesha mfululizo katika maeneo hayo.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kutoa pole za dhati kwa wanafamilia na wananchi wote ambao wamekumbwa na janga hili kubwa , kwani limesababisha maafa makubwa sana ya vifo, kupoteza mali na miundombinu mbalimbali kuharibiwa vibaya kwenye maeneo husika. Tunapenda kuwahakikishia wananchi hawa kuwa tutakuwa nao pamoja katika kipindi hiki kigumu katika maisha yao kutokana na madhara waliyopata yaliyosababishwa na maafa haya.

Kutokana na janga hili limetukumbusha jambo moja kuwa kama Taifa hatujajiandaa kikamilifu kuweza kukabiliana na majanga kama haya pindi yanapotokea na hata vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimeonyesha dhahiri kuwa havijaandaliwa kimfumo na kinyenzo katika kuweza kukabiliana na majanga kama haya na huu ni udhaifu mkubwa sana kwa taifa lenye miaka 50 baada ya uhuru wake .

Mathalani mpaka sasa hatujaona jitihada zozote ambazo zimechukuliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa katika kuonyesha juhudi za kukabiliana na janga hili kubwa kwa taifa letu,hii inaonyesha wazi kuwa kitengo hiki hakijaandaliwa kuweza kukabiliana na maafa kama ambavyo majukumu yake yanavyopaswa kuwa . Na hii ni hatari kwani kama chombo cha kukabiliana na maafa hakiwezi kufanya hivyo kwa wakati ni kuendelea kuwaacha wananchi waendelee kupata madhara makubwa zaidi. Na haswa ikizingatiwa kuwa idara ya hali ya hewa ilishatahadharisha kuhusiana na mvua hizi.

CHADEMA tunapenda kuikumbusha serikali kuhusiana na ilani yetu ya uchaguzi ya mwaka 2010 ambayo ilieleza wazi kuhusiana na kukosekana kwa mifumo thabiti ya kujulisha umma kuhusiana na majanga mbalimbali katika miji yetu (Early Warning Systems) kama ambavyo ipo katika nchi nyingi , mfumo huu ni muhimu sana katika kuweza kuufanya umma uwe na elimu ya jinsi ya kuweza kujikinga na majanga haya kwa lengo la kupunguza madhara yasiwe makubwa kama ambavyo taifa hivi sasa linashuhudia.

CHADEMA inapendekeza hatua zifuatazo ziweze kuchukuliwa haraka na serikali ili kuweza kukabiliana na majanga/maafa mbalimbali hapa nchini yanapojitokeza;

I) Kuandaa mfumo wa awali wa kutahadharisha umma juu ya ujio wa majanga (Early Warning Systems) kwa kutumia vyombo na nyenzo mbalimbali ili kuepusha madhara makubwa kwa watu na mali zao.

II) Kutunga sheria mpya ya ujenzi na kuweka viwango vya ujenzi viwe vyenye hadhi ya kimataifa na haswa ujenzi wa kuta mbalimbali na majengo marefu na kuhakikisha kuwa ujenzi holela haujitokezi kwenye miji na majiji yetu hapa nchini.

III) Kuhakikisha kuwa kwenye miji yote mikubwa mtandao wa mabomba ya maji ya dharura unawekwa ili kuweza kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea.

IV) Serikali ijiandae mara moja kukabiliana na magonjwa ya milipuko kama vile kuhara ,kipindupindu na mengineyo ambayo yatajitokeza kutokana na mafuriko haya kuharibu miundombinu ya kusambaza maji, makazi ya watu n.k.

V) Kitengo cha maafa kiwe na vifaa wakati wote , na haswa vifaa kwa ajili ya uokoaji na wawe na utaratibu wa kutoa elimu kwa umma jinsi ya kuweza kutumia vifaa hivyo kuweza kujiokoa na sio kuacha hali iwe kama ambavyo imejionyesha Dar Es Salaam jana baada ya baadhi ya majaketi okozi kufikishwa kwa wahanga na kushindwa kuyatumia kikamilifu.

VI) Serikali itoe elimu ya jinsi ya kujikinga na magonjwa ya milipuko kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko haya ili kuepusha wananchi wengi kukumbwa na magonjwa hayo pindi yakijitokeza.

Mwisho tunapenda kuendelea kutoa pole kwa wanafamilia wote na wananchi kwa ujumla kutokana na madhara makubwa waliyoyapata , Mungu awajaze nguvu katika kipindi hiki kigumu.
Tamko hili limetolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu CHADEMA .

……………….

DR. Willbroad P. Slaa.

Katibu Mkuu –CHADEMA.


22/12/2011.

Dec 21, 2011

CHANGIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO DAR!!!!


Naomba nichukue fursa hii kuwapa pole wote kwa namna moja au nyingine kutokana na maafa yaliyosababishwa na mvua hizi zinazoendelea katika jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi yetu.

Ni dhahiri kuwa waliothirika ni wengi na hivyo basi watakuwa na mahitaji muhimu ya dharura . Hivyo basi ni wakati wa kusaidiana na kufarijiana , pale unapoweza basi msaidie mwenzako aliyeathirika.

Naomba nichukue fursa hii kuwaomba wote wenye nia ya kuchangia waliothirika na maafa haya basi wawasiliane na TPN Staff Miss. Anna Machanga machangaanna@yahoo.com, 0652 945422 ; na Mr. ASED KIPEPE: sdkipepe@gmail.com, 0716 898685 . Michango inayopokelewa ni fedha taslimu au hundi, vifaa vya nyumbani, vyakula, vinywaji, nguo mpya na zilizotumika n.k.

Kama unataka kuchangia kwa M-Pesa , Tigo Pesa, Airtel Money etc wasiliana na Mr. Gervas Lufingo +255 (0784/0767/0658) 48 25 97 : nasemaasante@yahoo.com

Wafanyakazi hao wa TPN watakufuata ulipo na kupokea mchango wako na kukabidhi risiti.

Michango yote itakayopatikana itawekwa hadhani na itawasilishwa kwa Mkuu wa Mkoa wa DSM, Mhe. Mecky Sadik kwa ajili ya kufikishwa kwa waathirika.

Kutoa ni Moyo na wala si utajiri.

Nachukua fursa hii kuwatakia wote siku kuu njema ya Krismas kwa wale wanaosherehekea, mapumziko mema ya mwisho wa mwaka na pia nawatakia wote mwaka mpya mwema na wenye mafanikio tele.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania, Mungu awabariki wote.

Phares Magesa

Rais- TPN

www.tpntz.org

WAKAZI PERFORMANCE AT REPRESENT AFRICA SHOW. (WITH YAYLOW, LOLA SAVAGE & SLV)

This is a little piece of the performances at the Represent Africashow in Chicago at The Shrine. All the other artists were from Nigeria and wakazi was the only one representing East Africa. be on the lookout for the performance video from the Halloween Show in Ohio where Wakazi shared the Stage with Vinnie Chwani, Fey, NTO and E-Breezy. The release of Wakazi's Third Mixtape is due at the end of the year as we bout to enter 2012.

MAFURIKO YAONGEZA VIFO, MAJERUHI, MADARAJA,NYUMBA ZABOMOKA, BARABARA KUU ZAFUNGWA



kwa msaada wa mwananchi newspaper

WATU 11 wakiwamo watatu wa familia moja, wameripotiwa kufariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mvua zilizoendelea kunyesha jana katika Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake na kuvuruga mfumo wa usafiri na shughuli za kiuchumi.Miondombinu mbalimbali ya Jiji hilo ikiwamo madaraja na nyumba vilivunjwa na kusababisha adha kubwa kwa wakazi ambao wengi wao, walishindwa hata kwenda kazini.

Baadhi ya barabara zikiwamo Morogoro eneo la Jangwani na Ali Hassan Mwinyi eneo la daraja la Salenda zilifungwa kwa muda kutokana na kujaa maji kiasi cha kuhatarisha maisha ya watumiaji wake.


Mvua hiyo ya siku mbili mfululizo kunyesha jijini Dar es Salaam, jana ilifanya maeneo mengi zikiwamo barabara muhimu kama Nyerere kuanzia Uwanja wa Ndege, Kawawa eneo la Kigogo Darajani na Mandela eneo la Tabata Matumbi, kushindwa kupitika kwa saa kadhaa kutokana na kujaa maji.

Katika barabara ya Mandela hali ilikuwa tete baada ya maelfu ya abiria waliokuwa wanasafiri kutoka Buguruni kwenda Ubungo, kukwama katika daraja la Matumbi.

Kwa zaidi ya saa nne tangu saa 1:00 asubuhi abiria walioonekana wakishuka kutoka kwenye magari na kutembea kwa miguu mithili ya maandamano, huku makumi ya magari yakiwa yamezimika barabarani.

Wakati hayo yakitokea, watumiaji wa barabara ya Mandela walikwama kutokana na msururu mrefu wa magari kufuatia baadhi yake kuzima na kufunga barabarani.

Katika barabara hiyo eneo la TIOT, ulionekana moshi mkubwa angani uliotokana na moshi wa gesi baada ya bomba linalopitisha gesi hiyo kupasuka. Moshi huo uliwafanya watu waliokuwa kwenye magari kupatwa na vikohozi.

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetaja mvua zilizonyesha jana na juzi kuwa hazijawahi kutokea katika miaka ya karibuni, na kwamba mara ya mwisho mvua kubwa kama hiyo ilirekodiwa mwaka 1954.

Madaraja yasombwa
Baadhi ya madaraja yalisombwa au kuvunjwa na maji hivyo kusababisha shida ya usafiri katika jiji hilo.

Daraja la Mbezi katika barabara ya Morogoro lililoko jirani na kibanda cha mkaa eneo la Tanesco lilivunika na kusababisha kukatika mawasiliano ya safari za kutoka na kwenda katikati ya jiji.

Mawasiliano katika daraja hilo yalikatika saa 11:00 alfajiri, na kusababisha misururu ya magari yaliyokuwa yakisubiri maji yapungue ili yapite.

"Hii leo sio kawaida, heri ya jana, sisi tumekwama tangu saa 10:30 alfajiri na mpaka sasa 1:45 asubuhi hatujui tutaondoka saa ngapi," alisema mmoja wa abiria waliokwama eneo hilo, ambaye alipiga simu ofisi za gazeti hili bila kutaja jina lake.

Vitus Andrew aliyejitambulisha kuwa ni dereva wa gari aina ya Mitsubishi fuso, alisema alifika eneo hilo saa 11.20 alfajiri na kukuta msururu wa magari ukiwa hautembei hivyo kumalazimu kuzima gari na kulala.

“Ndugu yangu, nimefika hapa mapema nikiwa naelekea Tabora, lakini naona safari yangu imeishia hapa kwa leo na kibaya zaidi hakuna kiongozi ama askari yeyote aliyefika kusimamia usalama wa abiria na magari kwani hali ya usalama si nzuri,” alisema Andrew.

Taarifa zilizopatikana baadaye, zilisema magari yalianza kupita kwenye daraja hilo saa 2:20 asubuhi.

Daraja la Mbezi Bondeni linalounganisha Mbezi Beach na Mwenge, wilayani Kinondoni limekatika upande mmoja kutokana na mafuriko hivyo kufanya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi cha Lugalo kuweka kambi maalumu kwa ajili ya kulinda usalama.

Hatua hiyo imesababisha wananchi wanaotoka Mbezi kuelekea Mwenge, kushindwa kutumia magari na kulazimika kuvuka kwa miguu kutokana na magari yote kuzuiwa kupita eneo hilo.

Daraja lililopo Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lilijaa maji hivyo kulazimisha uongozi wa jeshi kuzuia magari yasipite kwa muda.

Maeneo mengine ya Jiji
Usalama wa maisha na mali kwa wananchi katika Bonde la Mto Msimbazi umekuwa hatarini kutokana na mvua hizo.

Mamia ya watu waliyakimbia makazi yao huku wengine wakiwa juu ya mapaa ya nyumba wakisubiri kuokolewa kutokana na nyumba zao kuzingirwa na maji.
Wengine walionekana juu ya minazi wakisubiri msaada kutoka kwa wasamaria wema huku helikopta ya polisi ikipita bila kuweza kutoa msaada wowote.
Mvua hizo zilisababisha balaa kwa wakazi wa eneo la Ubungo External, ambako maji ya Mto Ubungo yalisambaa kwenye makazi ya watu na kusomba mali zao.

Mwanamke ambaye ni mkazi wa eneo hilo ambaye jina lake halikufahamika mara moja, alisikika akisema tangu kuishi kwake Dar es Salaam miaka 34 iliyopita, hakuwahi kuona mafuriko ya aina hiyo.

Eneo la Mikocheni nako hali haikuwa shwari baada ya nyumba nyingi za wakazi wa eneo hilo kuzolewa na maji yaliyokuwa yanatokea katika bonde la mpunga, lenye mkondo wa maji ya bahari.

Hata hivyo, baadhi ya wakazi walitaja sababu za eneo hilo kujaa maji kuwa ni ujenzi holela wa makazi ya watu hasa maeneo ya My Fair Plaza.

Amos John mkazi wa eneo hilo alisema umefika wakati Serikali ikachukua hatua za makusudi kuhakikisha mkondo huo wa maji unaachwa huru ili kunusuru maisha ya wakazi wa eneo hilo.

Katika eneo la Tandale kwa Tumbo, Mwananchi lilishuhudia watu wakiwa katika hali mbaya huku wakiomba msaada baada ya kuzidiwa na maji.

Hali hiyo ilisababisha baadhi ya nyumba kusombwa na maji, huku baadhi ya wamiliki wake wakionekana katika makundi wakiomba msaada.

Wakizungumza katika eneo hilo jana, walisema hali imezidi kuwa mbaya tofauti na juzi na kwamba sasa ndio wamepoteza mwelekeo wa maisha kabisa kwa kupoteza mali zao na vitu muhimu ambavyo wanavitegemea kwa ajili ya kuendesha maisha yao.

“Sio jambo jepesi kurudi katika hali ambayo nilikuwa nayo kwa sababu nimepoteza mali zangu zote hasa ukizingatia nilikuwa nafanya biashara. Vitu vilivyokuwa dukani kwangu vimechukuliwa na maji na sasa sijui wapi nitakimbilia kupata msaada,” alisema Salum.

Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Kwa Tumbo, Zinduna Kimbonaga, alisema: “Hali siyo nzuri, kipindi hiki kunahitajika hatua za dharura ili kuwakomboa wakazi wa eneo hili”.

“Watu hawana makazi wala vyakula. Hali ni mbaya, Serikali inatakiwa kufanya jitihada za kutoa misaada ya chakula na malazi ili kuepusha magonjwa ya milipuko,” alisema

Kimbonaga ambaye pia alibainisha kuwa juzi, Mbunge wa Kinondoni Idd Azan, aliwapa misaada ambayo inahitajika kuongezwa.

Mbagala, Tabata Kimanga
Wakazi wa kata ya Kijichi, jana walilazimika kutembea kwa miguu hadi maeneo ya Mtongani na Misheni kutokana na kukatika ghafla kwa mawasaliano ya usafiri katika daraja la Kijichi.

Daraja hilo lilifurika maji na hivyo kufanya magari madogo zikiwamo Hiace kushindwa kupita eneo hilo na yale yaliyofanikiwa kupita yaliongeza nauli hadi Sh500 badala ya kati ya Sh300 na Sh400.

Daraja lililopo kati ya eneo la madukani na chama, lilifurika maji hivyo kufanya watu wanaoishi Tabata Kimanga kushindwa kwenda makazini.

Daraja hilo lilianza kufurika maji saa 12:00 asubuhi na kupungua saa 3:00 asubuhi ambapo magari yenye uwezo mkubwa kama Toyota Land Cruiser na Defender yalianza kupita.

Magari mengi ya abiria yalishindwa kuendelea na safari kutokana foleni pamoja na barabara nyingi kujaa maji.

Pia nyumba zilizopo katika bonde hilo zilifurika maji huku nyingine zikibomoka kabisa hali iliyofanya watu walioshindwa kuwahi kuyakimbia maji hayo, kupanda juu ya dari na kubaki kuchungilia nje jinsi mali zao zinavyosombwa na maji.

Hali hiyo pia ilijitokeza eneo la Tabata Msimbazi, ambako taharuki ilijitokeza baada ya maji ya mto Msimbazi kujaa kwenye nyumba za watu.

Maji hayo yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha kuanzia saa 10 alfajiri ya kuamkia jana na yalisababisha wakazi wa eneo la Msimbazi Nyaluhela na Kwa Swai, hususan wanawake na watoto kutimua mbio kwenda maeneo ya Mwinuko kwa ajili ya hifadhi.

Cosmas Ndijo kutoka eneo Tabata Bima kwenye mwinuko alisema aliona mto huo ukisomba mizoga ya ng’ombe, mbuzi, kondoo, meza, viti na magodoro.

Naye Baraka Bansy alisema Mto Msimbazi ulijaa maji mengi na kusomba miti mingi kutoka mbali na kwamba, nyumba nyingi eneo la Msimbazi zilikuwa zimezingirwa na maji.
“Maji yamefika msikiti wa Msimbazi, wanawake na watoto wanazidi kutimua mbio kuokoa maisha yao,” alisema Baraka.

Kadhalika mvua hiyo ya jana ilisababisha barabara ya Umoja kuanzia Bima kwenda kwa Msimbazi kujaa maji na kusababisha watu kuvua viatu kupita eneo hilo.

Usafiri wa daladala na teksi kutoka Tabata kwenda Buguruni ama Ubungo, ulisimama asubuhi ya jana kutokana na maji ya mto Msimbazi kupita juu ya daraja.

Matumbi huku eneo la Tabata Relini nalo likijaa maji ambayo yalisababisha kupasuka kwa bomba la gesi.

Mabomba ya gesi yalipasuka kwenye eneo la viwanda vilivyopo Kituo cha TOT barabara ya Mandela na kusababisha moshi uliojaa harufu mbaya ambayo ilisababisha watu wengi kufadhaika.

Vifo Kinondoni
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema maji yalikuwa yamejaa pia kwenye ofisi za Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Taifa (UNDP).

Kamanda Kenyela alifafanua kwamba juhudi za uokoaji zilikuwa zikiendelea kwa watu waliokuwa ndani ya ofisi hizo.

Habari kutoka katika Hospitali ya Mwananyamala zinasema, kulipokelewa maiti saba na majeruhi watano katika hosipitali hiyo.

Muuguzi wa zamu wa hospitali hiyo Marry Shayo aliliambia gazeti hili kuwa kati ya maiti hao watatu ni wa familia moja. aliwataja kuwa ni Tatu, Sharifa na Amran wote wa ukoo wa Abeid. Maiti wengine ni wanne hawajatambuliwa.

Shayo alitaja majeruhi kuwa ni Husna Rashid mkazi wa Kigogo, Amina Rashid, Yonas Maganga, Sharifa Said na Ally Mdowa.

Kwa upande wake, diwani wa Kata ya Tabata, Mtumwa Mohamed alisema ameshuhudia miili ya watu sita ikielea katika maji yaliyokuwa yanapita kwa kasi katika Mto Msimbazi eneo la Matumbi, Tabata jijini Dar es Salaam, jana.

"Wale ni marehemu, hiyo haina ubishi kwani hakuna hata mmoja ambaye alikuwa anajaribu kujitetea" alisema na kuongeza kuwa watu hao ni tofauti na wengine zaidi ya sita waliokuwa wamepanda juu ya mti aina ya mwarobaini ambao nao ulisombwa na maji na kudondoka nao," alisema na kuongeza:,

"Hali si nzuri nafikiri watu wengi zaidi watakuwa wamepoteza maisha. Pia kuna taarifa za mtu mwingine kuchukuliwa na maji baada ya kurudi nyumbani kwake kwenda kuwaokoa watoto wake."

Alisema mwanaume ambaye ni maarufu kwa jina la Bonge wa eneo la Matumbi, alitoka nje kwa madai kwamba anawafuata watoto wake na hakuweza hata kupiga hatua tatu akasombwa na maji.

"Nilifika pale muda mfupi baada ya tukio na kuelezwa kuwa kuna mtu kasombwa, alikuwa anairudia familia yake," alisema na kuongeza kuwa hali ni mbaya katika kata yake na watu wengi zaidi huenda wamepotza maisha.

Baadhi ya watu wamedai kuwa kundi la watu wanane ambao walishika mikono kuvuka katika eneo la Matumbi ambalo lilijaa maji, lilisombwa na maji wakati wakijaribu kuvuka hali ambayo iliwafanya vijana wa eneo hilo kuzuia mtu yeyote asijaribu kuvuka.

Katika eneo la Kigogo, watoto watano wa familia moja waliripotiwa kupotea na tayari baba yao Issa Rajabu Mkazi wa Kigogo, aliliambia gazeti hili kuwa watoto hao na mama yao, walipotea muda mfupi baada ya maji kujaa kwenye nyumba yao.
“Mpaka sasa hivi nimewapata watoto wawili, bado watatu sijui walipo,” alisema Rajabu.
Rugimbana
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na Kaimu Mkuu wa Wilaya za Ilala na Temeke, Jordan Rugimbana alisema watu wanne walifariki dunia katika tukio hilo katika wilaya ya Kinondoni.

Alisema kutokana na janga hilo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick ameagiza kuundwa vikosi kazi maalumu kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa msaada kwa wananchi walioathirika hasa katika Bonde la Msimbazi ambalo lilionekana kuathirika sana.

Alisema vikosi kazi hivyo vitafanya kazi kutambua maeneo yaliyoathirika kwa kiasi kikubwa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na Msalaba Mwekundu, kutenga maeneo maalumu ya kupokelea wananchi.

Alitaja maeneo hayo kuwa ni Shule ya Sekondari Kibasila katika Wilaya ya Temeke, Shule ya Msingi Kilimani Rutihinda (Kinondoni) na Msimbazi katika Manispaa ya Ilala.

Hosipitalini Muhimbili
Ofisa Uhusiano Msaidizi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Jeza Waziri alisema wamepokea majeruhi wawili na maiti moja.

Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Deo Joseph (24) kutoka Tandale na Ibrahim Batazani (30) anayetokea Ilala na kwamba walifikishwa hospitalini hapo saa 9.30 mchana.

“Tumepokea majeruhi wawili na wametambulika na maiti moja ya mwanamke ambayo hadi hivi sasa haijatambulika, hawa majeruhi wanafanyiwa uchunguzi haijajulikana kama watalazwa au wataruhusiwa,”alisema Waziri

Mbowe asitisha ziara
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amelazimika kukatisha ziara jimboni kwake Hai kutokana na maafa yaliyowapata wananchi wa Dares Salaam.

Mbowe alifafanua kwamba amelazimika kusitisha shughuli hizo jimboni na nyingine kitaifa katika kipindi hiki kigumu, ambacho taifa kimeingia.

Mwenyekiti huyo ambaye pia ni kiongozi wa Upinzani Bungeni, aliwapa pole wote walioguswa na maafa hayo kwa namna moja au nyingine, ikiwa ni pamoja na kupoteza mali na ndugu.

Zitto Kabwe atoa change moto
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amewapa pole watu wote wa Dar es Salaam kutokana na madhara ya mvua.

“Ninawapa pole watu wote wa Dar es Salaam, pia tujitokeze kwa wingi kusaidia Watanzania wenzetu waweze kurejea katika maisha ya kawaida. Pia kwa upande wa Serikali hii ni changamoto ya kuboresha mipango miji ya Jiji la Dar es Salaam,” alisema

Zitto alisema kwamba viongozi waache kukaa ofisini katika kipindi hiki na badala yake watembee makazi ya watu ambao wamepata maafa haya. “Nimepita maeneo mbalimbali, hali ya maisha ya hawa Watanzania wenzetu inatisha. Tushirikiane na tuwe wamoja kipindi hiki kigumu,” alisema

Habari hii imeandaliwa na Fredy Azzah, Hadija Zuberi, Ibrahim Yamola, Boniface Meena, Aidan Mhando, Lauden Mwambona, Joseph Zablon, Keneth Goliama na Pamela Chilongola


THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA