Aug 31, 2010

INTERVIEW MAN X,O TEN NA JANEROSE STUDIO ZA MLIMANI RADIO LEO

KUTOKA JUKWAA LA SANAA,BASATA-FILAMU NA MAADILI YETU

Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Marerego (Kushoto) akisisitiza jambo wakati akichangia mada kwenye Jukwaa la Sanaa kuhusu Filamu na Maadili ya Mtanzania. Kulia ni Mwasilishaji wa Mada Richard Kallling, Rais wa Chama cha Wamiliki wa Video Library.

Mwongozaji chipukizi wa Filamu nchini, Christian Kauzeni ambaye pia ni msanii kutoka Kundi la Kidedea akitoa mchango wake kwenye Jukwaa.

Mtaalamu na Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anayefanya masters yake kwenye masuala ya sanaa, Issa Mbura akifafanua juu ya utafiti wake alioufanya kuhusu filamu za kibongo.

Mwalimu Rashidi Masimbi akichangia kwa hisia kali juu ya Maadili katika Filamu zetu.Kulia kwake Ni Mkongwe wa Muziki wa Dansi, Kassim Mapili.

Sehemu ya umati wa wadau wa sanaa waliohudhuria kwenye Jukwaa la Sanaa Jumatatu hii.

FILAMU ZA KIBONGO MAADILI YAKE NI KIFO KWETU?
Wadau,kama kawaida leo hapa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwenye Jukwaa la Sanaa kulikuwa na Mjadala Mkali kuhusu Filamu za Kibongo na maadili yake kwa jamii za kitanzania.

Mjadala huo uliohudhuliwa na zaidi watu 100 na kuchokozwa na Rais wa Chama Cha Wamiliki wa Video Library,Richard Kallinga, ulijikita kwenye haja ya waandaaji wa filamu za kibongo kutengeneza filamu zenye ubora, zenye kubeba maadili ya mtanzania, zilizo na uhalisia wa maisha yetu ya kila siku,zisizokuwa za kuiga kutona Nollywood (Nigeria), zenye ujumbe unaoeleweka na kwa ujumla zenye mvuto.

Katika mjadala wake, wadau wengi walisema kwamba, Industry ya Filamu hapa Bongo imeajiri vijana wengi na inafanya vizuri ila hawakusita kutaja matatizo sugu ambayo lazima yafanyiwe kazi ili kubadili industry hii ambayo hapana shaka imekuwa kimbilio la wengi.Matatizo yaliyoainishwa ni pamoja na:

1. Wizi wa kazi za wasanii (Piracy) ambapo ilishauriwa kwamba Cosota lazima ibadilike, ipewe meno na iweze kupambana vilivyo na tatizo hili ambalo limekuwa likiwakwamisha wasanii wengi.


2.
Kunakiri (copying) kazi za wasanii wa Nigeria na kutumia muziki (Sound Tracks) za wasanii wa muziki bila idhini yao.Katika haya wasanii wa Filamu wameshauriwa kuwa makini kwani sheria ya Hakimiliki inaweza kuwafunga.Kwa ujumla wasanii walishauriwa kuwekeza ubunifu binafsi na kubeba uhalisia wa sanaa yetu badala ya ilivyo sasa ambapo filamu zetu zimekuwa zikifanana fanana na zile za Nigeria.


3.
Uchafu wa Filamu-Wadau wengi wamesema kwamba, filamu za kibongo zimekuwa na maadili mabovu yanayotokana uvaazi wa vichupi kwa wasanii wa kike, uoneshaji wa matendo ya faragha (mapenzi) mara kwa mara, script zenye kushabikia matendo maovu na yasiyofaa kwa jamii nk.Wadau walishauri Bodi ya Filamu, vituo vya TV na wasanii wenyewe kuhakikisha wanadhibiti filamu zisizo na maadili kwani zimekuwa zikitia aibu/kichefuchefu.Ilielezwa kwamba, baadhi ya filamu hazibebi uhusika wenye ufanano na maisha/maadili ya kitanzania.

4. Wasanii kuact maisha ya juu mara kwa mara tofauti na uhalisia wao.Mtaalamu wa Filamu kutoka Chuo Kikuu,Bw.Ndunguru alieleza kwamba,filamu nzuri ni ile inayobeba uhalisia.Aliongeza kwamba, wasanii wanapenda kutumia magari ya gharama kama Hammer, majumba ya thamani, maisha ya anasa nk. kwenye filamu zao kueleza uhalisia usiokuwepo katika maisha yetu.

5. Ubunifu mdogo wa waongozaji, watengenezaji na mameneja wa Filamu ambao umekuwa ukiwafanya muda mwingi wautumie kunakiri (copying) kazi za kigeni.Ilishauriwa kwamba, wataalamu hawa wafikirie walau kupata elimu,semina na mafunzo ya muda mfupi kwenye taaluma zao badala ya ilivyo sasa.

6. Kutokuzingatia mikataba kwenye kazi zao.Ilielezwa kwamba, wasanii wengi wamekuwa wakiwalalamikia wasambazaji wa kazi (Distributors) huku wakiwa wamesainiana mikataba.Kumbe tatizo lililopo ni wasanii wenyewe kusaini mikataba kwa pupa, uroho wa fedha, bila kuisoma mikataba husika na wakati mwingine bila kuandikiana bali kwa mazungumzo tu.Ilishauriwa kwamba, wasanii lazima wasimamie mikataba na kuhakikisha inawanufaisha.Wasilalame tu, wachukue hatua pia.
JUMATATU IJAYO KWENYE JUKWAA LA SANAA

Mchango wa Kituo cha Utamaduni cha Kimataifa cha Ufaransa na Ubalozi wa Ufaransa Katika Ukuzaji wa Sanaa na Utamaduni Wetu.Tutakuwa na Wataalam kutoka Ubalozi wa Ufaransa.USIKOSEKANE.

Picha/Habari na Afisa Habari wa BASATA,

Alistide Kwizela

TENDWA KUTOA MAAMUZI PINGAMIZI LA CHADEMA BAADA YA SIKU TANO!

Msajili wa Vyama Vya Siasa Nchini John Tendwa amesema atatoa uamuzi wake dhidi ya malalamiko yaliyowasilishwa ofisini kwake jana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA)kuhusu mgombea wa urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM) baada ya siku tano.

Bwana Tendwa ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari hayo ofisini kwake jijini Dar es salaam baada ya kupokea malalamiko hayo rasmi leo.

‘’Nitatoa maamuzi hayo baada ya kupokea maelezo kutoka kwa mlalamikiwa dhidi ya malalamikaji yaliyowasilishwa,na nitatoa nakala ya maamuzi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi na Katibu Mkuu wa chama cha CHADEMA’’,Alisema Tendwa.

Akifafanua suala hilo Tendwa amesema baada ya maamuzi yake mlalamikaji na mlalamikiwa kama hawataridhika na uamuzi wake wanayo haki ya kwenda kutafuta haki yao kwenye vyombo vya sheria.

Aidha Msajili huyo Vyama ameongeza kuwa amepokea malalamiko hayo kwa mujibu wa sheria ya gharama za uchaguzi inachomkataza mgombea yeyote ambaye yeye mwenyewe, wakala wake au Chama chake kitafanya kitendo ambacho kimekatazwa kama ilivyoelekezwa kwenye sheria hiyo atakuwa au kitakuwa kimepoteza sifa za kushiriki mchakato wa uteuzi au uchaguzi.

Pingamizi hilo liliwasilishwa jana ofisi ya masajili huyo na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika wakimlalamikia Mgombea urais wa chama cha mapinduzi Jakaya Mrisho Kikwete kutumia madaraka yake kutoa ahadi kwenye kampeni na kutangaza nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi wakati wa kampeni.

WAREMBO VODACOM MISS TANZANIA WAELEZWA FAIDA ZINAZOTOKANA NA BIDHAA ZA VODACOM!!

Afisa Bidhaa wa Vodacom Tanzania Elihuruma Ngowi akiweka sawa picha kwenye Projekta wakati alipokuwa akiwasilisha mada kwa warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania juu ya umuhimu wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kutolewa na kampuni ya Vodacom katika semina ambayo imefanyika kwenye kambi ya warembo hao Hoteli ya Giraffe Ocen View Mbezi Beach jijini Dar es salaam leo.
Meneja Mauzo wa M-PESA Jerome Munishi akitoa ufafanuzi juu ya huduma za hizo zinazotolewa na kampuni ya Vadacom Tanzania wakati wa semina ya warembo wanaoshiriki kwenye shindano la Vodacom Miss Tanzania katika Hoteli ya Giraffe Ocean View Mbezi Beach leo hii shindano hilo linatarajiwa kufanyika Septemba 11 mwaka huu.

JARIDA NUMBER 10 LIMETOKA JIPATIE COPY YAKO.


PRECISION AIR YAZINDUA NDEGE MPYA !!

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.Mohammed Babu akikata utepe kama ishara ya kuzindua ndege mpya ya Precision ART 42- 500 iliyopewa jina la "Bukuoba" yenye uwezo wa kubeba abiria 48 ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es salaam na Bukoba na kurudi Dar es salaam, ndege hiyo iliruka kutoka Dar es salaam kwenda Zanziar na kurudi kwa majaribio na inatarajia kuanza safari zake mwezi ujao, wanaoshuhudia katika picha kutoka kulia ni Jamal Hussein Afisa Mtendaji Mkuu Citi Bank, Allan Sharra Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air na kushoto ni Rubani wa Ndege hiyo Chohan Mbarouk

Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye alikuwa mgeni rasmi Mh. Mohamed Babu katikati akisubiri ndege itue ili kufanya uzinduzi rasmi kwa kukata utepe kulia ni Allan Sharra Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air kushoto ni Jamal Hussein Afisa Mtendaji Mkuu Citi Bank na mwisho kushoto ni Lucy Malu Meneja Mkazi Kenya Airways.
Hii ndiyo ndege mpya ya Precision Air ATR 42- 500 yenye uwezo wa kubeba abilia 48 itakayofanya safari zake kati ya Dar es salaam na Bukoba.
baadhi wa Marubani wa Precisiano Air wakiwa katika uzinduzi huo leo.
Meneja wa Uhusiano wa Kampuni ya SCANAD Barnabas Lugwisha akiwa na mmoja wa waalikwa katika ndege hiyo mpya ilifanya safari kati ya Zanzibar na Dar es salaam leo kwa ajili ya uzinduzi rasmi

Designers visiting the Textile Sector Development Unit


Designers being shown the Modern industral Patern cutter BY PRODUCTION MANAGER PATRRICK LUMUMBA.
Designers Kemi Kalikawe , Manju Msitta and Ailinda Sawe seeing how a machine operates.
Designer listening to Patrick Lumumba of the Production Facility they Visited on 30 September 2010.
Designers attending to how the pattern drafting works

Dr. Bilal Aendelea na ziara ya kampeni masasi na nayumbu!!!


Mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM,Dk. Bilal akizungumza na wanachi wa Wilaya ya Nanyumbu baada ya kuingia mpakani mwa wilaya hiyo na Masasi leo
Kamanda wa Chipukizi wa Wilaya ya Masasi, Fatuma Rajab akimvisha skafu Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal alipokuwa akiingia mpakani mwa Wilaya ya Masasi akitokea Wilaya ya Newala leo mchana
Mgobea Mwenza wa urais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na wananchi na viongozi wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Masasi, baada ya kuingia mpakani mwa wilaya hiyo na Newala, leo
Baadhi ya makada wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Newala Mkoa wa Mtwara, wakiwa katika magari kwenye msafara wa kumsindikiza Mgombea Mwenza wa nafsi ya urais, Dk Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akitoka Wilaya hiyo kuelekea Wilaya ya Masasi leo asubuhi
wananchi wa Kijiji cha Lukuledi Wilaya ya Masasi Mkoa wa Mtwara, waliojitokeza kumsikiliza mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia na kuwanadi wagombea Ubunge wa Jimbo la Lulindi,Bwanausi Dismas na Mariam Kasembe wa Jimbo la Masasi leo
Wananchi wa Kijiji cha Mangaka Wilaya ya Nanyumbu Mkoa wa Mtwara Jimbo la Nanyumbu, wakimsikiliza mgombea mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Kijiji hicho leo mchana.

(Picha na Muhidin Sufiani)

tano Wa Marais Wastaafu Wafanyika Jijini Dar


Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi (katikati) akiongea na washiriki wa mkutano unaowahusisha marais wastaafu wa Afrika walioachia madaraka kwa njia ya amani leo jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni balozi Charles Stith ambaye pia ni mkurugenzi wa kuhifadhi kumbukumbu za marais wa Afrika.
Baadhi ya viongozi wastaafu wa nchi za Afrika na wale walioko madarakani wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa ufunguzi wa mkutano unaowahusisha marais wa Afrika walioachia madaraka kwa njia ya amani leo jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Rais mstaafu wa Jamuhuri ya Mauritius, Dkt. Kenneth Kaunda rais mstaafu wa Zambia, Waziri mkuu wa sasa wa Msumbiji Bi. Luisa Diogo na Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania Fredrick Sumaye. Washiriki wa mkutano wa marais wastaafu wa Afrika walioachia madaraka kwa njia ya amani kutoka nchi mbalimbali za Afrika na vyuo vikuu kutoka ndani na nje ya Afrika wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa mkutano wa marais wa Afrika walioachia madaraka kwa njia ya amani leo jijini Dar es salaam.
(Picha na Aron Msigwa)

Aug 29, 2010

Chama cha NCCR Mageuzi chazindua ilani yake ya uchaguzi

Pichani ni mgombea urais kwa Chama cha NNCR Mageuzi, Hashim Rungwe akionyesha ilani ya uchaguzi ya chama hicho wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chama hicho leo jijini Dar. CHAMA cha NCCR Mageuzi leo kimezindua ilani yake ya Uchaguzi huku kikitaja mambo 12 ambayo chama hicho kitaelekeza nguvu iwapo kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi.Wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa chama hicho taifa James Mbatia alisema chama chake kitazindua kampeni zake kitaifa Septemba 11 baada ya mfungo wa ramadhani ili kutowakwaza Waislam ambao wako kwenye mfungo wa mwezi mtukufu.“Ajenda yetu kuu itakuwa ni katiba, tumeainisha mambo yatakayokuwemo kwenye katiba hiyo, hili ndilo nataka wagombea wetu mlizungumzie kwa kina,” alisema Mbatia.

VODACOM YAFUTURISHA PANGANI NA KUGAWA MISAADA YA CHAKULA KWENYE MADRASA!!

Mwamvua Mlangwa Mratibu wa Uhusiano Vodacom Foundation kulia akikabidhi madaftari kwa watoto wa mji Vituo vya watoto yatima na Madrasa mbalimbali Pangani. mara baada ya kufuturu katika futari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation, wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kushoto ni, Sheikh Mohamed Khalili Mwakilishi kutoka Tanga mjini, Sheikh Khamis Rashid mwakilishi wa Sheikh wa Pangani na Grace Lyon Afisa Vodacom Foundation.

Mtoto Bwaga Abdallah akipokea mfuko wa sukari kutoka kwa Maafisa wa Vodacom Foundation Grace Lyon kulia na Mwamvua Mlangwa wa pili kutoka kulia huku akisaidiwa na Sheikh Mohamed Khalili kushoto kutoka Tanga mjini na Sheikh Khamis Rashid Mwakilishi wa Sheikh wa Pangani wa pili kutoka kushoto, katika msaada huo pia Vodacom Foundation iligawa Mchele, Maharage, mafuta ya kula pamoja na vifaa vya shule.

: wakazi wa mji wa Pangani waliojitokeza katika futari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation wakisubiri muda ufike ili waweze kufuturu Vodacom Foundation pia iligawa misaada ya Mchele, Mafuta ya kula, maharage na vifaa vya shule kwa watoto wa Dadrasa mbalimbali na vituo vya watoto yatima mjini Pangani
Wakazi wa mji wa Pangani wakipata futari mwishoni wa wiki ambapo Vodacom Foundation iliwafuturisha na kugawa vyakula na vifaa vya shuleni wa watoto yatima na madrasa mbalimbali mjini humo ambavyo ni Mchele, maharage, mafuta ya kula, sukari na vifaa vya shuleni kwa ajili ya wanafunzi.
Wakazi wa mji wa Pangani wakipata futari mwishoni wa wiki ambapo Vodacom Foundation iliwafuturisha.

CUF wazindua kampeni zaao


Mwenyekiti wa CUF na mgombea urais wa chama hicho cha wananchi, Prof. Ibrahim Lipumba akisalimia wanachama wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni ya chama hicho katika viwanja vya Kidongo Chekundu jijini Dar
Prof. Lipumba akisalimiana na Mh. Hamad Rashid mmoja wa wanachama na viongozi waandamizi wa CUF.
Sehemu ya umati wa wana CUF mkutanoni hapo

Rais Kikwete Awasili Mkoani Mbeya


Rais Jakaya Kikwete akihutubia umati wa wakazi wa Tunduma jioni hii wakati akianza kampeni yake mkoa wa Mbeya.
Rais Jakaya Kikwete akihutubia jioni hii mjini Tunduma ambako kumetia fora sana kwa umati mkubwa wa watu katika vituo vidogo vya mikutano ya kampeni za Chama tawala CCM
Uwanja wa mkutano Tunduma ulikuwa hautoshi
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Mark Mwandosya akimfagilia njia JK ya kuhutubia wananchi wa Tunduma leo

Dr.Bilal aendeleaa kuinadi ilani ya CCM mkoani mtwara


Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,Dk. Mohamed Gharib Bilal akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika Kijiji cha Ntiniko Wilaya ya Mtwara Vijijini Mkoa wa Mtwara.
Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal akipita katikati ya chipukizi baada ya kupokelewa katika mpaka wa Wilaya ya Mtwara Mjini na Tandahimba Mkoa wa Mtwara wakati akiwa kwenye ziara yake ya mikutano ya kampeni leo mchana.
Mgombea Mwenza wa nafasi ya urais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Nanguruwe Wilaya ya Mtwara Vijijini baada ya kusimama eneo hilo wakati akielekea Kijiji cha Ntiniko katika mkutano wa kunadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) leo.
Wananchi wa Kijiji cha Nahyanga Wilaya ya Tandahimba Mkoa wa Mtwara, wakimsikiliza Mgombea mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati wa mkutano wa kampeni.

Rais Kikwete apokelewa kwa shangwe sumbawanga na mpanda


Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete akimnadi kwa wananchi mgombea Ubunge wa jimbo la Sumbawanja mjini kupitia chama hicho,Bw.Khalfan Hayeshi pindi alipokuwa katika mkoa wa Rukwa jana.
Rais Jakaya Kikwete akigombewa kusalimiwa na wananchi wa Sumbawanga alipokuwa akiwasili katika uwanja wa Mandela.
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi pindi alipowasili mjini Mpanda na kufanya mkutano wa kampeni.
Rais Jakaya Kikwete akishuka kwenye Helkopta mara baada ya kuwasili Sumbawanga mjini tayari kwa mkutano uliofanyika jana kwenye uwanja wa Mandela.
Wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akihutubia.

Wanachi wa mji wa Sumbawanga wakiwa wamefurika ndani ya Uwanja wa Mandela kumsikiliza Rais Jakaya Kikwete wakati akiwahutubia.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA