Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
Aug 29, 2010
VODACOM YAFUTURISHA PANGANI NA KUGAWA MISAADA YA CHAKULA KWENYE MADRASA!!
Mwamvua Mlangwa Mratibu wa Uhusiano Vodacom Foundation kulia akikabidhi madaftari kwa watoto wa mji Vituo vya watoto yatima na Madrasa mbalimbali Pangani. mara baada ya kufuturukatika futari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation, wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kushoto ni, Sheikh Mohamed Khalili Mwakilishi kutoka Tanga mjini, Sheikh Khamis Rashid mwakilishi wa Sheikh wa Pangani na Grace Lyon Afisa Vodacom Foundation.
Mtoto Bwaga Abdallah akipokea mfuko wa sukari kutoka kwa Maafisa wa Vodacom Foundation Grace Lyon kulia na Mwamvua Mlangwa wa pili kutoka kulia huku akisaidiwa na Sheikh Mohamed Khalili kushoto kutoka Tanga mjini na Sheikh Khamis Rashid Mwakilishi wa Sheikh wa Pangani wa pili kutoka kushoto, katika msaada huo pia Vodacom Foundation iligawa Mchele, Maharage, mafuta ya kula pamoja na vifaa vya shule.
: wakazi wa mji wa Pangani waliojitokeza katika futari iliyoandaliwa na Vodacom Foundationwakisubiri muda ufike ili waweze kufuturu Vodacom Foundation pia iligawa misaada ya Mchele, Mafuta ya kula, maharage na vifaa vya shule kwa watoto wa Dadrasa mbalimbali na vituo vya watoto yatima mjini Pangani
Wakazi wa mji wa Pangani wakipata futari mwishoni wa wiki ambapo Vodacom Foundation iliwafuturisha na kugawa vyakula na vifaa vya shuleni wa watoto yatima na madrasa mbalimbali mjini humo ambavyo ni Mchele, maharage, mafuta ya kula, sukari na vifaa vya shuleni kwa ajili ya wanafunzi.
Wakazi wa mji wa Pangani wakipata futari mwishoni wa wiki ambapo Vodacom Foundation iliwafuturisha.
Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)
No comments:
Post a Comment