Sep 6, 2012

HUYU NDIO MWANDISHI ALIEJISALIMISHA POLISI MWENYEWE KATI YA WALE WATATU WALIOTANGAZWA KUSAKWA BAADA YA KIFO CHA MWANGOSI.

Kwa sababu za kiusalama ilikua picha yake isiwekwe hapa lakini yeye mwenyewe ameidhinisha iwekwe kwa sababu haogopi, Francis Godwin ni huyo mwenye nguo nyeusi.
Siku mbili baada ya kifo cha mwandishi mwenzao wa habari (Daudi Mwangosi) aliefariki kutokana na kulipukiwa na bomu akiwa mikononi mwa polisi waliokuwa wanatawanya wafuasi wa Chadema huko Iringa, mwandishi wa habari Francis Godwin ambae alikua rafiki wa marehemu amejisalimisha polisi kufata masharti ya taarifa iliyotolewa kwa yeye na wenzake wawili kusakwa na polisi.
Exclusive na millardayo.com namkariri Godwin akisema “kutokana na hali halisi ya kushuhudia tukio la mauaji ya Mwangosi, nilifukuziwa kwa nyuma na gari lisilokua na namba pia nilipofika nyumbani niliambiwa kuna watu walikuja kuniulizia lakini hawafahamiki, na taarifa zikatoka kwamba tunasakwa”
Kuhusu kujisalimisha, Godwin amesema aliamua kufanya huo uamuzi baada ya kusikia taarifa za kusakwa kwake pamoja na waandishi wengine wawili, jana (september 5) aliamua kujisalimisha mwenyewe Polisi akiwa amesindikizwa na waandishi wa habari kama hamsini ambapo baada ya kufika pale walikutana na  kamishna wa makosa ya jinai Tanzania Robert Manumba ambae ilibidi ahoji polisi Iringa kama ni kweli wanamtafuta Godwin na wenzake.
.
Namkariri Godwin akisema “baada ya kumuuliza mmoja kati ya maofisa wake kama ni kweli wanamtafuta Godwin ofisa huyo alijiumauma na baadae akasema hatumtafuti, baada ya hapo waandishi wa habari tulisimama tukaondoka kwa sababu ya kutokubaliana na kilichotaka kuendelea kuhusu taarifa ya uchunguzi ya Manumba”
Kingine kilichoendelea baada ya hapo ni Club ya waandishi wa habari Iringa kuziomba redio mbalimbali za iringa ambazo zimekua zikirusha matangazo ya polisi jamii kusimamisha matangazo hayo ambapo wamiliki wa vyombo hivyo wamekubali ombi.
Francis Godwin ambae alikua karibu na marehemu Daudi Mwangosi muda mfupi kabla ya kuuwawa kwa bomu amesema “Nilijua kwamba mimi ni miongoni mwa waandishi watatu wanaotafutwa kwa sababu marehemu kabla ya kifo akiwa amekamatwa nilitaka kwenda kumuokoa pale lakini nilipokua namsogelea Daudi akaniambia Godwin mdogo wangu kimbia… wakati nakimbia kama hatua 20 mbele nyuma nageuka nasikia mlipuko mkubwa, kuangalia ni Wangosi amekufa na nilibahatika kupiga baadhi ya picha ambapo askari waliokuwepo walipoona narudi kwenye eneo hilo walinionyeshea bunduki ikabidi ninyooshe mikono juu kwamba jamani mimi nakuja kwa heri wakaniambia potea”
Muda mfupi baada ya Marehemu Daudi kulipukiwa na bomu.
Godwin amesema baada ya kugeuka na kuanza kukimbia walianza kumfukuzia ila bahati nzuri gari yake ilikua mbali, baada ya kutishwa na polisi walipokwenda hospitali ulipopelekwa mwili wa marehemu ilibidi waanze kutoa mabango ya wanahabari yaliyobandikwa kwenye gari yao pamoja na kutoa namba za gari, alianza safari ya kuondoka lakini kuna gari zilikua zinamfukuzia kwa nyuma mpaka alipofika nje kidogo ya mji wa Iringa na kuingia mitaani ndio akafanikiwa kukimbia.
Kwenye sentensi ya mwisho Godwin anasema ameibiwa siri na askari mmoja ambae alimwambia kuhusu kutafutwa kwake yeye na waandishi wa habari awengine mbapo alimuonya kwamba msimamo na kauli aliokua ameutoa pamoja na ushahidi wa tukio la mauaji ndio vimefanya atafutwe.

MAGAZETI YA TRH 6/9/12

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

ALICHOSEMA PRODUCER MANECK BAADA YA KUONA DOGO JANJA ANATAKA KUMGOMBANISHA NA MARCO CHALI.

.
Producer Maneck ambae ni mshindi wa tuzo kwenye KTMA 2012 ameamua kuzungumza ya moyoni kwa kuijibu kauli Dogo Janja aliyoitoa kwamba Producer huyo kauponda uwezo wa Marco Chali.
Ishu ilianza wakiwa club Maisha Dar es salaam jumapili iliyopita ambapo Dogo Janja anadai alikwenda sehemu ya V.I.P na kumsalimia Maneck ambae hakujibu salamu ila aliporomosha matusi mazito kwa Dogo Janja pamoja na kumpiga biti kwamba asimsogelee.
Baada ya hapo Dogo Janja akashuka chini kwenda kumwita meneja wake wa WATANASHATI ambae ni Ustaz Juma ambapo kwa maelezo ya Dogo Janja, Maneck alianza kuiponda single mpya ya Dogo Janja na PNC waliyoirekodi kwa Marco Chali ambayo mwanzoni ilikua irekodiwe kwa Maneck alieiponda kwa kusema ni ya kawaida sana kwa sababu imefanywa na Marco Chali.
Jibu alilolitoa Maneck baada ya kusikia kwamba Dogo Janja amenukuliwa kwa hayo maneno, namkariri akisema “ndio ninavyokwambia sitakagi watu masnich kama huyo, Marco Chali ni mtu ambae namfil sana anafanya kazi nzuri, siwezi kuongea kitu kibaya kwa Marco kwa sababu leo na kesho nitamfata nitamuomba msaada wa kitu chochote kile hata material sasa nitawezaji kusema hivyo kwa mfano sasa, Dogo Janja ni mtu ambae anataka tu kufanyaga vitu watu wapishane kauli mambo ya kijinga ni utoto akikua nadhani ataacha hizo tabia zake, na ndio maana nikamwambia kaa mbali sitaki uongee na mimi that’s all”(kwa hisani ya www.millardayo.com)

MBWANA SAMATTA - THE KING IN THE MAKING


Hili ni moja ya bango la kumsifia Mbwana Samatta lilochorwa na washabiki wa Mazembe

Huyu ni shabiki wa Mazembe akiwa na jezi yenye jina la Samatta

Kama Spain -vile ni vigari maalum kubebea wachezaji wanaoumia uwanjani katika uwanja wa TP Mazembe

Mbwana Samatta mwenye jezi namba 15 akiwa anapigwa konga na beki wa Al Ahly

Huyu ndio mshabiki aliyevaa jezi yenye jina la Samatta

Mfalme wa Mazembe Tresor Mputu akiwafanyia balaa waarabu

Kidiyaba ndani ya uzi wake wa golikipa

Majembe ya Kitanzania Thomas Ulimwengu na Mbwana Ally Samatta wakiwapeleka puta mabeki wa Al Ahly katika mechi ya robo fainali ya kombe la mabingwa wa Afrika iliyofanyika juzi jumapili.(kwa hisani ya www.shaffihdauda.com)

MATUMIZI MABAYA YA FEDHA YANAVYOTISHIA KUMFILISI MWANASOKA NEYMAR


Hakuna ubishi juu ya kipaji alichonacho mwanasoka wa kibrazil Neymar .
Neymar kwa sasa sio tu mwanasoka anayependwa sana kuliko wote nchini Brazil, bali pia ni tumaini kubwa la kuiwezesha nchi hiyo kutwaa kombe la dunia mwaka 2014, ambalo litafanyika katika taifa hilo la bara la Amerika ya kusini.


Ameelezewa na Pele, ambaye anatajwa kama mwanasoka bora kabisa kuwahi kutokea katika historia ya mchezo huo - kuwa na mtaalam wa soka, mwenye miguu ya majaabu, huku akiwa na umri wa miaka 20. Lakini kipaji cha Neymar uwanjani ni tofauti kabisa na akili yake linapokuja suala la matumizi ya fedha. Anatengeneza fedha nyingi sana lakini anatumia karibu na chote anachoingiza.


Gari aina ya Porsche Panamer
 Ndani ya miaka miwili tu, Neymar ameripotiwa kununua jumba ambao ndani lina nyumba zingine tatu tofauti kwa $750,000 na hekalu lingine lenye thamani ya $2million - zote zikiwa kwenye eneo la pwani ya kaskazini ya jiji la Sao Paolo; pia amenunua flat yenye thamani ya $150,000 hapo hapo Sao Paolo. Amenunua gari aina ya Porsche Panamera Turbo yenye thamani kati ya $400,000 mpaka $550,000.  Pia alimpa mama wa mtoto wake mwenye umri wa miaka 18 Apartment iliyo kwenye moja ya majengo marefu pale Santos ambayo ina thamani ya $1,000,000 - huku akiwa anatoa $15,000 kwa mwezi kwa ajli ya malezi ya mtoto. Lakini kubwa kuliko ni pale aliponunua boti ya kifahari ambayo hata baadhi ya matajiri wakubwa duniani hawana - yenye thamani ya $8 million, ambayo gharama yake ya matengenezo na services kwa muda ni kiasikisichopungua $120,000 kwa mwaka.

Yatch ya Neymar
Ingawa hakuwemo kwenye listi ya wanasoka wanaolipwa fedha nyingi duniani ambayo ilitolewa na jarida la Forbes la Marekani mwezi wa nne mwaka huu huku nafasi ya kwanza ikishikwa na David Beckham, Neymar anarudi nyumbani kwa mwaka na mshahara wa $4million kwa mwaka kutoka Santos, kalbu yake ya kibrazil ambayo ana mkataba nayo mpaka 2014. Shukrani kwa dili za udhamini kutoka Nike ($1 million kwa mwaka) na Red Bull na dili nyingine kutoka kwenye makampuni kadhaa ya kibrazil ambayo yanamfanya Neymar apeleke benki kiasi kingine cha fedha kipatacho $4 million kwa mwaka - kwa maana hiyo ingizo lake lote kwa mwaka ni $8million. Fedha hizi ni kidogo ukilinganisha na wanasoka wengine wakubwa kama Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Kaka na hata Beckham , ambao wote wanatumia fedha zao vizuri sana. Kwa mfano Beckham ambayo yeye hupendelea kukodisha boti ya kifahari kwa maana ya kupunguza gharama nyingi za kununua na kuihudumia boti hiyo.

Neymar na mwanae ambaye anamgharimu zaidi ya $15,000 kwa mwezi kumlea.
Miezi kadhaa iliyopita vyombo vya habari vya Brazil vilikuwa vinapotosha na kusema kwamba Neymar anaingiza kiasi cha $18 million kwa mwaka, jambo ambalo lilikuja kuonekana sio sahihi pale alipoanza kufanya mazungumzo mapya juu ya mahitaji yake kwenye mshahara mpya na klabu yake ya Santos. Kwa maana hiyo Neymar bado hajaweza kuingiza fedha nyingi kiasi cha kuweza kununua matoi  ya kuchezea kwa matajiri kama boti za Yatch.
"Kiukweli anatumia fedha nyingi sana karibu na kile chote anachoingiza," anasema mtaalam wa mambo ya fedha wa jarida la Forbes bwana Settimi huku akisisitiza lazima klabu yake itakuwa inamsaidia kwa kumpa fedha nyingine nje ya mkataba wake. 


"Inawezekana Santos wana mkono wao kwa sababu ukiangalia matumizi yake ndani ya kipindi cha miaka miwili iliyopita unaona kwamba ametumia zaidi ya kile alichoingiza - kuna taarifa zinasema klabu yake inampa fedha nyingi hata nje ya mkataba ili kumridhisha na kumfanya asahau kwenda barani ulaya."

Mhariri mkuu wa jarida la Forbes Kurt Badenhausen anamfananisha Neymar na Mike Tyson: " neymar ndio kwanza anakuwa na anatengeneza fedha nzuri sana.  Kama ilivyokuwa kwa Tyson ambaye nae alianza kutengeneza fedha akiwa na miaka 18 na miaka kadhaa baadae alikuwa na utajiri wa $400 million - hivi ndivyo nahisi Neymar akavyokuwa ikiwa itaacha kutumia vibaya fedha zake."


Mike Tyson akiwa kwenye kiwango cha juu, pambano lake moja alikuwa akitia ndani kiasi cha $30 million. Lakini wakati wa kipindi hicho, Tyson alinunua mahekalu, magari ya kifahari, chui wa kufuga. Mwishoni mwa mwaka 2002,  aliingia kwenye duka la kuuza vito na kununua cheni ya dhahabu yenye thamani ya $174,000 huku ikiwa imenakishiwa na almasi kiasi. Miezi nane baadae Tyson akatangaza kufulisika huku akiwa na madeni yanayofikia $23 million.


Watu wengine maarufu ni kama vile star wa NBA Antoine Walker, ambaye alitengeneza zaidi ya $110 million wakati akicheza bado, na Evander Holyfield, wote wamefilisika.


Mfano mwingine mzuri haupo mbali na yeye. Nchini Brazil mwanasoka Romario, ambaye  alikuwa mchezaji muhimu sana kwa Brazil katika fainali za kombe la dunia 1994, alikamatwa mwaka 2009  kwa kesi ya kushindwa kutoa fedha ya malezi ya mtoto. Huku akiwa na deni linalofikia $5 million.


Neymar anatakiwa kufuata mfano wa gwiji wa soka wa nchi hiyo Ronaldo De Lima ambaye aliwekeza fedha zake vizuri. Ronaldo sasa hivi anamiliki asilimia 45 za kampuni ya 9ine Sports and Entertainment  Agency, kampuni inayodili na masuala ya soka, ambapo moja ya wateja wao ni Neymar.


Shukrani kwa 9ine inayofanya vizuri sana kwenye biashara zake, Ronaldo de lima sasa ana thamani ya utajiri unaofikia $250 million. Kwa maana hiyo Neymar itabidi afuate nyayo za huyu jamaa ili aweze kuwa na mafanikio miaka kadhaa ijayo, na sio kufuata nyayo za Romario na akina Tyson.

SIMBA NA YANGA WAKABIDHIWA VIFAA VYA MILLIONI 68 NA KILIMANJARO KWA AJILI YA MSIMU MPYA

Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ (kulia), wakionesha baadhi ya vifaa vya michezo  walivyokabidhiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ambao ndio wadhamini wakuu wa klabu hizo. Wa pili kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe na Mkurugenzi wa Mashindano, Saad Kawemba. Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jijini Dar es SalaamMeneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe  
 Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ akizungumza katika hafla hiyo.
Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu akizungumza katika hafla hiyo
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (kushoto) akimkabidhi baadhi ya vifaa vya michezo Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na katikati ni Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba.
Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu (kushoto) akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe. 
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe

Na Clezencia Tryphone
KLABU kongwe nchini za Simba na Yanga, zimekabidhiwa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya sh milioni 34 kila moja kutoka kwa mdhamini wao mkuu, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager.
Akikabidhi vifaa hivyo katika Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, alisema, kukabidhi vifaa hivyo ni moja ya sehemu katika mkataba baina yao na klabu hizo.
Kavishe alisema lengo kubwa la kudhamini timu hizo ni kutokana na historia kubwa ya klabu hizo, pamoja na kuleta ushindani wenye burudani kwa Watanzania, ambao ni wadau wakubwa wa kunywa kinywaji hicho.
“Sisi tunafanya kazi vema na klabu hizi, tunajisikia faraja kubwa kutokana na timu hizi kuwa na historia kubwa hapa nchini na ushindani mkubwa katika soka na huu ni udhamini wa nusu msimu peke yake,” alisema Kavishe.
Alivitaja vifaa hivyo walivyotolewa kuwa ni jezi, bukta, soksi, viatu, bips, nguo za kusafiria, vikinga ugoko na mifuko.
Katika hatua nyingine, Kavishe alisema, kuhusu mabasi ya timu hizo, wako katika hatua za mwisho kuyakabidhi kwa wahusika, kwani tayari yamewasili hapa nchini, ambapo kuna mambo kadhaa wanayakamilisha.
Akizungumza kwa niaba ya klabu ya Simba, Makamu Mwenyekiti, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, aliwashukuru wadhamini hao kwa moyo walionao, huku akiwaahidi kuhakikisha wanafanya vema na kushinda ili kuonesha umuhimu wa vifaa ambavyo wamewapa.
“Nawashukuru TBL kwa kutudhamini na kuona umuhimu kwa sisi Simba bila ya kupepesa macho na ndiyo maana hata sisi tutapigana kufa na kupona ili kuhakikisha tunavitendea haki vifaa hivi,” alisema Kaburu.
Kwa upande wa Yanga, Ofisa Habari wake, Louis Sendeu, naye aliishukuru TBL, huku akiwaomba kutoishia kwa Simba na Yanga, bali waziangalie na timu nyingine.
“Tunawashukuru sana ila msiishie kwa Yanga na Simba tu, mziangalie na klabu nyingine ambazo zinasuasua,” alisema Sendeu.
Source: http://francisdande.blogspot.com

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA