
Mara ya mwisho msanii Juma Nature alipotoa wimbo mpya,baadhi ya wapenzi wa muziki wake hawakusita kuelezea hisia zao kwamba Nature amebadilika. Kivipi? Walisema haimbi na hana tena yale mashairi yaliyomfanya akakubalika sana hapo mwanzoni. Wakamsihi arudi kule kule alipoanzia.Kule kule kwenye nyimbo kama vile Hili Gemu,Kighetogheto,Sitaki Demu,Mzee wa Busara na nyinginezo.
Huenda ombi la washika dau hao wa muziki likawa limesikilizwa.Wimbo mpya wa Nature unaitwa Msichana Mtundu.Kwa upande wangu kilichonivutia zaidi katika wimbo huu ni ujumbe uliomo. Shule,maisha,baba-sukari,mapenzi,jamii.
No comments:
Post a Comment