



Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
NA ZAHRA MAJID- MAELEZO.
MSIMU wa ununuzi wa korosho kwa mwaka 2010/2011 nchini unatarajiwa kuanza Jumatano ya wiki.
Ununuzi huo unatarajia kutumia Mfumo wa Stakabadhi ghalani ambapo Vyama vya Ushirika vitapeleka korosho kwenye maghala ya Serikali ambapo ndipo mnada utafanyikia.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar-es-salaam na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Hemedi Mkali wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari ( MAELEZO).
Alisema kuwa korosho zitauzwa kwa mnada utakaofanyika katika Bodi ya Korosho na katika Ofisi za Bodi katika mikoani Tanga, Mtwara, Pwani, Dar-es salaam, Morogoro, Ruvuma na Wilaya za Kyela na Ludewa Tunduru.
Mkali alisema kuwa korosho zitakazouzwa ni zile tu zitakazokuwa kwenye magulio yaliyosajiliwa na Serikali na kuongeza uuzaji wa korosho kinyume cha utaratibu huo , wahusika watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria namba 12 ya mwaka 2009.
“ Wanunuzi wa korosho wanaombwa wafuate taratibu hizi za ununuzi kwani watakaojaribu kukiuka taratibu hizi za ununuzi basi wajue Sheria hii inayohusu sekta ya korosho itachukua mkondo wake” Mkali alisema.
Mkali alizitaja kuwa timu zitakazoendesha mnada huo kuwa na wawakilishi toka Bodi ya Korosho,Vyama vya Ushirika Benki ya CRDB na NMB, Bodi ya Leseni za maghala Tanzania, Maafisa Ushirika watakaoteuliwa kama waalikwa na wengine wanaohitaji kushuhudia watafuata utaratibu maalum wa minada hiyo.
Halikadhalika, alisema kuwa,katika mfumo wa stakabadhi za mazao maghalani, kwa niaba ya wakulima korosho zitakusanywa na chama cha ushirika cha msingi katika magulio yaliyosajiliwa kwa kuwalipa wakulima asilimia 70 ya bei dira kwa korosho daraja la kwanza.
Mkali alisema kuwa watalipwa malipo ya pili asilimia 30 baada ya korosho kuuzwa mnadani.
“Aidha watalipwa malipo ya tatu (ya majaliwa) kutokana na bei itakayopatikana kwenye mauzo mnadani” Aliongeza Mkali.
Mkali alitaja viwango vya bei za korosho kuwa ni Tshs. 800 kwa kilo moja kwa daraja la kwanza(STD) na Tshs. 640 kwa kilo moja kwa daraja la pili(UG).
YOU CAN AS WELL GET A COPY DIRRECTLY FROM US, NO MINIMUM ORDER!
For wholesale and interested Distributers and for more details contact:-
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mh. Dr. Jakaya Kikwete akionesha ilani za uchaguzi za CCM. Shoto ni ilani ya mwaka 2005 na kuume ni ilani ya uchaguzi mpya ambayo ni nene zaidiMh. Dr. Jakaya Kikwete akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Morogoro Mjini, bw. Abdulaziz Abood wakati akiendelea na kampeni zake mkoani Morogoro leo.
Mh. Kikwete akiwasalimia wananchi wa Mkoa wa Morogoro waliofurika katika uwanja wa Jamhuri mjini humo.
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM,Mh. Dr. Jakaya Kikwete akiwahutubia wanachama wa CCM pamoja na wapenzi wa chama hicho waliofika leo katika uwanja wa Jamhuri,mjini Morogoro.
Vuvuzela asilia likipuliwa na mmoja wa wakazi wa Morogogo.
Baadhi ya wazee wa mji wa Ngerengere wakimsikiliza mgomea urais kwa tiketi ya CCM,Mh. Dr. Jakaya Kikwete leo.
maandamano ya pikipiki wakatika wa kumlaki Mh. Kikwete mkoani Morogoro leo.
Kepteni John Komba akiwa sambamba na TOT wakitumbuiza katika uwanja wa Jamhuri,mjini Morogoro leo.
wengi walijitokeza kumsikiliza Mh. Kikwete leo.
Moja ya mabango ya Kampeni ya Mh. Kikwete.
Mimi kama mwenyekiti wa kamati ya ushindi kwa timu yetu ya Taifa (Taifa Stars) ninayofuraha kubwa kuwapa pongezi uongozi mzima wa timu yetu ya Taifa pamoja na wachezaji wetu kwa ushujaa waliouonyesha katika mechi yao dhidi ya Timu ya Taifa ya Algeria iliyochezwa siku ya Ijumaa tarehe 3/9/2010 ikawa ni kampeni za kuelekea katika kombe la mataifa ya Afrika.
Kwa nini nasema ni ushujaa? Ni kwa sababu ya kuweza kuonyesha mchezo safi ile hali kukiwa na uonevu ulioonekana wazi ukiwa na lengo la kukandamiza timu yetu isipate ushindi. Hakuna mtu yoyote ambaye aliyeshuhudia mechi hiyo atapingana nami eti kulikwa hakuna uonevu! Lakini matokeo tuliyoyapa yamedhihirisha ukomavu wetu katika soka la kimataifa, Pongezi zangu za dhati zimfikie kocha mkuu wa Jean Paulsen kwa kuweza kuwataarisha wachezaji kiakili ili kukabiliana vilivyo na hali hiyo ya uonevu na pia nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitampa pongezi nyingi Abdi Kassim (Babi) kwa goli zuri alilolifunga katika kipindi cha kwanza cha mchezo.
Vilevile tukumbuke haya yote ni matunda ya mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kuamua kuweka nguvu kubwa katika mchezo wa soka nchini naye pia nampa pongezi kubwa na ninafahamu naye anasheherekea pamoja nasi matokeo haya popote pale alipo.