(Picha na Aron Msigwa)
Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
Aug 31, 2010
KUTOKA JUKWAA LA SANAA,BASATA-FILAMU NA MAADILI YETU
FILAMU ZA KIBONGO MAADILI YAKE NI KIFO KWETU?
2. Kunakiri (copying) kazi za wasanii wa Nigeria na kutumia muziki (Sound Tracks) za wasanii wa muziki bila idhini yao.Katika haya wasanii wa Filamu wameshauriwa kuwa makini kwani sheria ya Hakimiliki inaweza kuwafunga.Kwa ujumla wasanii walishauriwa kuwekeza ubunifu binafsi na kubeba uhalisia wa sanaa yetu badala ya ilivyo sasa ambapo filamu zetu zimekuwa zikifanana fanana na zile za Nigeria.
3. Uchafu wa Filamu-Wadau wengi wamesema kwamba, filamu za kibongo zimekuwa na maadili mabovu yanayotokana uvaazi wa vichupi kwa wasanii wa kike, uoneshaji wa matendo ya faragha (mapenzi) mara kwa mara, script zenye kushabikia matendo maovu na yasiyofaa kwa jamii nk.Wadau walishauri Bodi ya Filamu, vituo vya TV na wasanii wenyewe kuhakikisha wanadhibiti filamu zisizo na maadili kwani zimekuwa zikitia aibu/kichefuchefu.Ilielezwa kwamba, baadhi ya filamu hazibebi uhusika wenye ufanano na maisha/maadili ya kitanzania.
JUMATATU IJAYO KWENYE JUKWAA LA SANAA
Mchango wa Kituo cha Utamaduni cha Kimataifa cha Ufaransa na Ubalozi wa Ufaransa Katika Ukuzaji wa Sanaa na Utamaduni Wetu.Tutakuwa na Wataalam kutoka Ubalozi wa Ufaransa.USIKOSEKANE.
Picha/Habari na Afisa Habari wa BASATA,
Alistide Kwizela
TENDWA KUTOA MAAMUZI PINGAMIZI LA CHADEMA BAADA YA SIKU TANO!

Msajili wa Vyama Vya Siasa Nchini John Tendwa amesema atatoa uamuzi wake dhidi ya malalamiko yaliyowasilishwa ofisini kwake jana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA)kuhusu mgombea wa urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM) baada ya siku tano.
Bwana Tendwa ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari hayo ofisini kwake jijini Dar es salaam baada ya kupokea malalamiko hayo rasmi leo.
‘’Nitatoa maamuzi hayo baada ya kupokea maelezo kutoka kwa mlalamikiwa dhidi ya malalamikaji yaliyowasilishwa,na nitatoa nakala ya maamuzi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi na Katibu Mkuu wa chama cha CHADEMA’’,Alisema Tendwa.
Akifafanua suala hilo Tendwa amesema baada ya maamuzi yake mlalamikaji na mlalamikiwa kama hawataridhika na uamuzi wake wanayo haki ya kwenda kutafuta haki yao kwenye vyombo vya sheria.
Aidha Msajili huyo Vyama ameongeza kuwa amepokea malalamiko hayo kwa mujibu wa sheria ya gharama za uchaguzi inachomkataza mgombea yeyote ambaye yeye mwenyewe, wakala wake au Chama chake kitafanya kitendo ambacho kimekatazwa kama ilivyoelekezwa kwenye sheria hiyo atakuwa au kitakuwa kimepoteza sifa za kushiriki mchakato wa uteuzi au uchaguzi.
Pingamizi hilo liliwasilishwa jana ofisi ya masajili huyo na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika wakimlalamikia Mgombea urais wa chama cha mapinduzi Jakaya Mrisho Kikwete kutumia madaraka yake kutoa ahadi kwenye kampeni na kutangaza nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi wakati wa kampeni.
WAREMBO VODACOM MISS TANZANIA WAELEZWA FAIDA ZINAZOTOKANA NA BIDHAA ZA VODACOM!!


PRECISION AIR YAZINDUA NDEGE MPYA !!




Designers visiting the Textile Sector Development Unit
Dr. Bilal Aendelea na ziara ya kampeni masasi na nayumbu!!!





tano Wa Marais Wastaafu Wafanyika Jijini Dar
(Picha na Aron Msigwa)
Aug 29, 2010
Chama cha NCCR Mageuzi chazindua ilani yake ya uchaguzi

VODACOM YAFUTURISHA PANGANI NA KUGAWA MISAADA YA CHAKULA KWENYE MADRASA!!

Mtoto Bwaga Abdallah akipokea mfuko wa sukari kutoka kwa Maafisa wa Vodacom Foundation Grace Lyon kulia na Mwamvua Mlangwa wa pili kutoka kulia huku akisaidiwa na Sheikh Mohamed Khalili kushoto kutoka Tanga mjini na Sheikh Khamis Rashid Mwakilishi wa Sheikh wa Pangani wa pili kutoka kushoto, katika msaada huo pia Vodacom Foundation iligawa Mchele, Maharage, mafuta ya kula pamoja na vifaa vya shule.

CUF wazindua kampeni zaao


Rais Kikwete Awasili Mkoani Mbeya
Dr.Bilal aendeleaa kuinadi ilani ya CCM mkoani mtwara




Rais Kikwete apokelewa kwa shangwe sumbawanga na mpanda
Wanachi wa mji wa Sumbawanga wakiwa wamefurika ndani ya Uwanja wa Mandela kumsikiliza Rais Jakaya Kikwete wakati akiwahutubia.