May 16, 2013

CHANONGO NDANI YA TAIFA STARZ AJIANDAA KUIKABIRI MOROCCO UGENINI

Na Boniface Wambura
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 16 mwaka huu) ametaja kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kujiwinda kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco.
Katika kikosi hicho, Kim ameita wachezaji wapya sita ingawa baadhi yao wamewahi kuchezea timu hiyo, huku akiacha wengine watatu aliokuwa nao kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Morocco ambapo Taifa Stars ilishinda mabao 3-1.
Wapya aliowaita katika kikosi hicho kitakachoingia kambini Mei 20 mwaka huu, saa 1 jioni kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam ni Ally Mustafa, Vicent Barnabas, Juma Luzio, Haruna Chanongo, Mudhathiri Yahya na Zahoro Pazi. Wachezaji aliowaacha ni Shabani Nditi, Nassoro Masoud Cholo na Issa Rashid.
Kikosi kamili cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ambacho kabla ya kwenda Morocco kitapita jijini Addis Ababa, Ethiopia kucheza mechi ya kirafiki Juni 2 mwaka huu dhidi ya Sudan ni kama ifuatavyo;
Makipa ni nahodha Juma Kaseja (Simba), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar) na Waziri Salum (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Mudathiri Yahya (Azam) na Salum Abubakar (Azam).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Juma Luzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Zahoro Pazi (JKT Ruvu).
Kocha Kim amesema kikosi kitakachoingia kambini kitakuwa na wachezaji 24 ambapo Samata na Ulimwengu watajiunga na timu jijini Marrakech, lakini wachezaji atakaondoka nao Dar es Salaam kwenda Addis Ababa ni 22 ambapo ataacha kipa mmoja na mchezaji mmoja wa ndani.
Awali TFF ilikuwa imeitafutia Taifa Stars mechi ya kirafiki Juni 1 mwaka huu dhidi ya Algeria, Libya au Misri. Lakini baadaye Algeria ikasema itacheza na Togo, wakati Misri ilitaka mechi hiyo ichezwe Juni 4 jijini Cairo, jambo ambalo lisingewezekana kwa Stars kwani ina mechi ya mashindano Juni 8 mwaka huu.
Kwa upande wa Libya mechi hiyo ilikubaliwa ichezwe Tunis, Tunisia, Juni 2 mwaka huu. Lakini baadaye Libya ikataka mechi hiyo ichezewe jijini Tripoli ambapo TFF ilikataa kutokana na sababu za kiusalama.
Wakati huo huo: Taifa Stars imejitoa kwenye michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) it

akayofanyika nchini Zambia kuanzia Julai 2-26 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah amesema Stars ambayo iliingizwa katika michuano hiyo kama timu mwalikwa imejitoa kutokana na mwingiliano wa ratiba kati ya michuano hiyo na mechi za Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).
Amesema awali Tanzania ilithibitisha kushiriki michuano kwa matarajio kwamba Uganda ingekubali ombi la TFF la kubadilisha ratiba ya mechi za CHAN, lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda (FUFA) likagoma kwa vile kipindi ambacho kilipendekezwa lenyewe litakuwa na uchaguzi wa viongozi wao.
Taifa Stars itacheza na Uganda (The Cranes) katika mechi za CHAN ambapo mechi ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Julai 12-14 mwaka huu wakati ya marudiano itafanyika jijini Kampala kati ya Julai 26-28 mwaka huu.
Akizungumzia michuano ya COSAFA, Kocha Kim amesema angependa kushiriki michuano hiyo kwani ingekuwa kipimo kizuri kwa kikosi chake, lakini kwa sasa malengo makubwa ya Stars kwenye mechi za mchujo za Kombe la Dunia na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambayo fainali zake zitafanyika mwaka 2015.

Beyonce aandika barua ya kuomba radhi kwa kuahirisha show yake

BEYONCE amelazimika kuandika barua kwa mkono kuwaomba radhi mashabiki wake Ubelgiji baada ya kuahirisha show yake ya juzi.

tumblr_mmtnbfsSiA1rqgjz2o1_1280
Muimbaji huyo aliahirisha show yake ya Antwerp iliyo sehemu ya ziara yake ya dunia ya Mrs Carter kutokana na uchovu na kupungikiwa maji hali iliyokuza tetesi za kuwa ni mjamzito tena.
Queen Bey alipost picha hiyo kwenye ukurasa wake wa Facebook na website yake akiomba radhi.

SAKATA LA LADY JAY DEE LALETA WARAKA TOKA KWA WADAU. NAOMBA USOME KWA MAKINI NA UFIKIRI BAADA YA HAPO

Wadau wa huu muziki wameniomba pasipo ku-edit huu waraka wa kwanza kati ya 88 uende hewani. Ni waraka unazungumzia hali ya muziki na vita ya wasanii na wale wanaoitwa wanyonyaji wa muziki. Blog iko kwa kila upande, hivyo nauwakilisha kwenu waraka ambao mdau wake wameomba asitajwe kwa sasa..
WARAKA NAMBA 1(ZIPO 88) KILA WIKI UTAPATA WARAKA MMOJA-

Ni wazi na dhahiri kabisa kesi iliofunguliwa mahakamani dhidi ya Lady JayDee haina maana yoyote isipokuwa ni hofu ya mafisadi wa muziki nchini (Kusaga na Ruge) kwa kuwa waraka wa pili ulikuwa utoke tar 15 may na mwingine tar 17 may mwaka huu wa 2013.
Hapa la kujiuliza ni juu ya interview ya Rugen a kinachoendelea sasa,eti suala limefika mahakamani,kweli Kusaga na Ruge mmeweza kuthibitisha nyie ni mafisadi na mnamuaibisha Rais Kikwete ambaye nina uhakika anajua kuwa nyie ndio kikwazo kikubwa na hata Bungeni alishawahi kuzungumza kuwa alitoa studio na pango kumbe tatizo sio hilo,tujiulize wote kuna nini wanachoficha hadi kumtafutia kesi raia mwema asie na hatia?

Tena anaejitafutia rizki ambayo wao wanapigana nayo kwa kumkandamiza?
Huku wakitumia mabavu wakilindwa na baadhi ya viongozi wa serikali na waandishi ambao majina yao mtayapata kupitia nyaraka zinazokuja (zipo 88) na huu ndio wa kwanza.
Nimesikitika sana na njia pekee ya kuufahamisha umma juu ya ufisadi huu wa Ruge na Kusaga ni kuyaanika yote ambayo jamii na Viongozi wa Serikali kama mlikuwa hamjui sasa ndio wakati muafaka wa kuwajua watu hawa ambao kila kukicha ni kuimarisha ufisadi wao na kujipendekeza kwa Viongozi sambamba na watoto wao (mtajua mpaka majina yao)
Naanza kupatwa na wasiwasi nikijiuliza, endapo Lady JD angekuwa amegombana na msanii mwenzake mkubwa kama Prof Jay, Ray C au Juma Nature wanasiasa wangeingilia kati? Ni wazi wasingesogea kwa kuwa hakuna maslahi zaidi ya kuingilia mgogoro huu ambao hawataki jamii ijue maovu yao.

Napatwa mashaka jinsi wanasiasa wanavyolivalia njunga jambo binafsi
Kama hili na kulifanya ni la kiserikali basi tafuteni chanzo cha tatizo mjue ni sehemu gani sahihi ya kuanza kutatua kilichopo na sio kukimbilia kuunda vikao ambavyo naamini vimeshaitishwa vingi sana lakini hakuna kilichosaidia.
Wanasiasa badala ya kutafuta sababu zinazofanya wasanii wanalalamika mnakimbilia kutatua mgogoro wa Ruge na JD ili kusuluhisha mambo yasiendelee kuongelewa jamii ijue uovu wa mafisadi hawa.

Haitasaidia kwa sababu wanaojua maovu ya hawa mafisadi Rugen na Kusaga ni wasanii wengi wakubwa na watu wengine binafsi (kumbukeni waraka zipo 88)
Vijana mnaowategemea katika kampeni zenu na mnawaita Taifa la kesho, lakini mnakubali waendelee kukandamizwa na kunyanyasika huku wakizidi kuwaneemesha kina Ruge na Kusaga.
Tatizo mnalijua kaeni na wasanii wote wawaelezee matatizo yao, msikae na wasanii ambao wanaamrishwa na kina Ruge. Sikilizeni kilio cha wasanii wengine pia na itafutwe njia ya kupata maoni ya kila mmoja na kuachana na watu wengine ambao wanaendesha mtandao wa ufisadi chini ya kivuli cha Ruge (Fella na Babu Tale) ambao mtapata kujua kila kitu kuhusu ufisadi wao na kinachoendelea (kumbuka waraka zipo 88)

Ruge amekuwa ni tatizo na janga la Kitaifa katika tasnia ya muziki kwa ujumla, amekuwa akiwagawa wasanii kwa kutumia redio Cloudz kwa vitisho vya kutopigiwa nyimbo, au kwa danganyio la kufanyiwa promotion mpaka kwenye magazeti endapo tu utakuwa chini ya bawa lake.
Wasanii wamekuwa hawalipwi vizuri ili waendelee kumtegemea fisadi huyu.
Kwani wasanii wote wangekuwa na kipato cha kuweza kusimama imara leo hii kauli kama ya Lady JD ingezungumzwa karibu na kila mwanabongoflava.

Fredie Kavish (fisadi mwingine) ambae anasimamia Kili music awards yuko bega kwa bega na Ruge kudanganya wananchi nani ni bora katika tuzo hizo ili kulinda maslahi yao binafsi.
Na wao huchagua wale wasanii ambao hawana sauti za kudai haki yao ili wawatumie kadri wanavyotaka.Tuzo za Kili ni uozo mtupu.Imefikia wakati basata itoe vibali kwa wadau wengine wa muziki (nako kuna ufisadi)wasio na interest binafsi na wasanii wao, kuendesha hizi shughuli ili kukuza muziki.Kutokuwepo na tuzo zingine kunasababisha ionekane kuwa basata nao wamo kwenye mgao wa mabepari hao wanaoua sanaa ya Tanzania

JINSI RUGE NA KUSAGA WANAVYOTAWALA
Njia anayoitumia Ruge na Kusaga iko wazi, wao wana redio na hapo hapo wana wasanii wao.Hivyo promotion inabidi wafanyie wasanii wao ambao ni waoga ili waweze kuwatumia bila wasanii hao kufanya fyoko fyoko.
Wasanii wengine ambao sio chini ya Cloudz kwa kuwa hawana jinsi nyingine ya kupata hela inabidi wainyenyekee Cloudz wakiamini ndio njia pekee ya kuwapatia vipato
Huku wakisubiri show moja ya fiesta ya kila mwaka.
Huko katika fiesta kuna wengine wanalipwa mpaka laki tatu na bado katika hiyo ili upangwe kwenye list ya kupanda jukwaani B12 nae lazima akate laki moja yake.

Hapo msanii anabakiwa na nini akirudi nyumbani?
Hivi laki tatu ni nini kwa maisha ya msanii?
Njia pekee ya kuwatawala ni kuwafanya waendelee kuwa maskini.
Leo hii mtangazaji wa redio ana sauti kuliko msanii.
Kwanini redio zingine hazilaumiwi? Ni kwa sababu hazijihusishi moja kwa moja na wasanii.Hilo ni kosa kubwa sana linalofanywa na Cloudz au pengine ndio mtazamo wao walioamua kuufuata kwa sababu wanaamini Serikali ipo mikononi mwao.
Maisha na ajira za watoto wa watu ambao wengi hawajasoma wanategemea vipaji, mnayakatili bila huruma

Mwisho tumuombee Lady JD Mahakama imruhusu azungumze yote, kila mtu anataka kusikia sio siri Cloudz, Ruge na Kusaga ni nyonya damu.
Mahakama itambue kuwa wanaojua maovu ya Rugen a Kusaga sio Lady JayDee pekee ni wengi mno na kama njia ya kukimbilia mahakamani ndio wameichagua basi ongezeni mahakama kwa kuwa tupo wengi tutakuja kuyaongea kuhusu mafisadi hawa wa Cloudz (siku hizi wanaitwa wafu)
Hela ina nguvu hata palipo na haki, JD hajatukana matusi na amekuwa makini katika kutoa kauli zake sasa anashitakiwa kwa kosa gani? Anashitakiwa kwa kudai haki yake. Anaconda wewe songa na sisi tunakuja kizimbani na sasa ndio TANZANIA itawajua Ruge na Kusaga ni kina nani na walianzia wapi,walikuwa wapi,wako wapi na nani wanaoshirikiana nao,

JIPANGENI!
MDAU.

MASTER JAY TUZO ZA KILIMANJARO MUSIC AWARDS ZINALENGO LA KUDHALILISHA



MTAYARISHAJI nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini, Joachim Kimario 'Master Jay' amesema amekosa imani na Tuzo za Kilimanjaro Music, kwa kuwa zinalengo la kuwadhalilisha baadhi ya wasanii.

Master jay amekosa imani kumetokana na Kamati ya Kilimanjaro Academia ambayo imepewajukumu la kuchagua wasanii kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho kukosa sifa.

Akizungumza Dar es Salaam, Master Jay alisema tatizo linaanzia kwenye kamati hiyo kuchagua wasanii waliokosa sifa na vigezo, huku ikiwa haiko wazi kwa wadau pamoja na wasanii ambao ni washiriki wa tuzo hizo.

Alisema watu waliochaguliwa kwenye kamati hiyo, wamekosa uelewa wa muziki na ndiyo maana wanachagua baadhi ya wasanii waliokosa ubora na kusababisha kupoteza imani ya tuzo hizo kwa jamii nzima.

Mtayarishaji huyo alisema ndiyo maana baadhi ya wasanii wanajitoa kwenye kinyang'anyiro hicho kwa kuogopa kudhalilika.

"Sijui ni akina nani wanaounda kamati hiyo kwani imepoteza sifa na ndipo tatizo linapoanzia hapo kila mwaka, kukosa uelewa kwenye kamati hiyo na kutokuwa na uwazi kunachangia malalamiko ya kila siku kwa baadhi ya wadau wa muziki.

"Baadhi ya wasanii wanalalamika sana kuhusu tuzo hizi na ndiyo maana wengi wanajitoa, si kwamba wanajitoa kwa kuogopa kushindana hapana bali kudhailika kwani hizi tuzo sasa zinadhalilisha baadhi ya wasanii," alisema Master Jay

Hata hivyo aliwapongeza kwa kuongeza vipengele vingine kwenye tuzo hizo, ambapo mwaka jana kulikuwa na vipengere 29 na sasa vimeongezwa na kuwa 32.

"Kila mwaka wanapiga hatua 10 mbele na kurudi hatua 30 nyuma, hali ambayo inaonesha hakuna maendeleo yoyote kwenye upande wa tuzo hizo, hivyo wanahitaji marekebisho ili kuwe na usawa na kurudisha imani ya tuzo hizo kwa wasanii," alisema Master Jay.

Kwa upande wake Mratibu wa tuzo hizo kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Angelo Luhala alisema tatizo lipo kwa waandaaji ambao ni Kampuni Bia Tanzania (TBL) kushindwa kutoa elimu ya kutosha kwa wadau wote wa muziki nchini.

Alisema TBL inatakiwa kuelimisha umma kujua kazi ya Kilimanjaro Academia, inavyofanya kazi pamoja na mchakato mzima wa tuzo hizo zinavyokwenda, ili kuepuka ulalamikaji unaojitokeza kwa baadhi ya wadau wa muziki.

"Elimu ikitolewa kwa washiriki pamoja na wadau wa muziki, imani itarudi kwenye tuzo hizo na watajua mchakato mzima unavyofanyika hivyo uwazi wa jambo hilii ndiyo utapunguza malalamiko katika tuzo hizo," alisema Luhala.

Sep 6, 2012

HUYU NDIO MWANDISHI ALIEJISALIMISHA POLISI MWENYEWE KATI YA WALE WATATU WALIOTANGAZWA KUSAKWA BAADA YA KIFO CHA MWANGOSI.

Kwa sababu za kiusalama ilikua picha yake isiwekwe hapa lakini yeye mwenyewe ameidhinisha iwekwe kwa sababu haogopi, Francis Godwin ni huyo mwenye nguo nyeusi.
Siku mbili baada ya kifo cha mwandishi mwenzao wa habari (Daudi Mwangosi) aliefariki kutokana na kulipukiwa na bomu akiwa mikononi mwa polisi waliokuwa wanatawanya wafuasi wa Chadema huko Iringa, mwandishi wa habari Francis Godwin ambae alikua rafiki wa marehemu amejisalimisha polisi kufata masharti ya taarifa iliyotolewa kwa yeye na wenzake wawili kusakwa na polisi.
Exclusive na millardayo.com namkariri Godwin akisema “kutokana na hali halisi ya kushuhudia tukio la mauaji ya Mwangosi, nilifukuziwa kwa nyuma na gari lisilokua na namba pia nilipofika nyumbani niliambiwa kuna watu walikuja kuniulizia lakini hawafahamiki, na taarifa zikatoka kwamba tunasakwa”
Kuhusu kujisalimisha, Godwin amesema aliamua kufanya huo uamuzi baada ya kusikia taarifa za kusakwa kwake pamoja na waandishi wengine wawili, jana (september 5) aliamua kujisalimisha mwenyewe Polisi akiwa amesindikizwa na waandishi wa habari kama hamsini ambapo baada ya kufika pale walikutana na  kamishna wa makosa ya jinai Tanzania Robert Manumba ambae ilibidi ahoji polisi Iringa kama ni kweli wanamtafuta Godwin na wenzake.
.
Namkariri Godwin akisema “baada ya kumuuliza mmoja kati ya maofisa wake kama ni kweli wanamtafuta Godwin ofisa huyo alijiumauma na baadae akasema hatumtafuti, baada ya hapo waandishi wa habari tulisimama tukaondoka kwa sababu ya kutokubaliana na kilichotaka kuendelea kuhusu taarifa ya uchunguzi ya Manumba”
Kingine kilichoendelea baada ya hapo ni Club ya waandishi wa habari Iringa kuziomba redio mbalimbali za iringa ambazo zimekua zikirusha matangazo ya polisi jamii kusimamisha matangazo hayo ambapo wamiliki wa vyombo hivyo wamekubali ombi.
Francis Godwin ambae alikua karibu na marehemu Daudi Mwangosi muda mfupi kabla ya kuuwawa kwa bomu amesema “Nilijua kwamba mimi ni miongoni mwa waandishi watatu wanaotafutwa kwa sababu marehemu kabla ya kifo akiwa amekamatwa nilitaka kwenda kumuokoa pale lakini nilipokua namsogelea Daudi akaniambia Godwin mdogo wangu kimbia… wakati nakimbia kama hatua 20 mbele nyuma nageuka nasikia mlipuko mkubwa, kuangalia ni Wangosi amekufa na nilibahatika kupiga baadhi ya picha ambapo askari waliokuwepo walipoona narudi kwenye eneo hilo walinionyeshea bunduki ikabidi ninyooshe mikono juu kwamba jamani mimi nakuja kwa heri wakaniambia potea”
Muda mfupi baada ya Marehemu Daudi kulipukiwa na bomu.
Godwin amesema baada ya kugeuka na kuanza kukimbia walianza kumfukuzia ila bahati nzuri gari yake ilikua mbali, baada ya kutishwa na polisi walipokwenda hospitali ulipopelekwa mwili wa marehemu ilibidi waanze kutoa mabango ya wanahabari yaliyobandikwa kwenye gari yao pamoja na kutoa namba za gari, alianza safari ya kuondoka lakini kuna gari zilikua zinamfukuzia kwa nyuma mpaka alipofika nje kidogo ya mji wa Iringa na kuingia mitaani ndio akafanikiwa kukimbia.
Kwenye sentensi ya mwisho Godwin anasema ameibiwa siri na askari mmoja ambae alimwambia kuhusu kutafutwa kwake yeye na waandishi wa habari awengine mbapo alimuonya kwamba msimamo na kauli aliokua ameutoa pamoja na ushahidi wa tukio la mauaji ndio vimefanya atafutwe.

MAGAZETI YA TRH 6/9/12

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

ALICHOSEMA PRODUCER MANECK BAADA YA KUONA DOGO JANJA ANATAKA KUMGOMBANISHA NA MARCO CHALI.

.
Producer Maneck ambae ni mshindi wa tuzo kwenye KTMA 2012 ameamua kuzungumza ya moyoni kwa kuijibu kauli Dogo Janja aliyoitoa kwamba Producer huyo kauponda uwezo wa Marco Chali.
Ishu ilianza wakiwa club Maisha Dar es salaam jumapili iliyopita ambapo Dogo Janja anadai alikwenda sehemu ya V.I.P na kumsalimia Maneck ambae hakujibu salamu ila aliporomosha matusi mazito kwa Dogo Janja pamoja na kumpiga biti kwamba asimsogelee.
Baada ya hapo Dogo Janja akashuka chini kwenda kumwita meneja wake wa WATANASHATI ambae ni Ustaz Juma ambapo kwa maelezo ya Dogo Janja, Maneck alianza kuiponda single mpya ya Dogo Janja na PNC waliyoirekodi kwa Marco Chali ambayo mwanzoni ilikua irekodiwe kwa Maneck alieiponda kwa kusema ni ya kawaida sana kwa sababu imefanywa na Marco Chali.
Jibu alilolitoa Maneck baada ya kusikia kwamba Dogo Janja amenukuliwa kwa hayo maneno, namkariri akisema “ndio ninavyokwambia sitakagi watu masnich kama huyo, Marco Chali ni mtu ambae namfil sana anafanya kazi nzuri, siwezi kuongea kitu kibaya kwa Marco kwa sababu leo na kesho nitamfata nitamuomba msaada wa kitu chochote kile hata material sasa nitawezaji kusema hivyo kwa mfano sasa, Dogo Janja ni mtu ambae anataka tu kufanyaga vitu watu wapishane kauli mambo ya kijinga ni utoto akikua nadhani ataacha hizo tabia zake, na ndio maana nikamwambia kaa mbali sitaki uongee na mimi that’s all”(kwa hisani ya www.millardayo.com)

MBWANA SAMATTA - THE KING IN THE MAKING


Hili ni moja ya bango la kumsifia Mbwana Samatta lilochorwa na washabiki wa Mazembe

Huyu ni shabiki wa Mazembe akiwa na jezi yenye jina la Samatta

Kama Spain -vile ni vigari maalum kubebea wachezaji wanaoumia uwanjani katika uwanja wa TP Mazembe

Mbwana Samatta mwenye jezi namba 15 akiwa anapigwa konga na beki wa Al Ahly

Huyu ndio mshabiki aliyevaa jezi yenye jina la Samatta

Mfalme wa Mazembe Tresor Mputu akiwafanyia balaa waarabu

Kidiyaba ndani ya uzi wake wa golikipa

Majembe ya Kitanzania Thomas Ulimwengu na Mbwana Ally Samatta wakiwapeleka puta mabeki wa Al Ahly katika mechi ya robo fainali ya kombe la mabingwa wa Afrika iliyofanyika juzi jumapili.(kwa hisani ya www.shaffihdauda.com)

MATUMIZI MABAYA YA FEDHA YANAVYOTISHIA KUMFILISI MWANASOKA NEYMAR


Hakuna ubishi juu ya kipaji alichonacho mwanasoka wa kibrazil Neymar .
Neymar kwa sasa sio tu mwanasoka anayependwa sana kuliko wote nchini Brazil, bali pia ni tumaini kubwa la kuiwezesha nchi hiyo kutwaa kombe la dunia mwaka 2014, ambalo litafanyika katika taifa hilo la bara la Amerika ya kusini.


Ameelezewa na Pele, ambaye anatajwa kama mwanasoka bora kabisa kuwahi kutokea katika historia ya mchezo huo - kuwa na mtaalam wa soka, mwenye miguu ya majaabu, huku akiwa na umri wa miaka 20. Lakini kipaji cha Neymar uwanjani ni tofauti kabisa na akili yake linapokuja suala la matumizi ya fedha. Anatengeneza fedha nyingi sana lakini anatumia karibu na chote anachoingiza.


Gari aina ya Porsche Panamer
 Ndani ya miaka miwili tu, Neymar ameripotiwa kununua jumba ambao ndani lina nyumba zingine tatu tofauti kwa $750,000 na hekalu lingine lenye thamani ya $2million - zote zikiwa kwenye eneo la pwani ya kaskazini ya jiji la Sao Paolo; pia amenunua flat yenye thamani ya $150,000 hapo hapo Sao Paolo. Amenunua gari aina ya Porsche Panamera Turbo yenye thamani kati ya $400,000 mpaka $550,000.  Pia alimpa mama wa mtoto wake mwenye umri wa miaka 18 Apartment iliyo kwenye moja ya majengo marefu pale Santos ambayo ina thamani ya $1,000,000 - huku akiwa anatoa $15,000 kwa mwezi kwa ajli ya malezi ya mtoto. Lakini kubwa kuliko ni pale aliponunua boti ya kifahari ambayo hata baadhi ya matajiri wakubwa duniani hawana - yenye thamani ya $8 million, ambayo gharama yake ya matengenezo na services kwa muda ni kiasikisichopungua $120,000 kwa mwaka.

Yatch ya Neymar
Ingawa hakuwemo kwenye listi ya wanasoka wanaolipwa fedha nyingi duniani ambayo ilitolewa na jarida la Forbes la Marekani mwezi wa nne mwaka huu huku nafasi ya kwanza ikishikwa na David Beckham, Neymar anarudi nyumbani kwa mwaka na mshahara wa $4million kwa mwaka kutoka Santos, kalbu yake ya kibrazil ambayo ana mkataba nayo mpaka 2014. Shukrani kwa dili za udhamini kutoka Nike ($1 million kwa mwaka) na Red Bull na dili nyingine kutoka kwenye makampuni kadhaa ya kibrazil ambayo yanamfanya Neymar apeleke benki kiasi kingine cha fedha kipatacho $4 million kwa mwaka - kwa maana hiyo ingizo lake lote kwa mwaka ni $8million. Fedha hizi ni kidogo ukilinganisha na wanasoka wengine wakubwa kama Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Kaka na hata Beckham , ambao wote wanatumia fedha zao vizuri sana. Kwa mfano Beckham ambayo yeye hupendelea kukodisha boti ya kifahari kwa maana ya kupunguza gharama nyingi za kununua na kuihudumia boti hiyo.

Neymar na mwanae ambaye anamgharimu zaidi ya $15,000 kwa mwezi kumlea.
Miezi kadhaa iliyopita vyombo vya habari vya Brazil vilikuwa vinapotosha na kusema kwamba Neymar anaingiza kiasi cha $18 million kwa mwaka, jambo ambalo lilikuja kuonekana sio sahihi pale alipoanza kufanya mazungumzo mapya juu ya mahitaji yake kwenye mshahara mpya na klabu yake ya Santos. Kwa maana hiyo Neymar bado hajaweza kuingiza fedha nyingi kiasi cha kuweza kununua matoi  ya kuchezea kwa matajiri kama boti za Yatch.
"Kiukweli anatumia fedha nyingi sana karibu na kile chote anachoingiza," anasema mtaalam wa mambo ya fedha wa jarida la Forbes bwana Settimi huku akisisitiza lazima klabu yake itakuwa inamsaidia kwa kumpa fedha nyingine nje ya mkataba wake. 


"Inawezekana Santos wana mkono wao kwa sababu ukiangalia matumizi yake ndani ya kipindi cha miaka miwili iliyopita unaona kwamba ametumia zaidi ya kile alichoingiza - kuna taarifa zinasema klabu yake inampa fedha nyingi hata nje ya mkataba ili kumridhisha na kumfanya asahau kwenda barani ulaya."

Mhariri mkuu wa jarida la Forbes Kurt Badenhausen anamfananisha Neymar na Mike Tyson: " neymar ndio kwanza anakuwa na anatengeneza fedha nzuri sana.  Kama ilivyokuwa kwa Tyson ambaye nae alianza kutengeneza fedha akiwa na miaka 18 na miaka kadhaa baadae alikuwa na utajiri wa $400 million - hivi ndivyo nahisi Neymar akavyokuwa ikiwa itaacha kutumia vibaya fedha zake."


Mike Tyson akiwa kwenye kiwango cha juu, pambano lake moja alikuwa akitia ndani kiasi cha $30 million. Lakini wakati wa kipindi hicho, Tyson alinunua mahekalu, magari ya kifahari, chui wa kufuga. Mwishoni mwa mwaka 2002,  aliingia kwenye duka la kuuza vito na kununua cheni ya dhahabu yenye thamani ya $174,000 huku ikiwa imenakishiwa na almasi kiasi. Miezi nane baadae Tyson akatangaza kufulisika huku akiwa na madeni yanayofikia $23 million.


Watu wengine maarufu ni kama vile star wa NBA Antoine Walker, ambaye alitengeneza zaidi ya $110 million wakati akicheza bado, na Evander Holyfield, wote wamefilisika.


Mfano mwingine mzuri haupo mbali na yeye. Nchini Brazil mwanasoka Romario, ambaye  alikuwa mchezaji muhimu sana kwa Brazil katika fainali za kombe la dunia 1994, alikamatwa mwaka 2009  kwa kesi ya kushindwa kutoa fedha ya malezi ya mtoto. Huku akiwa na deni linalofikia $5 million.


Neymar anatakiwa kufuata mfano wa gwiji wa soka wa nchi hiyo Ronaldo De Lima ambaye aliwekeza fedha zake vizuri. Ronaldo sasa hivi anamiliki asilimia 45 za kampuni ya 9ine Sports and Entertainment  Agency, kampuni inayodili na masuala ya soka, ambapo moja ya wateja wao ni Neymar.


Shukrani kwa 9ine inayofanya vizuri sana kwenye biashara zake, Ronaldo de lima sasa ana thamani ya utajiri unaofikia $250 million. Kwa maana hiyo Neymar itabidi afuate nyayo za huyu jamaa ili aweze kuwa na mafanikio miaka kadhaa ijayo, na sio kufuata nyayo za Romario na akina Tyson.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA