Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Dodoma mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Dodoma leo kwa ajili ya kukutana na Rais Jakaya Kikwete ikiwa ni maandaliazi ya kuunda Serikali mpya ya awamu ya pili ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete ambapo kesho jina la Waziri Mkuu linatarajiwa kutajwa. Picha na Muhidin SufianiNi globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
Nov 16, 2010
Aneth Kushaba Arejea Nyumbani
Aneth Kushaba Arejea Nyumbani
MAKAMU WA RAIS DR. MOHAMMED GHARIB BILAL AWASILI DODOMA KUSAIDIANA NA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE KUUNDA SERIKALI
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Dodoma mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Dodoma leo kwa ajili ya kukutana na Rais Jakaya Kikwete ikiwa ni maandaliazi ya kuunda Serikali mpya ya awamu ya pili ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete ambapo kesho jina la Waziri Mkuu linatarajiwa kutajwa. Picha na Muhidin SufianiGrand Malt kudhamini Tamasha la Wanavyuo Vya Elimu ya Juu



Nov 12, 2010
SITTA AAPISHWA NA ANNA MAKINDA KUWA MBUNGE
RAIS KIKWETE AMPONGEZA ANNA MAKINDA KUSHINDA USPIKA WA BUNGE
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
MBIO ZA VODACOM MWANZA CYCLE CHALLENGE ZATIMUA VUMBI UPANDE WA "WALEMAVU" LEO
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Said Ally Amanzi, akiinua bendera kama ishara ya uzinduzi rasmi kwa mbio za Vodacom Mwanza Cycle Challenge kwa upande wa walemavu,zilizofanyika leo katika.
Afisa udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude(kushoto) na Mtaalamu wa Mambo ya Habari wa kampuni hiyo Matina G. Nkurlu wakiwavalisha namba za ushiriki wa mashindano ya Vodacom Mwanza cycle Challenge kwa upande wa wanawake walemavu kabla ya mashindano hayo kuanza.
Mshindi wa mashindano ya Vodacom Mwanza Cycle Challenge Helena Mwendesha (48) kwa upande wa wanawake walemavu akimalizia mbio hizo na kuibuka mshindi kuwa mshindi wa kwanza kwa kutumia dakika 40:27 kwa kilometa 10.
Mshindi wa mashindano ya Vodacom Mwanza Cycle Challenge Omary Matangajo(37) kwa upande wa wanaume walemavu akimalizia mbio hizo na kuibuka mshindi kuwa mshindi wa kwanza kwa kutumia dakika 42:48:02 kwa kilometa 15.
Washiriki wa mashindano ya Vodacom Mwanza Cycle Challenge wakichuana vikali katika mbio hizo.
Maafisa usalama barabarani Mkoa wa Mwanza wakiweka mikakati ya kudhibiti hali ya usalama barabarani wakati wa mashindano ya Vodacom Mwanza cycle Challenge kwa walemavu kabla ya mashindano kuanza rasmi.Akizungumza na Waandishi wa habari jana, Ofisa Matukio na Udhamini wa Vodacom, Rukia Mtingwa alisema taratibu za mashindano hayo zimekamilika kwa kiasi kikubwa ambako taratibu za usalama zimekamilika sambamba na masuala mengine yanayohusu mashindano.
Mtingwa alisema wakazi wa maeneo zinapofanyika mbio hizo ambako wajitahadhari na ajali kutoka kwa wakimbiaji watakaoshiriki mashindano hayo.
Aidha mbali ya mashindano ya leo, katika mashindano ya walemavu yaliyofanyika jana, bingwa wa mwaka jana kwa alemavu wa kiume, Omar Matangajo wa Sengerema alinyakua kwa mara nyingine sh 400,000 baada ya kutumia dakika 42:48.02 ambaye alishiriki mbio za umbali wa Kilomita 15 wakati mshindi wa pili Sayuda Pigi alitumia dakika 44:03.33 ambaye alinyakua sh 250,000.
Kwa upande wa wanawake bingwa wa mwaka jana Hellena Mwendesha wa Igoma alinyakua kwa mara nyingine nafasi ya kwanza baada yakutumia dakika 40.27 na kupata sh 400,000 wa pili ni Elizabeth Kishiwa wa Igoma ambaye alitumia dakika 41.29 na unyakua sh 250,000 na wa tatu ilikwenda kwa Exaverina Exavery wa Isamilo alitumia dakika 46.02 na kunyakua sh 150,000.
Katika mashindano hayo walipata matatizo barabarani ni Emmanuel Matiku wa Isamilo ambaye alipata kizunguzungu akiwa mashindanoni na Shija Kidesheni wa Mbagala Dar es Salaam aliharibikiwa pedal zake mashindanoni.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Said Ally Amanzi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya leo ambako pia jana ndiye alikuwa mgeni rasmi akimwailisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandooro ambaye yuko bungeni Dodoma.
NayeKatibu Mkuu wa Chama cha Baiskeli Tanzania (CHABATA),Lado Haule alisea mikoa zaidi ya 15 imejitokeza kuwania taji la mashindano hayo ni wenyeji Mwanza, Arusha, Shinyanga, Dodoma, Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Iringa,
Mshindi wa kwanza wa mashindano hayo kwa wanaume atazawadiwa sh 1500,000, wa pili atajitwalia sh 1000,000 wa tatu atazoa sh 700,000, mshindi wa ne hadi wa 10 kila mmoja atapata sh 500,000 na wa 11-30 kila mmoja atapata sh 250,000 na kuanzia wa 21 hadi 30 kila mmoja atapata sh 90,000.
Kwa upande wa wanawake mshindi atapata sh 1100,000 wa pili sh 800,000 wa tatu sh 600,000, wa nne hadi 10 kila mmoja atapata sh 350,000, wa 11-20 kila mmoja atazawadiwa sh 130,000 na kuanzia wa 21-30 kila mmoja atajitwalia sh 70,000.
Wadhamini wa mashindano hayo ni Knight Support kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi sambamba na Alphatel.
Nov 11, 2010
chenge,sitta kimenuka uspika

Matokeo hayo yamewatupa nje wagombea wanaume walioomba nafasi hiyo kupitia CCM wakiwemo mahasimu wawili Samuel Sitta aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa na Andrew Chenge. Wanachama 13 wa CCM waliomba kuteuliwa kuwania nafasi hiyo nyeti katika Bunge ambacho ni chombo cha juu cha kutunga sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba alisema wamechukua uamuzi huo wakizingatia kuwa umefikia wakati wanawake waongoze vyombo vya dola.
"Watanzania wote wanafahamu utendaji wa Spika aliyepita hatuna tatizo naye, lakini chama chetu kupitia Kamati Kuu kimeona kuwa umefika wakati wa wanawake kupewa muhimili japo mmoja wa dola," alisema Makamba.
Spika aliyemaliza muda wake Samuel Sitta akisalimiana na Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati kuu ya CCM mjini Dodoma.
Kupitishwa kwa akina mama hao ambao wanaonekana kuwa na uzoefu wa aina tofauti katika siasa ndani na nje ya CCM, kunakipa chama hicho changamoto kubwa katika kuongoza Bunge la 10 ambalo lina wabunge wengi wa upinzani na wenye uwezo mkubwa tofauti na ilivyokuwa katika mabunge yaliyopita.
Mara baada ya kutolewa taarifa hizo umati watu waliouwa wamefika katika mkutano huo uliofanyika katika jengo Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma walinyong'onyea, huku baadhi yao wakisema mapendekezo ya kamati kuu ni tofauti ya matarajio yao.
Chini ya Sitta, Bunge lililopita liliweza kuonyesha dhahiri uwezo wake kwa kuzingatia Sheria na kutoa maamuzi yalioongeza demokrasia bungeni.
Awali mahasimu wawili waliokuwa wakiwania kiti cha uspika, Chenge na Sitta walionekana kuficha uhasama wao kwa kukumbatiana mbele ya wajumbe wa Kamati Kuu walipokuwa ukumbini.
Kikao cha Kamati Kuu kilichokutana kwa ajili ya kuteua majiba ya wanaowania uspika kupitia CCM kilianza saa 9:25 za jioni na kilihudhuriwa na wajumbe 35 kati ya wajumbe 39 waliotakiwa kushirikia katika kikao.
Chenge aliyekuwa amekaa na Makinda kwenye ukumbi wa mkutano alikuwa wa kwanza kumuita Sitta alipoingia ukumbini.
Sitta alipoingia ukumbini aliwasalimia wajumbe wa mkutano huo kwa kuwapungia mkono, lakini Chenge alimuita kumtaka wasalimiane kwa karibu naye bila ya kusitaalikwenda katika kiti wakasalimiana na kukumbatiana.
“Haya ni mambo ya kawaida naona waandishi wa habari wanataka kuchukua na picha wakidhani kuwa ni jambo kubwa. Ndani ya CCM hivi ni vitu vya kawaida tu,” alisema Sitta.
Kikwete aliwaambia wajumbe wa kamati hiyo kuwa kikao kilikuwa ni halali kwani kilihudhuriwa na wajumbe wengi na kuwataja walishindwa kuhudhuria kuwa ni Benjamin Mkapa, Dk Salmin Amour pamoja na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambaye hata hivyo, cheo hicho hakipo kwa sasa.
Kabla ya mkutano huo kuanza katibu wa CCM, Yusufu Makamba alimuita Naibu Katibu Mkuu, Kapteni George Mkuchika na kuteta naye kabla ya kumuita Katibu wa Itikadi na Uenezi, Kapteni John Chiligati amba walisimama kwa dakika kadhaa kisha wakaingia kwenye chumba alichokuwepo mwenyekiti Jakaya Kikwete.
Kikwete aliingia katika kikao hicho akiongozana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa, Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Aman Karume, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassani Mwinyi na Waziri MKuu Mstaafu, John Malecela.
Baada ya kikao kufunguliwa hicho Mwenyekiti wa CCM aliwaambia wajumbe kuwa cheo kilichokuwa cha Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hakipo tena hivyo nafasi hiyo itachukuliwa na makamu wa pili wa rais.
“Hapa katiba haisemi hivyo, lakini huu ndio ukweli kuwa cheo cha Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hakipo tena, hivyo naamini kuwa nafasi hiyo inatakiwa kuchukuliwa na Makamu wa Pili wa Rais ingawa,” alisema Kikwete.
chanzo-global publisherz
Dr. Bilal awasili Dodoma tayari kwa kuhudhuria mkutano wa kamati ya halmashauri kuu
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na wazee wa mkoa wa Dodoma, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Dodoma leo Nov 10, ikiwa ni ziara yake ya kwanza kufanya mkoani hapa tangu apate wadhifa huo. Kiongozi huyo atakuwa mkoani hapa kuhudhuria mikutano ya CCM katika ngazi za Kamati Kuu na Halmshauri Kuu na kisha sherehe za kuapishwa wabunge sambamba na uteuzi wa Waziri Mkuu.
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwasalimu wananchi wa mkoa wa Dodoma, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Dodoma leo Nov 10, ikiwa ni ziara yake ya kwanza kufanya mkoani hapa tangu apate wadhifa huo. Kiongozi huyo atakuwa mkoani hapa kuhudhuria mikutano ya CCM katika ngazi za Kamati Kuu na Halmshauri Kuu na kisha sherehe za kuapishwa wabunge sambamba na uteuzi wa Waziri Mkuu
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asli ya Kabila la Wagogo baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa mjini Dodoma leo Nov 10, ikiwa ni ziara yake ya kwanza kufanya mkoani hapa tangu apate wadhifa huo. Kiongozi huyo atakuwa mkoani hapa kuhudhuria mikutano ya CCM katika ngazi za Kamati Kuu na Halmshauri Kuu na kisha sherehe za kuapishwa wabunge sambamba na uteuzi wa Waziri Mkuu.
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwasalimu wazee wa mkoa wa Dodoma, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Dodoma leo Nov 10, ikiwa ni ziara yake ya kwanza kufanya mkoani hapa tangu apate wadhifa huo. Kiongozi huyo atakuwa mkoani hapa kuhudhuria mikutano ya CCM katika ngazi za Kamati Kuu na Halmshauri Kuu na kisha sherehe za kuapishwa wabunge sambamba na uteuzi wa Waziri MkuuNov 9, 2010
LEO NDO LEO USPIKA KWA TIKETI YA CCM
Wanachama 13 wamejitokeza ndani ya CCM wakisaka kuteuliwa kuwania nafasi hiyo nyeti katika Bunge ambacho ni chombo cha juu cha kutunga sheria.
Kikao hicho cha CC, kinafanyika wakati mpasuko ulioundiwa kamati maalumu ya mzee Ali Hassan Mwinyi, ukiwa na kila dalili ya kurejea upya baada ya mmoja wa wagombea uspika Andrew Chenge, kuibuka hadharani na kugusa majeraha ambayo yamekuwa yakishughulikiwa na Waziri Mkuu.
Makombora hayo ambayo Chenge aliyaelekeza kwa uongozi wa Bunge la Tisa, lililoongozwa na Samuel Sitta, yalichefua Watanzania wa kada mbalimbali ambao walimshambulia mwanasheria mkuu huyo wa zamani, wakisema hana mamlaka ya kimaadili kumnyooshea kidole mkuu huyo wa bunge lililomalizika kutokana na kazi nzuri aliyoifanya.
Lakini, vita hiyo ya maneno aliyoanzisha Chenge, mwelekeo wake unatarajiwa kuanza kuonekana leo, baada ya ratiba ya CCM kuonyesha kuwa kamati hiyo, itaanza kikao chake mchana hadi jioni na kupitisha majina matatu.
Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, aliliambia gazeti hili jana, akielekea Dodoma kuhudhuria kikao hicho kwamba, madhumuni ni kufanya mchujo wa wagombea na kubakisha majina matatu yatakayopelekwa kwenye Kamati ya Wabunge wa CCM.
Hata hivyo, Makamba alipoulizwa iwapo haoni kama tuhuma nzito za Chenge alizotoa dhidi ya Sitta, zimeongeza mpasuko ambao CCM ilijaribu kutafutia mwarobini kwa kuunda kamati ya mzee Mwinyi, alihoji, "Wewe ulitaka nimfunge Chenge mdomo na kamba?"
Makamba alimtetea Chenge akisema kuwa anao uhuru wa kutoa maoni na kamwe, chama kisingeweza kumzuia kutoa maoni yake kwa vyombo vya habari.
"Chenge kaitisha mkutano na waandishi mwenyewe, kalipia hoteli, kazungumza maoni yake wewe unaniuliza kwa nini tunamruhusu kutoa maneno kama yale, ana uhuru," alitetea Makamba.
Hata alipoelezwa kuna tofauti kati ya uhuru wa kutoa maoni na kushambulia mtu kwa maneno makali, Makamba alihoji akisisitiza: "Maneno makali gani?, Mimi nisingeweza kumzuia Chenge kusema anachoamini."
Kwa ukali, Makamba alipinga vikali tuhuma za kuhusika na mpango unaodaiwa wa genge la watuhumiwa wa ufisadi kumshughulikia Sitta, ambaye amejijengea nguvu kubwa kwa umma kutokana na kulibadili bunge la jamhuri kuwa lenye demokrasi pana, kwa kuruhusu mijadala mizito ikiwemo ya ufisadi .
"Ukianiambia natumiwa na mafisadi hayo ni matusi, wewe (mwandishi), naona siku nyingi unaniambia mimi natumiwa na mafisadi, alifoka Makamba na kuongeza:
Ujue unanitukana!, Mimi kwetu ni Lushoto niko Dar es Salaam kikazi, nikistaafu naweza kurudi kwetu, siko hapa Dar es Salaam kwa kulishwa na mafisadi. "
Kwa upande wake Sitta, tangu aliposhambuliwa na Chenge, amekuwa kimya huku akisisitiza anaheshimu kazi nzuri iliyofanywa na kamati ya mzee Mwinyi ambayo utekelezaji wake unafanywa na waziri mkuu.
"Nadhani huu si wakati wa malumbano, ipo kazi iliyofanywa na wazee wetu kumaliza haya matatizo sasa kuanza kuturudisha nyuma itakuwa si vema. Mimi siwezi na sihitaji malumbano, chama kitaamua," alisisitiza Sitta.
Genge linaloongozwa na watuhumiwa wakubwa wa ufisadi nchini wenye kujikinga kwa mwavuli wa kisiasa ndani ya CCM, limeapa kumshughulikia Sitta kwa kuhakikisha jina lake halipiti ngazi ya Kamati Kuu.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, shabaha kubwa ya mafisadi ni kumpa uspika mmoja wa wabunge wanawake ambaye naye wamemteka hivi karibuni, kwa kutumia kigezo cha usawa wa kijinsia na uzoefu, baada ya kumlipia deni la Sh1bilioni la kampuni yake.
Vyanzo hivyo vilifafanua kwamba, asilimia kubwa walioingia katika kinyang'anyiro hicho ni watu walioshinikizwa na genge hilo la mafisadi, lakini watu wawili mmoja mwanaume na mwanamke ndiyo wanaandaliwa kuwa spika, endapo mmoja wao ataangushwa.
Hata hivyo, wadadisi wa mambo ya kisiasa wanaangalia CCM kama chama kinachopita katika wakati mgumu kisiasa na kitendo chochote cha kumng'oa Sitta, kitazidi kuongeza hasira za umma na kutoa mwelekeo wa mwaka 2015.
MAALIM SEIF ATINGA SUTI NA KUSHIKA HATAMU YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS RASMI ZNZ
Salma Said, Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein amemteua Maalim Seif Shariff Hamad kuwa Makamu wa Kwanza wa rais na Seif Iddi kuwa Makamu wa Pili.
Vilevile Dk Shein alimteua Balozi Seif Ali Idd Makamu wa Pili wa rais kwa mujibu mamlaka aliyopewa chini ya kifungu 39 (1),(2) na (6) cha katiba ya Zanzibar.
Viongozi hao wawili waliapishwa jana saa 10 jioni wakitanguliwa na shamrashamra zilizofanyika katika maeneo mbalimbali ya katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Utuezi wa Maalim Seif ambaye ni Katibu Kkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) kuwa makamu wa kwanza wa rais unafuatia mwafaka uliofikiwa baina na CUF na CCM Zanzibar kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kulingana na matokeo ya uchaguzi mkuu.
Katika makubuliano hayo, mshindi wa kwanza kwenye kinyang’anyiro hicho ndiye anakuwa rais na mshindi wa pili anakuwa makamu wa kwanza wa rais. Chini ya maridhiano hayo makamu wa pili ambaye ndiye kiongozi wa shughuli za serikali huchaguliwa kutoka katika chama cha rais.
Matokeo ya uchaguzi wa rais wa Zanzibar yalimpa ushindi Dk. Shein wa CCM akifuatiwa na Maalim Seif wa CUF, hivyo kwa mujibu wa maridhiano hayona marekebisho ya Katiba ya Zanzibar, Maalim anakuwa makamu wa pili na Seif Iddi kutoka CCM anakuwa makamu wa pili na mkuu wa shughuli za serikali.
Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar kifungu cha 20 (6), Makamu wa Pili wa Rais anateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka katika chama anachotoka Rais.
Marekebisho hayo ya katiba yanaeleza kuwa Makamu wa Pili wa Rais ndiye atakuwa mshauri wa Rais katika kutekeleza majukumu yake na pia atakuwa mkuu wa shughuli za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Dk Shein ambaye anakuwa rais wa saba tangu visiwa hivyo viuondoe utawala wa kisultani mwaka 1964 alimshinda kwa tofauti ya kura chache mgombea wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad.
Katika hotuba yake baada ya kuapishwa kuwa Rais SMZ wiki iliyopita, Dk Shein alisema licha ya urais kuwa jukumu kubwa na gumu, atatumia nguvu na uwezo wake wote kutekeleza wajibu wake kwa maslahi ya taifa na watu wake bila ubaguzi ili kudumisha umoja wa kitaifa visiwani humo.
Sherehe za kumwapisha Dk Shein zilizofanyika Jumatano wiki mjini Zanzibar iliyopita zilihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Jakaya Mrisho Kikwete, marais wastaafu wa Serikali ya Muungano, Benjamin Mkapa, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais SMZ anayemaliza muda muda wake, Aman Karume, aliyekuwa Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha Rais wa Awamu ya Tano wa SMZ, Dk Salmin Amour na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda.
Wakati huo huo, Wajumbe wateule wa Baraza la wawakilishi wamemrejesha Spika Pandu Ameir Kificho katika kiti chake uspika kwa ushinda wa kura 45 dhidi ya mpinzani wake Abass Juma Mhunzi aliyepata kura 32 kati 78 zilizopiwa na kura moja iliharibika.
Viti Maalumu moto, CCM YAVUNA 65, CHADEMA 23, CUF 10
| |
|
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana Jijini Dar es Salaam jana chama cha CUF bado hakijawasilisha orodha ya majina ya wanawake watakaowania viti maalumu, lakini orodha hiyo ya Nec inaonyesha kuwa baadhi ya wabunge waliokuwemo wako hatarini kuachwa huku waliko katika nafasi za kwanza katika vyama vyote wakiwa na matumiani ya kupeta. |
Nov 8, 2010
Nov 7, 2010
uzinduzi wa mobile monday jijini dar






Wadau woote wa habari na teknolojia ya mawasiliano (ICT) waliofika katika uzinduzi wa mtandao wa Mobile Monday walipata nafasi ya kupata picha ya pamoja kabla ya kuondoka ukumbini hapo.Nov 6, 2010
SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA RAIS DK JAKAYA MRISHO KIKWETE KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUNGANO WA TANZANIA HII LEO''SHAMBA LA BIBI''UWANJA WA UHURU!!!!
Rais Jakaya Kikwete ndiyo ameingia na msafara wake kwenye Uwanja wa Uhuru kama unavyoona na tayari ameshakula kiapo cha kuitumikia Tanzania kama rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa sasa zinaendelea taratibu zingine kutokana na ratiba inavyokwenda haya ni matukio ya mwanzo wakati akiingia kwenye uwanja wa tukio zima la kiapo tutakuletea baada ya muda kaa mkao wa kula kuona matukio hayo.
Makachero wakiingia kwa staili ya aina yake wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akiingia kwenye uwanja wa Uhuru mmchana huu.
Marais wa nchi mbalimbali wamehudhuria katika sherehe za kuapishwa kwa rais Jakaya Kikwete kutoka kushoto ni rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Rais Joseph Kabila wa DR Congo, Rais Rupia Babda wa Zambia Mke wa Rais wa Zanziba na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein Kiongozi wa Kutoka Swaz na wageni wengine.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma naye amehudhuria katika Sherehe hizo kama unavyomuona akielekea jukwaa kuu.
Huu ni umati wa wageni waalikwa katika jukwaa la upand wa kulia kwenye uwanja wa Uhuru ambapo sherehe za kuapishwa kwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete zinaendelea sasa.
Wadau nipo katika eneo la tukio ili kuwaletea kila kitakachoendelea juu ya shughuli hii ya kuapishwa kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na hapa ni Taji Liundi Mwongozaji au MC wa hafla hiyo katikati akiwa katika maadalizi ya ratiba pamoja na maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ na maafisa wa Serikali ili kuhakikisha utaratibu unakwenda kama ulivyopangwa wakati wa kumuapisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete Asubuhi hii kwenye uwanja wa Uhuru. Wengine katika picha ni Asumpta Masoi wa pili kuliaKanali Dominic Basil Mrope kulia na kushoto ni Meja Juma Muhogoyi Kasi. Wageni mbalimbali ikiwa ni mabalozi mawaziri na maafisa wa Serikali pamoja na wageni mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali wanaendelea kuwasili ambapo pia marais kutoka nchi kadhaa wanatarajiwa kuhudhuria katika shughuli hiyo ya kumuapisha Rais Jakaya Kikwete. Marais watakaokuwepo ni pamoja na Mwai Kibaki wa Kenya, Joseph Kabila wa Congo,Rupia Banda wa Zambia, Jacob Zuma Afrika Kusini,Therence Sinunguriza Makamu rais Burundi, Bernard Rkuza Wazirio Mkuu Rwanda, Aires Bonifancio Ali Waziri Mkuu Msumbiji, Eriya Kategaya Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza Uganda pamoja naye Maiko Hausiku Naibu Waziri Mkuu Namibia. Wadau wa FULLSHANGWE haya ni matukio ya mwanzo tu matukio zaidi tutawaletea baadae mara baada ya kukamilika kwa kazi nzima ya kumuapisha Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Waheshimiwa mabalozi na wageni mbalimbali wakiwasili katika uwanja wa uhuru ili kushuhudia kuapishwa kwa rais Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi hii ili kushika kipindi kingine cha miaka mitano kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hapa ndipo mahari ambapo Rais Mteule Dk Jakaya Mrisho Kikwete ataapishwa asubuhi hii kama unavyoona likiwa linaaandaliwa katika hatua za mwishomwisho ili kuhakikisha mambo yote yanakwenda sawa katika shughuli hiyo.
Waheshimiwa Mawaziri, Wabunge wateule, Mabalozi pamoja na wageni waalikwa mbalimbali wakiwa tayari wamekaa jukwaa kuu kwenye uwanja wa Uhuru wakisubiri kuapishwaq kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi hii ili kushika urais wa Tanzania kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo. 





