MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ( NEC), Jaji Mstaafu, Lewis Makame leo jioni amemtangaza mshindi wa kiti cha urais wa Tanzania wa mwaka 2010 kuwa ni Ndugu Jakaya Kikwete kutoka Chama cha Mapinduzi(CCM).
Matokeo hayo ya uchaguzi huo, yalitangazwa leo majira ya saa kumi jioni na Mwenyekiti huyo katika viwanja wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Jaji Mstaafu , Makame alisema kwa mujibu wa Ibara ya 41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1977 mgombea wa kiti cha urais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa rais iwapo tu amepata kura nyingi kuliko mgombea mwingine yeyote.
Aidha Makame alisema kwa mujibu wa ibara ya 47(2) ya Katiba hiyo, mgombea wa kiti cha urais akichaguliwa basi na mgombea mwenza wake atakuwa Makamu wa Rais.
“Kwa kuwa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wa CCM amepata kura yingi kuliko mgombea yeyote, kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kwa mujibu wa vifungu vya 35E, 35F (8) na 81 B vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura 343, ninatangaza rasmi matokeo ya uchaguzi wa urais wa 2010.
“Mheshimiwa Kikwete Jakaya Mrisho amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Bilal Mohammed Gharib amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Mwenyekiti huyo.
Aliongeza kuwa idadi ya wapigakura waliojiandikisha ni 20,137,303, waliopiga kura ni 8,626,283 sawa na asilimia 42.84 ya wapiga kura wote waliojiandikisha, zilizoharibika ni 227,889 ambazo ni sawa na asilimia 2.64 ya kura zilizopigwa.
Alizitaja idadi ya kura halali kuwa ni 8,398,394 sawa na asilimia 97.36 ya kura zote zilizopigwa, hivyo Kikwete amepata kura 5,276,827 ambazo ni sawa na asilimia 61.17 ya kura zote halali.
Wagombea waliofuatia ni wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ambaye ni Slaa Willibrod Peter amepata kuwa 2,271,941 ambazi ni sawa na silimia 26.34 ya kura zote halali, Lipumba Ibrahim Haruna wa chama cha CUF, amepata kura 695,667 sawa na asilimia 8.06 ya kura zote halali, Mziray Kuga Peter wa APPT – Maendeleo amepata kura 96,933 sawa na asilimia 1.12 ya kura zote halali.
Wengine ni Rungwe Hashim Spunda wa NCCR- MAGEUZI amepata kura 26,388 sawa na asilimia 0.31 ya kura zote halali, Mgaywa Muttamwega Bhatt wa TLP amepata kura 17,482 sawa na silimia 0.20 na Dovutwa Yahmi Nassoro Dovutwa wa UPDP amepata kura 13,176 sawa na asilimia 0.15 ya kura zote halali.
Akitoa salamu kwa niaba ya wenzake badala ya Slaa ambaye ahakuwepo uwanjani hapo, Lipumba ambapo alimpongeza Kikwete na Makamu huku akisisitiza suala ya ushiriki wa watu katika kupiga kura liangaliwe na kusema Rais aliyeshinda ni Watanzania wote.
Alisisitiza suala la elimu bora , ajira, ujengaji wa miundombinu na uvumulivu wa kisiasa ni muhimu, hivyo alimshauri Rais Mteule Kikwete kujiwekea malengo katika kipindi cha miaka 5 ijayo, ambayo ni uongozi wa demokrasi, ujenzi wa uchumi ajira kuboresha miunbombinu, utawala na kupamban na rushwa.
Pia alimkabidhi Rais Mteule Kikwete Ilani ya chama chake kwa ajali ya kusaidia katika utendaji wake wa kazi.
Kwa Upande wake Rais Mteule Kikwete, alitoa shukura za ushindi alioupata na kusema watazifanyia kazi changamoto zilizibuliwa wakti wa kampeni yakiwemo mawazo ya Lipimba.
Alivishukuru vyombo vya habari kwa tendaji wao wa kazi , lakini aliviomba kufanmya kazi zaidi ya kusaidia kutibu majeraha ya nchi ili kurejesha umoja na amani badala ya kuongeza chumvi.
Naye Dovutwa alisema sasa ni wakti wa kumsaidia Rais Mteule kujenga nchi malumbano yamekisha.
Mziray amesema hajakata tama ananjiandaa kwa baade , huku Muttamwega alisema matokeo yameenda vizuri.
Rais Mteule Jakaya Kikwete akiingia kwenye viwanja vya Karimjee leo mchana wakati Tume ya Uchaguzi ilipotangaza matokeo ya Kura za urais na mgombe huyo kupitia chama cha Mapinduzi kuibuka mshindi matukio zaidi ya picha tutawaletea baadae. ----------------------------------------
WALIOJIANDIKISHA KUPIGA KURA: 20, 137, 303
WALIOJITOKEZA KUPIGA KURA: 8, 626 (42.64%)
KULA HALALI ZILIZOPIGWA: 8,398,394
KURA ZILIZOHARIBIKA 227,889 (2.64)
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akionyesha cheti cha ushindi katika mbio za urais mwaka 2010 muda mfupi baada ya tume ya Uchaguzi kumtangaza kuwa mshindi wa kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka huu 2010.Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo mchana.
Rais wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa akimpongeza Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya tume ya Uchaguzi kutmangaza Rais Kikwete kuwa mshindi wa kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwaka huu 2010 katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo mchana(picha na Freddy Maro)
Mgombea urais kwa tiketi ya CUF Profesa Ibrahim Lipumba akimpongeza Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya tume ya Uchaguzi kumtangaza Dr.Jakaya Kikwete kuwa mshindi katika kinyang’anyiro cha Urais katika uchaguzi wa mwaka huu 2010.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Lewis Makame amkikabidhi cheti Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kumtangaza kushinda katika mbio za urais katika uchaguzi wa mwaka huu.Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

































