
Vodacom Miss Tanzania Geneviva Mpangala akiwa na washindi wenzie mara baada ya kutangazwa mshindi kwenye shindano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam usiku huu kulia ni mshindi wa tatu Consolata Msofe na kulia ni mshindi wa pili Groly Mwanga, Geneviva ataiwakilisha nchi katika shindano kubwa la Dunia Miss World litakalofanyika mwishoni mwa mwaka huu. Katika shindano hilo wanamuziki mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wamefanya vitu vyao wakiwemo Temba na Chege kutoka TMK Family, Ambwene Yessaya (AY) Mataluma, Mwasiti na kundi la THT kutoka jijini Dar es salaam na wengine wengi.

Hii ni Tano Bora ya Vodacom Miss Tanzania mara baada ya kutangazwa ambapo waliulizwa maswali na kuyajibu kabla ya kutangaza mshindi wa shindano hilo kwa mwaka huu wa 2010.

Hii ndiyo kumi bora ya Vodacom Miss Tanzania mara baada ya kutangazwa kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam usiku huu.

Washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania wakipita jukwaani na vazi la ufukweni ilikuwa si mchezo.

Utambulisho

Utambulisho

Warembo wakipita na kujitambulisha kwa wageni waalikwa na mashabiki wa urembo.

Wakuu wa Kampuni ya MUZASHA TOURS wakishuhudia shindano hilo kulia ni Benedictor Mulokozi Mkurugenzi wa CM Co. Limited Charles Mtawali Mkurugenzi wa MUZASHA TOURS Muzamir Katunzi pamoja na Pamela ambaye ni maiwaifu wa Charles Mtawali.

Warembo wanaoshiriki kwenye shindano la Vodacom Miss Tanzania wakiingia kwa shoo ya utambulisho.

Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam William Lukuvi aliyekaa chini pamoja na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk Ladslaus Komba akiingia na ujumbe wake kutoka Bodi ya Utalii na Mamlaka ya hifadhi za Ngorongoro kabla ya kuanza kwa shindano hilo huku akisindikizwa na Mkurugenzi wa Kamti ya Miss Tanzania Hashim Lundenga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare akihojiwa na mtangazaji wa Star Tv kabla ya kuanza kwa shindano hilo.

Warembo wakiingia kwenye ukumbi wa Mlimani City tayari kwa kupanda jukwaani.
No comments:
Post a Comment