Sep 17, 2010

US Ambassador visited to the TWENDE platform at Diamond Jubilee yestarday


Ambassador Alfonso Lenhadt delivering his massage to women entrepreneurs
Mustafa Hassanali, founder of TWENDE showing the US ambassador a basket created by a women entrepreneur.
Ambassador Alfonso looking at a batik shirt created by Farha Sultan
American Ambassador, Alfonso Lenhhard listerning to Ms Caroline Kessy during his visit to the TWENDE platform at Diamond Jubilee yestarday
The Ambassador discussing the quality of products among the women participating to TWENDE
Ms Teresia Mistry from Zanzibar disussing with Ambassador Alfonso Lenhardt.
US Amassador Alfonso Lenhardt (Right) and his Wife, Jacqueline Lenhardt in picture with some women entrepreneurs participating in TWENTE platfrom.
Tanzanian women entrepreneurs as they listnen to the Ambassador's speech
US Ambassor Alfonso Lenhardt, listerning to contrubutions from women entrepreneurs.(mtaa kwa mtaa-blogspot)

MANENO YA NAKAAYA BAADA YA KUICHAGUA CCM.

Changes from within. Lots of guys are quick to judge, If I could do something where I was, I would.
The support system was very low. its easy to talk about what you don't know... but I did what I had to do.
sikutegemea nyote mtafurahia but #this is politics#
(djchoka.blogspot.com)

BASATA LAWAFUNDA VIONGOZI WA MASHIRIKISHO YA WASANII NCHINI!!


Na Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka viongozi wa mashirikisho ya wasanii kuhakikisha wanakuwa imara na thabiti ili kuleta ufanisi kwenye mashirikisho ya wasanii nchini yaliyoundwa na kupata viongozi wake hivi karibuni. Hayo yamesisitizwa na Wakufunzi kutoka BASATA wakati wakitoa semina kwa viongozi wa mashirikisho ya wasanii nchini iliyofanyika wiki hii kwenye ukumbi wa Baraza hilo na kuhudhuriwa na viongozi wote wa mashirikisho ya wasanii na wajumbe wao. Mashirikisho yaliyohusika kwenye semina hiyo ni pamoja na lile la Sanaa ya Muziki,Maonyesho,Ufundi na Filamu ambapo mada mbili zilizotolewa kwa viongozi hao ambazo ni Wajibu na Maadili ya Uongozi wa Mashirikisho ya Sanaa iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mfuko na Uwezeshaji wa BASATA,Bw.Ruyembe Mulimba na na ile ya Mchakato wa Kuandaa Mpango Mkakati wa Shirikisho iliyowasilishwa na Mwalimu Rashid Masimbi kutoka Kituo cha Sanaa za Maonyesho Tanzania. Akizungumza kwenye semina hiyo,Ruyembe alisema kwamba, viongozi wa mashirikisho ya wasanii hawana budi kuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya wasanii,kuwa na mwenendo mwema, kuzingatia maadili ya uongozi, kuzingatia dhana ya kutangulia na kuelekeza huku mtangulizi akiwa anafahamu anakowapeleka watu anaowaongoza. “Kiongozi mzuri lazima aelewe majukumu na mwenendo mwema katika kazi ya kusimamia watu ambao wanahusika na utendaji wa shughuli husika kwa ushirikiano na kwa pamoja kulingana na Katiba iliyopo” alisisitiza Ruyembe. Aliongeza kwamba, historia inaonesha vyama vingi na shirika za wasanii zimekuwa kwenye migogoro isiyoisha kutokana na viongozi kutokuwa na utashi wa kuongoza., kutanguliza maslahi binafsi na kushindwa kabisa kuwa na maono ya kutekeleza mikakati inayokuwa imewekwa. Alizidi kufafanua kwamba, wasanii wanakumbwa na changamoto nyingi sana zikiwemo za wao kuibiwa kazi zao, kunyonywa kupitia mikataba, kulipwa malipo kidogo na ukosefu wa masoko hivyo viongozi wa mashirikisho hawana budi kuwa mstari wa mbele kuhakikisha changamoto hizo zinawekewa mikakati ya kupunguzwa kama si kumalizwa kabisa. Naye Mwalimu Rashid Masimbi alisema kwamba, moja ya kazi ya viongozi hao wa mashirikisho ya wasanii ni kuhakikisha wanakuja na Mpango Mkakati wa muda mfupi na mrefu ambao utalenga kujenga dira ya utendaji na mafanikio ya mashirikisho. Aliongeza kwamba, viongozi hawana budi kuwa na mpango mkakati ambao utaeleza nini kitafanyika,nani atakifanya, kwa namna gani na kwa muda gani. “Mpango Mkakati ndiyo dira, dhamira, malengo, shughuli na matokeo ya utendaji wa shirikisho lolote hivyo lazima nyinyi viongozi mtuoneshe ni kwa jinsi gani tutayafikia haya” alisisitiza. Baadhi ya viongozi waliohudhuria semina hiyo waliishukuru BASATA kwa mpango huo na kusisitiza kwamba, semina kama hizo ziandaliwe mara kwa mara ili kujenga ufanisi wa mashirikisho ya wasanii na sekta ya sanaa kwa ujumla.

MTANGAZAJI WA RFA KID BWAY' AVAMIWA NA ALIYEJITAMBULISHA KUWA NI MSANII, APOTEZA FAHAMU, HAJITAMBUI HADI SASA.

MTANGAZAJI WA RADIO FREE AFRIKA AMBAYE VILEVILE YU PRODUCER WA KUREKODI MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NDANI YA TETEMESHA PRODUCTION SANDU GEORGE MPANDA MAARUFU KWA JINA LA KID BWAY AMELAZWA HOSPITALI YA BUGANDO MARA BAADA YA KUVAMIWA NA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI NA JAMAA ASIYEFAHAMIKA.

TAARIFA ZINASEMA KUWA KID BWAY AKIWA NYUMBANI KWAKE LUMALA JIJINI MWANZA, JAMAA ALIYEMVANIA ALIFIKA NYUMBANI HAPO MAJIRA YA SAA 2:30 USIKU NA KUJITAMBULISHA KAMA MSANII AKIHITAJI KUFANYA RECORDING, BAADA YA MAZUNGUMZO NA KUJITAMBULISHA ALIKARIBISHWA NDANI HADI CHUMBA CHA KUREKODIA STUDIO.

NYUMBANI KWA MTANGAZAJI HUYO ANAISHI NA JAMAA ZAKE WAWILI AMBAO WAKATI KID AKIMKARIBISHA MTENDA UHALIFU HUO NYUMBANI HAPO JAMAA HAO WALIMWONA KIJANA HUYO KISHA KILA MMOJA AKAINGIA CHUMBANI KWAKE. DAKIKA KADHAA WAKASIKIA KWA KIPINDI KIREFU SPIKA ZA STUDIO ZIKIKOROMA ISIVYO KAWAIDA NA KUANZA KUDADISI HUKU WAKIMWITA KID BWAY KUWA INAKUWAJE! WAKAITA NA KUITA NDIPO WALIPO AMUA KUINGIA STUDIO NA KUMKUTA SAKAFUNI KAANGUKA DABU ZIKIMTOKA MASIKIONI, PUANI NA KWENYE MAJERAHA SEHEMU ZA KICHWA.

KWA HIVI SASA KID YUPO HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO AKIWA HOI HAJITAMBUI YAANI KAPOTEZA FAHAMU, ALITUNDIKIWA DRIPU YA MAJI IKIWA NI HUDUMA YA KWANZA AMBAYO AMEPATIWA JANA MARA BAADA YA KUFIKA HOSPITALINI HAPO AKISUBIRI KIPIMO CHA T SCAN KUONA KWA UNDANI ZAIDI SEHEMU ALIZODHURIKA. HAKUNA TAARIFA YOYOTE YA UPOTEVU WA MALI HALI INAYOPELEKEA WADADISI WA MAMBO KUDHANI KUWA YAWEZEKANA KULIKUWA NA VITA YA KICHINI CHINI AKA BIFU(AMBAYO HAIJAFAHAMIKA).

UCHUNGUZI KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI UNAENDELEA KUFANYWA ILI KUJUA NINI SABABU ZA UVAMIZI HUO.

TAARIFA ZAIDI TUTAENDELEA KUKUJULISHA.
TWAMWOMBA MWENYEZI MUNGU AKUPE NGUVU BROTHER UPATE PONA.

Ridhiwani Kikwete atinga na kameni Liwale, Nachingwea!

Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji Halmashauri ya baraza la umoja wa vijana wa CCM Ridhiwani Kikwete aliyevaa skafu) akikagua gwaride la viaja wa CCM, baada ya
kulakiwa eneo la eneo la Ngunichile akitokea kufanya kampeni za ndani Liwale kwenda
Nachingwea mkoani Lindi juzi, ambapo katika mkoa huo amefanya mikutano ya kuweka mikakati ya
ushindi wa chama hicho. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Kikundi cha Kwaya cha vijana wa CCM kikitumbuiza wakati wa kampeni za ndani za chama hicho uliohutubiwa na Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete, mjini Liwale juzi
Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Ridhiwani Kikwete akiwahutubia wafuasi Wanachama na wafuasi wa chama hicho, wakati
wa mapokezi eneo la Ngunichile akitokea kufanya kampeni za ndani Liwale kwenda Nachingwea
mkoani Lindi jUZI, ambapo katika mkoa huo amefanya mikutano ya kuweka mikakati ya ushindi wa
chama hicho.

VODACOM SASA NI BWERERE

Vodacom Tanzania imepunguza gharama zake katika huduma ya kupiga simu, ambapo wateja wa Vodacom wataweza kupiga simu kwenda mitandao mingine nchini kwa punguzo la zaidi ya asilimia 50.Hii ni katika jitihada za kampuni hii kuhakikisha kuwa mawasiliano yanapatikana kwa gharama nafuu, nchi nzima.

Gharama hizi mpya zitamruhusu mteja wa Vodacom kuweza kupiga kwenda mitandao mingine kwa kiasi kidogo cha shilingi tatu tu za kitanzania kwa sekunde, wakati hapo awali gharama ya kupiga simu kwenda mitandao mingine ilikuwa shilingi sita na nusu.

Huduma hii imekuja miezi michache tu baada ya Vodacom kuzindua huduma nyingine ya shilingi moja kwa sekunde , maarufu kama HABARI NDIO HII.

Ikiwa na wateja milioni nane nchini, kampuni ya Vodacom imeendelea kutoa bidhaa na huduma kwa wateja wake,na kuwawezesha kupata mawasiliano kwa gharama nafuu.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Vodacon Tanzania, Mwamvita Makamba alisema jana kwamba kuwa gharama hizi mpya zimeleta mapinduzi katika sekta ya mawasiliano ya simu nchini.

“Kama tulivyozindua huduma ya Habari Ndio Hii, tumejikita kuhakikisha kuwa mtandao wetu unatoa bidhaa na huduma bora kwa wateja wetu ili kuwajenga kiuchumi.”

Kampuni ya Vodacom imekuwa nchini kwa miaka kumi sasa na inatabiri kukua zaidi katika sekta hii mwaka huu na miaka mingine ijayo.

“Tutamatumaini makubwa juu ya utendaji wetu hapo mbeleni na tunashauku kubwa kuweza kutoa huduma zetu zenye ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu.”

Huduma zingine za Vodacom kama Vodajamaa na Cheka Time zitabaki kama zilivyo.

“Vodacom inawahakikishia wateja wake kuwa itaendelea kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu hapo mbeleni” Bi Pendaeli alihitimisha kusema.

JARIDA LA MAN LAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM!!

Wanaume wa Tanzania sasa wanachokitu cha kujivunia kutokana kuanzishwa kwa Jarida la Man ambalo lilianza kuonekana mitaani mwishoni mwa mwaka jana.

Jarida hili limekuwa likigusa mambo mbalimbali yanayohusu wanaume kuanza kwenye afnya, biashara na maisha ya kawaida.

Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Euro Consultancy Limited, Dismas Masawe alisema Jarida la Man linachapishwa na wazawa ambapo kwa sasa linapatikana nchini kote na likiwa katika toleo lake la nne.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana uliofanyika kwenye hoteli ya New Africa, Dar es Salaam, Masawe alisema jarida hilo litakuwa linatoka kila baada ya miezi miwili na limeanzishwa ili kuziba pengo lililokuwepo katika sekta ya majarida kutokana na yale yaliyopo kuandika zaidi habari za wanawake.

“Jarida letu linachimbua mambo mbalimbali ambayo msomaji angependa kuyajua kuanzia magari, mambo ya ujenzi, taasisi za fedha, mambo ya uchukuzi, michezo, teknolojia, mitindo, uhusiano na kupitia mambo mbalimbali yanayotuzunguka katika jamii,” alisema.

Massawe, alisema jarida la Man linachapishwa katika kiwanda cha Jamana Dar es Salaam, na kwamba ni sehemu ambayo wanawake wanaweza kutumia kama jiwe muhimu la kuwatambua wanaume na kufahamu nini jinsia nyingine.

Alisema katika matoleo manne ambayo yamekwishatoka mpaka sasa Man limewahoji watu mbalimbali maarufu nchini. Katika toleo la kwanza Man, ilimfanyia mahojiano ndugu Azim Jamal ambaye ni mhamasishaji mkubwa, mchambuzi na mzungumzaji mkubwa. Toleo la pili Nehemiah Kyando Mchechu ambaye alikuwa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika na sasa ni Mtendaji Mkuu wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC).

Katika jarida la tatu Man, ilimhoji Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mohamed Enterprises Tanzania Limited, ambaye pia ni Mbunge wa Singida, Mohamed Dewji, na katika toleo la mwisho Man lilimhoji Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Executive Solutions Limited, NduguAggrey Marealle. Marealle aafahamika kwa uwezo wake mkubwa katika kazi za Uhusiano wa Umma na Serikali kwa ujumla.

Massawe alisema Jarida la Man hivi karibuni litafungua milango kwa nchi za jirani za Kenya na Uganda na baadaye Kusini mwa Afrika kutokana na kuwepo kwa soko zuri la katika eneo hilo.

Pia katika siku zijazo, Jarida hili litakuwa likipatikana kwenye mtandao ambapo wasomaji watakuwa na uwezo wa kulipia ili waweze kulisoma.

Kwa mujibu wa Mtendaji huyo, Jarida hilo linawachangiaji wengi ambao wako katika ngazi juu katika serikali na taasisi mbalimbali mpaka raia wa kawaida. Massawe alisema wachangiaji wengine pia ni wanawake.

Aliwataka watanzania kujenga utamaduni wa kusoma ili kuweza kujua mambo mbalimbali yanayotokea duniani na pia kujua vitu mbalimbali.

“Watu wengi hawapendi kujisomea, lakini kusoma ni mojawapo ya njia ya kufanya mtu asiwe na muda kupoteza na pia kujifunza mambo mengi zaidi yanayotokea duniani,” alisema.

Amesema japokuwa Jarida hilo linahusu wanaume, lakini imeonekana wanawake wengi wameonekana kuvutiwa nalo na kulisoma.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na

Dismas Massawe

CEO, Euro Consultancy Limited.

Mobile: 0784407475/0655407475

Email: dismas@eurocom.co.tz

au

Taji Liundi

Chief Editor, Man Magazine,

Mobile: 0787888799

mbio za pool table zaanza jini arusha



Mchezaji wa pool kutoka timu ya mkoa wa Ilala, Evansi Mushi akipiga mpira wakati wa ufunguzi wa mashindano ya taifa ya mchezo huo yaliyoanza kutimua vumbi huko jijini Arusha.mashindano haya yanaendelea kwa udhamini mkubwa wa bia ya Safari Lager.
baadhi ya wachezaji wa mchezo wa pool toka katika timu za mikoa mbali mbali zinazoshiriki katika mashindano hayo,wakiendelea kufuatilia mechi zilizokuwa zikiendelea wakati huo.

jide na machozi band ndani ya savannah lounge usiku huu



Lady Jay Dee a.k.a Binti Komando akiwajibika leo katika kiwanja chake cha kila alhamisi cha Savannah Lounge kilichopo ndani ya jengo la Benjamin Mkapa Tower.
timu nzima ya Machozi Band ikiongozwa na mwanadada Lady Jay Dee ikitoa burudani la kufa mtu usiku huu katika kiota cha Savannah lounge ndani ya Benjamin Mkapa Tower.
Sam,Mau na Joniko wakienda sambamba katika kuimba usiku huu.
mie na mdau Husna ndani ya Savannah Lounge usiku huu.
Detah na Don wakiwakilisha ndani ya Savannah Lounge usiku huu.
Detah (kulia) akigawa zawadi kwa mdau aliekuwa anapata kilaji cha Savannah usiku huu.
Detah (kulia) akiendelea na zoezi la kutoa zawadi kwa wadau waliokuwa wakijipatia kilaji cha Savanna kilichokuwa kikinyweka kwa kasi ya ajabu usiku huu.

Wadau wa Savannah Lounge wakiwa katika libeneke lao usiku huu.
wadau wakiserebuka na mapini ya Machozi Band yaliyokuwa yakiangushwa usiku huu ndani ya Savannah Lounge

Sep 16, 2010

ngoma mupya toka hot pot family


Mambo vipi waungwana?Nachukua fursa hii kushukuru kwa support mnayonipa mimi na ndugu zangu wote wa Hotpot family.Nadhani mlikuwa hamjui kuwa Hotpot Family ni kundi ambalo linajumuisha wasanii wa kila fani lakini kwenye muziki tunaofanya tuko kumi akiwemo Suma-G,Dulayo,Chriss,Baby,Nico,Chorus,Chid Blast,Dogo Mfaume,Salim na mimi.
Tumeamua kufanya project ya kundi zima kwa mara ya kwanza na wimbo huu tumerekodi chini ya producer Muba na tumeona tuwaachie madogo waonyeshe uwezo wao ila mimi na Suma tumeimba chorus tu...
Wimbo unaitwa UNA MIPANGO?Tukiimanisha una deal?Au una pesa?

Mwenyekiti wa WAMA mama Salma Kikwete akiwa Mkoani Mwanza

Matukio ya picha mbalimbali za Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete katika mkoa wa Mwanza ambapo anawatembelea wanachama wa UWT na kuzungumza nao akiwahamasisha kuhusu umuhimu wa Kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu ifikapo Oktoba 31,mwaka huu nchini kote. Picha zote na Mwanakombo Jumaa.
Picha hii inaonyesha Mama Salma Kikwete akisalimiwa na mwanachama wa UWT baada ya kufika Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza
Jamani mmemuona MGOLE, amapendeza........NDIVYO ALIVYOSEMA MWENYEKITI WA UWT MKOA MWANZA MARIA HEWA
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akimtambulisha mgombea Ubunge wa jimbo la Nyamagana (CCM) Lawrence Masha mjini Mwanza.
Mama Salma Kikwete akiongea na wakina mama wa UWT mkoani Mwanza.
Wanachama wa UWT wa Wilaya ya Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza wakimshangilia Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete wakati alipokuwa akiwahutubia mjini Mwanza.

Ridhiwani Kikwete avunja makundi Lindi Mjini!!

Na Richard Mwaikenda, Lindi.
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Lindi mjini kupitIa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mohammed Abdulaziz amewaomba radhi wana CCM aliowakosea wakati wa kinyang'anyiro cha kura za maoni baada ya kutakiwa hivyo na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, Ridhiwani Kikwete ili kuvunja makundi katika jimbo hilo.
Abdulaziz,alifanya hivyo juzi katika kikao cha ndani cha viongozi wa Umoja huo wilayani Lindi juzi, ambapo baadhi ya viongozi walieleza wazi mbele ya Ridhiwani kuhusu kuwepo kwa mgawanyiko mkubwa ambao walidai ulisababishwa na wagombea wawili, Abdulazizi na Maguo pamoja na wapambe wao wakati wa mchakato wa kura za maoni.
Baada ya wanachama kueleza hivyo na Ridhiwani kugundua ufa huo uliopo Lindi mjini na kuhatarisha umoja ndani ya CCM, ndipo akaamua kutumia fursa hiyo kuweka mambo sawa kwa kumtaka Abdulaziz aliyeshinda kura za maoni na kupitishwa na Halmashauri Kuu ya CCM, afanye uungwana kwa kupita kwenye matawi kuwaomba radhi wana CCM ili kuvunja makundi na kurudisha umoja ndani ya chama.
"Mwenye nafasi ya kuvunja makundi ni yule aliyeshinda.Hawa jamaa wametukanwa na kunyanyasika hivyo inatakiwa aliyeshinda ajishushe aende kwenye matawi kuwaomba radhi ili wote wawe kitu kimoja na kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, Mwaka huu,"alisema Ridhiwani huku akishangilia na wanachama.
"Wanachama wenzangu wa CCM, huwa makundi yanakufa moyoni na si machoni kwa mtu, kwani kuna mtu anaweza akakuchekea na kukuambia mambo yameisha, lakini kumbe moyoni bado anayo.Alisema katika kipindi cha harakati za kugombea uongozi makundi yanakuwepo, lakini mchakato ukishapisha na mmoja wao kuteuliwa inatakiwa kuvunja makundi na wote kumuunga mkono aliyeshinda na ndivyo tunavyotakiwa kufanya Jimbo la Lindi Mjini na kingineko". aliongeza Ridhiwani.
Alisema kuwa wakati wa kinyang'anyiro kuwania uongozi ndani ya chama ni kawaida katika kampeni huzuka makundi lakini baada ya kuwapata washindi huvunja mkundi na wote huamua kuwaunga mkono walioshinda.
Baada ya Ridhiwani kumalizia kuzungumza, alikaribishwa Abdulaziz ambaye alisimama na kuwaomba radhi wote aliowakosea na kuahidi kuwa atapita kwenye matawi ya chama jimboni humo kuwaomba radhi ikiwezekana kuwapigia magoti na hata kwa kugharaghara mbele yao.
"Kwa wale wote niliowakosea nawaomba radhi, nitapita kila tawi kuomba radhi ikiwezekana kwa kupiga magoti hata kwa kugharaghara kwani naamini vijijini na mjini wote walinipigia kura ndiyo maana nimeteuliwa kuwa mgombea katika jimbo hili,"Abdulazizi alisema na kuanza kukumbatiana na wanachama kitendo ambacho kiliashiria kumaliza tofauti zao.
Ridhiwani ambaye ameongozana baadhi ya vijana makada wa CCM,anafanya ziara ya kuhamasisha wanaCCM na wafuasi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kuhakikisha wanawapigia wagombea wa chama hicho ili washinde na kuunda dola kwa kipindi kingine cha mikaka mitano.Ziara hiyo ataifanya katika mikoa ya Lindi,Mtwara, Ruvuma, Mbeya, Iringa na Pwani.

Kikwete anguruma Moshi



Mgombea urais kwa tiketi ya CCM,Dr. Jakaya Kikwete akiwahutubia wanachama na wapenzi wa chama hicho huko Himo,Moshi jana.
Wananchi wa Kilema wakimlaki Mgombe urais wa CCM,Dr. Jakaya Kikwete alipokuwa anawasili kijijini hapo.

Dr. Kikwete akimwaga sera huku maelfu ya wanaCCM wakimsikiliza.

Maelefu ya wakaazi wa Moshi waliojitokeza kumsikiliza Mgombea urais wa CCM,Dr. Jakaya Kikwete uwanja wa Mashujaa

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia maelfu ya wakazi wa mji wa Moshi wakati alipokuwa akiingia katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi na kuhutubia katika mkutano mkubwa wa Kampeni (Picha Freddy Maro na Muhidin Issa Michuzi).
Mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM Dr. Jakaya Kikwete na Mgombea ubunge wa jimbo la Rombo Mh. Basil Mramba wakionesha alama ya dola ambayo CCM inatumia
Wananchi kibao wakiwa uwanja wa Mashujaa kumsikiliza Jakaya Kikwete mjini Moshi
akimnadi mgombea ubunge Vunjo Bw. Meela aliposimama Marangu Mtoni
Jakaya Kikwete akiwasili Kiboriloni akitokea Tarakea
Jakaya Kikwete akisalimiana na mgombea ubunge wa jimbo la Rombo Basil Mramba.
Jakaya Kikwete akisalimia maelfu ya wakazi wa Mwika
Kadamnasi ikimsikiliza JK Himo
Kinamama wa Tarakea wakimshangilia

Sep 15, 2010

SIMBA YAIBANJUA JKT RUVU 2-1, YANGA YABANWA MBAVU NA MTIBWA!!

Simba ya jijini Dar es salaamleo imefanikiwa kuifunga JKT Ruvu ya Pwani baada ya mshabuliaji wa timu hiyo Mussa Hassan Mgosi kuifungia timu hiyo katika kipindi cha kwanza cha mchezo goli moja na kuongeza msumari wa mwisho katika kipindi cha pili. Timu ya JKT Ruvu nayo imejitutumua baada ya kupata goli la kufutia machozi katika kipindi cha
pili cha mchezo huo na kufanya Simba kuibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja, kwa ushindi huo Simba sasa inafikisha Pointi 9 ikiongoza Ligi kuu ya Vodacom Huko Morogoro pia kulikuwa na mchezo kati ya Yanga ya jijini Dar es salaam na timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Morogoro ambapo msemaji wa klabu hiyo amesema timu Yanga imetoka sare ya magoli 1-1 dhidi ya timu ya Mtibwa Sugar goli la Yanga likifungwa na mchezaji Abdi Kassim

NAIBU WAZIRI WA UINGEREZA ATEMBELEA KITUO CHA AFYA MNAZI MMOJA!!


Naibu Waziri wa Idara inayoshughulikia Misaada ya Kimataifa ya Uingereza (Dfid) Stephen Brian (kushoto) akibadilishana mawazo jana jijini Dar es salaam na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Dkt Asha Mahita(kulia) na Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Mnazi Mmoja Dkt Felister Kwayu(katikati) . Naibu Waziri huyo alitembelea Kituo cha Afya cha Mnazi Mmoja kujionea utaratibu wa utoaji wa vyandarua kwa Mama wajawazito chini ya Mpango wa Hati punguzo. (Picha zote na Vicent Tiganya wa Maelezo Dar es salaam)
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Dkt Asha Mahita (kulia) akitoa ufafunizi jana jijini Dar es salaam kwa Naibu Waziri wa Idara inayoshughulikia Misaada ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) Stephen Brian(kushoto) jinsi Manispaa hiyo inavyosambaza vyandarua kwa wakinamama wajawazito chini ya mpago wa Hati Punguzo kwa ajili ya kukabiliana na malaria.
Naibu Waziri wa Idara inayoshughulikia Misaada ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) Stephen Brian (kulia) akimwangalia mtoto mchanga na mama yake jana jijini Dar es salaam wakiwa katika Kituo cha Afya cha Manazi Mmoja wakisubiri kuandikishwa kwa ajili ya kupata vyandarua vinavyotolewa chini ya utaratibu wa Hati Punguzo kwa mama wajawazito na watoto

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA