Sep 15, 2010

NAIBU WAZIRI WA UINGEREZA ATEMBELEA KITUO CHA AFYA MNAZI MMOJA!!


Naibu Waziri wa Idara inayoshughulikia Misaada ya Kimataifa ya Uingereza (Dfid) Stephen Brian (kushoto) akibadilishana mawazo jana jijini Dar es salaam na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Dkt Asha Mahita(kulia) na Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Mnazi Mmoja Dkt Felister Kwayu(katikati) . Naibu Waziri huyo alitembelea Kituo cha Afya cha Mnazi Mmoja kujionea utaratibu wa utoaji wa vyandarua kwa Mama wajawazito chini ya Mpango wa Hati punguzo. (Picha zote na Vicent Tiganya wa Maelezo Dar es salaam)
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Dkt Asha Mahita (kulia) akitoa ufafunizi jana jijini Dar es salaam kwa Naibu Waziri wa Idara inayoshughulikia Misaada ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) Stephen Brian(kushoto) jinsi Manispaa hiyo inavyosambaza vyandarua kwa wakinamama wajawazito chini ya mpago wa Hati Punguzo kwa ajili ya kukabiliana na malaria.
Naibu Waziri wa Idara inayoshughulikia Misaada ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) Stephen Brian (kulia) akimwangalia mtoto mchanga na mama yake jana jijini Dar es salaam wakiwa katika Kituo cha Afya cha Manazi Mmoja wakisubiri kuandikishwa kwa ajili ya kupata vyandarua vinavyotolewa chini ya utaratibu wa Hati Punguzo kwa mama wajawazito na watoto

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA