Sep 16, 2010

Ridhiwani Kikwete avunja makundi Lindi Mjini!!

Na Richard Mwaikenda, Lindi.
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Lindi mjini kupitIa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mohammed Abdulaziz amewaomba radhi wana CCM aliowakosea wakati wa kinyang'anyiro cha kura za maoni baada ya kutakiwa hivyo na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, Ridhiwani Kikwete ili kuvunja makundi katika jimbo hilo.
Abdulaziz,alifanya hivyo juzi katika kikao cha ndani cha viongozi wa Umoja huo wilayani Lindi juzi, ambapo baadhi ya viongozi walieleza wazi mbele ya Ridhiwani kuhusu kuwepo kwa mgawanyiko mkubwa ambao walidai ulisababishwa na wagombea wawili, Abdulazizi na Maguo pamoja na wapambe wao wakati wa mchakato wa kura za maoni.
Baada ya wanachama kueleza hivyo na Ridhiwani kugundua ufa huo uliopo Lindi mjini na kuhatarisha umoja ndani ya CCM, ndipo akaamua kutumia fursa hiyo kuweka mambo sawa kwa kumtaka Abdulaziz aliyeshinda kura za maoni na kupitishwa na Halmashauri Kuu ya CCM, afanye uungwana kwa kupita kwenye matawi kuwaomba radhi wana CCM ili kuvunja makundi na kurudisha umoja ndani ya chama.
"Mwenye nafasi ya kuvunja makundi ni yule aliyeshinda.Hawa jamaa wametukanwa na kunyanyasika hivyo inatakiwa aliyeshinda ajishushe aende kwenye matawi kuwaomba radhi ili wote wawe kitu kimoja na kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, Mwaka huu,"alisema Ridhiwani huku akishangilia na wanachama.
"Wanachama wenzangu wa CCM, huwa makundi yanakufa moyoni na si machoni kwa mtu, kwani kuna mtu anaweza akakuchekea na kukuambia mambo yameisha, lakini kumbe moyoni bado anayo.Alisema katika kipindi cha harakati za kugombea uongozi makundi yanakuwepo, lakini mchakato ukishapisha na mmoja wao kuteuliwa inatakiwa kuvunja makundi na wote kumuunga mkono aliyeshinda na ndivyo tunavyotakiwa kufanya Jimbo la Lindi Mjini na kingineko". aliongeza Ridhiwani.
Alisema kuwa wakati wa kinyang'anyiro kuwania uongozi ndani ya chama ni kawaida katika kampeni huzuka makundi lakini baada ya kuwapata washindi huvunja mkundi na wote huamua kuwaunga mkono walioshinda.
Baada ya Ridhiwani kumalizia kuzungumza, alikaribishwa Abdulaziz ambaye alisimama na kuwaomba radhi wote aliowakosea na kuahidi kuwa atapita kwenye matawi ya chama jimboni humo kuwaomba radhi ikiwezekana kuwapigia magoti na hata kwa kugharaghara mbele yao.
"Kwa wale wote niliowakosea nawaomba radhi, nitapita kila tawi kuomba radhi ikiwezekana kwa kupiga magoti hata kwa kugharaghara kwani naamini vijijini na mjini wote walinipigia kura ndiyo maana nimeteuliwa kuwa mgombea katika jimbo hili,"Abdulazizi alisema na kuanza kukumbatiana na wanachama kitendo ambacho kiliashiria kumaliza tofauti zao.
Ridhiwani ambaye ameongozana baadhi ya vijana makada wa CCM,anafanya ziara ya kuhamasisha wanaCCM na wafuasi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kuhakikisha wanawapigia wagombea wa chama hicho ili washinde na kuunda dola kwa kipindi kingine cha mikaka mitano.Ziara hiyo ataifanya katika mikoa ya Lindi,Mtwara, Ruvuma, Mbeya, Iringa na Pwani.

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA