Sep 17, 2010

MTANGAZAJI WA RFA KID BWAY' AVAMIWA NA ALIYEJITAMBULISHA KUWA NI MSANII, APOTEZA FAHAMU, HAJITAMBUI HADI SASA.

MTANGAZAJI WA RADIO FREE AFRIKA AMBAYE VILEVILE YU PRODUCER WA KUREKODI MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NDANI YA TETEMESHA PRODUCTION SANDU GEORGE MPANDA MAARUFU KWA JINA LA KID BWAY AMELAZWA HOSPITALI YA BUGANDO MARA BAADA YA KUVAMIWA NA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI NA JAMAA ASIYEFAHAMIKA.

TAARIFA ZINASEMA KUWA KID BWAY AKIWA NYUMBANI KWAKE LUMALA JIJINI MWANZA, JAMAA ALIYEMVANIA ALIFIKA NYUMBANI HAPO MAJIRA YA SAA 2:30 USIKU NA KUJITAMBULISHA KAMA MSANII AKIHITAJI KUFANYA RECORDING, BAADA YA MAZUNGUMZO NA KUJITAMBULISHA ALIKARIBISHWA NDANI HADI CHUMBA CHA KUREKODIA STUDIO.

NYUMBANI KWA MTANGAZAJI HUYO ANAISHI NA JAMAA ZAKE WAWILI AMBAO WAKATI KID AKIMKARIBISHA MTENDA UHALIFU HUO NYUMBANI HAPO JAMAA HAO WALIMWONA KIJANA HUYO KISHA KILA MMOJA AKAINGIA CHUMBANI KWAKE. DAKIKA KADHAA WAKASIKIA KWA KIPINDI KIREFU SPIKA ZA STUDIO ZIKIKOROMA ISIVYO KAWAIDA NA KUANZA KUDADISI HUKU WAKIMWITA KID BWAY KUWA INAKUWAJE! WAKAITA NA KUITA NDIPO WALIPO AMUA KUINGIA STUDIO NA KUMKUTA SAKAFUNI KAANGUKA DABU ZIKIMTOKA MASIKIONI, PUANI NA KWENYE MAJERAHA SEHEMU ZA KICHWA.

KWA HIVI SASA KID YUPO HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO AKIWA HOI HAJITAMBUI YAANI KAPOTEZA FAHAMU, ALITUNDIKIWA DRIPU YA MAJI IKIWA NI HUDUMA YA KWANZA AMBAYO AMEPATIWA JANA MARA BAADA YA KUFIKA HOSPITALINI HAPO AKISUBIRI KIPIMO CHA T SCAN KUONA KWA UNDANI ZAIDI SEHEMU ALIZODHURIKA. HAKUNA TAARIFA YOYOTE YA UPOTEVU WA MALI HALI INAYOPELEKEA WADADISI WA MAMBO KUDHANI KUWA YAWEZEKANA KULIKUWA NA VITA YA KICHINI CHINI AKA BIFU(AMBAYO HAIJAFAHAMIKA).

UCHUNGUZI KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI UNAENDELEA KUFANYWA ILI KUJUA NINI SABABU ZA UVAMIZI HUO.

TAARIFA ZAIDI TUTAENDELEA KUKUJULISHA.
TWAMWOMBA MWENYEZI MUNGU AKUPE NGUVU BROTHER UPATE PONA.

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA