Sep 21, 2010

SERIKALI YASEMA HAKUTAKUWA NA MGAWO WA UMEME WAKATI WA UCHAGUZI!!

NA MAGRETH KINABO – MAELEZO

KAMPUNI ya Borodino kutoka nchini Urusi ya uwekezaji wa umeme imetia saini na Serikali ya Tanzania mkataba wa mradi wa umeme unaozalishwa kwa nguvu ya maji wenye uwezo wa kuzalisha 222 MV wenye thamani ya dola za Marekani milioni 700.

Makubaliano ya mkataba huo, yalitiwa saini jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya hiyo Razmik Tarverdyan katika ukumbi wa mkukutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

Mradi huo unaojengwa katika eneo la Rumakali ,mkoani Iringa unatarajiwa kukamilika mwaka 2018.

Akizungumzia kuhusu jijitahada za Serikali katika masuala ya umeme, Katibu Mkuu huyo, Jairo alisema wizara yake itahakikisha kuwa Tanzania haitarudi nyuma katika masuala ya nishati hiyo ili iweze kuwa chanzo kikuu cha usambazaji wa umeme kwa Afrika Mashariki na ya Kati.

“Tunataka tuondokane na mgawo wa umeme na kuwa na umeme wa kutosha ambao hutasafirishwa nchi za jirani,” alisisitiza Katibu Mkuu huyo Jairo. Huku akiongeza kuwa hawatarajii kuwa na mgawo wa umeme wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Katibu Mkuu huyo alisema vyanzo vya umeme vitaendelezwa mfano vya maji ili kuifanya Tanzania iwe na umeme wa uhakika, tulivu na safi wenye bei nafuu.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya hiyo Tarverdyan alisema mradi huo ni mkubwa katika uwekezaji wa nishati hiyo katika Afrika Mashariki, hivyo wamewekeza fedha hizo ili kubadilisha maisha ya Watanzania hususan walio kwenye eneo hilo .

Mahitaji halisi ya umeme nchini ni MW 897 wakati uzalishaji wa sasa ni zaidi ya MW 600.

DR. SALIM ASEMA NCHI BILA AMANI HAIWEZI KUFANYA SHUGHULI ZA MAENDELEO

Mary Kweka, MAELEZO 21/09/2010

Amani ni msingi wa maendeleo na hivyo ni muhimu kwa nchi yoyote duniani kuhakikisha inalinda na kuidumisha ili iweze kufanya shughuli zake za maendeleo ,kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika Dkt. Salim Ahmed Salim katika Siku ya Amani Duniani.

Dkt Salim, mwanadiplomasia mkongwe amesema kuwa bila amani nchi haiwezi kufanya shughuli za maendeleo na kuongeza kuwa hata pale ambapo maendeleo yameishapatikana huweza kuvurugwa endapo amani itatoweka katika nchi, ambapo mwaka huu kaulimbiu ni Wezesha Uwepo wa Amani.

Kwa nchi ambazo miaka ya hivi karibuni zimejitahidi kupiga hatua za maendeleo na zinaendelea kufanya jitihada kuhakikisha kuwa zinapiga hatua kubwa zaidi ya kudumisha amani ili kuleta maendeleo kwa faida ya wananchi wote”. Alifafanua Mh. Salim.

Amesema migogoro imekuwa ni kikwazo kikubwa kwa shughuli za maendeleo sio tu kwa watu binafsi bali pia kwa taifa kwani nchi nyingi zenye migogoro Barani Afrika zimekuwa zikitumia fedha nyingi kusuluhisha migogoro na kununua silaha badala ya kuelekezwa kwenye huduma za kijamii kama Afya, Elimu ,Maji na zinginezo kuboresha maisha ya wananchi wao.

Matokeo ya migogoro yamesababisha hasara ya kiuchumi inayokadiriwa kuwa wastani wa Dola Bilon kumi na nane kwa kila mwaka kwa sababu ya migogoro na kulifanya Bara la Afrika kujulikana kama bara la mapigano jambo ambalo ni dhahiri linasikitisha.

Akitolea mfano wa nchi zenye migogoro ya muda mrefu kama Somalia, Dkt. Salim amesema ni changamoto kubwa kwa Bara hili na kwa jamii ya kimataifa kwa jumla na kwamba Afika haina budi kuendelea kufanya juhudi kwa kushirikiana na jumuiya ya kimatifa kupata ufumbuzi wa haraka.

Pia amevitaja vyanzo vya vya migogoro kuwa ni umaskini uliokithiri, ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala bora, usambaratishaji wa demokrasia ,utumiaji wa siasa za ukabila na udini kwa maslahi ya muda mfupi ya wanasiasa na kutoheshimu matakwa ya watu wengi katika uchaguzi na kuwataka wanachi kuwa makini zaidi hasa kipindi hiki cha uchaguzi hapa nchini.

Aidha mwandiplomasia huyo amempongeza Dkt. Rais Jakaya Kikwete kwa mchango wake mkubwa katika kumaliza migogoro mbalimbali, ikiwemo migogoro ya ndani kama ya nchi jirani Kenya

Maadhimisho ya siku ya Amani Duniani yamefanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es salaam ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya mwaka wa Amani Barani Afrika kufuatia maamuzi yaliyotolewa na wakuu Nchi na Serikali za Wanachama wa Umoja wa Afrika 31 Agosti 2009.

FM ACADEMIA KUTAMBULISHA VUTA NIKUVUTE MBAGALA KUU!!

BENDI ya muziki wa dansi ya FM Academia Wazee wa
Ngweasuma' Ijumaa Septemba 24 watafanya utambulisho
maalum wa albamu yao mpya ya Vutanikuvute kwenye Ukumbi
wa Nawina Resort Mbagala Kuu.
Mratibu wa Onesho hilo Zahor Said, alisema kuwa usiku huo
maalum wa Ngwasuma utakuwa na burudani mbalimbali ambazo
zitausindikiza utambulisho huo.
Said alisema watafanya utambulisho huo kwa kusindikizwa na
vikundi vya unenguaji vya kiduku.
Alisema utambulisho huo wa albamu ya Vuta nikuvute utakuwa
chini ya Rais waNyoshi El Saadat watapiga nyimbo zote 11
zilizopo kwenye Albamu hiyo ikiwa ni pamoja na nyimbo za
zamani.
Nyimbo zilizobeba albamu hiyo kuwa ni Heshima kwa
Wanawake ambayo ilipata tunzo mwaka jana,Mwili wangu,
Usiku wa juma tano na Jasmini.
Nyimbo zingine ni Angalia shida yangu,Mgeni,Heiken
Ngwasuma,Moses Katumbi,Fadhila kwa mama Intro Ngwasuma
Mathematics na vuta ni kuvute ambayo imebeba jina la albam.
Usiku huo umedhaminiwa na Henkein Bear, Kampuni ya Inoch,
Blog za JaneJohn5, Mamapipiro na Full Shangwe.
Mwisho

Precision Air yazindua ndege yake ya saba mpya!

Precision Air -Shirika la ndege linaloongoza Tanzania, leo imezindua ndege yake ya saba mpya aina ya ATR 72-500 katika sherehe iliyofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere-Terminal Two jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi wa ndege hiyo uliongozwa na Mwenyekiti wa IPP media Bw. Reginald Mengi kama mgeni rasmi na kuhudhuriwa pia na mabalozi, wadau wa biashara wa Precision Air pamoja na wafanyakazi wa shirika la ndege hilo.

Mkurugenzi Mkuu na Meneja

Mwendeshaji wa Precision Air, Bw. Alfonse Kioko alisema, “Mpango wetu wa kuongeza idadi za ndege ni mkakati madhubuti kabisa katika ukuaji wa kampuni na kutimiza huduma iliyo bora kwa wateja.”

Aliendelea: “Kutimia kwa ndege hizi mpya saba ni kuongezea nguvu ndege zetu tatu za zamani, kitu ambacho itatuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuweza kutimiza mahitaji ya wateja wetu kwa gharama nafuu zaidi. Hii ni kwa manufaa yetu sote, sisi na wateja wetu.”

Ndege hii mpya iliwasili tarehe 18 Septemba 2010 kutokea Toulouse-Ufaransa ambapo makao makuu ya ATR na kiwanda cha ndege kilipo. Ndege hizi aina ya ATR zimetengenezwa mahususi kabisa kwa namna ambayo madhara yake kwa mazingira na ya hali ya hewa ni mfinyu mno, kwa maana utoaji wake wa gesi aina ya kaboni ni mdogo. Hakika hii ni hatua na chaguo la kipekee kabisa kwa Precision Air kujali mazingira.

Ndege hiyo yenye usajili nambari 5H-PWG imepewa jina la Kilimanjaro, na imetengenezwa ikiwa na vifaa vya kisasa vya burudani kwa ajili ya wasafiri kuangalia sinema na kusikiliza muziki watakapokuwa wakisafiri. Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 66 tu ili iweze kutoa pia nafasi zaidi kwaajili ya mizigo ya abiria.

“Ndege hii imepewa jina la Kilimanjaro kwa sababu tofauti; Mosi, ni kwa heshima ya mchango mkubwa wa kibiashara ambao Precision inapata kutoka kwa watu wa Kilimanjaro, pili, kila sehemu ambayo ndege hii itakwenda, itatangaza kivutio cha utalii wa mlima mrefu kuliko yote Afrika, na ya mwisho, kama tu jinsi jina lake lilivyo, lengo letu ni kuwa shirika la ndege liliyojuu kuliko yote barani Afrika,” alisema Bw. Kioko.

Ridhiwani uso kwa uso na Chifu wa Wayao Tunduru!

Mlemavu wa viungo,Omar Chutira akitoa shukrani katika mkutano wa kampeni za kuhamasisha ushindi wa kishindo kwa CCM. katika Kata ya Namasakata, Tunduru,baada ya kupatiwa msaada wa sh. 160,000 za kununulia baiskeli ya magurudumu matatu zilizotolewa na Umoja wa Vijana wa CCM kwa maagizo ya Katibu Mkuu wa Chama hicho, Yusufu Makamba kufuatia ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo katika Jimbo la Tunduru.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, Amoni Anastas akihutubia wakati wa mkutano wa kampeni za kuhamasisha ushindi kwa CCM juzi katika Kata ya Namasakata, Tunduru, mkoani Ruvuma.Amon ambaye ni mlemavu wa kuona, ana taaluma ya uanasheria.
Chifu Sultani Kalolo wa Kabila la Wayao, akijadiliana jambo na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ridhiwani Kikwete katika makazi ya chifu huyo katika Kijiji cha Jakika, Tunduru, mkoani Ruvuma juzi. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

Historia na utafiti kwa sanaa ya ubunifu ni muhimu kwa watanzania.

Imeelezwa kuwa ipo haja ya kufanyika utafiti wa kina na kuandika historia ya sanaa ya ubunifu wa mavazi hapa nchi, ili kuifahamisha jamii sanaa ya ubunifu ilikuwaje hapo nyuma, hivi sasa na mueleko wake wa baadae.

Ushauri huo umetolewa na mbunifu maarufu wa mavazi Tanzania Ndugu Mustafa Hassanali alipoluwa akiwasilisha mada ya hali ya sanaa ya ubunifu na changamoto wanazokabiliana nazo wasanii mbalimbali ambao wamejikita katika fani hiyo katika mkutano wa jukwaa la sanaa linalowakutanish wadau wa sanaa kutoka fani tofauti katika ukumbi wa BASATA, Ilala Sharifu Shamba jijini Dar es salaam.

“Ni vizuri tukajua kwa miaka iliyopita jamii ya watanzania walikuwa wakivaa mavazi ya aina gani? na kwa staili ipi?walikuwa wakifungaje vilemba, ni vazi la aina gani lilikuwa likipendwa zaidi, na mambo kama hayo ili kujua kama khanga, kitenge au vazi gani lilikuwa bora kwa wakati ule” Alisema Mustafa Hassanali.

Amesema BASATA iwapo itafanya hivyo itaisaidia jamii kupata taarifa hizo muhimu ambazo zitasaidia kujenga ufahamu wa kutosha wapi fani hii ilianzia, kwa sasa upo vipi na wasanii wafanye kuikuza na kunufaika nayo kama kazi nyingine.

Sambamba na hayo, aliishauri serikali kupitia wizara ya utamaduni na michezo, kuandaa sera ya sanaa ya ubunifu wa mavazi itakayosaidia kutoa muongozo katika sekta hiyo na ya sanaa ya ubunifu ambayo inakuwa siku hadi siku hapa nchini.

Hassanali amesema sambamba na sekta hiyo kukua bado haijatoa ajira tosha kwa wasanii kwani haijafikia uwezo wa kuuza na kufikiwa kwa malengo ya wasanii ambao siku zote wamekuwa mstari wa mbele katika ubunifu.

Aidha Mustafa amesema kuwa itakuwa ni jambo la busara iwapo itaandaliwa siku maalumu ya sanaa hapa nchini, siku itakayoakutanisha wasanii wa fani mbalimbali na kukaa pamoja kuweza kuangalia wapi wametoka, walipo na changamoto mbalimbali zinazowakabli na jinsi ya kukabiliana nazo.

“Siku zote umoja ni nguvu, na itapendeza iwapo wasanii watakutana pamo

ja na kupata fursa ya kujadili na kuzungumza mambo mbalimbali, pamoja na kuibua mbinu mpya za kuleta mafanikio katika fani ya sanaa hapa nchini.

Aidha mbunifu huyo wa mavazi aliongeza kuwa wasanii wa fani ya ubunifu wa mavazi wapatiwe fursa za kushiriki katika matukio mbailimbali yanayoandaliwa na serikali na taasisi mbalimbali kwani wanaowezo wa kutoa mchango mkubwa kufanikisha matukio hayo kupitia kazi zao.

MAKAMU WA RAIS WA SHIRIKA LA HABARI LA XINHUA -CHINA ATEMBELEA TANZANIA.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Clement Mshana (kushoto) akiwa ameongozana na Makamu wa Rais wa Shirika la Habari la Xinhua - China Mr. Liu Yue mara baada ya kumpokea jana usiku katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.Katikati ni Mwakilishi wa shirika hilo nchini Tanzania Bi. Guo Chunju.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Clement Mshana akiwa katika mazungumzo mfupi na Makamu wa Rais wa Shirika la Habari la la Xinhua - China Mr. Liu Yue jana usiku jijini Dar es salaam mara baada ya kumpokea. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Raphael Hokororo, Mshauri wa masuala ya siasa wa ubalozi wa China- Tanzania Mr. Fu Jiqun na Mwakilishi wa shirika Xinhua nchini Tanzania Bi. Guo Chunju.Picha na Aron Msigwa

MAMA SALMA KIKWETE AKIWA KOROGWE!!

Wagombea Ubunge kutoka jimbo la Korogwe Mjini Mkoani Tanga Yussuph Nassir (kulia) na Mgombea wa Jimbo la Korogwe vijijiniProf. Ngonyani Majimarefu wakitambulishwa kwa wanachama wa UWT 20-9-2010 katika mkutano wa ndani wa wanachama wa UWT anmapo Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete amezungumza nao kuhusu umuhimu wa kuja kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu ifikapo Oktoba 31 mwaka huu.Picha na Mwanakombo Jumaa.
Mama Salma Kikwete akiongea na wanachama wa UWT wa Wilaya ya Tanga mjini
Baadhi ya wagombe Udiwani kupitia CCM Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga wakitambulishwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake (WAMA) Mama Salma Kikwete 20-9-2010 katika mkutano wa ndani wakuongea na wanachama wa UWT wa wilaya hiyo kuhusu umuhimu wa kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 31,mwaka huu. Picha na Mwanakombo Jumaa
mtu na Mke wake walikuwa wanachama wa CUF lakini wamekihama chama cha CUF na kujiunga na CCM huko Kabuku Wilaya ya Handeni Mkaoni Tanga.

wamiliki wa kumbi watakiwa kusajili kumbi zao BASATA


Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego akisisitiza jambo.Alisema kwamba,BASATA linatoa muda hadi Desemba mwaka huu wamiliki wote wa kumbi wawe wamesajili kumbi zao vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Mjumbe wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi,Mzee Nkwama Bhalanga alipendekeza kwamba, waandaaji wa matukio ya sanaa wawe wanapewa masharti magumu yakiwemo ya kutaja idadi ya watu wanaohudhuria kwenye onyesho lao na sifa za ukumbi.
Mbunifu wa mavazi maarufu nchini,Mustapha Hassanally naye aliwasilisha mada yake kuhusu Soko la Sanaa ya Ubunifu wa Mavazi Tanzania na Changamoto zinazowakabili.



********** ******** ***********

Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo imetoa miezi mitatu hadi Desemba 31 mwaka huu kwa wamiliki wa kumbi kuhakikisha wanafuata kanuni, taratibu na sheria za kuendesha kumbi zao ikiwa ni pamoja na kuzisajili Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.


Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu BASATA, Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Bw.Seth Kamuhanda alisema kwamba, kumekuwa na ukiukwaji wa makusudi wa sheria,kanuni na taratibu za kuendesha kumbi hali ambayo imekuwa ikisababisha maafa makubwa yakiwemo yale yaliyotokea Tabora mwaka jana na yale ya Sherehe za Idd El Fetri kwenye Ukumbi wa Luxury wilayani Temeke,Dar es Salaam.


“Tatizo kubwa la watanzania, ni kufanya mambo kiholela, kutokufuata sheria, kanuni na taratibu.Hili limekuwa kwenye mazoea na kwa kiasi kikubwa limekuwa likisababisha matatizo mengi yakiwemo majanga kama yale ya Tabora na Temeke kwenye Ukumbi wa Luxury” alisema.


Alisisitiza kwamba, serikali kamwe haiwezi kuendelea kufumbia macho vitendo visivyozingatia sheria hivyo wamiliki wa kumbi lazima wahakikishe wanafanya marekebisho kwenye kumbi zao na kuhakikisha kufikia Desemba mwaka huu zinakuwa ziko kwenye kiwango kinachokubalika kisheria na zimesajiliwa Baraza la Sanaa la Taifa.


“Serikali inasikitishwa sana na vifo ambavyo vimekuwa vikitokea kwenye kumbi za burudani hasa vya watoto na vijana na inaagiza wadau wote wa burudani hasa wamiliki wa kumbi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo zinazosimamiwa na BASATA”, aliongeza.


Awali Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alizitaja sifa za kumbi zinazokubalika kisheria kuwa ni pamoja na kuwa na milango ya kutosha inayofungukia nje,vyoo nadhifu vya wanawake na wanaume, miundombinu kwa walemavu, vifaa vya kuzimia moto, maegesho ya vyombo vya usafiri na ulinzi kamili.


Aidha, alisema kuwa kumbi zote lazima zisajiliwe Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lakini changamoto kubwa ni kasi ndogo ya wamiliki kusajili kumbi zao.Katika hili Katibu Mkuu,Bw.Kamuhanda alisema kwamba, ifikapo Desemba mwaka huu kama kutakuwa na kumbi zitakuwa hazijasajiliwa basi hatua kali za kisheria zichukuliwe.


Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni Bw.Profesa Hermas Mwansoko alisisitiza kwamba, muda uliotolewa kwa wamiliki wa kumbi kurekebisha kumbi zao ili ziendeshwe kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu ni wa mwisho na baada ya hapo hakutakuwa na huruma yoyote.


“Nafasi hii ni ya mwisho kwa wamiliki wa kumbi,BASATA wameshatoa maelekezo yote kuhusu sifa za kumbi.Hatutakuja kukumbushana tena suala hili lazima wamiliki wa kumbi watumie fursa hii iliyotolewa na serikali kufanya marekebisho” aliongeza Profesa Mwansoko.


Pamoja na Jukwaa la Sanaa wiki hii kujikita kwenye suala la kumbi masuala mbalimbali yaliibuka ikiwemo mada ya Soko la Sanaa ya Ubunifu wa Mavazi Tanzania na Changamoto zinazowakabili iliyowasilishwa na mbunifu maarufu wa mavazi Mustapha Hassanaly na kuvuta hisia za wadau wengi.


Wiki ijayo katika Jukwaa la Sanaa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari nchini (MCT) Bw.Kajubi Mkajanga atazungumzia mada ya Vyombo vya Habari na Utandawazi Katika Tasnia ya Sanaa.

Sep 20, 2010

TIMU YA KINONDONI YANYAKUWA UBINGWA WA POOL BAADA YA KUICHAPA TEMEKE!!

Timu ya mkoa wa kinondoni baada ya kutoa ubingwa wakiwa wamenyakua kombe kwa furaha kabisa na ubingwa huo umetokana na kuifunga temeke magoli 15 kwa 10 . Timu ya Kinondoni imenyakua ubingwa wa taifa wa mashindano ya pool baada ya kuifunga Temeke huku mchezaji wa kike Viorety Mrema akitokea Kinondoni akinyakua ubingwa huo na kujishindia tiketi ya kwenda nchini ufaransa mwaka huu kushiriki mashindano ya dunia. Katika mashindano hayo pia mchezaji BONIFACE JOHN kutoka Arusha amenyakua ubingwa kwa upande wa wanaume na kufanikiwa kuitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Pool itakayokwenda nchini Ufaransa Picha kwa hisani ya www.Janejohn5.blog

TPDF na makakati wa kuboresha huduma zake!!

Mwandishi Wetu, JESHI la Wananchi Tanzania (TPDF) limesema litaendelea kushirikiana na kampuni, watu binafsi na mashirika mbalimbali katika kuhakikisha linaboresha huduma za kijamii kwa wanajeshi na familia zao. Akizungumza Dar es Salaam mwishoni mwa wiki Mkuu wa Kitengo cha Maduka, Vinywaji na Mikopo jeshini Meja C.J Kapandamtava alisema hatua hiyo pamoja na kujenga mahusiano na jamii ya kitanzania lakini pia itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wanajeshi wake kupata huduma wanazozitaka kwa wakati kulingana na mahitaji. Meja Kapandamtava aliyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji kipya cha bia ya Kopo ya Heineken 25cl ‘Heineken Balozi ‘ maalumu kwa matumizi ya Jeshi iliyofanyika katika ukumbi wa jeshi wa kambi ya Lugalo Dar es Salaam. Alisema huduma za kijamii zinazopatikana katika maeneo ya makambi ikiwemo vinywaji vya aina mbalimbali havilengi kupata faida na kwamba hatua hiyo ni maalumu kwa wanajeshi kutokana na majukumu ya kitaifa waliyonayo. “Kuzinduliwa kwa kinywaji hiki jeshini kutatufanya tuendelee kuboresha wigo wa upatikanaji wa huduma za kijamii na kama tunavyojua sisi huku kwetu tunatoa huduma zaidi kuliko kulenga faida ikiwa ni utaratibu maalumu kwa jeshi kutokana na majukumu yao kitaifa,’ alisema. Aliwaasa wanajeshi kuitumia huduma hiyo kama ilivyolengwa na kuhakikisha kuwa vinywaji hivyo havipelekwi kwenye maduka uraiani. Kwa upande wake Kanali Harry Andrew Msechu aliyekuwa mgeni rasmi alisema jeshi kama mhimili mmojawapo wa taifa linapaswa kuangaliwa na kupewa huduma zenye ubora wa kimataifa kama kilivyo kinywaji hicho kinachotumiwa na nchi nyingi duniani. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mabibo Benedicta Rugemalira alisema ingawa bia ya Heineken tayari ilikuwepo jeshini katika ujazo wa 33cl bado wameona kuna umuhimu wa kupanua wigo wa kupatikana kwa kinywjai hicho hususani kwa kuzingatia bei. Alisema Heineken 33cl ya chupa yenye shingo fupi kwa kipindi kirefu imekuwa ikitumika jeshini na kuuzwa kwa sh. 1,300/- na kwamba kinywaji hicho kipya cha kopo katika ujazo wa 25cl kimeingizwa jeshini na kitauza kwa sh. 1,000/-. Alisema hatua hiyo ni katika kuwajali wanajeshi kutokana na majukumu mazito waliyonayo katika ujenzi wa taifa na kwamba hiyo ni sehemu ya uwajibikaji wa kampuni hiyo kwa jamii ya kitanzania kulingana na majukumu yanayowakabili. Rugemalira aliongeza kwa kushukuru uongozi wa Makao Makuu ya Jeshi hususani upande wa vinywaji kutokana na ushirikiano mkubwa wanaoupata na kwamba kampuni hiyo itahakikisha mahusiano hayo yanaendelea kudumishwa kadri siku zinavyoendelea. “Tayari tulikuwa na Heineken jeshini lakini kwa ujazo wa 33cl inayouzwa sh. 1,300/- na kwamba bei hii wakati fulani ilikuwa inawanyima haki wale waliokuwa na uwezo mdogo hivyo tumeona tupeleke kinywaji kingine kwa bei ambayo wengi wataimudu,tunawashukuru jeshi kwa ushirikiano wanaotupa,” alisema Rugemalira.

Eric Shigongo aleta Chuo Kikuu mtaani!!

Mwalimu wa Kimataifa wa somo la Ujasiriamali, Eric James Shigongo amesogeza elimu nyumbani kwako na kukupa mafundisho yenye hadhi ya Chuo Kikuu cha Mtaani.
Shigongo atazindua CD inayoitwa Street University (Chuo Kikuu cha Mtaani) hivi karibuni, lengo likiwa kuwawezesha watu mbalimbali kujifunza somo la Ujasiriamali. Akizungumza na gazeti hili wikiendi iliyopita, Shigongo alisema kuwa ameamua kutoa CD hiyo ili kutoa fursa pana kwa wajasiriamali chipukizi kujifunza mbinu mbalimbali za kunufaika kibiashara. “Ndani ya CD hiyo natoa elimu bora kabisa. Elimu ya kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wakubwa. Elimu ya kuwakomboa Watanzania katika mambo ya kiuchumi,” alisema Shigongo na kuongeza: “Nahitaji kuzalisha mabilionea wengi kadiri inavyowezekana, kwahiyo Watanzania wenye kiu ya kutaka kuwa mabilionea, wanaweza kunufaika kupitia CD yangu.” Shigongo aliendelea: “Watu wajiandae kuipata hivi karibuni. Itapatikana kwenye maduka ya Zizzou Fashions.” "Great achievement, involves great risks" Abdallah Mrisho www.abdallahmrisho.blogspot.com

Rais Kikwete Katika mazishi ya Julius Msekwa Dar es Salaam!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu Julius Msekwa ambaye ni mtoto wa Makamu mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwa nyumbani kwao Bongoyo Oysterbay, jijini Dar es Salaam jana jioni.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Julius Msekwa ambaye ni mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwa wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa wazazi wa marehemu , Bongoyo Oysterbay jijini Dar es Salaam jana jioni.Marehemu Julius Msekwa aliyefariki wiki iliyopita huko Nicosia Cyprus ambapo alikuwa akifanya kazi ya mtaalamu Mshauri bingwa katika fani ya teknolojia ya Mawasiliano, alizikwa jana katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete,(wapili kushoto) Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwa(kushoto) na mkewe Mama Anna Abdallah(watatu kushoto) pamoja na Rais mstaafu awamu ya tatu Mzee Ali Hassan Mwinyi(kulia) wakishiriki ibada ya mazishi ya kumuombea Marehemu Julius Msekwa aliyefariki huko Nicosia Cyprus wiki iliyopita na kuzikwa jana katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.(picha na Freddy Maro).

WILLBROAD SLAA KATIKA KAMPENI WILAYANI SIHA

Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akimnadi mgombea ubunge katika jimbo la Hai kupitia chama hicho, Freeman Mbowe, wakati wa mkutano wa kampeni zilizofanyika Bomang'ombe mjini jana. (Picha na Joseph Senga)
Waendesha pikipiki wakiwa katika maandamano ya msafara wa mghombea urais wa TanzaNia kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, kuelekea katika mikutano yake ya kampeni katika jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro jana. (Picha na Joseph Senga)
Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edwin Mtei, akiwahutubia wanachi wa Siha mkoani Kilimanjaro, wakati wa mkutano wa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa (kulia) juzi. (Picha na Joseph Senga)

PPF Stakeolders Conference cocktail at Naura Springs Arusha!!

NBC Marketing Manager Mr. William Kallaghe speaking during a cocktail hosted in Arusha recently. The Bank hosted the cocktail for the 20th PPF Stakeolders Conference.(left) is NBC MD Mr. Lawrence Mafuru.

NBC MD Mr. Lawrence Mafuru (left) speaking to guests during a cocktail hosted by the bank at Naura Springs Hotel in Arusha during the recently concluded 20th PPF stakeholders’ conference

Participants of the 20th PPF Stakeholders Conference chat during a cocktail hosted by the National Bank of Commerce in Arusha recently.

Participants of the 20th PPF Stakeholders Conference chat during a cocktail hosted by the National Bank of Commerce in Arusha recently.

President Kikwete opens the African Court on Human and Peoples' Rights 18th Session n Dar es Salaam!!

The President of the African Court on Human and People’s Rights Jean Mutsinzi escorts President Jakaya Mrisho Kikwete out of the Golden tulip hotel in Dar es Salaam shorly after President Kikwete opened the 18th Ordinary Session of the African Court on Human and People’s Rights this morning.
President Jakaya Mrisho Kikwete in a group picture with Judges of the African Court On huma and People’s Rights shortly after the opening of the Court’s 18th Ordinary Session held the Golden Tulip Hotel in Dar es Salaam this morning.
President Jakaya Mrisho Kikwete in a group picture with Judges of the African Court On huma and People’s Rights shortly after the opening of the Court’s 18th Ordinary Session held the Golden Tulip Hotel in Dar es Salaam this morning.

BAHATI NASIBU YA KUSISIMUA SUPA PESA YAZINDULIWA RASMI NCHINI!

Bahati nasibu ya kipekee inayojulikana kama SUPA PESA itakayowawezesha watumiaji wa simu kujishindia mamilioni ya pesa kila siku imezinduliwa rasmi nchini jana.

Akiongea kwenye uzinduzi wa bahati nasibu hiyo mkurugenzi wa Supa pesa Bwana Harm Fourie alisema “SUPA PESA ni bahati nasibu inayohusisha ujumbe mfupi wa simu ambayo ni kama mchezo utakaowawezesha wahusika kubahatisha kushinda zawadi za pesa, vocha na nyinginezo nyingi kirahisi tu kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu. Kutakuwa na droo na zawadi za kila siku na ya kila wiki itakayowawezesha wateja kushindania zaidi ya tshs milioni 25 kila wiki.

Supa Pesa inahusisha watumiaji wa simu wa mitandao yote ambayo ni Zain, Tigo, Vodacom na Zantel kwa gharama ya Tshs 500 tu. Baada ya kutuma ujumbe mfupi, mhusika atatumiwa ujumbe wa kumuidhinisha kushiriki kwenye droo. Baada ya hapo mitambo ya kisasa kabisa inachagua washindi bila mpangilio maalumu.

Mr Fourie aliongeza kusema “Supa Pesa itajikita kuisaidia jamiii haswa kwenye maswala ya elimu. Tunaelewa kwamba serikali ina changamoto kubwa sana kwenye hili swala na tunaamini kuwa elimu ina mchango mkubwa sana katika maendeleo ya jamii. Tunapenda kujihusisha moja kwa moja kwenye kutoa mchango utakaoleta mabadiliko katika maisha ya watanzania.

Msemaji mkuu wa Supa Pesa Nancy Sumari alinukuliwa akisema “kutakuwa na droo za kila siku kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa ambapo washindi watatu watajinyakulia Tshs milioni 1 kila siku. Washindi hao watajulishwa ushindi wao kupitia ujumbe mfupi wa simu na watatumiwa hela zao ndani ya masaa 24 kupitia huduma ya malipo ya Mpesa kutoka Vodacom. Pia kutakuwa na droo ya kila Ijumaa itakayohusisha wale wote waliotuma zaidi ya SMS nne (4) katika wiki hiyo,mshindi atajinyakulia Tshs. Milioni Kumi. Mshindi huyu wa wiki atapigiwa simu kupitia redio ya Clouds FM kujulishwa kuhusu ushindi wake. Dhumuni kubwa ni kuhakikisha tunawafurahisha wateja wetu kwa kutajirisha maisha ya watu wengi kwa kutoa washindi wengi kila wiki. Bahati nasibu hii ni rahisi sana kushiriki hivyo tunawahimiza watanzania wengi washiriki na kushinda na SUPA PESA!“

Supa pesa imepanga kwenda na wakati na kujumuisha mambo mbalimbali ya kufurahisha kwenye kuendesha mchezo huu ili kuhakikisha kuwa inawaridhisha wateja wake kwa kutajirisha na kubadilisha maisha yao.

MWAMVITA MAKAMBA AWAPA SOMO WAHITIMU WA JITEGEMEE SEKONDAR!!

Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akimkabidhi Mwanafunzi Anyelwisye Mwakibinga cheti cha kutambuliwa kama kiongozi bora wa Scout katika shule ya JKT Jitegemee kwenye mahafali ya 26 ya kidato cha nne shuleni hapo, wanaoshuhudia kulia ni Kaimu Mkuu wa shule hiyo Meja Michael Mtenjele na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule Raymond Mpazi.
Baadhi ya wanafunzi wavulana wa JKT Jitegemee wa kidato cha Nne walioshiriki katika mahafali ya 26 yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo.
Baadhi ya wanafunzi wasichana wa JKT Jitegemee wa kidato cha Nne walioshiriki katika mahafali ya 26 yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo.

Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akimkabidhi Mwanafunzi Mwanahawa Amiry cheti pamoja na zawadi kwa kufanya vizuri katika kipaji cha kucheza ngoma za asili katika shule ya JKT Jitegemee kwenye mahafali ya 26 ya kidato cha nne yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo, katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo Raymond Mpazi.

. Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akimkabidhi Mwanafunzi Anyelwisye Mwakibinga cheti cha kutambuliwa kama kiongozi bora wa Scout katika shule ya JKT Jitegemee kwenye mahafali ya 26 ya kidato cha nne shuleni hapo, wanaoshuhudia kulia ni Kaimu Mkuu wa shule hiyo Meja Michael Mtenjele na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule Raymond Mpazi.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA