Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
Oct 19, 2010
Rais Jakaya Kikwete katika kampeni Mkuranga.
WAANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU KUTOKA SADC WAWASILI NCHINI.
Oct 18, 2010
Ziara ya Mama Salma Kikwete- Rukwa
MAISHA BILA UONI YANAWEZEKANA!
JAKAYA KIKWETE ALIPOITEKA KAWE
- Waiaga CUF na kuchukua kadi za CCM
- Waahidi wengi zaidi wanakuja nyuma yao visiwani humo
Wakongwe wawili wa siasa za vyama vingi visiwani Zanzibar Mheshimiwa Fatma Maghimbi na Juma Othman Juma wamerudisha kadi zao za CUF na kuchukua za CCM leo jimboni Kawe jijini Dar es salaam na kuahidi wenzao wengi watafuata nyayo zao kutoka CUF.
Akielezea sababu zake za kurudi CCM, Juma Othman Juma amesema ameguswa kwa kazi kubwa aliyofanya Mheshimiwa Kikwete Tanzania Bara na Visiwani hususan aliporejesha amani na utulivu visiwani Unguja na Pemba kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Alisema tangu historia ya vyama vingi ianze Tanzania, kila wakati wa uchaguzi wananchi wengi wa visiwa vya Unguja na Pemba hulazimika kukimbia visiwani humo kwa kuhofia hali ya kutokuwa na usalama katika kipindi hicho.
"Lakini sasa napenda kumshukuru sana Mheshimiwa Kikwete kwa kurudisha heshima ya nchi yetu duniani kwani mwaka huu wa kampeni, hakuna hata mmoja aliyehama visiwani humo kukimbia uchaguzi" alimaliza Juma Othman akishangiliwa na umati mkubwa wa wana CCM waliojitokeza kwenye mkutano huo wa kampeni.
Mama Fatma Maghimbi amewahi kuwa waziri kivuli wa Katiba na Sheria ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kama mbunge wa Chama Cha Wananchi CUF. Naye Juma Othman Juma amewahi kuwa muanzilishi wa Chama Cha Siasa visiwani kabla ya kujiunga na Chama cha Wananchi CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Mh. Jakaya Kikwete akimnadi Mama Kizigha, mgombea ubunge wa CCM jimbo la kawe leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Parkers jijini Dar es salaam. Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge, na Madiwani unatarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu nchini kote. (Picha na Muhidin Issa Michuzi) |
sehemu ya nyomi uwanja wa Tanganyika Packers, Kawe, jijini Dar leo |