Oct 19, 2010

WAANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU KUTOKA SADC WAWASILI NCHINI.

Mwenyekiti wa waangalizi wa uchaguzi mkuu kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika (SADC) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia Kabinga Pande (kulia) akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa siasa, waandishi wa habari na waangalizi wa uchaguzi kutoka SADC juu ya ujio wa ujumbe wa waangalizi hao na majukumu yao wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 31 mwezi huu leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine ametoa wito kwa watanzania kudumisha amani na kuonyesha ukomavu wa kisiasa uliopo nchini hasa kabla na baada ya uchaguzi. (Picha Aron Msigwa na Fullshagwe Crew)
Baadi yAAa Wanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nao pia walikuwepo.
Baadhi ya Mabalozi na wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.
Mchungaji Christopher Mtikila ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party DP akiuliza swali kwa waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi mkuu kutoka SADC ambao walikutana na waandishi wa habari leo kwenye Hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam.
Washiriki wa mkutano wa ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi mkuu kutoka nchi za SADC wakifuatilia masuala mbalimbali leo jijini Dar es salaam.

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA