Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Lukumanda Kata ya Ufana Wilaya ya Babati Vijijini, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika jana.
Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbulu, Philp Marmo wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Wilaya ya Mbulu jana.
Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, DK. Mohamed Gharib Bilal akipokea kadi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Tawi la NCCR Mageuzi Kijiji cha Guse, Lucas Albin aliyerejesha kadi ya chama chake na kujiunga na CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Lukumanda Wilaya ya Babati Vijijini Mkoa wa Manyara jana.
Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akitoka katika uwanja wa mkutano wa Kijiji cha Lukumanda baada ya kumaliza mkutano wa kampeni jana
Wananchi wa Kijiji cha Endabash Kata ya Endabash Wilaya ya Karatu, wakimsikiliza mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk Mohamed Gharib Bilal, wakati alipofanya mkutano wa kwanza wa kampeni katika Wilaya hiyo jana.Picha na Muhidin Sufiani.
No comments:
Post a Comment