Oct 17, 2010

YANGA WATUA DAR KWA SHANGWE

Beki mahiri wa timu ya Yanga na timu ya Taifa Taifa Stars Nadir Haroub (Cannavaro) akihojiwa na vyombo mbalimbali vya habari kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere leo mara baada ya timu hiyo kuwasili ikitokea mkoani Mwanza ambako ilicheza mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati yake na watani wao wa jadi timu ya Simba zote za jijini Dar es salaam. Katika mchezo huo Mchezaji Jerrison Tegete ndiye aliyefunga goli katika dakika ya 71 kipindi cha pili ambapo kwa mujibu wa mtangazaji wa TBCEnock Bwigane aliyekuwa akitangaza mchezo huo Jerry Tegete akiwa na mpira alimuita golikipa wa Simba Juma K. Juma na kumwambia "Poooooooooooooooooooooo!!!!" wakati kaseja akishanga jina hilo ndipo tegete akafunga goli safi lililoipa ushindi timu hiyo ya Jangwani na matokeo kuwa Yanga 1-Simba 0.
Nadir Haroub Cannavaro akisindikizwa na mashabiki wa timu hiyo mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa J.K.Nyerere leo.
Kiungo wa timu ya Yanga Nurdin Bakari naye alikuwemo klatika msafara huo.
Mchezaji Athman Idd (Chuji ) akitoka kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere huku akiongea na simu mara baada ya timu hiyo kuwasili jijini Dar es salaam leo.

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA