Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekitunuku Chama Cha Mawakili cha Tanzania Bara kwa kifupi "CHAMA" hadhi ya uangalizi wa uchaguzi mkuu ujao, kwa mara ya kwanzachama kitasambaza wanachama wake katika mikoa kumi ya Tanzania bara yote ili kushiriki katika uangalizi wa vituo vya uchaguzi, pia kufuatilia mchakato mzima wa kampeni za uchaguzi. Chama hiki ni chama cha Wanasheria wa Tanzania Bara kama jukumu lake chama kinatetea mfumo wa jamiiambapo haki na sheriavinaheshimiwa shabaha kuu ya chama kipindi kinachoelekea uchaguzi mkuu ni kwamba uchaguzi ufanyika kwa utaratibu unaokidhi utawala wa sheria na unaoshabihiana na viwango bora na uzoefu wa kimataifa. Kwa usemi wa rais wa chama Bwna Felix George Kibodya ni msimamo wetu kwamba matakwa ya wananchi yawe msingi wa mamlaka ya serikali Jambo hili ndiyo mwanzo na hatima ya usimamizi wetu wa uchaguzi mkuu ujao. Kwa lengo hili chama kimeanda Ilani ya uchaguzi inayofafanua shabaha na mchango wa chama chetu kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika tarehe 31 Oktoba 2010 nchini kote, Shabaha zinazotajwa zitaweka misingi ya mchakato wetu wa ufuatiliaji na uangalizi. Siku ya Uchaguzi kila mwanaglizi atafuatilia shughuli zinjavyoendelea katika vituo vya uchaguzi hususan atafuatilia matukio ya ukiukaji wa taratibu za upigaji kura, usalama na hujuma kwa makasha ya kura, Hitirafu za kuhesabu kura na uandishi wa matokeao. Wanachama wetu watasambazwa Tanzania Bara katika mikoa 10 yaani Tanga, Arusha, Tabora, Mwanza, Tanga, Dodoma, Dar es salaam, Mbeya, Mtwara,Kilimanjaro na Mara, Bw. Felix Kibodya amesema chama hicho pia kitapokea taarifa mbalimbali kutoka kwa wananchi zinazohusiana na uchaguzi kupitia ujumbe utakaotumwa kwa nja ya simu za mkononi katika mitandao yote ya simu wakituma kwa kuandika neno Tufumbue acha nafasi kisha wataandika ujumbe na kuutuma katika namba 15540 gharama ikiwa ni shilingi 150 kwa ujumbe mmoja. Baada ya kumaliza uangalizi wake chama kitatangaza tathmini wiki mbili baadae mara baada ya uchaguzi na matokeo kutangazwa.
Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ME MYSELF & I
THE DON HIMSELF
Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)
No comments:
Post a Comment