Oct 18, 2010

JAKAYA KIKWETE ALIPOITEKA KAWE

-Kaongozana na Juma Othman Juma

- Waiaga CUF na kuchukua kadi za CCM

- Waahidi wengi zaidi wanakuja nyuma yao visiwani humo

Wakongwe wawili wa siasa za vyama vingi visiwani Zanzibar Mheshimiwa Fatma Maghimbi na Juma Othman Juma wamerudisha kadi zao za CUF na kuchukua za CCM leo jimboni Kawe jijini Dar es salaam na kuahidi wenzao wengi watafuata nyayo zao kutoka CUF.

Akielezea sababu zake za kurudi CCM, Juma Othman Juma amesema ameguswa kwa kazi kubwa aliyofanya Mheshimiwa Kikwete Tanzania Bara na Visiwani hususan aliporejesha amani na utulivu visiwani Unguja na Pemba kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Alisema tangu historia ya vyama vingi ianze Tanzania, kila wakati wa uchaguzi wananchi wengi wa visiwa vya Unguja na Pemba hulazimika kukimbia visiwani humo kwa kuhofia hali ya kutokuwa na usalama katika kipindi hicho.

"Lakini sasa napenda kumshukuru sana Mheshimiwa Kikwete kwa kurudisha heshima ya nchi yetu duniani kwani mwaka huu wa kampeni, hakuna hata mmoja aliyehama visiwani humo kukimbia uchaguzi" alimaliza Juma Othman akishangiliwa na umati mkubwa wa wana CCM waliojitokeza kwenye mkutano huo wa kampeni.

Mama Fatma Maghimbi amewahi kuwa waziri kivuli wa Katiba na Sheria ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kama mbunge wa Chama Cha Wananchi CUF. Naye Juma Othman Juma amewahi kuwa muanzilishi wa Chama Cha Siasa visiwani kabla ya kujiunga na Chama cha Wananchi CUF.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Mh. Jakaya Kikwete akimnadi Mama Kizigha, mgombea ubunge wa CCM jimbo la kawe leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Parkers jijini Dar es salaam.
Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge, na Madiwani unatarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu nchini kote. (Picha na Muhidin Issa Michuzi)
Bw. Juma Othman Juma akiwa na Mama Fatma Maghimbi baada ya kurejesha kadi za CUF na kupewa za CCM leo.
Msanii wa Bongo Fleva Diamond akitumbuiza leo Kawe kwenye mkutano wa kampeni wa Jakaya Kikwete
Nyomi uwanja wa Tanganyika Packers kwenye mkutano wa kampeni wa Jjakaya Kikwete leo.
sehemu ya nyomi uwanja wa Tanganyika Packers, Kawe, jijini Dar leo

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA