Oct 16, 2010

MAPACHA WA3 WAZINDUA "JASHO LA MTU" KWA MBWEMBWE TRAVELTINE!

Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka ambaye alikuwa mgeni rasmi akizindua rasmi albam ya kundi la Mapacha WA3 inayoitwa Jasho la Mtu katika uzinduzi wa nguzu uliofanyika kwenye hoteli ya Traveltine Magomeni jijini Dar es salaam, kundi la Mapacha WA3 linaundwa na Mwanamuziki Josse Marra kutoka FM Academia, Kalala Junior na Harid Chokoraa. Katika picha kulia ni Bw. Ahmed Magoma na kushoto mwisho ni Bw. Bitusi Mkurugenzi wa B2C Transport katikati ni Masoud Wanani Mkurugenzi wa CDS wakishuhudia uzinduzi huo.
Mwimbaji Harid Chokoraa akionyesha uwezo wake katika kucheza wakati wa onesho la uzinduzi wa albam yao inayoitwa Jasho la Mtu kundi hilo la Mapacha wa3 lilikonga nyoyo za mashabiki na kuwakuna vilivyo usiku wa kuamkia leo kwenye hoteli ya Travltine Magomeni jijini Dar es salaam kulia ni Kalala Junio na kushoto ni Josse Marra.
Mzee Yusuf mwimbaji wa muziki wa Taarab na Kiongozi wa bendi ya taarab ya Jahazi Molden Taarab akiimba huku akiwa amezungukwa na vimwana jukwaani wakati aliposhiriki katika uzinduzi wa albam ya Mapacha wa3 inayoitwa Jasho la Mtu.
Queen Suzy kichaa wa Jukwaani mnenguaji wa bendi ya Frican Stars akifunika na shoo yake matata.
Mamaa Monica kushoto naye akajimwaga stejini na rafiki yake huku mzee akiwa jukwaani akifanya mambo makubwa.
Sasa ni zamu ya wanenguaji hawa hebu wacheki mdau kazi kwako.
Vijana Twende Kazi! Mwanamuziki wa FM Academia Josse Mara akiongoza wanenguaji pamoja na wanamuziki wenzake wanaounda kundi la Mapacha wa3 katika kuzindua albam yao ya Jasho la Mtu ulifanyika usiku wa kuamkia leo kwenye hoteli ya Traveltine Magomeni jijini Dar es salaam ukisindikizwa na bendi ya African Stars na Mzee Yusuf kutoka Jahazi Molden Taarab.
Huyu alikuwa mjamzito lakini yeye akaamua kuja kwenye onesho la mapacha watatu na hatimaye akawazaa mapacha watatu palepale Traveltine Magomeni ambao ni Josse Mara wa FM Academia, Harid Chokoraa na Kalala Jujior ambao jana walizindua albam yao ya Jasho la Mtu.
Rapa wa bendi ya Frican Stars anayeitwa Furgason akicheza na mmoja wa wanenguaji wa bendi ya African Stars jana usiki wakati wa onesho la uzinduzi wa albam ya Jasho la Mtu.
Mamaa Lwiza Mbutu Kiongozi wa bendi ya African Stars kulia akiongoza wanamuziki wenzaka katika kucheza shoo ya nguvu kwenye uzinduzi wa albam ya Jasho la Mtu ya Mapacha wa3.
Mwanamuziki mkongwe Mafumu Bilal Bombenga akijilipua kwa shoo kali jukwaani wakati wa onesho la uzinduzi wa Albam ya Mapacha wa3 inayoitwa "Jasho la Mtu" kwenye ukumbi wa Traveltine Magomeni.

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA