Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
Sep 20, 2010
Eric Shigongo aleta Chuo Kikuu mtaani!!
Rais Kikwete Katika mazishi ya Julius Msekwa Dar es Salaam!!
WILLBROAD SLAA KATIKA KAMPENI WILAYANI SIHA
PPF Stakeolders Conference cocktail at Naura Springs Arusha!!
NBC Marketing Manager Mr. William Kallaghe speaking during a cocktail hosted in Arusha recently. The Bank hosted the cocktail for the 20th PPF Stakeolders Conference.(left) is NBC MD Mr. Lawrence Mafuru.
Participants of the 20th PPF Stakeholders Conference chat during a cocktail hosted by the National Bank of Commerce in Arusha recently.
Participants of the 20th PPF Stakeholders Conference chat during a cocktail hosted by the National Bank of Commerce in Arusha recently.
President Kikwete opens the African Court on Human and Peoples' Rights 18th Session n Dar es Salaam!!
BAHATI NASIBU YA KUSISIMUA SUPA PESA YAZINDULIWA RASMI NCHINI!
Bahati nasibu ya kipekee inayojulikana kama SUPA PESA itakayowawezesha watumiaji wa simu kujishindia mamilioni ya pesa kila siku imezinduliwa rasmi nchini jana.
Akiongea kwenye uzinduzi wa bahati nasibu hiyo mkurugenzi wa Supa pesa Bwana Harm Fourie alisema “SUPA PESA ni bahati nasibu inayohusisha ujumbe mfupi wa simu ambayo ni kama mchezo utakaowawezesha wahusika kubahatisha kushinda zawadi za pesa, vocha na nyinginezo nyingi kirahisi tu kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu. Kutakuwa na droo na zawadi za kila siku na ya kila wiki itakayowawezesha wateja kushindania zaidi ya tshs milioni 25 kila wiki.
Supa Pesa inahusisha watumiaji wa simu wa mitandao yote ambayo ni Zain, Tigo, Vodacom na Zantel kwa gharama ya Tshs 500 tu. Baada ya kutuma ujumbe mfupi, mhusika atatumiwa ujumbe wa kumuidhinisha kushiriki kwenye droo. Baada ya hapo mitambo ya kisasa kabisa inachagua washindi bila mpangilio maalumu.
Mr Fourie aliongeza kusema “Supa Pesa itajikita kuisaidia jamiii haswa kwenye maswala ya elimu. Tunaelewa kwamba serikali ina changamoto kubwa sana kwenye hili swala na tunaamini kuwa elimu ina mchango mkubwa sana katika maendeleo ya jamii. Tunapenda kujihusisha moja kwa moja kwenye kutoa mchango utakaoleta mabadiliko katika maisha ya watanzania.
Msemaji mkuu wa Supa Pesa Nancy Sumari alinukuliwa akisema “kutakuwa na droo za kila siku kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa ambapo washindi watatu watajinyakulia Tshs milioni 1 kila siku. Washindi hao watajulishwa ushindi wao kupitia ujumbe mfupi wa simu na watatumiwa hela zao ndani ya masaa 24 kupitia huduma ya malipo ya Mpesa kutoka Vodacom. Pia kutakuwa na droo ya kila Ijumaa itakayohusisha wale wote waliotuma zaidi ya SMS nne (4) katika wiki hiyo,mshindi atajinyakulia Tshs. Milioni Kumi. Mshindi huyu wa wiki atapigiwa simu kupitia redio ya Clouds FM kujulishwa kuhusu ushindi wake. Dhumuni kubwa ni kuhakikisha tunawafurahisha wateja wetu kwa kutajirisha maisha ya watu wengi kwa kutoa washindi wengi kila wiki. Bahati nasibu hii ni rahisi sana kushiriki hivyo tunawahimiza watanzania wengi washiriki na kushinda na SUPA PESA!“
Supa pesa imepanga kwenda na wakati na kujumuisha mambo mbalimbali ya kufurahisha kwenye kuendesha mchezo huu ili kuhakikisha kuwa inawaridhisha wateja wake kwa kutajirisha na kubadilisha maisha yao.
MWAMVITA MAKAMBA AWAPA SOMO WAHITIMU WA JITEGEMEE SEKONDAR!!
Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akimkabidhi Mwanafunzi Mwanahawa Amiry cheti pamoja na zawadi kwa kufanya vizuri katika kipaji cha kucheza ngoma za asili katika shule ya JKT Jitegemee kwenye mahafali ya 26 ya kidato cha nne yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo, katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo Raymond Mpazi.
. Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akimkabidhi Mwanafunzi Anyelwisye Mwakibinga cheti cha kutambuliwa kama kiongozi bora wa Scout katika shule ya JKT Jitegemee kwenye mahafali ya 26 ya kidato cha nne shuleni hapo, wanaoshuhudia kulia ni Kaimu Mkuu wa shule hiyo Meja Michael Mtenjele na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule Raymond Mpazi.
Tanzania imepewa Tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Millenium Development Goals (MDGs) 2010 !!
Ridhiwani katika kampeni Masasi na Nanyumbu!!
MASHINDANO YA VODACOM LATHAM OPEN 2010 YAFANA HUKO SINDA KISIWANI!!
Washiriki wa mashindano ya kuvua samaki ya Vodacom Lathan Open 2010 waliokuwa wakiendesha boti ya Natasha wakishangilia kwa kunyoosha vidole vyao juu mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao za ushindi wa kuvua samaki wengi zaidi, mashindano hayo yamefanyika jana kwenye kisiwa cha Sinde kwenye Bahari ya Hindi, kushoto ni Necta Foya Meneja wa Mawasiliano Vodacom
Bw. David Sutton wa boti ya uvuvi ya Simba kulia akionyesha zawadi yake aliyoipokea kutoka kwa Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza mara baada ya boti yao kuwa miongoni mwa washindi wa jumla walioshinda kuvua samaki wengi zaidi katika mashindano ya Vodacom Lathan Open 2010 yaliyofanyika kwenye kisiwa cha Sinda jana, kushoto ni Necta Foya Meneja wa Mawasiliano Vodacom Tanzania.
Sep 18, 2010
Pinda Amwakilisha JK Umoja Wa Mataifa.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda na mkewe Mama Tunu Pinda wakizungumza na Balozi wa Tanzania umoja wa Mataifa Ombeni Sefue (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mwanaidi Maajar baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa JFK jijini New York leo kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo ya Millenia. (Picha:Ofisi ya Waziri Muu)
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA KUENDELEA KULINDA HAKI ZA WATOTO NCHINI!!
Na. Mary Kweka – MAELEZO.
Dar es Salaam.
Tume ya haki za Binadamu na Utawala bora imesema itaendelea kulinda, kutetea , na kushughulikia malalamiko mbalimbali ya uvunjwaji wa Haki za binadamu kwa watoto nchini.
Kauli hiyo ilitolewa jana Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Kiongozi Mstaafu Ramadhani Manento wakati akizungumza na viongozi wa mabaraza ya watoto waliofanya ziara ofisi kwake ikiwa ni sehemu ya kongamano lao la mwaka huu linalomalizika leo ( jumamosi) jijini Dar es salaam.
Alisema ili kujenga taifa bora lenye maadili , jamii inao wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa watoto wanalindwa na kuthaminiwa pamoja na kupatiwa mahitaji mbalimbali yakiwemo Elimu, Malazi bora, haki ya kupendwa, uhuru wa kucheza na kutoa maoni.
Aliongeza kuwa katika kulinda na kutetea haki za watoto, Serikali kupitia tume ya haki za binadamu na Utawala Bora imeanzisha Dawati la watoto ambalo linawajibika na kupokea malalamiko mbalimbali ya uvunjwaji wa haki za biadamu kwa watoto.
“Dawati la watoto linawajibika kulinda na kutetea haki za watoto wanaoishi katika mazingira magumu, walioachishwa shule,matatizo ya miradhi, utekelezaji wa sheria ya ubakaji wa watoto kwa watuhumiwa na mazingira ya watoto walio magerezani “Alifafanua Jaji Manento.
Aliendelea kufafanua kuwa Dawati hilo linatoa elimu kwa watu hasa wazazi kutambua umuhimu wa haki za watoto na kuwa makini pale wanapotoa adhabu kwa watoto huku akitoa angalizo kwa wazazi kuwa makini na adhabu hizo kuwa ziwe na vikomo na si zakuwajeruhi watoto na kuwasababishia ulemavu na kuwapotezea maisha.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utafiti na Nyaraka wa tume hiyo Bi Epifania Mfundo alisema mwaka huu dawati la watoto limepokea jumla ya malalamiko 114 mpaka sasa, na wamefanikiwa kushughulikia malalamiko 28 kati ya 114 yaliyowasilishwa kwenye tume ya haki za binadamu na utawala bora.
Rais Kikwete katika kampeni Mbulu na Babati!!
Sep 17, 2010
Mrembo Julieth kuwakilisha Tanzania katika shindano la Miss Progress Italia!
Nape Nape Nnauye ateuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi
Benjamin Sawe
Maelezo
Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua ndugu Nape Moses Nnauye kuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.
Bwana Nnauye amechukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi Said Ali Amanzi ambaye amebadilishiwa kituo chake cha kazi na kuhamishiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Kabla ya uteuzi huo Ndugu Nnauye alikuwa ni Katibu Msaidizi Idara ya Siasa na Mahusiano ya Kimataifa CCM Makuu Dar es Salaam wakati Bwana Said Ali Amanzi amechukua nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Ndugu Cleopas Rugarabamu ambaye alifariki mwezi Julai mwaka huu akiwa kwenye matibabu nchini India.
SERIKALI KUNUNUA MAHINDI YA WAKULIMA- AGIZO LA RAIS JAKAYA KIKWETE!
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
SERIKALI imetoa sh. bilioni 23.8 kwa ajili ya kununua mahindi tani 200,000 kutoka kwa wakulima wa ili kuweza kuyahifadhi katika Hifadhi ya Taifa kwa ajili ya matumizi ya baadae, vikiwemo vifaa vingine kama vile ni mizani , dawa za kufukuzia wadudu na mashine.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira jijini Da res Salaam jana(leo) ambapo alisema Rais Jakaya Kikwete ameagiza tani 400, 000 za mahindi zinunuliwe ikiwa ni lengo la Serikali katika kuyahifadhi mahindi hayo ambayo uzalishaji wake umeongezeka katika kipindi cha mwaka .
“ Serikali imeshatoa fedha hizo ili kuweza kununua tani hizo katika kipindi cha msimu huu”alisema Waziri Wasira huku akifafanua kwamba tayari serikali imeshanunua tani za mahindi 52,000 katika kipindi cha msimu huu hivyo ifikapo mwisho wa mwezi huu ambazo tani za mahindi 105,000 za mahindi zitakuwa zimenunuliwa na Serikali .
Aliongeza pia Serikali itaomba fedha nyingine sh. bilioni 33 kutoka Hazina kwa ajili ya kununua tani za mahindi nyingine za mahindi 95,000 ili kufikisha lengo la awamu ya kwanza ya ununuaji wa mahindi hayo ambayo jumla yake ni tani 200,000.
Hata hivyo aliongeza kwamba baada ya ununuzi huo watafanya tathimini ili kuweza kufikisha lengo la kununua tani nyingine za mahindi 200,000 zilizobakia kama ilivyoagizwa na Rais Kikwete.
Waziri Wasira alisema hifadhi ya Taifa hivi sasa ya ina tani za 52,000 zilizonunuliwa msimu huu na nyingine tani za mahindi za awali 47,000. Hata hivyo alisema uwezo wake wa kuhifadhi ni tani 240,000.
Akizungumzia kuhusu uzalishaji wa mahindi katika kipindi cha mwaka huu alisema umeongezeka,hivyo hayo ni mafanikio mazuri kutokana na hali ya hewa ilikuwa nzuri.
Alisema katika kipindi cha mwaka huu uzalishaji wa mahindi umeongezeka hadi kufikia tani milioni 4.7 wakati katika kipindi cha mwaka jana ulikuwa tani milioni 3.5.
“ Uzalishaji huu katika kipindi cha mwaka jana ulituwezesha kuwalisha watu milioni mbili wa mikoa yote iiliyokuwa na uhaba wa chakula ya kanda ya Kaskazini bila ya kuagiza chakula toka nje ya nchi au kuomba msaada wa namna hiyo,” alisema Waziri Wasira.
Waziri Wasira alisema tayari wameshafanya maandalizi ya kuagiza mbegu za mahindi tani 20,000, hivyo tani 9000 za mbegu hizo zimeshaagizwa kutoka nchi mbalimbali Tanzania ikiwemo na kampuni zitazipeleka karibu na wakulima. Hhata hivyo alisema mahitaji ya sasa ya mbegu hizo ni tani 30,000.
Kwa upande wa mbolea tani tayari kuna tani 201,000 wakati mahitaji ni tani 385,000, lakini tani nyingine zinaendelea kuagizwa.
Akizungumzia kuhusu ziara aliyoifanya Iran wiki iliyopita, Waziri Wasira alisema itasaidia kutoa ushirikiano katika masuala ya kilimo kati ya nchi hiyo na Tanzania. Hivyo Iran , itawekeza nchini Tanzania kwenye zana na kilimo, umwagiliaji, uongezaji thamani wa mazaokwa kuwekeza viwanda na kufanya utafiti ili kuhamasisha kilimo kwanza katika kukuza viwanda.