Sep 20, 2010

MASHINDANO YA VODACOM LATHAM OPEN 2010 YAFANA HUKO SINDA KISIWANI!!

Washiriki wa mashindano ya kuvua samaki ya Vodacom Lathan Open 2010 waliokuwa wakiendesha boti ya Natasha wakishangilia kwa kunyoosha vidole vyao juu mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao za ushindi wa kuvua samaki wengi zaidi, mashindano hayo yamefanyika jana kwenye kisiwa cha Sinde kwenye Bahari ya Hindi, kushoto ni Necta Foya Meneja wa Mawasiliano Vodacom Tanzania.

Bw. David Sutton wa boti ya uvuvi ya Simba kulia akionyesha zawadi yake aliyoipokea kutoka kwa Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza mara baada ya boti yao kuwa miongoni mwa washindi wa jumla walioshinda kuvua samaki wengi zaidi katika mashindano ya Vodacom Lathan Open 2010 yaliyofanyika kwenye kisiwa cha Sinda jana, kushoto ni Necta Foya Meneja wa Mawasiliano Vodacom Tanzania.

Wafanyakazi wa Yachit Club ya jijini Dar es salaam wakiwapima samaki uzito rekodi mbalimbali za boto zilizoshiriki kwenye mashindano ya uvuvi ya Vodacom Latham Open 2010 yaliyofanyika kwenye kisiwa cha Sinda jana, mara baada ya mashindano Club hiyo huuza samaki hao kwa mnada na fedha zinazopatikana kupelekwa katika kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali nchini.
Baadhi wa washiriki wakirejea mara baada ya kufanya uvuvi.
Hizi ni baadhi ya boti za uvuvi zilizoshiriki kwenye mashindano ya Vodacom Latham Open 2010 zikiwa zimeegeshwa ufukweneni mwa bahari ya Hindi huko katika kisiwa cha Sinda.

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA