Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo( kulia) akitangaza uamuzi wa Serikali ya Uingereza wa kuchangia katika Bajeti ya Taifa(GBS) kiasi cha bilioni 240 leo mjini Zanzibar . Kushoto ni Naibu Waziri wa Idara inayoshughulikia Misaada ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) Stephen O’Brian.Tiganya Vincent-MAELEZO- Zanzibar
Na Tiganya Vincent-MAELEZO- Zanzibar
Serikali ya Uingereza imetoa kiasi cha bilioni 240 sawa na Paundi milioni 103.5 kwa ajili ya kuchangia Bajeti ya Tiafa (GBS) kwa mwaka wa fedha wa 2010/2011.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Zanzibar na Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo na Naibu Waziri wa Idara inayoshughulikia Misaada ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) Stephen O’Brien.
wakati wakitoa ufafanuzi huo kwa waandishi wa habari mjini Zanibar.
Mkulo alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kutekeleza vipaumbele katika kutekeleza maeneo muhimu katika Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania(MKUKUTA).
Kufuatia hali hiyo ameishukuru Uingereza kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za kuleta maendeleo ya Watanzania.
Alisema kuwa hali hiyo imejidhihirisha katika miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imekuwa ikifadhiliwa na Uingereza kwa ajili ya kuboresha maisha ya Watanzania wengi.
Mkulo alitaja wafadhili wengine walichangia Bajeti ya mwaka 2010/2011 kuwa ni Denmark Dola milioni 16.3, Finland Dola milioni 18.8, Norway Dola milioni 31.4 na Ireland Dola milioni 14.2.
Aidha aliwahakikishia wafadhili wote wa Tanzania kuwa Serikali itahakikisha kuwa kuna usimamizi mzuri wa misaada na fedha zote zinazotoka kwa wahisani ili kuendelea kujenga imani kwao.
“Napenda kuwahakikishia kuwa wafadhili na wahisani katika Bajeti ya Taifa kuwa fedha zitakazotolewa na wahisani zitatumika katika miradi na malengo yaliyokusudiwa ili kuhakikisha thamani halisi ya fedha zinazotolewa na wahisani”alisistiza Mkulo.
Kwa upande Naibu Waziri wa Idara inayoshughulikia Misaada ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) Stephen O’Brien alitoa wito kwa Serikali ya Tanzania kuhakikisha kila kiasi cha fedha zinazotolewa na Uingereza zinatumika katika malengo yaliyokusudiwa ili matokeo yake yaweze kupimika.
No comments:
Post a Comment