Na Mwandishi Wetu MREMBO Julieth William aliyeshika nafasi ya tatu katika mashindano ya Miss Tanzania 2009, ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia ya Miss Progress International yatakayofanyika nchini Italia Septemba 26 mwaka huu. Mrembo huyo aliyetarajiwa kuondoka nchini jana jioni kuelekea nchini Italia kwa ajili ya kinyang’anyiro hicho alikabidhiwa bendera jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Aloyce Nzuki. Akizungumza baada ya kukabidhiwa bendera, mrembo huyo alisema aliteuliwa na waandaaji wa mashindano hayo kupitia mtandao wa mashindano ya Miss Tanzania na kwamba Tanzania inashiriki mchuano huo kwa mara ya kwanza mwaka huu. Alisema kabla ya kushiriki watakuwa kambini kwa wiki mbili na yeye kama mwakilishi wa Tanzania ana jukumu la kuutangaza utalii wa ndani ya nchi kupitia Utamaduni. “Nimefarijika kuwakilisha nchi kupitia mashindano haya kwani hii ni mara ya kwanza kwetu kushiriki hivyo ni changamoto kubwa kwangu binafsi na nchi kwa ujumla,” alisema. Alisema ana imani ataiwakilisha vyema Tanzania na ushiriki wake katika mashindano hayo utaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la watalii na pato la taifa kwa ujumla. Kwa upande wake Nzuki alisema TTB inajivunia ushiriki wa mrembo huyo katika mashindano hayo ya utalii ya ngazi ya kidunia kwani pamoja na mambo mengine mrembo husika atakuwa balozi mzuri wa kazi za bodi hiyo katika kuutangaza utalii wa ndani. Alisema waandaaji wameifanya Tanzania iendelee kusomeka vizuri katika soko la utalii duniani na kwamba kuchaguliwa kwa mwakilishi huyo ni kitu cha kujivunia kwani ni nchi chache za kiafrika zinazoshiriki mashindano hayo. Mashindano hayo ambayo yanaandaliwa na Taasisi ya Miss Progress International ya Italia yanafanyika kwa mara ya tatu tangu kuanzishwa kwake na yanashirikisha warembo kutoka nchi 60 tofauti duniani zikiwemo sita za Afrika ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Ethiopia,Algeria na Nigeria
Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ME MYSELF & I
THE DON HIMSELF
Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)
No comments:
Post a Comment