Aug 25, 2010

Dr. Bilali aanza kampeni mkoani Pwani


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kilwa Kusini, Ramadhan Madabida (kulia) akiteta jambo na Mgombea Mwenza, Mohamed Gharib Bilal, wakati wakimpokea kutoka Wilaya ya Rufiji kuingia Wilaya ya Kilwa Masoko akiwa katika safara ya Kampeni kwenye Mkoa huo wa Pwani.
Mkuu wa Wialaya ya Kilwa Masoko, Nurdin Babu akiongozana na Mgombea Mwenza wa Urais, Dr. Mohamed Gharib Bilali wakati alipompokea mpakani mwa Wilaya ya Rufiji kuingia kwenye Wilaya yake kuendelea na mkutano wa Kampen
Mgombea Mwenza wa urais,Dr. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Rufiji kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dk. Seif Rashid, wakati wa mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Muhoro, Tarafa na Kata ya Muhoro, Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani.
Umati wa watu, Wakazi wa Somanga wakimzunguka Mgombea Mwenza na kufunga barabara kwa muda ili kumpokea mgombea huyo alipokuwa akipita eneo hilo kuelekea Wilaya ya Kilwa Masoko.
(Picha na Muhidin Sufiani)


Na Mwandishi Wetu,Pwani

MGOMBEA mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),Dr. Mohamed Bilal amesema ifikapo mwaka 2015 kila shule ya msingi kote nchini itapaswa kuwa na darasa moja la wa chekechea.

Dk.Bilali aliyasema hayo jana wakati akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Rufiji katika mkutano wa adhara uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Mhoro Kata ya Chumbi mkoani Pwani sambamba na kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Rufiji Dk. Seif Rashid na mgombea ubunge wa Jimbo la KIbiti,Abdul Marombwa,alisema mpango huo mkakata umeainishwa katika Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015.

Dk.Bilali ambaye jana ndiyo alianza ziara ya kampeni yake rasmi mkoani hapa alisema lengo la mpango huo kuingizwa kwenye ilani hiyo ya CCM, ni chama hicho kupitia serikali yake inataka kuona wanafunzi wa shule wanaomaliza shule za awali wanajiunga na shule za msingi na sekondari na kisha kujiunga na vyuo vikuu.

“Hivi sasa taifa lisilo na wasomi ni dhahiri halitaweza kupiga hatua za kimaendeleo kwa wakati hivyo kwakuwa inapenda kuona wananchi wake wakubwa kwa wadogo wakipita elimu ndiyo maana ilani ya mwaka 2010-2015 imewekea mkazo suala la ukuzwaji wombea sekta ya elimu kwa ngazi zote hivyo nawasii sana wazazi na wananchi kote nchini muwaruhusu watoto wenu waende mashuleni kupata elimu kwani hakuna ulithi usiooza kama elimu.

Huku hotuba yake ikikatishwa mara kwa mara na vibwagizo vya nyimbo za kukisifu chama na kumpongeza rais Jakaya Kikwete kumchagua Dk.Bilali kuwa mgombea mwenza, alisema ili mpango huo utimie wananchi wa kada zote hawana budi kuinga mkono serikali ya ccm ilikuweza ujenzi huo wa madarasa ya wananfunzi wa shule za awali yanajengwa na kuongeza kwa kuwataka wananchi wote wanampatia kura za ndiyo mgombea urais wa ccm,Kikwete Leo mgombea mwenza ataendelea na ziara yake ya kampeni mkoani Kilwa.

Aug 24, 2010

Wanja Jipya La Mdau




unaweza kumpembelea kwa link yake hiyo hapo.
http://www.mateja20.blogspot.com/

vodacom miss tanzania watembelea mbuga ya ngorongoro


Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiangalia Simba anayepita karibu na magari yao wakati warembo hao walipotembelea Hifadhi ya Ngorongoro kujionea wanyama na mambo mbali mbali yalipo katika hifadhi hiyo.
Baadhi ya warembo wanoshiriki mashindano ya Kumsaka Vodacom Miss Tanzania wakicheza ngoma ya Kimasai wakati walipokaribishwa katika Boma la wafugaji hao lililopo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro wakati wakiwa katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Mikoa ya Kaskazini, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani.
Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakitoka katika nyumba za Tembe za wafugaji wa jamii ya Kimasai waishio katika Hifadhi ya Ngorongoro wakati wakiwa katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Mikoa ya Kaskazini, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani.
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakinunua shanga za kimasai kutoka kwa wauzaji waliopo katika Boma lililopo katika Hifadhi ya Ngorongoro wakati warembo hao walipotembelea hifadhi hiyo wakiwa katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Mikoa ya Kaskazini, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani.

Rais Kikwete Akiwa Sengerema


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wananchi katika kata ya Nyehunge jimbo la Buchosa,wilaya ya Sengerema leo mchana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na kumfariji msichana mwenye ulemavu wa ngozi aliyejitambulisha kwa jina la Rehema Mahaluko muda mfupi baada ya kuhutubia katika mkutano wa hadhara huko Nyehunge, wilayani Sengerema leo mchana.
(Picha na Freddy Maro)

MKALI AMBAYE KIDUMU AMEKOPY NA KUPEST STYLE YA MELODY NA SAUTI YAKE.(LINEX - LINENGA)

O ten akiwa na LINEX wakiingia ndani ya uwanja wa taifa kuhudhuria moja ya matamasha ya muziki wa kizazi kipya siku za hivi karibuni.
anajulikana kama LINEX SUNDAY wengi humuita LINENGA ambaye kwa sasa anasumbua kwa ngoma yake inayokwenda kwa jina la MAMA HALIMA.

LINEX & O TEN wakiwa kwenye moja ya matamasha yao
linex

Aug 22, 2010

ZIARA YA WAREMBO WA VODACOM MISS TANZANIA (KINAPA)

Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiwa wamebeba mabegi mngongoni mithili ya watalii wanaoteremka mlima Kilimanjarto wakati wa rembo hao walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) iliyopo Marangu mkoani humo jana. Warembo 30 wa Vodacom Miss Tanzania wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakizungumza na mmoja wa vijana wanaojishughulisha na kazi ya kusindikiza watalii kupanda Mlima Kilimanjaro jana wakati warembo hao walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) iliyopo Marangu mkoani humo. Warembo 30 wa Vodacom Miss Tanzania wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiangalia michoro ya ramani ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kialimanjaro (KINAPA) wakati warembo hao walipotembelea KINAPA jana. Warembo 30 wa Vodacom Miss Tanzania wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Mhifadhi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), David Loosurutia (kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya mazingira ya hifadhi hiyo kwa warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakati wa rembo hao walipotembelea KINAPA jana. Warembo 30 wa Vodacom Miss Tanzania wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

DEWJI APITA BILA KUPINGWA, PINGAMIZI DHIDI YAKE ZATUPWA.

Na Hillary Shoo,

Singida.

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya (CCM) jimbo la Singida mjini (pichani) Mohammed Dewji ameteuliwa kuwa mgombe pekee wa jimbo hilo baada ya pingamizi lililotolewa na wapinzani wake kutupwa na msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya wagombe wa vyama vingine vya upinzani, Josephat Isango wa CHADEMA na Omary Sombi wa chama cha AFP kuwasilisha pingamizi kwa msimamizi kuwa Dewji alikiuka sheria ya gharama za chaguzi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Singida mjini Yona Lucas Maki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida ilieleza kuwa baada ya kupitia kwa kina pingamizi hizo, imeonekana kuwa Dewji hakukiuka sheria ya gharama za uchaguzi kama walivyodai wapinzani wake.

Kwa mujibu wa barua yenye kumb Na. HM/SI/U.10/16/VOL.1/140 ya Agosti 21 mwaka huu kwa wagombea hao ilieleza kuwa ninawaletea uamuzi wa pingamizi hizo, mimi Yona Lucas Maki ambaye ni msimamizi wa uchaguzi jimbo la Singida, baada ya kupata maelezo ya utetezi uliyoyatoa dhidi ya pingamizi uliyowekewa ya kupinga uteuzi wa wewe Mohammed Dewji.

“Ninakataa pingamizi zilizotolewa kwa sababu haujatenda vitendo vinavyokataza chini ya sheria ya gharama za uchaguzi.”alisema Maki.

Aidha alisema kwa mujibu wa maeleekezo kwa wasimamizi wa uchaguzi , uchaguzi wa Rais , wabunge na madiwani , 2010 aya ya 5.16 kifungu cha 44 kinasema, “Kwa mujibu wa kifungo cha 44 cha sheria ya uchaguzi Na.1 ya mwaka 1985( sura ya 343) endepo mgombea aliyeteuliwa ni mmoja , baada ya kukamilisha hatua ya pingamizi atatangazwa kuwa amepita bila kupingwa , na uchaguzi hautafanyika katikaaa jimbo hilo. Tume ya Taifa ya uchaguzi itatangaza katika gazeti la serikali kuwa mgombea huyo amechaguliwa kuwa Mbunge.

“ Kwa nukuu hii hapa juu nakutangaza rasmi kuwa mgombea Ubunge ambaye umepita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu kwa mwaka 2010 katika jinbo la singida mjini.”ilisema taarifa hiyo ya Maki.

Hata hivyo Dewji alitoa maelezo yake kwa msimamizi huyo kuwa kwamba pingamizi lililotolewa chini ya sheria ya gharama za uchaguzi ni lazima lielezee matendo yasiyoendana na kifungu cha 9 cha sheria ambacho kinatamka mgombea aeleze fedha na vyanzo vingine vya fedha atakazotumia wakati wa kampeni kwa chama chake ndani ya siku 7 zitakazotamkwa na sheria.

Dewji alisema si hivyo tu sehemu ya tano ya sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010 iko wazi kwa kutamka wazi matendo ambayo yanaweza kubatilisha haki ya mtanzania kuwa mgombea ubunge.

“Kutokana na na sheria hiyo ninaomba pingamizi lililotolewa na Josephat Isango wa Chadema na Omary Sombi wa AFP yatupiliwe mbali kwa sababu limetokana na sheria isiyokuwepo hapa Tanzania.” Alisema Dewji.

Rais Kikwete Atua Mwanza na Kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Misungwi


Rais Jakaya Kikwete akimnadi Charles Kitwanga a.k.a Mawe Matatu, mgombea ubunge wa CCM wa jimbo la Misungwi Mwanza leo, akiwa ni mbunge wa kwanza kunadiwa na mwenyekiti huyo wa CCM ambaye kaanza rasmi ziara ya mikoani leo

Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride la chipukizi mara baada ya kutua jijini Mwanza leo kwa kampeni mkoa huo wa kanda ya ziwa
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Nyamagana Mh. Lawrence Masha ambaye kapita bila kupingwa katika jimbo lake. Anayemfuata ni Mh. William Ngeleja mbunge wa Sengerema ambaye naye kapita bila kupingwa
Wagombea ubunge wa CCM kanda ya ziwa wakimsubiri Rais Jakaya Kikwete alipotua jijini Mwanza leo.
Viongozi mbali mbali walijitokeza kumpokea Rais Jakaya Kikwete leo jijini Mwanza
Viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali wakisubiri kumlaki Rais Jakaya Kikwete jijini Mwanza leo kwa kampeni mkoa huo wa kanda ya ziwa.

Aug 21, 2010

'ARI ZAIDI,KASI ZAIDI NA NGUVU ZAIDI-PAMOJA TUTASHINDA'KAULI MBIU ILIYOZINDULIWA RASMI HAPO JANA

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wanachama wa CCM na wapenzi wa Chama hicho waliofika leo katika Viwanja vya Jangwani Jijini Dar wakati wa uzinduzi wa Kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu 2010.
Mgombea Mwenza wa Rais Jakaya Kikwete,Dr. Mohamed Gharib Bilal akiwahutubia wanaCCM wa Dar es Salaam waliofika katika Viwanja vya Jangwani leo.
Makamu Mwenyekiti CCM (Visiwani) na Rais wa Zanzibar anaemaliza muda wake,Rais Aman Abeid Karume nae aliongea machache na wanaCCM wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani waliojitokeza leo katika viwanja vya Jangwani,jijini Dar wakati Chama Cha Mapinduzi kilipozindua rasmi kampeni za uchaguzi mkuu 2010.
Makamu Mwenyekiti CCM (Bara),Mh. Pius Msekwa akiteja jambo na Katibu Mkuu wa CCM,Mh. Yussuf Makamba wakati wa mkutano wa ufunnguzi wa kampeni za uchaguzi mkuu zililofanyika leo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar.
Rais Mstaafu,Alhaj Ally Hassan Mwinyi akiteja jambo na Rais wa Zanzibar,Mh. Aman Karume na huku wakisikilizwa na wake zao na wadau wengine.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti CCM (Bara),Mh. Pius Msekwa.
Rais Kikwete akiwapungia wanaCCM wakati akiondoka.
Jukwaa Kuu.
Orijino Komedi wakifanya vitu vyao.
T.O.T wakifan ya vitu vyao huku wakiongozwa na Mh. John Komba.
Wazee wa kazi wakila mzigo.
Marlaw akiwabembeleza wanaCCM leo.
Marlaw na timu yake.Vijana wa Kiumeni wakikamua.
umati mkubwa wa wanaCCM waliofika katika viwanja vya Jangwani leo.

LIBENEKE JIPYA LA JK HILI HAPA!

Libeneke rasmi la JK na Dk. M. Gharib Bilal sasa lipo hewani:

www.kikwete2010.co.tz

Libeneke hili maalumu la Mgombea Uraisi na Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM mwaka 2010 limesheheni habari mbalimbali kama:

· Wasifu wa Wagombea – Mhe. Jakaya M. Kikwete na Dr. Mohammed Gharib Bilal.
· Mafanikio katika sekta mbalimbali.
· Sera na Malengo 2010 – 2015.
· Ratiba za kampeni.
· Hotuba maalumu.
· Matoleo ya Habari.
· Video na picha.
· Mitandao ya Facebook,Twitter na Youtube.
Kupitia tovuti hii na mitandao yake utaweza kupata taarifa mbalimbali na kutoa maoni yako.

“ PAMOJA TUZIDI KUSONGA MBELE”

SIMBA YAIBANJUA AFRICA LYON 2-0, YANGA YAIPA ADABU POLISI DODOMA 1-0!!

Timu ya Simba leo imeibanjua timu ya Africa Lyon magoli mawili kwa bila kwenye uwanja wa Uhuru katika uzinduzi wa ligi kuu ya Vodacom iliyoanza leo jijini Dar es salaam, timu hiyo ilifanya umafia huo huku mashabiki mwake wakiishangilia kwa nguvu kwenmye uwanja huo. Alikuwa ni mchezaji mpya wa timu hiyo aliyetokea kwa watani wao wa jadi timu ya Young African ya mtaa wa Jangwani jijini Dar es salaam Amir Maftaha wakati alipoandika goli la kwanza katika dakika ya kumi na nne ya mchezo huo katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo. Mpaka mapumziko Simba ndiyo ilikuwa ikiongoza goli 1-0 katika mchezo huo uliofungua pazia la ligi kuu ya Vodacom huku mahasimu wao wakuu timu ya Yanga ikiifunga timu ya Polisi Dodoma goli 1-0 kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. Katika kipindi cha pili Amir Maftaha tena alifunga goli la pili katika dakika ya sitini na nne ya mchezo na kuifanya timu ya Simba kuibuka na magoli 2-0 hivyo kuifanya timu ya Africa Lyon kuondoka uwanjani ikiambulia patupu, ushindi huo wa timu ya Simba unaipa pointi tatu za mwanzo katika ligi hiyo.

WAREMBO VODACOM MISS TANZANIA WATOA MSAADA WA VYANDARUA MOSHI!!

Baadhi ya warembo wanaoshiriki mashindano ya Vodacom Miss Tanzania 2010 wakimpatia chandarua ya kujizuia na mbu Miriam Joseph ambaye amelazwa Marangu ikiwa ni kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya Malaria Haikubaliki. kampeni iliyoanzishwa na rais Jakaya Mrisho Kikwete
Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010 wakimpatia chandarua cha kujizuia na mbu Herieth masawe ambaye amelazwa hospitani hapo ikiwa ni kutekeleza kauli mbiu ya Malaria Haikubaliki.

Katibu wa hospital ya Marangu, Godrick Njau akikapokea vyandarua toka kwa Mkurugenzi wa Vodacom kanda ya kaskazini Nguvu Kamando mara baada ya kutembelea hospitalini hapo wakiwa wameambatana na warembo wanaoshiriki mashindano ya Vodacom Miss Tanzania.

Mchungaji Mtikila Aenguliwa Katika Uchaguzi Mkuu 2010

Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP),Mchungaji Christopher Mtikila.

Na Mwandishi Wetu

WAKATI kampeni za uchaguzi mkuu zikifunguliwa rasmi leo hii, Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) imemuengua aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, kutokana na kutotimiza masharti yaliyowekwa kwa wagombea urais.

Mtikila aliyefika jana katika ofisi za NEC akiwa na mgombea mwenza wake Kibwana Said Kibwana, alienguliwa mara baada ya tume kubahini kwamba hakuwa ametimiza idadi ya wadhamini waliojitokeza kumdhamini.

Jaji Lewis Makame alisema kwamba NEC imefikia uamuzi wa kukitoa chama cha DP, baada ya Mtikila kupata wadhamini

mikoa 10, ingawa kati ya mikoa hiyo katika Mkoa wa Pwani wamepatikana wadhamini 220 wakiwamo 25 wenye kasoro.

Pia Jaji Makame alisema kwamba Mtikila pia alipata wadhamini 220 katika mkoa wa Kilimanjaro kati ya hao 27 wakiwa na kasoro.

Alisema kwamba katika Mkoa wa Dodoma kati ya wadhamini 220, wadhamini 29 walionekana kuwa na kasoro jambo liloifanya tume kuona kuwa Mtikial ahakukidhi vigezo vya kuwania urais.

Si Mtikila pekee ambaye alienguliwa, mgombea mwingine ambaye naye alikutwa na yaliyomkuta Mtikila ni Paul Kyara wa chama cha Sauti ya Umma (SAU) aliyeenguliwa baada ya kutokidhi idadi ya mikoa kumi ambayo mgombea urais anatakiwa kupata udhamini.

Baada ya kuenguliwa, Mtikila alikiri kuwa hasikitiki wala kuhudhunika kutokana na kutolewa huko, kwamadai kwamba hakuwa ameweka uhai wake katika kinyang’anyiro cha kugombea urais.

Alisema kwamba atapitia kwa makini nakala za fomu zake pamoja na viambatanisho vya udhamini, hili aweze kujua

kama atachukua hatua gani.

Vyama vingine vya Demokrasia Makini, Jahazi Asilia na NRA, vilijitoa vyenyewe baada ya kushindwa kufika leo hii katika ofisi za NEC kwaajili ya kurudisha fomu.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA