Na Hillary Shoo,
Singida.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya (CCM) jimbo la Singida mjini (pichani) Mohammed Dewji ameteuliwa kuwa mgombe pekee wa jimbo hilo baada ya pingamizi lililotolewa na wapinzani wake kutupwa na msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya wagombe wa vyama vingine vya upinzani, Josephat Isango wa CHADEMA na Omary Sombi wa chama cha AFP kuwasilisha pingamizi kwa msimamizi kuwa Dewji alikiuka sheria ya gharama za chaguzi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Singida mjini Yona Lucas Maki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida ilieleza kuwa baada ya kupitia kwa kina pingamizi hizo, imeonekana kuwa Dewji hakukiuka sheria ya gharama za uchaguzi kama walivyodai wapinzani wake.
Kwa mujibu wa barua yenye kumb Na. HM/SI/U.10/16/VOL.1/140 ya Agosti 21 mwaka huu kwa wagombea hao ilieleza kuwa ninawaletea uamuzi wa pingamizi hizo, mimi Yona Lucas Maki ambaye ni msimamizi wa uchaguzi jimbo la Singida, baada ya kupata maelezo ya utetezi uliyoyatoa dhidi ya pingamizi uliyowekewa ya kupinga uteuzi wa wewe Mohammed Dewji.
“Ninakataa pingamizi zilizotolewa kwa sababu haujatenda vitendo vinavyokataza chini ya sheria ya gharama za uchaguzi.”alisema Maki.
Aidha alisema kwa mujibu wa maeleekezo kwa wasimamizi wa uchaguzi , uchaguzi wa Rais , wabunge na madiwani , 2010 aya ya 5.16 kifungu cha 44 kinasema, “Kwa mujibu wa kifungo cha 44 cha sheria ya uchaguzi Na.1 ya mwaka 1985( sura ya 343) endepo mgombea aliyeteuliwa ni mmoja , baada ya kukamilisha hatua ya pingamizi atatangazwa kuwa amepita bila kupingwa , na uchaguzi hautafanyika katikaaa jimbo hilo. Tume ya Taifa ya uchaguzi itatangaza katika gazeti la serikali kuwa mgombea huyo amechaguliwa kuwa Mbunge.
“ Kwa nukuu hii hapa juu nakutangaza rasmi kuwa mgombea Ubunge ambaye umepita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu kwa mwaka 2010 katika jinbo la singida mjini.”ilisema taarifa hiyo ya Maki.
Hata hivyo Dewji alitoa maelezo yake kwa msimamizi huyo kuwa kwamba pingamizi lililotolewa chini ya sheria ya gharama za uchaguzi ni lazima lielezee matendo yasiyoendana na kifungu cha 9 cha sheria ambacho kinatamka mgombea aeleze fedha na vyanzo vingine vya fedha atakazotumia wakati wa kampeni kwa chama chake ndani ya siku 7 zitakazotamkwa na sheria.
Dewji alisema si hivyo tu sehemu ya tano ya sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010 iko wazi kwa kutamka wazi matendo ambayo yanaweza kubatilisha haki ya mtanzania kuwa mgombea ubunge.
“Kutokana na na sheria hiyo ninaomba pingamizi lililotolewa na Josephat Isango wa Chadema na Omary Sombi wa AFP yatupiliwe mbali kwa sababu limetokana na sheria isiyokuwepo hapa Tanzania.” Alisema Dewji.
No comments:
Post a Comment