Aug 21, 2010

Mchungaji Mtikila Aenguliwa Katika Uchaguzi Mkuu 2010

Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP),Mchungaji Christopher Mtikila.

Na Mwandishi Wetu

WAKATI kampeni za uchaguzi mkuu zikifunguliwa rasmi leo hii, Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) imemuengua aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, kutokana na kutotimiza masharti yaliyowekwa kwa wagombea urais.

Mtikila aliyefika jana katika ofisi za NEC akiwa na mgombea mwenza wake Kibwana Said Kibwana, alienguliwa mara baada ya tume kubahini kwamba hakuwa ametimiza idadi ya wadhamini waliojitokeza kumdhamini.

Jaji Lewis Makame alisema kwamba NEC imefikia uamuzi wa kukitoa chama cha DP, baada ya Mtikila kupata wadhamini

mikoa 10, ingawa kati ya mikoa hiyo katika Mkoa wa Pwani wamepatikana wadhamini 220 wakiwamo 25 wenye kasoro.

Pia Jaji Makame alisema kwamba Mtikila pia alipata wadhamini 220 katika mkoa wa Kilimanjaro kati ya hao 27 wakiwa na kasoro.

Alisema kwamba katika Mkoa wa Dodoma kati ya wadhamini 220, wadhamini 29 walionekana kuwa na kasoro jambo liloifanya tume kuona kuwa Mtikial ahakukidhi vigezo vya kuwania urais.

Si Mtikila pekee ambaye alienguliwa, mgombea mwingine ambaye naye alikutwa na yaliyomkuta Mtikila ni Paul Kyara wa chama cha Sauti ya Umma (SAU) aliyeenguliwa baada ya kutokidhi idadi ya mikoa kumi ambayo mgombea urais anatakiwa kupata udhamini.

Baada ya kuenguliwa, Mtikila alikiri kuwa hasikitiki wala kuhudhunika kutokana na kutolewa huko, kwamadai kwamba hakuwa ameweka uhai wake katika kinyang’anyiro cha kugombea urais.

Alisema kwamba atapitia kwa makini nakala za fomu zake pamoja na viambatanisho vya udhamini, hili aweze kujua

kama atachukua hatua gani.

Vyama vingine vya Demokrasia Makini, Jahazi Asilia na NRA, vilijitoa vyenyewe baada ya kushindwa kufika leo hii katika ofisi za NEC kwaajili ya kurudisha fomu.

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA