Aug 18, 2010

dr shein ahutubia wagombea wa ubunge uwakilishi zanzibar

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wagombea wa Viti vya Ubunge, Uwakilishi na Udiwani pamoja na Wananchi mbalimbali katika ukumbi wa salama Hoteli ya Bwawani Zanzibar leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na wananachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi wa Zanzibar, baada ya kuwahutubia kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika leo katika ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Zanzibar.

Wagombea wa Viti vya Ubunge, Uwakilishi, Udiwani pamoja na Wananchi mbalimbali wa Zanzibar, kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa Hadhara katika ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Zanzibar leo.

(Amour Nassor -VPO)

HILI NDO LIBENEKE JIPYA LA MDAU MUHIDINI ISSA MICHUZI.

Asalaam Aleikhum Wadau, Kwa furaha, heshima na taadhima naomba kutangaza rasmi libeneke jipya la www.michuzipost.com ambalo wikiendi ilopita lilipaa hewani katika kile kiitwacho uzinduzi laini (soft launch). Kunradhi kwa kutowataarifu mapema, kwani ilibidi mambo kadhaa yawekwe sawa kwanza kabla ya kuthubutu kutia neno kama nifanyavyo sasa. Wadau wa Globu ya Jamii naomba baraka zenu pamoja na maoni juu ya libeneke hili ambalo azma ya kulianzisha ni ile ile ya Kuendeleza Libeneke kwa njia ya kisasa zaidi na kwa upana mkubwa. Hivyo nakaribisha maoni, ushauri pamoja na neno lolote lile litalonkisaidia kuboresha libeneke hili. Kama nilivyotamka awali, bado niko katika uzinduzi laini, kwani kama ujuavyo libeneke kama hili halitaki papara. Linahitaji subira, sikion sikivu la neno toka kwa wadau ambao sapoti yao naithamini kama lulu kwa muda wote huu. Globu ya Jamii itaendelea kuwepo hewani kama kawaida, na itaenda sambamba na Libeneke hili la www.michuzipost.com pamoja na lile la www.michuzi-matukio.blogspot.com. Hivyo wadau Globu ya Jamii itaendelea kudunda kama kawaida, ikiwa ni chapuo la Libeneke jipya ambalo kama utavyoliona, litakuwa na habari na taarifa motomoto kwa mapana na undani zaidi. Inshaallah panapo majaaliwa Libeneke hili jipya litazinduliwa rasmi mnamo September 8, mwaka huu - ikiwa ni siku ya kuadhimisha miaka mitano kamili ya kuzaliwa kwa Globu ya Jamii kama link hii inavyojionesha http://issamichuzi.blogspot.com/2005/09/michuzi-and-ndesanjo.html#comments. Namshukuru Muumba wa Yote kwa kunipa nguvu na uwezo kufikia hapa nilikofikia. Pia natoa shukrani kwa kila mdau ambaye amekuwa akinipa sapoti ya nguvu kila siku kwa kutembelea Globu ya Jamii. Ni mategemeo yangu kwamba baada ya kwikwi ya kuwa na Libeneke jipya wakati fulani huko nyuma, sasa mambo yanaonekana kuwa mswano na Libeneke litaendelea kama kawa. Libeneke hili jipya la www.michuzi.post.com limewezekana kwa ushauri na msaada pamoja na ushirikiano mkubwa wa Bw. Zubeir Masabo na Bw. Alistair Horsburgh, washirika wangu walio Uingereza ambao kwa pamoja tutaendesha Michuzi Post Ltd. kampuni rasmi itayosimamia uzalishaji wa bidhaa za www.michuzipost.com. Sambamba nasi pia kuna kikosi kazi kikubwa ambacho kitakuwa kinashughulika katika kuendeleza Libeneke hili. Muhidin Issa Michuzi Mkurugenzi Michuzi Post Ltd.

Tume ya Kurekebisha Sheria Yaanza Kupitia Ripoti Ya Sheria Za Mila!!

Katibu Tawala wa Wilaya ya Ulanga Bw. Alfred Shayo aliyesimama akizungumza kabla ya kuanza kiako cha kupitiwa ripoti ya Rasimu ya Sheria za Mila zinazofuata mkondo wa ukoo wa mama, katikati ni Ofisa Sheria wa Tume Shadrack Makongoro.

(Picha zote na Ofisa Habari wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Munir Shemweta)

Ofisa Sheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Shadrack Makongoro (kulia )akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Bw. Francis Miti baadhia ya vifaa kwa ajili ya kuitangaza Tume katika Wilaya yake, wa kwanza kushoto ni Katibu Twala wa Wilaya ya Ulanga Bw. Alfred Shayo.

Ofisa Sheria wa Tume Shadrack Makongoro akisikiliza maoni ya washiriki wa kikao hicho.
Baadhi ya Washiriki wa kikao cha kujadili rasimu ya Sheria za Mila zinazofuata mkondo wa ukoo wa mama katika wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.

Rais Kikwete azindua mnara wa Mashujaa wa Majimaji, Azindua mtambo wa kuzalisha umeme kutumia Gesi Asilia huko Somanga-Kilwa!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuzindua mradi wa Umeme unaotumia gesi ya aslia huko Somanga Fungu jana jioni.Huko waziri wa Nishati na madini William Ngeleja(watatu kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Wiliam Mhando(wane kushoto) wakiangalia.Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Said Meck Sadiq.(picha na Freddy Maro)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria kuzindua mradi wa umeme wa gesi ya asilia huko kijiji cha Somanga Fungu, mkoani Lindi jana jioni.Kushoto ni Waziri wa Nishati na madini William Ngeleja na kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa TANESCO William Mhando.
Amiri Jeshi mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka silaha za kijadi katika mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa wa vita vya Majimaji katika kijiji cha Nandete, kata ya Kipatimu wilayani Kilwa jana mchana.(kwa msaada wa blog jirani(full shangwe))

Mwakalebela ajisalimisha, asomewa mashitaka, yuko nje kwa dhamana

Na www.wavuti.com

Frederick Mwakalebela na mkewe, Celina, kizimbani Iringa

Aliyekuwa mshindi wa kura za maoni jimbo la Iringa mjini Bw Frederick Mwakalebela na (suti nyeusi ) akiwa na mkewe (suti nyeupe) wakisindikizwa na marafiki kuingia mahakamani.

Umati mkubwa wa wananchi wa mji wa Iringa na vitongoji vyake ulifurika kusikiliza kesi ya tuhuma za rushwa iliyofunguliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU, dhidi ya aliyekuwa mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, bwana Frederick Mwakalebela.

Kesi hiyo ndivyo iliyotamkwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM kuwa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, NEC-CCM kama kigezo kikuu cha kuliengua jina la Frederick Mwakalebela katika nafasi hiyo hata ikiwa alishinda katika kura ya maoni, na badala yake nafasi hiyo kupewa mbunge aliyemaliza muda wake na anayewania tena nafasi hiyo, bi Monica Mbega.

Inasimuliwa na Francis Godwin kupitia blogu yake kuwa umati mkubwa wa wananchi wa jimbo la Iringa waliacha shughuli zao na kufika kusikiliza kesi ya Mwakalebela kiasi cha watu kukosa nafasi za kuketi ndani na hivyo kuifuatilia kesi hiyo wakiwa nje ya chumba cha Mahakama ilikokuwa ikiendelea kesi hiyo.

Anasema kuwa baadhi ya wananchi walikuwa na barua zao tayari kwa ajili ya kumdhamini bwana Mwakalebela endapo ingehitajika kufanya hivyo, vile vile, “…mahakimu wasema haijapata kutokea toka kuanzishwa kwa mahakama hiyo umati mkubwa kama huo kuja mahakamani kusikiliza kesi”.

Mwalalebela, ambaye alikuwa kajiandaa kikamilifu, alipataa dhamana iliyosainiwa ya shilingi Milioni 5 na wadhamini wawili.

Mwakalebela akisubiri kusomewa shitaka mahakamani Iringa

Aug 17, 2010

rais karume amwakilisha rais kikwete mkutano wa sadc nchini namibia

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akiwa ni miongoni mwa Viongozi wa Nchi za SADC akimuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano wa siku mbili unaohusu masuala mbali mbali ya Kiuchumi na Kijamii,uliofanyika katika ukumbi wa Safari Court Hotel nchini Namibia,(kushoto) Rais wa Afrika Kusini
Jacob Gedleyihlekisa Zuma.
Rais wa Malawi Prof Bingu Wa Mutharika akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika,Rais wa Nchini Congo Joseph Kabila,wakati wa Mkutano wa siku mbil9i kwa Nchi za SADC pia uandhimisha miaka 30 tokea kuundwa kwa jumuiya hiyo.
Rais wa Nchini Malawi Prof Bingu Wa Mutharika akitoa hutuba yake wakati wa mkutano wa siku mbili Nchi za SADC,unaoendelea Nchini Namibia,mkutano huo pia unaadhimisha miaka 30 tokea kuundwa kwa jumuiya hiyo.
Marais wa Nchi Mbali mbali wakiisimama wkati wa Wimbo wa Taifa za Nchi kbla ya kuanz kwa mkutao wa Jumuiya ya SADC,uliofanyika Nchini Namibia pia mkutno huo unaadhimisha miaka 30 tkea kuundwa kwa jumuiya hiyo.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Shadya Karume,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Namibia Sam Nujoma,wakati wa Mkutano wa Nchi za, SADC Uliofanyika Nchini Namibia.
Waziri Nchi Afisi ya Rais anaeshuhulikia Fedha na Uchumi,Zanzibar Mwinyihaji Makame,akiteta jambo na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mohammed Aboud,wakati wa Mkutano wa siku mbili kwa Nchi za SADC,uliofanyika Nchini Namibia.
Washiriki wa Mkutano wa siku mbili wa Nchi mbali mbali za SADC wakisikiliza kwa makini harakati na matukio katika mkutano huo,liofanyika Nchini Namibia,katika ukumbi wa Safari Court Hotel pia mkutano huo unadhimisha miaka 30 tokea kuanzishwa jumuiya hiyo .
Wake za Marais wa Nchi za Jumuiya ya SADC,pamoja na Marais wastaafu wa Jumuiya hiyo kwa pamoja na washiriki wengine wa Mkutano wa siku mbili wa jumuiya hiyo,wakifuatilia kwa makini,matukio mbali mbali yanayoendelea katika ukumbi wa Safari Court Hotel.
Marais wastaafu wa Jumuiya hiyo kwa pamoja na washiriki wengine wa Mkutano wa siku mbili wa jumuiya hiyo,wakifuatilia kwa makini,matukio mbali mbali yanayoendelea katika ukumbi wa Safari Court Hotel.
Wake za Marais wa Nchi za Jumuiya ya SADC,pamoja na Marais wastaafu wa Jumuiya hiyo kwa pamoja na washiriki wengine wa Mkutano wa siku mbili wa jumuiya hiyo,wakifuatilia kwa makini,matukio mbali mbali yanayoendelea katika ukumbi wa Safari Court Hotel.
Wanafunzi wa Secondary School walioshinda Insha zinazoelezea masula a ya SADC,wakia na vyeti vyao baada ya kukabidhia na Rais Kabil,(kushoto) ni Chresencia Stephen Marwa kutoka Tanzania na Incinon Adaiano Ganga kutoka Angola wakiwa katika ukumbi wa Mkutano wa SADC,Safari Court Hotel.

Mwenyekiti Mpya wa SADC,Rais wa Namibia Hifikepunye Pohamba akitoa hutuba yake baada ya kuwa Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya hiyo,katika Ukumbi wa Mkutano wa siku mbili,uliofanyika Safari Court Hotel,Nchini Nambia,pia mkutano huo unadhimisha miaka 30 tokea kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi wakuu wa Nchi za SADC walioshiriki Mkutano wa Siku mbili uliofanyika Nchini Namibia,katika Ukumbi wa Mikutano wa Safari Court Hotel,Nchini Namibia,Rais karume anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete.

Orodha ya wagombea ubunge na uwakilishi katika uchaguzi mkuu wa Tanzania 2010 ya chama cha CUF

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Shariff Hamad

Dar es Salaam

Tanga

Hussein Siyovelwa (Ilala);
Kimangale Mussa (Segerea);
Heko Pori (Ukonga);
Shaban Mapeyo (Kawe);
Shabaan Nassor (Kinondoni)
Mustafa Mungwe (Kigamboni)

Mussa Mbarouk (Tanga Mjini);

Remmy Shundi (Handeni);
Bakar Mbega (Mkinga);
Abubakar Bakari (Muheza);
Gogola Gogola (Mlalo);
Fabi Sozi (Bumbuli);
Abassy Mkankamghanga (Lushoto),
Jumaa Magogo (Korogwe Mjini);

Mohamed Asiu (Korogwe Vijijini)

Omar Masomaso (Pangani)

Kilimanjaro

Awadh Mwarabu (Same Magharibi).
Mtwara ni Hassan Abdallah (Mtwara Mjini);
Katani Katani (Tandahimba);
Clara Mwatuka (Masasi);
Mtikita Mtikita (Lulindi);
Hakika Maarifa (Newala)
Chikamba Wanainuka (Mtwara Vijijini)

Lindi

Salum Barwany (Lindi Mjini);
Ayubu Nassor (Mchinga),
Khalfan Mandanje (Mtama);
Madaraka Beyi (Liwale),
Nanjase Nanjase (Nachingwea),
Abubakary Kondo (Ruangwa),
Seleman Bungara (Kilwa Kusini)
Said Manoro (Kilwa Kaskazini).

Tabora

Edward Zombwe (Urambo Mashariki),
Kirungi Kirungi (Urambo Magharibi),
Hassan Mwigwayasila (Igalula),
David Kassoga (Tabora Kaskazini),
Kidumla Kidumla (Bukene),
Dominic Kizwalo (Nzega)
Abdallah Katala (Sikonge)

Kagera

Christina Kasimbazi (Bukoba Vijijini),
Nicolaus Batalingaya (Karagwe),
Twaha Taslima (Bukoba Vijijini),
Hamida Issa (Biharamulo Magharibi),
David Tibanywana (Chato)
Yahya Ndyema (Nkenge)

Arusha

Ghariby Baalawy (Arusha Mjini),
John Pallangyo (Arumeru Mashariki),
Adella Kileo (Arumeru Magharibi)
Navaya Ndaskoi (Monduli)

Mara

Mustafa Wandwi (Musoma Mjini),
Vedastus Msita (Mwibara)
Wilegi Songambele (Bunda)
Pwani ni Jafar Ndende (Mkuranga),
Seif Porwe (Kibiti),
Ali Kihambwe (Rufiji),
Wahabi Twalut (Mafia),
Adui Kondo (Kisarawe),
Zahoro Vuai (Bagamoyo)
Miraj Mtibwiliko (Chalinze)

Shinyanga

Mwalimu Mbukuzi (Shinyanga Mjini),
Khanipha Ruhinda (Maswa Mashariki),
Seif Baya (Maswa Magharibi),
Jackson Deodatus (Bukombe),
Shashu Lugeye (Solwa),
Sauda Kasiga (Msalala),
Hamisi Makapa (Kahama),
Creoface Magere (Mbogwe)
James Matinde (Kisesa)

Kigoma

Fatma Kinguti (Kigoma Mjini),
Salum Kajanja (Buyungu),
Athumani Hamisi (Muhambwe),
Rashid Kaduguda (Kasulu Magharibi)
Ibrahim Magara (Buhigwe)

Mbeya

Ezekia Mtafya (Ileje),
Asukile Kabango (Mbozi Magharibi),
Nkuyuntila Siwale (Mbozi Mashariki),
Yusuf Said (Kyela)
Shaweji Salinyambo (Mbarali)

Iringa

Mussa Fufumbe (Isimani),
Godfrey Hongele (Njombe Kaskazini),
Stanley Fwila (Njombe Kusini)
Jacob Mhanga (Njombe Magharibi)

Manyara

Rashid Mgaya (Babati Mjini),

Juma Nyeresa (Kiteto)

Eliseus Amedeus (Mbulu)

Ruvuma

Mazee Mazee (Tunduru Kaskazini),
Mohammed Mambo(Tunduru Kusini)
Hassan Mtwangambati (Namtumbo)

Morogoro

Willy Dikundile (Kilosa Kati),
Abeid Mlapakolo (Morogoro Mjini)
Blandina Mwasabwite (Morogoro Kusini Mashariki)

Mwanza

Komanya Athanas (Buchosa),

Mbaraka Chiru (Sengerema),
Peter Malebo (Geita),
Oscar Ndalahwa (Busanda),
Andrea Mkanga (Nyang’hwale),
Abdallah Mtina (Misungwi),
Omar Mbalamwezi (Nyamagana),
Mtebe Msita (Ukerewe),
Ligawa Ndalahwa (Kwimba)
Julius Samamba (Sumve)

Katavi

Aram Ndimubenya (Mpanda Mjini),

Athumani Kababende (Mpanda Vijijini)

Abbas Ally (Katavi)

Singida

Rashid Mindicar (Singida Mjini),
Sizimwe Kanyota (Singida Kaskazini)
Dalfina Patric (Singida Magharibi)

Dodoma

Ngomoka Joseph (Mtera),
Ngomoka William (Chilonwa),
Yahya Deni (Kondoa Kaskazini),
Hassan Missanya (Kondoa Kusini)

Tabora

Kapasha Kapasha (Tabora Mjini)

Zanzibar

Faki Haji Makame (Mtoni),

Rashid Soud Khamis (Bububu),

Hassan Omar Issa (Mfenesini),
Khamis Msabaha Mzee (Dole),
Khatib Haji Ali (Fuoni),
Ussi Juma Hassan (Mwanakwerekwe),
Hamad Ali Hamad (Magogoni),
Hemed Said Nassor (Dimani),
Seif Suleiman Kombo (Amani)
Khamisi Ali Khamisi (Kwamtipura)
Ali Juma Khamisi (Chumbuni),
Khamisi Mussa Haji (Kwahani),
Idarous Habib Mohamed (Kikwajuni),
Khalid Rajab Mghanah (Rahaleo),
Suleiman Khamis Ally (Mpendae),
Muhammad Ibrahim Sanya (Mji Mkongwe),
Mohamed Yussuf Maalim (Jang’ombe)
Ahmed Khamis Hamad (Magomeni)
Ramadhan Ali Mbarouk (Bumbwini),
Ali Rashid Ali (Kitope),
Othman Habibu Juma (Donge),
Ali Mati Wadi (Matemwe),
Yussuf Haji Khamis (Nungwi),
Rashid Khamis Rashid (Tumbatu),

Khamisi Suleiman Kombo (Chaani),
Hassan Omar Nahodha (Mkwajuni),
Abdi Mohamed Adeyoum (Uzini),
Ali Khamis Ame (Chwaka)
Shabaan Iddi Ame (Koani)
Mohamed Kombo Ali (Makunduchi),
Vuai Issa Haji (Muyuni),
Mussa Haji Kombo (Chakechake),
Ahmed Juma Ngwali (Ziwani),
Hamad Rashid Mohammed (Wawi),
Haji Khatib Kai (Micheweni)

Rashid Ali Abdalla (Tumbe),

Khatib Said Haji (Konde),
Kombo Khamisi Kombo (Mgogoni),
Mbaruk Salum Ali (Wete),
Khalifa Suleiman Khalifa (Gando),
Said Suleiman Said (Mtambwe),
Rajab Mbarouk Mohamed (Ole),
Rashid Ali Omar (Kojani),
Salim Hemed Khamis (Chambani),
Mohamed Habib Mnyaa (Mkanyageni),
Masoud Abdalla Salim (Mtambile),
Abdalla Haji Ali (Kiwani)
Ali Khamisi Seif (Mkoani)

Watakaowania uwakilishi katika Baraza la Wawakilishi

Nassor Ahmed Mazrui (Mtoni),
Bakar Haji Muhammad (Bububu),
Masoud Nassor Seif (Mfenesini),

Hasne Abdalla Abeid (Dole),

Asha Ali Fakih (Fuoni),
Idrisa Hamad (Mwanakwerekwe),
Abdilah Jihad Hassan (Magogoni)
Manzi Ibrahim Juma (Kiembesamaki)
Ali Juma Ali (Dimani),
Khamis Rashid Abeid (Amani),
Dk. Majaliwa Juma Seif (Kwamtipura),
Maulid Suleiman Juma (Chumbuni),
Hassan Juma Hassan (Kwahani)
Bakar Hassan Bark (Kikwajuni).
Omar Mussa Makame (Rahaleo),
Maharouk Abdalla Suleiman (Mpendae),
Ismail Jussa Ladhu (Mji Mkongwe),
Haji Ameir Muhunzi (Jang’ombe),
Zainab Omar Mzee (Magomeni),
Zahran Juma Mshamba (Bumbwini),
Hassan Khatib Kheri (Kitope),
Machano Omar Masanja (Donge)
Shauri Makame Mkadam (Matemwe)
Haji Mwadini Makame (Nungwi),
Makame Hamad Makame (Tumbatu),

Khamis Amour Vuai (Chaani),

Vuai Kona Haji (Mkwajuni),
Salma Hussein Zaral (Uzini),
Ali Mrisho Haji (Chwaka),
Khamis Malik Khamis (Koani)
Ameir Mussa Ameir (Makunduchi)
Suleiman Hassan Suha (Muyuni),
Omar Ali Shehe (Chakechake),

Rashid Seif Suleiman (Ziwani),
Saleh Nassor Juma (Wawi),
Abdalla Juma Abdalla (Chonga),
Subeti Khamis Faki (Michweweni),
Rufai Said Rufai (Tumbe),
Suleiman Hemed Khamis (Konde),
Abubakar Khamis Bakary (Mgogoni)
Asaa Othman Hamad (Wete)
Said Ali Mbarouk (Gando),
Salim Abdalla Hamad (Mtambwe),
Hamad Masoud Hamad (Ole),
Omar Ally Jadi (Kojani),
Mohammed Mbwana Hamad (Chambani),
Haji Faki Shaali (Mkanyageni),
Muhamed Haji Khalid (Mtambile),
Haji Hassan Hija (Kiwani)
Abdalla Mohamed Ali (Mkoani)

IMETOLEWA NA CUF MAKAO MAKUU

warembo wa miss tanzania waingia kambini leo

warembo wa Miss Tanzania wanaoingia kambini leo hii,wakiwa katika usafiri wao tayari kwa safari ya kuelekea Kambini.
wakiingia katika usafiri wao.
walinzi wa warembo (Mabaunsa)

Warembo waliofanikiwa kuingia Fainali ya Taifa ya Mashindano ya Urembo ya VODACOM MISS TANZANIA 2010, leo wameingia kambini kwa ajili ya kuanza mchakato wa kumrithi mrembo anayemaliza muda wake, Miriam Gerald.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo mchana kabla ya warembo hao kuelekea Kambini, Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, alisema kuwa “Warembo hao Wakiwa kambini watakuwa na ratiba mbali mbali ikiwa ni pamoja na kufanya kazi za kijamii na kutembelea sehemu mbali mbali za vivutio vya kitalii”

Alizitaja sehemu hizo kuwa siku ya Tarehe 17 / 08 / 2010 warembo watapewa semina maalumu na viongozi wa kamati ya Miss Tanzania pamoja na kusaini mikataba kati yao na waandaaji.

Tarehe 19 / 08 / 2010 waandishi wa habari wote watapata nafasi ya kuongea na washiriki na kupata maoni yao na jinsi walivyojiandaa katika kunyakuwa taji la VODACOM MISS TANZANIA 2010

Mwishoni mwa wiki warembo wote wakiambatana na baadhi ya viongozi wa kamati watasafiri kwenda katika mikoa ya kanda ya kaskazini “KILIMANJARO: na “ARUSHA” kwa ajiri ya kutembelea vivutio vya utalii ili kuvitangaza na kuwahamasisha watanzania ili wajenge utamaduni wa kutembelea, kuvilinda na kuvithamini vivutio vyetu.

Huu ni mpango tunaoshirikiana na taasisi za serikali yaani ,BODI YA UTALII, TANAPA na NGORONGORO CONCERVATION AREA AUTHORITY.

Huu ni mwaka wa pili taasisi yetu “Miss Tanzania” kushirikiana na taasisi za serikali kuhamasisha watanzania kuthamini na kutembelea vivutio vilivyopo nchini kwetu.

Tunategemea kwenda mbele zaidi kwa kuvitembelea vivutio vya kusini mwa Tanzania, SELOUS, RUAHA NATIONAL PARK, MIKUMI na UDIZUNGWA, katika siku za usoni.

MBA NA YANGA ZAKABIDHIWA VIFAA KWA AJILI YA MCHEZO WA NGAO YA JAMII

mkuu wa udhamini vodacom george rwehumbiza na katibu wa yanga mwalusako wakionyesha jezi ya yanga
nyange kaburu na mkuu wa udhamini vodacom george rwehumbiza wakionyesha jezi ya simba
Raurence Mwalusako katibu mkuu yanga akipokea vifaa vya michezo

Wadhamini wa ligi kuu Tanzania bara kampuni ya simu za mikononi ya VODACOM itatumia kiasi shilingi milioni 35 kwaajili ya mchezo wa ngao ya hisani baina ya SIMBA NA yanga utakaochezea kesho kutwa jumatano katika uwanja wa taifa.
Mkuu wa udhamini wa vodacom GEORGE RWEHUMBIZA amesema wamefanya hivyo kwaajili ya kutambua umuhimu wa mchezo huo na kukabidhi jezi zitakazotumiwa siku hiyo .
Wakipokea vifaa hivyo katibu mkuu wa YANGA Raurence Mwalusako na makamu mwenyekiti wa SIMBA GEOFREY NYANGE wakisema mchezo huo utaonyesha ishara njema kwao kwenye msimu huu

Mchezo huo wa ngao ya HISANI utachezwa majira ya saa kumi jioni tofauti na hapo awali ambapo kulikuwa na taarifa kuwa mchezo huo ungechezwa usiku.

TUME YA TAIFA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YATOA TUZO


Waziri wa Sayansi na Tek nolojia Prof. Peter Msolla akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni ishirini Prof. Mathew Luhanga wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufuatia Taasisi ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kutoa tuzo za taifa za ugunduzi na ubunifu na kutoa Mwega kwa ajili ya utafiti mwaka 2010.

Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla akimtunuku cheti cha mshindi wa kwanza Prof. Mathew Luhanga wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufuatia Taasisi ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kutoa tuzo za taifa za ugunduzi na ubunifu na kutoa Mwega kwa ajili ya utafiti mwaka 2010.
Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla akiangalia mbegu za mahindi na kupata maelezo kutoka kwa mtaalam wa Kilimo Kutoka kituo cha utafiti Ilonga kilichoko kilosa mkoani Morogoro Dkt. Chaboba Mkangwa. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Hassan Mshindi.
Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Bw. Godfrey Kimarya mgunduzi wa tanuru la mkaa lenye uwezo wa kutoa mkaa mwingi na wenye ubora kwa gharama nafuu leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kutoa Tuzo za Taifa za Ugunduzi na Ubunifu pamoja na utoaji wa fedha za kusaidia shughuli za utafiti wa elimu, kilimo,ufugaji, ufundi na viwanda kwa taasisi na vikundi mbalimbali nchini.Wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine -Morogoro (SUA) Prof. Rhodes Makundi (kulia) na Christophe Cox (kushoto) wakitoa maelezo ya panya buku wenye uwezo kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini na vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu (TB) leo jijini Dar es salaam wakati sherehe ya kutoa Tuzo za Taifa za Ugunduzi na Ubunifu pamoja na utoaji wa fedha za kusaidia shughuli za utafiti wa elimu, kilimo,ufugaji, ufundi na viwanda kwa taasisi na vikundi mbalimbali nchini .Profesa Rhodes Makundi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine - Morogoro (SUA) akitoa ufafanuzi wa panya buku wenye uwezo wa kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini na vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu (TB) kwa Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kutoa tuzo za taifa za ugunduzi na ubunifu na kutoa Mwega kwa ajili ya utafiti

(Picha na Aron Msigwa - MAELEZO)

MAADILI KWA VYOMBO VYA HABARI/WASANII YAGONGANISHA VICHWA

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Ghonche Materego (Kulia) akisisitiza jambo wakati akichangia mada kwenye Jukwaa la Sanaa Jumatatu hii.Katikati ni mwasilishaji wa mada, Bi.Mabel Masasi na Katibu wa CAJAtz,Hassan Bumbuli.Mdau wa Sanaa na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Video Library nchini, Richard Kalinga akichangia mada kuhusu Mchango wa Sekta ya Utangazaji Katika Kulinda Maadili ya Mtanzania.Mkongwe wa Sanaa za Maonyesho,Nkwama Bhalanga akilia na rushwa kwenye vituo vya redio ambapo alisema kwamba ni kikwazo katika maendeleo ya muziki nchini.Alipendekeza vibanwe na TCRA kupitia utoaji leseni.Aliyekaa kulia kwake,ni Mkongwe wa dansi nchini,Kasim Mapili.

Umakini zaidi kwa wadau wa sanaa kwenye Jukwaa.Hapa wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa BASATA,Bw.Materego (hayuko pichani) wakati akihitimisha mada ya siku ya leo.


**************** *****************

Wadau, kama kawaida Jukwaa la Sanaa ambalo sasa limekuwa ni mkombozi kwa wasanii wetu na chanzo mahsusi cha habari na kisima cha elimu, Jumatatu hii lilibeba mada ya Mchango wa Sekta ya Utangazaji Katika Kulinda Maadili ya Mtanzania iliyowasilishwa na Bi.Mabel Masasi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Akiwasilisha mada yake ambayo ilivuta idadi kubwa ya watu,Bi Masasi aliyataja majukumu ya mamlaka yake ambayo ni pamoja na kulinda haki na maslahi ya wateja, kuchochea kuwepo kwa watoa huduma waliosajiliwa, kutoa leseni kwa watangazaji, posta na mawasiliano ya kielektroniki, kuweka viwango vya huduma katika mawasiliano nk.

Aidha, aligusia suala la maadili katika vyombo vya habari ambapo alisema kwamba, kumekuwa na kazi za sanaa chafu ambazo zimekuwa zikipita kwenye vyombo vya habari na mamlaka imekuwa ikichukua hatua na kuvitoza faini vyombo hivyo kwa kupitisha kazi chafu za sanaa.

Aliongeza kwamba, mamlaka ya mawasiliano imekuwa ikifuatilia kwa makini programu zote katika redio hususan zile zinazorusha muziki na filamu na kuhakikisha kuwa hakuna kazi chafu za sanaa zinazopita.Katika hili wadau wengi walihoji lugha chafu zinazotumiwa na watangazaji katika vituo vya redio hususan vya FM.

Hata hivyo, wadau wengi waliochangia mada hiyo, walilalamikia sana rushwa miongoni mwa watangazaji na Ma DJ wa redio na wamesema kwamba, zimepelekea gemu la muziki kupwaya.Katika hili wadau wameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuanza mkakati wa kuvibana vituo vya redio kwani vimekuwa ni tatizo kwa maendeleo ya muziki.

Suala lingine lililoibuka, ni suala la vituo vya redio kutokuwalipa wasanii mirabaha ambapo ilishauriwa kuwa TCRA iwaze sasa kuvibana vituo vya redio na TV ambavyo havilipi mirabaha kwa wasanii.Wazo hili liliungwa mkono na wadau wengi hasa ikizingatiwa kwamba,TCRA ndiyo wanaotoa leseni kwa vituo hivyo.TCRA walisema kwamba, watalifanyia kazi kwa kushirikiana na COSOTA.

Hata hivyo, kumekuwa na tatizo la wasanii wenyewe kusaini mikataba na vituo vya redio ya kutolipwa chochote na badala yake wanaruhusu kazi zao zichezwe bure.Ilielezwa kwamba, wasanii wamekuwa hawajali mikataba na wengine wamekuwa wakisaini kazi zao kupigwa bure bila wao kulipwa.Tatizo hili linaonekana kuwa kubwa na wasanii wamekuwa wakilalama bila kuchukua hatua na kujali kai zao.

Kwa ujumla wadau,Jukwaa la Sanaa ni Mahali ambapo wasanii wanapaswa kufika kwa wingi kila Jumatatu kuanzia saaa 4 hadi saa 6.Ni kupitia Jukwaa hili la Sanaa, tutaweza kufika mbele kutokana na mijadala inayoibuka, elimu inayotolewa na kuwepo kwa masuala ya msingi kuhusu sekta ya sanaa na utamaduni yanayoibuka na kujibiwa.

Jumatatu ijayo yaani Tarehe 23/8/2010, Jukwaa la Sanaa Kama kawaida litakuja na Mada ya URASIMISHAJI WA WASANII,ambayo pamoja na mambo mengine itahusu utambuzi wa wasanii ili kufuta dhana inayojengeka sasa kwamba Msanii ni mtu muongo,mbabaishaji, mchovu na asiye na dili.Tafadhali Usikosekane,Fika.

Aug 16, 2010

WANA CCM IRINGA KESHO KUFANYA MAANDAMANO KUPINGA MAAMUZI YA NEC YA CCM DODOMA KUMTEUA MONICA MBEGA


HASIRA zatawala kwa wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) jimbo la Iringa mjini na Njombe magharibi ambao wanapinga maamuzi ya wajumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Taifa chini ya mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete kukata majina ya washindi wa kura za maoni na kuwapa ridhaa wagombea wasiotakiwa ndani ya CCM.


Huku siri zaendelea kuvuja kuhusiana na Mwakalebela na Fadhil Ngijilo kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa ni njama za mfanyabiashara mmoja mkubwa mjini Iringa mwenye asili ya kiasia ambaye anatajwa kuwa ndiye aliyesuka mpango wa kuwafanya wagombea hao kufikishwa mahakamani na wagombea wengine kutoka jimbo la Mufindi kaskazin lengo likiwa ni saidia Mbega aonekane msafi.


Hivyo hatua hiyo imeonekana kuwakwaza zaidi jambo ambalo wamekusudia kesho jumatatu kukutana majira ya asubuhi ofisi za CCM wilaya na mkoa kurejesha kadi zao na kwenda ofisi za Chadema kuchukua kadi za uanachama .


Pamoja na hayo pia diwani mpambanaji wa ufisadi katika CCM kata ya Miyomboni Kitanzini Gravas Kalolo aliyeshindwa kura za maoni na mshindi wa pili wa kura za maoni (CCM) jimbo la Njombe kaskazin Alatanga Nyagawa kutangaza rasmi kujiunga na Chadema akiwemo aliyekuwa mwekahazina wa vijana TLP Taifa Abuu Changawa Majeck huku mshindi wa kura za maoni jimbo la Njombe Magharibi Thomas Nyimbo akiahidi kutoa uamuzi wake wamwisho dhidi ya CCM ndani ya masaa 48 kuanzia leo saa 5 asubuhi.


Maamuzi hayo ya CCM Taifa yameonyesha kuwakwaza zaidi wana CCM hao ambapo hadi majira majira ya saa 6 mchana katika jimbo la Iringa mjini na Njombe Magharibi zaidi ya wana CCM 1000 walitangaza kujiunga rasmi na chama cha demokrasia na maendeleo(Chadema) ikiwa ni pamoja na kurejesha kadi za CCM Chadema huku baadhi yao wakimtangaza rasmi mgombea ubunge wa Chadema Iringa mjini Mchungaji Peter Msingwa kuwa mbunge mteuli wa jimbo hilo.


Mchungaji Msigwa ameonyesha ni chaguo la wana Iringa bila kujali itikadi ya vyama vyao baada ya mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa mjini Iringa ambaye alikuwa msaada mkubwa kwa CCM kumkabidhi pipa moja la mafuta aina ya Dizel kwa ajili ya kampeni za ubunge.


baada ya halmashauri kuu ya CCM Taifa kukata jina la Thomas Nyimbo na Frederick Mwakalebela pamoja na kushinda kwa kishindo katika kura za maoni.


Nyimbo katika kura za maoni CCM jimbo la Njombe Magharibi alishinda kwa kura 6,795 akifuatiwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Yono Kevela aliyepata kura 3,434 huku mteule wa CCM atakayegombea ubunge jimbo hilo Gerson Lwenge akiambulia kura 2,971 japo mbalo linapingwa na wana CCM jimbo hilo la Njombe Magharibi kuwa ni vema hata wange mchukua mtu wa nne .



Danford Mpumilwa (854) ama msaidizi wa askofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya kusini Mch. Isaya Mengele (822) kuliko kumpata mshindi watatu ambaye ndiye aliongoza kwa kucheza rafu katika mchakato huo.


Daud Twengele na Yohana Mussa ambao ni wana CCM wa jimbo hilo la Njombe Magharibi walisema kuwa wanasikitishwa sana na maamuzi ya halmashauri kuu ya CCM kumtema Nyimbo kwa sababu zao wenyewe jambo ambalo walidai kuwa mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Kikwete asitegemee kura za wana CCM katika jimbo hilo ambalo wamefanya uchakatuaji mgombea wao .


" CCM yenyewe ilitueleza kuwa Nyimbo ambaye alikuwa amefungiwa kugombea nafasi yoyote ndani ya CCM kuwa amemaliza adhabu yake ..... sasa sisi wana CCM tumemchagua ili arudi kututumikia kama mbunge wetu bungeni wao wanakutana Dodoma na kupinga maamuzi yetu na kumleta mtu wao ambaye sisi tulimkataa ....sasa tunasema wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa waliompendekeza huyu tuliyemtema sisi ndio watakuja kumchagua katika uchaguzi mkuu octoba ila sisi kura zetu ni upinzani na hata kama leo Nyimbo atakwenda chama chenye mwelekeo kama Chadema ajue ushindi alioupata utakuwa mara tano zaidi "



Pamoja na wana CCM hao katika jimbo la Njombe Magharibi kutangaza msimamo wao wa kwenda na Nyimbo popote atakapotangaza kuwania ubunge ,wapambe wa Monica Mbega na wale wa Mwakalebela katika jimbo la Iringa mjini juzi usiku na jana wameshinda wakigombana kupinga maamuzi ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa kumpitisha Mbega kugombea tena jimbo hilo.


Walisema kuwa kura 2,989 alizoambulia Mbega katika mchakato huo dhidi ya kura 3,897 zilizompa ushindi Mwakalebela ni ishara tosha kuwa wana CCM jimbo hilo la Iringa mjini walikuwa wamechoka na uwakilishi wa Mbega na ndio sababu ya kumpumzisha kwa kumpa nafasi hiyo Mwakalebela .


Akizungumza kwa niaba ya wana CCM waliofika ofisi za Chadema kurejesha kadi na kujiunga na chama hicho Sarehe Ngole alisema kuwa kama wajumbe hao wa NEC waliona kuwa Mbega anafaa kuendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo wasingeruhusu wana CCM wengine kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo bali wangempitisha mgombea wao.


" CCM inataka kutufanya sisi ni hayawani tusiojua chochote ...kwani kama wana CCM tuliacha shughuli zetu na kwenda katika kampeni za kura za maoni na kuacha kwenda makanisani na kushiriki kuchagua mgombea wetu Mwakalebela iweje wao Dodoma wampitishe Mbega.....tunasema Mbega ni mbunge wa NEC Dodoma sio jimbo la Iringa mjini ....sisi jimbo la Iringamjini mbunge wetu ni Frederick Wilfredy Mwakalebela ndie ambaye tunamtaka asimame katika uchaguzi mkuu vinginevyo mgombea wa Chadema jimbo hilo mchungaji Peter Msigwa kuanzia sasa tunamkatanga rasmi kama mbunge wetu asubiri kuapishwa baada ya uchaguzi"


Hata hivyo alipinga sababu za NEC kumuengua Mwakalebela kwa tuhuma za Rushwa kwani walisema kuwa ndani ya CCM hakuna ambaye mgombea ambaye ameingia bila kutoa rushwa labda walioshika nafasi za mwisho ndio ambao walishindwa kwa kukosa pesa na kuwa katika jimbo hilo wote wasingepitishwa nafasi hiyo wangemteua John Kiteve ambaye kati ya wagombea 12 alikuwa wa mwisho kwa kupata kura 136 kuwa huyo ndiye mgombea safi na hakutumia rushwa ya aina yoyote kuomba kura zaidi ya maelezo yake.


Kwa upande wake mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Iringa mjini mchungaji Msingwa akiwapokea wana CCM hao alisema kuwa wana CCM wanajidanganya wenyewe kwa kupinga rushwa wakiwa ndani ya CCM huku na kuwa watanzania wamechoshwa na CCM sasa wanahitaji mageuzi ya kweli bila CCM.


Msigwa alisema kuwa inashangaza kuona watanzania wanaendelea kudanganywa na fulana za wagombea wa CCM huku wakiendelea kupata viongozi wabovu wasiojali maendeleo zaidi ya kuangalia maslahi yao .


Hata hivyo alisema baraka idadi ya wana CCM wakiwemo wale walioshindwa udiwani na ubunge ambao wametangaza kujiunga Chadema ni kielelezo tosha kuwa CCM jimbo la Iringa mjini haina chake na badala yake viongozi wake kuendelea kutoa ushirikiano kwa Chadema ambacho ni chama mbadala kwa CCM.


Pia Msigwa alisema tayari wana CCM wakiwemo wafanyabiashara ambao walikuwa wakikisaidia chama cha mapinduzi wameanza kuomba kukisaidia chadema kwa nguvu zote na hadi sasa pipa moja la mafuta ya kampeni limepatikana.

WAREMBO WA EASTERN ZONE 2010 WAAGWA

MREMBO ANGERINA NGEGE AKIWA AMEPOZI KWA PICHA
MKURUGENZI WA KAMPUNI YA KIMKEV ENTERTAINMENT AMBAO NI WAANDAJI
WA MISS EASTERN ZONE),BW.KIM KIMENYA AKIONGEA NA WAREMBO PAMOJA NA WAGENI WAALIKWA WAKATI AKIWAKARIBISHA DINNER ALIYOWAANDALIA WAREMBO WA EASTERN ZONE KWA AJILI YA KUWAAGA KABLA YA KUJIUNGA NA KAMBI YA MISS VODACOM TANZANIA KWENYE HOTELI YA CITY STYLE SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 14.08.2010.KAMBI YA MISS TANZANIA INATARAJI KUANZA TAREHE 16.08.2010MKURUGENZI WA KAMPUNI YA KIMKEV ENTERTAINMENT, BW.KIM KIMENYA AKIMKABIDHI POSHO YA KUJIKIMU MREMBO ANGELINA NDEGE.
MREMBO ANGELINA NDEGE AKIONGEA JAMBO WAKATI WA DINNER YA KUWAAGA WAREMBO WA EASTERN ZONE 2010 NDANI YA HOTELI YA CITY STYLE SINZA
VILAJI VIKIGONGANISHWA
PICHA YA PAMOJA NA WAREMBO,UOGOZI WA HOTELI YA CITY STYLE NA WADAU.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA