Aug 17, 2010

MAADILI KWA VYOMBO VYA HABARI/WASANII YAGONGANISHA VICHWA

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Ghonche Materego (Kulia) akisisitiza jambo wakati akichangia mada kwenye Jukwaa la Sanaa Jumatatu hii.Katikati ni mwasilishaji wa mada, Bi.Mabel Masasi na Katibu wa CAJAtz,Hassan Bumbuli.Mdau wa Sanaa na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Video Library nchini, Richard Kalinga akichangia mada kuhusu Mchango wa Sekta ya Utangazaji Katika Kulinda Maadili ya Mtanzania.Mkongwe wa Sanaa za Maonyesho,Nkwama Bhalanga akilia na rushwa kwenye vituo vya redio ambapo alisema kwamba ni kikwazo katika maendeleo ya muziki nchini.Alipendekeza vibanwe na TCRA kupitia utoaji leseni.Aliyekaa kulia kwake,ni Mkongwe wa dansi nchini,Kasim Mapili.

Umakini zaidi kwa wadau wa sanaa kwenye Jukwaa.Hapa wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa BASATA,Bw.Materego (hayuko pichani) wakati akihitimisha mada ya siku ya leo.


**************** *****************

Wadau, kama kawaida Jukwaa la Sanaa ambalo sasa limekuwa ni mkombozi kwa wasanii wetu na chanzo mahsusi cha habari na kisima cha elimu, Jumatatu hii lilibeba mada ya Mchango wa Sekta ya Utangazaji Katika Kulinda Maadili ya Mtanzania iliyowasilishwa na Bi.Mabel Masasi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Akiwasilisha mada yake ambayo ilivuta idadi kubwa ya watu,Bi Masasi aliyataja majukumu ya mamlaka yake ambayo ni pamoja na kulinda haki na maslahi ya wateja, kuchochea kuwepo kwa watoa huduma waliosajiliwa, kutoa leseni kwa watangazaji, posta na mawasiliano ya kielektroniki, kuweka viwango vya huduma katika mawasiliano nk.

Aidha, aligusia suala la maadili katika vyombo vya habari ambapo alisema kwamba, kumekuwa na kazi za sanaa chafu ambazo zimekuwa zikipita kwenye vyombo vya habari na mamlaka imekuwa ikichukua hatua na kuvitoza faini vyombo hivyo kwa kupitisha kazi chafu za sanaa.

Aliongeza kwamba, mamlaka ya mawasiliano imekuwa ikifuatilia kwa makini programu zote katika redio hususan zile zinazorusha muziki na filamu na kuhakikisha kuwa hakuna kazi chafu za sanaa zinazopita.Katika hili wadau wengi walihoji lugha chafu zinazotumiwa na watangazaji katika vituo vya redio hususan vya FM.

Hata hivyo, wadau wengi waliochangia mada hiyo, walilalamikia sana rushwa miongoni mwa watangazaji na Ma DJ wa redio na wamesema kwamba, zimepelekea gemu la muziki kupwaya.Katika hili wadau wameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuanza mkakati wa kuvibana vituo vya redio kwani vimekuwa ni tatizo kwa maendeleo ya muziki.

Suala lingine lililoibuka, ni suala la vituo vya redio kutokuwalipa wasanii mirabaha ambapo ilishauriwa kuwa TCRA iwaze sasa kuvibana vituo vya redio na TV ambavyo havilipi mirabaha kwa wasanii.Wazo hili liliungwa mkono na wadau wengi hasa ikizingatiwa kwamba,TCRA ndiyo wanaotoa leseni kwa vituo hivyo.TCRA walisema kwamba, watalifanyia kazi kwa kushirikiana na COSOTA.

Hata hivyo, kumekuwa na tatizo la wasanii wenyewe kusaini mikataba na vituo vya redio ya kutolipwa chochote na badala yake wanaruhusu kazi zao zichezwe bure.Ilielezwa kwamba, wasanii wamekuwa hawajali mikataba na wengine wamekuwa wakisaini kazi zao kupigwa bure bila wao kulipwa.Tatizo hili linaonekana kuwa kubwa na wasanii wamekuwa wakilalama bila kuchukua hatua na kujali kai zao.

Kwa ujumla wadau,Jukwaa la Sanaa ni Mahali ambapo wasanii wanapaswa kufika kwa wingi kila Jumatatu kuanzia saaa 4 hadi saa 6.Ni kupitia Jukwaa hili la Sanaa, tutaweza kufika mbele kutokana na mijadala inayoibuka, elimu inayotolewa na kuwepo kwa masuala ya msingi kuhusu sekta ya sanaa na utamaduni yanayoibuka na kujibiwa.

Jumatatu ijayo yaani Tarehe 23/8/2010, Jukwaa la Sanaa Kama kawaida litakuja na Mada ya URASIMISHAJI WA WASANII,ambayo pamoja na mambo mengine itahusu utambuzi wa wasanii ili kufuta dhana inayojengeka sasa kwamba Msanii ni mtu muongo,mbabaishaji, mchovu na asiye na dili.Tafadhali Usikosekane,Fika.

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA