Waziri wa Sayansi na Tek nolojia Prof. Peter Msolla akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni ishirini Prof. Mathew Luhanga wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufuatia Taasisi ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kutoa tuzo za taifa za ugunduzi na ubunifu na kutoa Mwega kwa ajili ya utafiti mwaka 2010.
Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla akimtunuku cheti cha mshindi wa kwanza Prof. Mathew Luhanga wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufuatia Taasisi ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kutoa tuzo za taifa za ugunduzi na ubunifu na kutoa Mwega kwa ajili ya utafiti mwaka 2010.
(Picha na Aron Msigwa - MAELEZO)
Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla akiangalia mbegu za mahindi na kupata maelezo kutoka kwa mtaalam wa Kilimo Kutoka kituo cha utafiti Ilonga kilichoko kilosa mkoani Morogoro Dkt. Chaboba Mkangwa. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Hassan Mshindi.
Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Bw. Godfrey Kimarya mgunduzi wa tanuru la mkaa lenye uwezo wa kutoa mkaa mwingi na wenye ubora kwa gharama nafuu leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kutoa Tuzo za Taifa za Ugunduzi na Ubunifu pamoja na utoaji wa fedha za kusaidia shughuli za utafiti wa elimu, kilimo,ufugaji, ufundi na viwanda kwa taasisi na vikundi mbalimbali nchini.Wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine -Morogoro (SUA) Prof. Rhodes Makundi (kulia) na Christophe Cox (kushoto) wakitoa maelezo ya panya buku wenye uwezo kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini na vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu (TB) leo jijini Dar es salaam wakati sherehe ya kutoa Tuzo za Taifa za Ugunduzi na Ubunifu pamoja na utoaji wa fedha za kusaidia shughuli za utafiti wa elimu, kilimo,ufugaji, ufundi na viwanda kwa taasisi na vikundi mbalimbali nchini .Profesa Rhodes Makundi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine - Morogoro (SUA) akitoa ufafanuzi wa panya buku wenye uwezo wa kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini na vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu (TB) kwa Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kutoa tuzo za taifa za ugunduzi na ubunifu na kutoa Mwega kwa ajili ya utafiti(Picha na Aron Msigwa - MAELEZO)
No comments:
Post a Comment