Aug 16, 2010

WANA CCM IRINGA KESHO KUFANYA MAANDAMANO KUPINGA MAAMUZI YA NEC YA CCM DODOMA KUMTEUA MONICA MBEGA


HASIRA zatawala kwa wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) jimbo la Iringa mjini na Njombe magharibi ambao wanapinga maamuzi ya wajumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Taifa chini ya mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete kukata majina ya washindi wa kura za maoni na kuwapa ridhaa wagombea wasiotakiwa ndani ya CCM.


Huku siri zaendelea kuvuja kuhusiana na Mwakalebela na Fadhil Ngijilo kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa ni njama za mfanyabiashara mmoja mkubwa mjini Iringa mwenye asili ya kiasia ambaye anatajwa kuwa ndiye aliyesuka mpango wa kuwafanya wagombea hao kufikishwa mahakamani na wagombea wengine kutoka jimbo la Mufindi kaskazin lengo likiwa ni saidia Mbega aonekane msafi.


Hivyo hatua hiyo imeonekana kuwakwaza zaidi jambo ambalo wamekusudia kesho jumatatu kukutana majira ya asubuhi ofisi za CCM wilaya na mkoa kurejesha kadi zao na kwenda ofisi za Chadema kuchukua kadi za uanachama .


Pamoja na hayo pia diwani mpambanaji wa ufisadi katika CCM kata ya Miyomboni Kitanzini Gravas Kalolo aliyeshindwa kura za maoni na mshindi wa pili wa kura za maoni (CCM) jimbo la Njombe kaskazin Alatanga Nyagawa kutangaza rasmi kujiunga na Chadema akiwemo aliyekuwa mwekahazina wa vijana TLP Taifa Abuu Changawa Majeck huku mshindi wa kura za maoni jimbo la Njombe Magharibi Thomas Nyimbo akiahidi kutoa uamuzi wake wamwisho dhidi ya CCM ndani ya masaa 48 kuanzia leo saa 5 asubuhi.


Maamuzi hayo ya CCM Taifa yameonyesha kuwakwaza zaidi wana CCM hao ambapo hadi majira majira ya saa 6 mchana katika jimbo la Iringa mjini na Njombe Magharibi zaidi ya wana CCM 1000 walitangaza kujiunga rasmi na chama cha demokrasia na maendeleo(Chadema) ikiwa ni pamoja na kurejesha kadi za CCM Chadema huku baadhi yao wakimtangaza rasmi mgombea ubunge wa Chadema Iringa mjini Mchungaji Peter Msingwa kuwa mbunge mteuli wa jimbo hilo.


Mchungaji Msigwa ameonyesha ni chaguo la wana Iringa bila kujali itikadi ya vyama vyao baada ya mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa mjini Iringa ambaye alikuwa msaada mkubwa kwa CCM kumkabidhi pipa moja la mafuta aina ya Dizel kwa ajili ya kampeni za ubunge.


baada ya halmashauri kuu ya CCM Taifa kukata jina la Thomas Nyimbo na Frederick Mwakalebela pamoja na kushinda kwa kishindo katika kura za maoni.


Nyimbo katika kura za maoni CCM jimbo la Njombe Magharibi alishinda kwa kura 6,795 akifuatiwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Yono Kevela aliyepata kura 3,434 huku mteule wa CCM atakayegombea ubunge jimbo hilo Gerson Lwenge akiambulia kura 2,971 japo mbalo linapingwa na wana CCM jimbo hilo la Njombe Magharibi kuwa ni vema hata wange mchukua mtu wa nne .



Danford Mpumilwa (854) ama msaidizi wa askofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya kusini Mch. Isaya Mengele (822) kuliko kumpata mshindi watatu ambaye ndiye aliongoza kwa kucheza rafu katika mchakato huo.


Daud Twengele na Yohana Mussa ambao ni wana CCM wa jimbo hilo la Njombe Magharibi walisema kuwa wanasikitishwa sana na maamuzi ya halmashauri kuu ya CCM kumtema Nyimbo kwa sababu zao wenyewe jambo ambalo walidai kuwa mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Kikwete asitegemee kura za wana CCM katika jimbo hilo ambalo wamefanya uchakatuaji mgombea wao .


" CCM yenyewe ilitueleza kuwa Nyimbo ambaye alikuwa amefungiwa kugombea nafasi yoyote ndani ya CCM kuwa amemaliza adhabu yake ..... sasa sisi wana CCM tumemchagua ili arudi kututumikia kama mbunge wetu bungeni wao wanakutana Dodoma na kupinga maamuzi yetu na kumleta mtu wao ambaye sisi tulimkataa ....sasa tunasema wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa waliompendekeza huyu tuliyemtema sisi ndio watakuja kumchagua katika uchaguzi mkuu octoba ila sisi kura zetu ni upinzani na hata kama leo Nyimbo atakwenda chama chenye mwelekeo kama Chadema ajue ushindi alioupata utakuwa mara tano zaidi "



Pamoja na wana CCM hao katika jimbo la Njombe Magharibi kutangaza msimamo wao wa kwenda na Nyimbo popote atakapotangaza kuwania ubunge ,wapambe wa Monica Mbega na wale wa Mwakalebela katika jimbo la Iringa mjini juzi usiku na jana wameshinda wakigombana kupinga maamuzi ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa kumpitisha Mbega kugombea tena jimbo hilo.


Walisema kuwa kura 2,989 alizoambulia Mbega katika mchakato huo dhidi ya kura 3,897 zilizompa ushindi Mwakalebela ni ishara tosha kuwa wana CCM jimbo hilo la Iringa mjini walikuwa wamechoka na uwakilishi wa Mbega na ndio sababu ya kumpumzisha kwa kumpa nafasi hiyo Mwakalebela .


Akizungumza kwa niaba ya wana CCM waliofika ofisi za Chadema kurejesha kadi na kujiunga na chama hicho Sarehe Ngole alisema kuwa kama wajumbe hao wa NEC waliona kuwa Mbega anafaa kuendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo wasingeruhusu wana CCM wengine kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo bali wangempitisha mgombea wao.


" CCM inataka kutufanya sisi ni hayawani tusiojua chochote ...kwani kama wana CCM tuliacha shughuli zetu na kwenda katika kampeni za kura za maoni na kuacha kwenda makanisani na kushiriki kuchagua mgombea wetu Mwakalebela iweje wao Dodoma wampitishe Mbega.....tunasema Mbega ni mbunge wa NEC Dodoma sio jimbo la Iringa mjini ....sisi jimbo la Iringamjini mbunge wetu ni Frederick Wilfredy Mwakalebela ndie ambaye tunamtaka asimame katika uchaguzi mkuu vinginevyo mgombea wa Chadema jimbo hilo mchungaji Peter Msigwa kuanzia sasa tunamkatanga rasmi kama mbunge wetu asubiri kuapishwa baada ya uchaguzi"


Hata hivyo alipinga sababu za NEC kumuengua Mwakalebela kwa tuhuma za Rushwa kwani walisema kuwa ndani ya CCM hakuna ambaye mgombea ambaye ameingia bila kutoa rushwa labda walioshika nafasi za mwisho ndio ambao walishindwa kwa kukosa pesa na kuwa katika jimbo hilo wote wasingepitishwa nafasi hiyo wangemteua John Kiteve ambaye kati ya wagombea 12 alikuwa wa mwisho kwa kupata kura 136 kuwa huyo ndiye mgombea safi na hakutumia rushwa ya aina yoyote kuomba kura zaidi ya maelezo yake.


Kwa upande wake mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Iringa mjini mchungaji Msingwa akiwapokea wana CCM hao alisema kuwa wana CCM wanajidanganya wenyewe kwa kupinga rushwa wakiwa ndani ya CCM huku na kuwa watanzania wamechoshwa na CCM sasa wanahitaji mageuzi ya kweli bila CCM.


Msigwa alisema kuwa inashangaza kuona watanzania wanaendelea kudanganywa na fulana za wagombea wa CCM huku wakiendelea kupata viongozi wabovu wasiojali maendeleo zaidi ya kuangalia maslahi yao .


Hata hivyo alisema baraka idadi ya wana CCM wakiwemo wale walioshindwa udiwani na ubunge ambao wametangaza kujiunga Chadema ni kielelezo tosha kuwa CCM jimbo la Iringa mjini haina chake na badala yake viongozi wake kuendelea kutoa ushirikiano kwa Chadema ambacho ni chama mbadala kwa CCM.


Pia Msigwa alisema tayari wana CCM wakiwemo wafanyabiashara ambao walikuwa wakikisaidia chama cha mapinduzi wameanza kuomba kukisaidia chadema kwa nguvu zote na hadi sasa pipa moja la mafuta ya kampeni limepatikana.

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA