Umati mkubwa wa wananchi wa mji wa Iringa na vitongoji vyake ulifurika kusikiliza kesi ya tuhuma za rushwa iliyofunguliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU, dhidi ya aliyekuwa mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, bwana Frederick Mwakalebela.
Kesi hiyo ndivyo iliyotamkwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM kuwa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, NEC-CCM kama kigezo kikuu cha kuliengua jina la Frederick Mwakalebela katika nafasi hiyo hata ikiwa alishinda katika kura ya maoni, na badala yake nafasi hiyo kupewa mbunge aliyemaliza muda wake na anayewania tena nafasi hiyo, bi Monica Mbega.
Inasimuliwa na Francis Godwin kupitia blogu yake kuwa umati mkubwa wa wananchi wa jimbo la Iringa waliacha shughuli zao na kufika kusikiliza kesi ya Mwakalebela kiasi cha watu kukosa nafasi za kuketi ndani na hivyo kuifuatilia kesi hiyo wakiwa nje ya chumba cha Mahakama ilikokuwa ikiendelea kesi hiyo.
Anasema kuwa baadhi ya wananchi walikuwa na barua zao tayari kwa ajili ya kumdhamini bwana Mwakalebela endapo ingehitajika kufanya hivyo, vile vile, “…mahakimu wasema haijapata kutokea toka kuanzishwa kwa mahakama hiyo umati mkubwa kama huo kuja mahakamani kusikiliza kesi”.
Mwalalebela, ambaye alikuwa kajiandaa kikamilifu, alipataa dhamana iliyosainiwa ya shilingi Milioni 5 na wadhamini wawili.
No comments:
Post a Comment