Aug 17, 2010

warembo wa miss tanzania waingia kambini leo

warembo wa Miss Tanzania wanaoingia kambini leo hii,wakiwa katika usafiri wao tayari kwa safari ya kuelekea Kambini.
wakiingia katika usafiri wao.
walinzi wa warembo (Mabaunsa)

Warembo waliofanikiwa kuingia Fainali ya Taifa ya Mashindano ya Urembo ya VODACOM MISS TANZANIA 2010, leo wameingia kambini kwa ajili ya kuanza mchakato wa kumrithi mrembo anayemaliza muda wake, Miriam Gerald.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo mchana kabla ya warembo hao kuelekea Kambini, Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, alisema kuwa “Warembo hao Wakiwa kambini watakuwa na ratiba mbali mbali ikiwa ni pamoja na kufanya kazi za kijamii na kutembelea sehemu mbali mbali za vivutio vya kitalii”

Alizitaja sehemu hizo kuwa siku ya Tarehe 17 / 08 / 2010 warembo watapewa semina maalumu na viongozi wa kamati ya Miss Tanzania pamoja na kusaini mikataba kati yao na waandaaji.

Tarehe 19 / 08 / 2010 waandishi wa habari wote watapata nafasi ya kuongea na washiriki na kupata maoni yao na jinsi walivyojiandaa katika kunyakuwa taji la VODACOM MISS TANZANIA 2010

Mwishoni mwa wiki warembo wote wakiambatana na baadhi ya viongozi wa kamati watasafiri kwenda katika mikoa ya kanda ya kaskazini “KILIMANJARO: na “ARUSHA” kwa ajiri ya kutembelea vivutio vya utalii ili kuvitangaza na kuwahamasisha watanzania ili wajenge utamaduni wa kutembelea, kuvilinda na kuvithamini vivutio vyetu.

Huu ni mpango tunaoshirikiana na taasisi za serikali yaani ,BODI YA UTALII, TANAPA na NGORONGORO CONCERVATION AREA AUTHORITY.

Huu ni mwaka wa pili taasisi yetu “Miss Tanzania” kushirikiana na taasisi za serikali kuhamasisha watanzania kuthamini na kutembelea vivutio vilivyopo nchini kwetu.

Tunategemea kwenda mbele zaidi kwa kuvitembelea vivutio vya kusini mwa Tanzania, SELOUS, RUAHA NATIONAL PARK, MIKUMI na UDIZUNGWA, katika siku za usoni.

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA