Aug 25, 2010

UZINDUZI WA KIPINDI CHA ZAMARADI CHA TAKE ONE KILIVYOFANA JANA,

Muhongo mchungu na baba hapo wakijadili jambo
Claud na mkewe walikuwepo jana.

Bi mwenda nae hakubaki nyuma

Zamaradi,dina na Dj Fetty...

Natasha na Bi mwenda
Kutoka kitengo chetu cha habari mwenye shati jeupe anaitwa Lazaro Matalange na Philip Mwihava..

Stella wa hapa clouds upande wa masoko na Wakuvanga wakishow love jana.


Singe Mtambalike a.k.a Richie richie hakubaki nyuma maana hili jambo ni lao pia.


Wasanii jana walipata pia nafasi ya kubadilishana mawazo,kwa mbali unamuona Dr.Cheni.


Utani ulikuwepo mwingi sanaYvone Sherry a.k.a Monalisa nampendaga sana huyu dada

Ben Kinyaiya


TANGAZO LA MSIBA (BANGALORE INDIA)

KWA NIABA YA FAMILIA YA MAREHEMU BWANA NA BIBI MWAKALASI YA KIJITONYAMA, BW RODRICK MWAMBENE NA BI JULIETH MWAKALASI WANAWATANGAZIA NDUGU NA JAMAA KUWA NDUGU YAO MPENDWA, EDWIN MBONELA MWAKALASI ALIYEKUWA ANASOMA NCHINI INDIA KATIKA CHUO CHA ACHARYA BANGALORE AMEFARIKI AGOSTI 21 BAADA YA KUUGUA KWA MUDA MFUPI.

MWILI WA MAREHEMU UMEKWISHA WASILI NCHINI NA IBADA YA KUMUOMBEA ITAFANYIKA NYUMBANI KWAO, KIJITONYAMA (KARIBU NA SHULE YA MSINGI KIJITONYAMA) NA BAADAYE MAZISHI KUFANYIKA KATIKA MAKABURI YA KINONDONI ENEO LA MWEMBENI 25 .8.2010 SAA 10.00 ALASIRI.

PIA IBADA YA HESHIMA ZA MWISHO ZITATOLEWA KUANZIA SAA 6.00 MCHANA HAPO HAPO NYUMBANI KWAO.

KWA NIABA YA FAMILIA YA WA WAFIWA, TUNAPENDA KUTOA SHUKRANI ZA DHATI KWA WAFUATAO AMBAO WALIJITAHIDI KUOKOA MAISHA YA MAREHEMU KWA UPANDE WA MATIBABU MPAKA KUSAFIRISHA MWILI WAKE KUJA TANZANIA.

SHUKRANI ZA HIZO ZIENDE KWA:-

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA KUPITIA KWA AFISA WAKE BW. MWAMANENGE AMBAYE PIA NI MSHAURI WA WANAFUNZI WA TANZANIA NCHINI HUMO, TANZANIA STUDENT ASSOCIATION OF ACHARYA (TASAA) CHINI YA MWENYEKITI WAKE BW. HAMIS FUPI, TANZANIA STUDENT ASSOCIATION OF MYSORE (TASAM), KAMPUNI ILIYOSAFIRISHA MWILI, KUMAR AMBULANCE CO. & INTERNATIONAL, RAMAYA HOSPITAL NA NRR HOSPITAL ZOTE ZA BANGALORE.

BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA, JINA LA MBWANA LIHIMIDIWE, AMEN.

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA BW RODRICK MWAMBENE KWA SIMU NAMBA 0754 362901, 0713 362901.

OpenSanit wazindua bidhaa zao jijini Dar


Mkurugenzi Mtendaji wa kampun ya Open Sanit,Bw.Octavian Mshiu akifafanua jambo kw a mgeni rasmi Naibu Waziri wa Viwanda, biashara na Masoko Dk. Cyril Chami kabla ya kuzindua bidhaa za kampuni ya Beier Safety Footwear ya Afrika Kusini ikishirikiana na kampuni ya Open Sanit Tanzania jioni ya leo ndani ya hoteli ya Sea Cliff jijini Dar
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya BEIER SAFETY FOOTWEAR,Bw.Silvio Ceriani akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua bidhaa za kampuni hiyo.
Naibu Waziri wa Viwanda, biashara na Masoko Dk. Cyril A. Chami akimpatia zawadi wa bahati nasibu ndogo ya viatu iliyofanyika katika uzinduzi huo,Bw. Victor Mushi,ambapo watu kadhaa walijinyakulia zawadi hizo za viatu vikiwemo viatu mbalimbali vya usalama..
Baadhi ya wageni waalikwa wakiangali baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa na kampuni hizo mbili,bidhaa hizo za aina mbalimbali zinazotumika katika masuala ya usalama hasa viwandani na kwenye makampuni.
Mmgeni rasmi Naibu Waziri wa Viwanda, biashara na Masoko Dk. Cyril Chami (tatu kulia) akioneshwa aina ya bidhaa mbalimbali zitakazokuwa zikitengenezwa na kampuni hizo mbili,ya Beier Safety Footwear ktoka Afrika Kusini ikishirikiana na kampuni ya Open Sanit (Tanzania) jioni ya leo hoteli ya Sea Cliff jijini Dar. Baadhi ya bidhaa zitakazokuwa zinatengenezwa na kampuni ya Beier Safety Footwear kutoka nchini Afrika ya Kusini ikishirikiana na kampuni ya Open Sanit ya Tanzania.kama vipi ingia http://www.opensanit.com/ kupata maelezo zaidi.

Kilimanjaro Lager Kudhamini Bongo Star Search 2010

Meneja wa bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akiongea jambo wakati wa utambulisho wa udhamini wa miaka mitatu kwa Bongo Star Search uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Paradise uliopo ndani ya jengo la Benjamin Mkapa,jijini Dar.kulia ni Mkurugenzi wa BenchMark Production,Madame Ritha Paulsen.
Mkurugenzi wa BenchMark Production,Madame Ritha Paulsen akiongea leo katika ukumbi wa hoteli ya Paradise uliopo ndani ya jengo la Benjamin Mkapa wakati wa utambulisho wa mdhamini mkuu mpya wa Bongo Star Search ambaye ni kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chak cha Kilimanjaro premium lager.kulia ni Afisa masoko na mafunzo wa TBL,Edith Bebwa.

Na Mwandishi Wetu

Bongo star search ni moja ya kipindi kinacho rushwa na television hapa nchini Tanzania ambacho kime fanikiwa kwa kiwango kikubwa kabisa kuinua vipaji vya wanamuziki wa Tanzania.

Ikumbukwe kuwa mwaka jana kampuni ya kutengeneza bia hapa nchini TBL kwa kupitia kinywaji chake kinachojihusisha na maswala ya muziki,Kilimanjaro premium lager. Ilishiriki kama mmoja wa wadhamini wa shindano hilo.

Uhusiano huu mkubwa wa kampuni hizi mbili umetokana na sababu kuu kwamba BSS inahusika kutafuta na kuinua vipaji vya wanamuziki hasa vijana wa umri wowote ambapo Kilimanjaro premium lager kufuatia kauli mbiu yake ya Kufikisha Muziki wa Tanzania Kilele cha mafanikio kwa upande mwingine ina husika na muziki wa vijana wa Kitanzania.

Kilimanjaro premium lager imekua ikunga mkono juhudi za kuendeleza Muziki hapa Tanzania kwa kiwango cha juu.. Ikiwa mdhamini mkubwa kwenye zoezi la kutoa Tunzo za Muziki Tanzania kila mwaka,Tunzo zinazojulikana kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards. Ndio maana Kilimanjaro premium lager imeona hakuna sababu ya wao kutoshirikiana na BSS 2010 katika kuinua vipaji vya wanamuziki wa Tanzania.

Kilimanjaro premium lager imeandikisha mkataba wa kuwa mdhamini wa Bongo star search kwa kipindi cha miaka mitatu ambayo ni BSS 2010, BSS 2011, BSS 2012.

Washiriki wa BSS watashirikishwa katika mambo mbali mbali yakiwemo mashindano yatakayo kua yanafanyika siku hadi siku katika jumba la BSS KILI HOUSE 2010.

BSS 2010 itakuwa ikirusha hewani kila jumapili saa tatu na robo usiku (3:15) kupitia television ya ITV ikishirikiana na Radio one na magazeti ya The Guardian ,Nipashe.unatakia kufuatilia shindano hilo bila kukosa na pia ni muhimu kupiga kura yako ili kuweza kuwachagua watakao weza kushiriki mpaka mwisho .


shiriki nasi ili kuweza kukamilisha ndoto za wanamuziki wetu.

ziara ya miss tanzania katika ziwa manyara


Baadhi ya warembo wanao shiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010 wakimsikiliza mmoja wa waongoza watalii katika Hifadhi ya Ziwa Manyara alipokuwa akiwapa maelezo juu ya hifadhi hiyo.
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakizungumza na watalii waliokutana nao jana katika hifadhi ya Ziwa Manyara.
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakipiga picha ndani ya hifadhi ya Ziwa Manyara wakati warembo hao walipotembelea ziwa hilo ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kuangalia vivutio vya utalii katika mikoa ya Kaskazini.
Baadhi ya warembo wanao shiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010 wakimsikiliza mmoja wa waongoza watalii (hayupo pichani) katika Hifadhi ya Ziwa Manyara alipokuwa akiwapa maelezo juu ya hifadhi hiyo.
Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na watalii waliotoka Chuo Kikuu cha Calfonia Los Angels Marekani waliotembelea Hifadhi ya Ziwa Manyara.



ZIARA ya warembo 30 wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010 kutembelea vivutio na rasilimali tofauti nchini zilizopo kanda ya kaskazini imeendelea na jana walikuwa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro (NCA) iliyopo mkoani Arusha.

Wakiwa ndani ya hifadhi hiyo licha ya kujionea moja ya maajabu saba ya dunia yaani bonde la Ngorongoro walipata fursa ya kujionea wanyama na baionuwai za aina mbalimbali kama vile Simba,Tembo,chui na ndege wa aina tofauti.

Mbali na hayo walijionea pia maboma ya Maasai ambayo nayo yanatumika kutangaza utamaduni wa kabila la wamaasai ambao na kuwezesha kuingiza serikali fedha nyingi za kigeni kutoka kwa watalii wanaotembelea hifadhi hiyo.

Akizungumzia kuhusiana na aliyojifunza ndani ya Ngorongoro mmoja wa warembo Angelina Ndege kutoka Mkoa wa Lindi kanda ya mashariki alisema amejifunza kwamba kuna hifadhi zingine siyo lazima waishi wanyama pori tu bali hata binadamu nao wanaishi.

“Tangia nizaliwe miaka 19 iliyopita sikuwahi kufikiri kama wanyamapori hawawezi kuishi na binadamu, lakini ndani ya bonde la Ngorongoro nimeshuhudia wanyama wakiishi na binadamu tena bila rabsha yoyote,” alisema Ndege.

Aidha alibainisha kuwa ameweza kujifunza kwamba wanyama huwa hawakai katika hifadhi moja bali huwa wanahama na kwenda sehemu zingine kutafuta malisho kuendana na hali ya hewa.

Kutokana na hilo aliwaomba Watanzania kujenga tabia ya kutembelea hifadhi za taifa zilizopo nchini na kuachana na fikra kwamba wanaopaswa kwenda katika maeneo hayo ya rasilimali za taifa ni watalii kutoka nje tu ili kusaidia kuinua uchumi wa nchi kupitia sekta ya utalii.


Mary Magali ambaye ni mrembo anaewakilisha mkoa wa Iringa aliwashukuru wadhamini wakuu wa mashindano haya ambao ni Vodacom Tanzania kwa kudhamini mashindano haya pamoja na gharama zote za kutembelea hifadhi za taifa kanda ya kaskazini ili kujionea na kujifunza kuhusiana na rasilimali za taifa.

“La muhimu nililojifunza baada ya kutembelea hifadhi za taifa ya Kinapa na Ngorongoro ni kufahamu kuhusiana na Simba wanaopanda miti wanaopatikana ndani ya kreta ikiwemo maji yam to wa mbu na kirurumo kukutana sehemu moja inayotumiwa na viboko kulala na kusambaa ziwani,” alisema Magali.

Naye Mlezi wa warembo hao ambae alikuwa mshiriki wa Vodacom Miss Tanzania 2009,Gladys Shao, alisema warembo wote wanaendelea vizuri na maandalizi na hawana matatizo yoyote ya kiafya na kwamba wanafurahia na kujifunza mambo mbalimbali ya utalii wa ndani kwani unaanza na Mtanzania mwenyewe.

bongocelebrity yafanya mahojiano na Madaraka Nyerere


Jina la Madaraka Nyerere (pichani) sio geni miongoni mwa watanzania.
Ukiachilia mbali ukweli kwamba yeye ni mtoto wa sita wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (kitu ambacho bila shaka kinampa automatic celebrity status), yeye pia ni mwandishi,mfanyabiashara na mtu ambaye huwa hasiti kuelezea hisia zake kuhusu mambo mbalimbali iwe ni katika nyanja za kisiasa,kijamii na hata kiuchumi kila mara fursa ya kufanya hivyo inapojitokeza.

Mwaka jana mwezi wa nne(April) yeye na Jaffar Amin(mtoto wa Iddi Amin-Rais wa zamani wa Uganda) waliingia katika vitabu vya kumbukumbu vya wapenda amani duniani walipokutana kwa mara ya kwanza ikiwa ni ishara ya amani na usuluhisho barani Afrika na kwingineko.

Hivi karibuni nilipata nafasi ya kuzungumza naye kuhusu mambo kadhaa yakiwemo ya kifamilia na pia kupata maoni yake kuhusu mambo mbalimbali.Je,ni kwanini mpaka leo hii hajajiingiza katika masuala ya siasa au uongozi?Anamuelezeaje Hayati Baba wa Taifa kama baba yake na kama kiongozi?

Ana ushauri gani kwa wapiga kura katika mwaka huu wa uchaguzi? Ana mtizamo gani kuhusu viongozi mbalimbali ambao hupenda kumuenzi Baba wa Taifa kwa maneno huku vitendo vyao vikiwa tofauti kabisa? Unataka kujua kwanini alipewa jina la “Madaraka”? Ana ushauri gani kwa vijana kuhusu suala zima la kujiletea maendeleo? Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo kwa ku
BOFYA HAPA

Dr. Bilali aanza kampeni mkoani Pwani


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kilwa Kusini, Ramadhan Madabida (kulia) akiteta jambo na Mgombea Mwenza, Mohamed Gharib Bilal, wakati wakimpokea kutoka Wilaya ya Rufiji kuingia Wilaya ya Kilwa Masoko akiwa katika safara ya Kampeni kwenye Mkoa huo wa Pwani.
Mkuu wa Wialaya ya Kilwa Masoko, Nurdin Babu akiongozana na Mgombea Mwenza wa Urais, Dr. Mohamed Gharib Bilali wakati alipompokea mpakani mwa Wilaya ya Rufiji kuingia kwenye Wilaya yake kuendelea na mkutano wa Kampen
Mgombea Mwenza wa urais,Dr. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Rufiji kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dk. Seif Rashid, wakati wa mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Muhoro, Tarafa na Kata ya Muhoro, Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani.
Umati wa watu, Wakazi wa Somanga wakimzunguka Mgombea Mwenza na kufunga barabara kwa muda ili kumpokea mgombea huyo alipokuwa akipita eneo hilo kuelekea Wilaya ya Kilwa Masoko.
(Picha na Muhidin Sufiani)


Na Mwandishi Wetu,Pwani

MGOMBEA mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),Dr. Mohamed Bilal amesema ifikapo mwaka 2015 kila shule ya msingi kote nchini itapaswa kuwa na darasa moja la wa chekechea.

Dk.Bilali aliyasema hayo jana wakati akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Rufiji katika mkutano wa adhara uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Mhoro Kata ya Chumbi mkoani Pwani sambamba na kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Rufiji Dk. Seif Rashid na mgombea ubunge wa Jimbo la KIbiti,Abdul Marombwa,alisema mpango huo mkakata umeainishwa katika Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015.

Dk.Bilali ambaye jana ndiyo alianza ziara ya kampeni yake rasmi mkoani hapa alisema lengo la mpango huo kuingizwa kwenye ilani hiyo ya CCM, ni chama hicho kupitia serikali yake inataka kuona wanafunzi wa shule wanaomaliza shule za awali wanajiunga na shule za msingi na sekondari na kisha kujiunga na vyuo vikuu.

“Hivi sasa taifa lisilo na wasomi ni dhahiri halitaweza kupiga hatua za kimaendeleo kwa wakati hivyo kwakuwa inapenda kuona wananchi wake wakubwa kwa wadogo wakipita elimu ndiyo maana ilani ya mwaka 2010-2015 imewekea mkazo suala la ukuzwaji wombea sekta ya elimu kwa ngazi zote hivyo nawasii sana wazazi na wananchi kote nchini muwaruhusu watoto wenu waende mashuleni kupata elimu kwani hakuna ulithi usiooza kama elimu.

Huku hotuba yake ikikatishwa mara kwa mara na vibwagizo vya nyimbo za kukisifu chama na kumpongeza rais Jakaya Kikwete kumchagua Dk.Bilali kuwa mgombea mwenza, alisema ili mpango huo utimie wananchi wa kada zote hawana budi kuinga mkono serikali ya ccm ilikuweza ujenzi huo wa madarasa ya wananfunzi wa shule za awali yanajengwa na kuongeza kwa kuwataka wananchi wote wanampatia kura za ndiyo mgombea urais wa ccm,Kikwete Leo mgombea mwenza ataendelea na ziara yake ya kampeni mkoani Kilwa.

Aug 24, 2010

Wanja Jipya La Mdau




unaweza kumpembelea kwa link yake hiyo hapo.
http://www.mateja20.blogspot.com/

vodacom miss tanzania watembelea mbuga ya ngorongoro


Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiangalia Simba anayepita karibu na magari yao wakati warembo hao walipotembelea Hifadhi ya Ngorongoro kujionea wanyama na mambo mbali mbali yalipo katika hifadhi hiyo.
Baadhi ya warembo wanoshiriki mashindano ya Kumsaka Vodacom Miss Tanzania wakicheza ngoma ya Kimasai wakati walipokaribishwa katika Boma la wafugaji hao lililopo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro wakati wakiwa katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Mikoa ya Kaskazini, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani.
Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakitoka katika nyumba za Tembe za wafugaji wa jamii ya Kimasai waishio katika Hifadhi ya Ngorongoro wakati wakiwa katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Mikoa ya Kaskazini, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani.
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakinunua shanga za kimasai kutoka kwa wauzaji waliopo katika Boma lililopo katika Hifadhi ya Ngorongoro wakati warembo hao walipotembelea hifadhi hiyo wakiwa katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Mikoa ya Kaskazini, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani.

Rais Kikwete Akiwa Sengerema


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wananchi katika kata ya Nyehunge jimbo la Buchosa,wilaya ya Sengerema leo mchana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na kumfariji msichana mwenye ulemavu wa ngozi aliyejitambulisha kwa jina la Rehema Mahaluko muda mfupi baada ya kuhutubia katika mkutano wa hadhara huko Nyehunge, wilayani Sengerema leo mchana.
(Picha na Freddy Maro)

MKALI AMBAYE KIDUMU AMEKOPY NA KUPEST STYLE YA MELODY NA SAUTI YAKE.(LINEX - LINENGA)

O ten akiwa na LINEX wakiingia ndani ya uwanja wa taifa kuhudhuria moja ya matamasha ya muziki wa kizazi kipya siku za hivi karibuni.
anajulikana kama LINEX SUNDAY wengi humuita LINENGA ambaye kwa sasa anasumbua kwa ngoma yake inayokwenda kwa jina la MAMA HALIMA.

LINEX & O TEN wakiwa kwenye moja ya matamasha yao
linex

Aug 22, 2010

ZIARA YA WAREMBO WA VODACOM MISS TANZANIA (KINAPA)

Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiwa wamebeba mabegi mngongoni mithili ya watalii wanaoteremka mlima Kilimanjarto wakati wa rembo hao walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) iliyopo Marangu mkoani humo jana. Warembo 30 wa Vodacom Miss Tanzania wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakizungumza na mmoja wa vijana wanaojishughulisha na kazi ya kusindikiza watalii kupanda Mlima Kilimanjaro jana wakati warembo hao walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) iliyopo Marangu mkoani humo. Warembo 30 wa Vodacom Miss Tanzania wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiangalia michoro ya ramani ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kialimanjaro (KINAPA) wakati warembo hao walipotembelea KINAPA jana. Warembo 30 wa Vodacom Miss Tanzania wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Mhifadhi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), David Loosurutia (kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya mazingira ya hifadhi hiyo kwa warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakati wa rembo hao walipotembelea KINAPA jana. Warembo 30 wa Vodacom Miss Tanzania wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

DEWJI APITA BILA KUPINGWA, PINGAMIZI DHIDI YAKE ZATUPWA.

Na Hillary Shoo,

Singida.

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya (CCM) jimbo la Singida mjini (pichani) Mohammed Dewji ameteuliwa kuwa mgombe pekee wa jimbo hilo baada ya pingamizi lililotolewa na wapinzani wake kutupwa na msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya wagombe wa vyama vingine vya upinzani, Josephat Isango wa CHADEMA na Omary Sombi wa chama cha AFP kuwasilisha pingamizi kwa msimamizi kuwa Dewji alikiuka sheria ya gharama za chaguzi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Singida mjini Yona Lucas Maki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida ilieleza kuwa baada ya kupitia kwa kina pingamizi hizo, imeonekana kuwa Dewji hakukiuka sheria ya gharama za uchaguzi kama walivyodai wapinzani wake.

Kwa mujibu wa barua yenye kumb Na. HM/SI/U.10/16/VOL.1/140 ya Agosti 21 mwaka huu kwa wagombea hao ilieleza kuwa ninawaletea uamuzi wa pingamizi hizo, mimi Yona Lucas Maki ambaye ni msimamizi wa uchaguzi jimbo la Singida, baada ya kupata maelezo ya utetezi uliyoyatoa dhidi ya pingamizi uliyowekewa ya kupinga uteuzi wa wewe Mohammed Dewji.

“Ninakataa pingamizi zilizotolewa kwa sababu haujatenda vitendo vinavyokataza chini ya sheria ya gharama za uchaguzi.”alisema Maki.

Aidha alisema kwa mujibu wa maeleekezo kwa wasimamizi wa uchaguzi , uchaguzi wa Rais , wabunge na madiwani , 2010 aya ya 5.16 kifungu cha 44 kinasema, “Kwa mujibu wa kifungo cha 44 cha sheria ya uchaguzi Na.1 ya mwaka 1985( sura ya 343) endepo mgombea aliyeteuliwa ni mmoja , baada ya kukamilisha hatua ya pingamizi atatangazwa kuwa amepita bila kupingwa , na uchaguzi hautafanyika katikaaa jimbo hilo. Tume ya Taifa ya uchaguzi itatangaza katika gazeti la serikali kuwa mgombea huyo amechaguliwa kuwa Mbunge.

“ Kwa nukuu hii hapa juu nakutangaza rasmi kuwa mgombea Ubunge ambaye umepita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu kwa mwaka 2010 katika jinbo la singida mjini.”ilisema taarifa hiyo ya Maki.

Hata hivyo Dewji alitoa maelezo yake kwa msimamizi huyo kuwa kwamba pingamizi lililotolewa chini ya sheria ya gharama za uchaguzi ni lazima lielezee matendo yasiyoendana na kifungu cha 9 cha sheria ambacho kinatamka mgombea aeleze fedha na vyanzo vingine vya fedha atakazotumia wakati wa kampeni kwa chama chake ndani ya siku 7 zitakazotamkwa na sheria.

Dewji alisema si hivyo tu sehemu ya tano ya sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010 iko wazi kwa kutamka wazi matendo ambayo yanaweza kubatilisha haki ya mtanzania kuwa mgombea ubunge.

“Kutokana na na sheria hiyo ninaomba pingamizi lililotolewa na Josephat Isango wa Chadema na Omary Sombi wa AFP yatupiliwe mbali kwa sababu limetokana na sheria isiyokuwepo hapa Tanzania.” Alisema Dewji.

Rais Kikwete Atua Mwanza na Kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Misungwi


Rais Jakaya Kikwete akimnadi Charles Kitwanga a.k.a Mawe Matatu, mgombea ubunge wa CCM wa jimbo la Misungwi Mwanza leo, akiwa ni mbunge wa kwanza kunadiwa na mwenyekiti huyo wa CCM ambaye kaanza rasmi ziara ya mikoani leo

Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride la chipukizi mara baada ya kutua jijini Mwanza leo kwa kampeni mkoa huo wa kanda ya ziwa
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Nyamagana Mh. Lawrence Masha ambaye kapita bila kupingwa katika jimbo lake. Anayemfuata ni Mh. William Ngeleja mbunge wa Sengerema ambaye naye kapita bila kupingwa
Wagombea ubunge wa CCM kanda ya ziwa wakimsubiri Rais Jakaya Kikwete alipotua jijini Mwanza leo.
Viongozi mbali mbali walijitokeza kumpokea Rais Jakaya Kikwete leo jijini Mwanza
Viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali wakisubiri kumlaki Rais Jakaya Kikwete jijini Mwanza leo kwa kampeni mkoa huo wa kanda ya ziwa.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA