Aug 25, 2010

ziara ya miss tanzania katika ziwa manyara


Baadhi ya warembo wanao shiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010 wakimsikiliza mmoja wa waongoza watalii katika Hifadhi ya Ziwa Manyara alipokuwa akiwapa maelezo juu ya hifadhi hiyo.
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakizungumza na watalii waliokutana nao jana katika hifadhi ya Ziwa Manyara.
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakipiga picha ndani ya hifadhi ya Ziwa Manyara wakati warembo hao walipotembelea ziwa hilo ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kuangalia vivutio vya utalii katika mikoa ya Kaskazini.
Baadhi ya warembo wanao shiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010 wakimsikiliza mmoja wa waongoza watalii (hayupo pichani) katika Hifadhi ya Ziwa Manyara alipokuwa akiwapa maelezo juu ya hifadhi hiyo.
Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na watalii waliotoka Chuo Kikuu cha Calfonia Los Angels Marekani waliotembelea Hifadhi ya Ziwa Manyara.



ZIARA ya warembo 30 wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010 kutembelea vivutio na rasilimali tofauti nchini zilizopo kanda ya kaskazini imeendelea na jana walikuwa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro (NCA) iliyopo mkoani Arusha.

Wakiwa ndani ya hifadhi hiyo licha ya kujionea moja ya maajabu saba ya dunia yaani bonde la Ngorongoro walipata fursa ya kujionea wanyama na baionuwai za aina mbalimbali kama vile Simba,Tembo,chui na ndege wa aina tofauti.

Mbali na hayo walijionea pia maboma ya Maasai ambayo nayo yanatumika kutangaza utamaduni wa kabila la wamaasai ambao na kuwezesha kuingiza serikali fedha nyingi za kigeni kutoka kwa watalii wanaotembelea hifadhi hiyo.

Akizungumzia kuhusiana na aliyojifunza ndani ya Ngorongoro mmoja wa warembo Angelina Ndege kutoka Mkoa wa Lindi kanda ya mashariki alisema amejifunza kwamba kuna hifadhi zingine siyo lazima waishi wanyama pori tu bali hata binadamu nao wanaishi.

“Tangia nizaliwe miaka 19 iliyopita sikuwahi kufikiri kama wanyamapori hawawezi kuishi na binadamu, lakini ndani ya bonde la Ngorongoro nimeshuhudia wanyama wakiishi na binadamu tena bila rabsha yoyote,” alisema Ndege.

Aidha alibainisha kuwa ameweza kujifunza kwamba wanyama huwa hawakai katika hifadhi moja bali huwa wanahama na kwenda sehemu zingine kutafuta malisho kuendana na hali ya hewa.

Kutokana na hilo aliwaomba Watanzania kujenga tabia ya kutembelea hifadhi za taifa zilizopo nchini na kuachana na fikra kwamba wanaopaswa kwenda katika maeneo hayo ya rasilimali za taifa ni watalii kutoka nje tu ili kusaidia kuinua uchumi wa nchi kupitia sekta ya utalii.


Mary Magali ambaye ni mrembo anaewakilisha mkoa wa Iringa aliwashukuru wadhamini wakuu wa mashindano haya ambao ni Vodacom Tanzania kwa kudhamini mashindano haya pamoja na gharama zote za kutembelea hifadhi za taifa kanda ya kaskazini ili kujionea na kujifunza kuhusiana na rasilimali za taifa.

“La muhimu nililojifunza baada ya kutembelea hifadhi za taifa ya Kinapa na Ngorongoro ni kufahamu kuhusiana na Simba wanaopanda miti wanaopatikana ndani ya kreta ikiwemo maji yam to wa mbu na kirurumo kukutana sehemu moja inayotumiwa na viboko kulala na kusambaa ziwani,” alisema Magali.

Naye Mlezi wa warembo hao ambae alikuwa mshiriki wa Vodacom Miss Tanzania 2009,Gladys Shao, alisema warembo wote wanaendelea vizuri na maandalizi na hawana matatizo yoyote ya kiafya na kwamba wanafurahia na kujifunza mambo mbalimbali ya utalii wa ndani kwani unaanza na Mtanzania mwenyewe.

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA