Oct 25, 2010

Oiko Credit Tanzania yakabidhi bilioni 2.6 kwa Saccos mbalimbali jijini dar


Meneja wa Oiko Credit Tanzania Deus Manyenye (Kushoto) akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi jumla ya bilioni 2.6 kwa Saccos za Mtoni KKKT, Bunju, Vision, Yosefo na Mgandini walizotoa kama mkopo kwa taasisi hizo ili zikatumike kusaidia kupunguza umasikini kwa jamii ya watu wa kipato cha chini. Katikati ni Mwenyekiti wa Saccos ya Yosefo Ernest Ndimbo na kulia ni Meneja wa Saccos ya Bunju Victoria Masika.
Meneja wa Oiko Credit Tanzania Deus Manyenye (Kulia) akimkabidhi Mwenyekiti msaidizi wa Saccos ya Vision Tuly Kyoma mfano wa hundi ya milioni 500/- walizotoa kama mkopo kwa taasisi hiyo ili zikatumike kusaidia kupunguza umasikini kwa jamii ya watu wa chini. Katikati ni Mjumbe wa bodi Ntully Huggins, katika hafla hiyo iliyofanyika leo Oiko Credit ilitoa mkopo wa bilioni 2.6/- kwa taasisi tano ziliwemo Mgandini, Bunju, Mtoni KKKT na Yosefo.

Oct 24, 2010

TIMOTHY ABEL MDINKA"ASALI YA ITIGI NDIYO BORA ZAIDI DUNIANI"

Mzee Abel Mdinka kulia akiwa ameongozana na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo Mijini. Kapteni John Chiligati wakati alipotembelea Shamba la Nyuki la MAUA lililopo kijiji cha Mwanzi Manyoni hivi karibuni kulia nyuma ni Timothy Abel Mdinka Mkurugenzi Mtendaji wa MAUA.
Katika pitapita yangu mkoani Singida nilikutana na Mkurugenzi wa Manyoni Asili Utilization Apiary (MAUA) Bw. Timothy Abel Mdinka ambaye anamiliki shamba kubwa la nyuki mkoani huo akishirikiana na baba yake mzee Abel Mdinka akanisimulia ni jinsi gani walifanya na kuamua kuanzisha shamba hilo kubwa.
Timoty alianza kwa kusema Manyoni Asili Utilization Apiary MAUA, ni Shamba la ufugaji nyuki ambalo lipo nje kidogo ya mji wa Manyoni, lina ukubwa wa ekari 216 ambayo inajumuisha banuai ya pekee duniani , banuai yenye uoto wa asili wa ITIGI THICKETS hupatikana sehemu mbili tu katika uso wa dunia nayo ni Manyoni na Zambia. Uoto huu wa asili unaotengeneza maua ya pekee unawezesha nyuki kupata asali yenye ubora wa hali ya juu na pekee kabisa duniani, mpaka sasa asali ya Itigi ndiyo asali bora zaidi kupita zote na ilipata ushindi wa kishindo katika maonyesho ya asali yaliyofanyika mwaka jana pale Mnazi mmoja.
Nia na madhumuni ya kuanzisha mradi huu ni 1)MAUA tunataka kutunza msitu huu wa pekee duniani 2)MAUA tunataka Kuwa mfano bora na wakuigwa na jamii inayotuzunguka katika utaunzaji wa mazingira na kufuga nyuki 3) MAUA tunataka kutumia maili asili ya pekee duniani tuliyopewa na Mungu katika kupunguza umasikini na kutunza mazingira .4) MAUA tunataka kufanya mradi wa kufuga nyuki uwe mradi mbadala wa kiuchumi ambao utasababisha watu waache kuuza mkaa na na wafuge nyuki ambayo ni sehemu ya kutunza mazingira. 5) MAUA tunataka kuitangaza Manyoni kitaifa na kimataifa ili tuweze kufungua soko la asali na bidhaa zake.
Mradi huu ulianza mwaka 2006 chini ya uongozi wa Mzee Abel Mdinka na Kijana wake Timothy Mdinka, uamuzi huu ulitokana na hali halisi ambayo mzee mdinka amakuwa akiiona ikiendelea kutokana na jinsi ambavyo misitu inakatwa kwa ajili ya maendeleo ya binadamu na kuanzisha mashamba pamoja na ufugaji mifugo usiozingatia utunzaji wa mazingira.
Safari ya kutembelea shamba hilo ilikuwa ni kubwa kwakuwa eneo la shamba ni kubwa sana kama unavyoona mizinga ya nyuki ikiwa imepangwa.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo Mijini. Kapteni John Chiligati akionyesha jinsi ya kutumia mizinga ya nyuki aliyoitoa kwa kikundi cha wanawake cha Upendo kwa ajili ya kufugia nyuki ili kuongeza uzalishaji wa asali na kuongeza kipato chao kiuchumi.
Hii ndiyo asali ambayo tayari imeshaandaliwa na Kampuni ya Manyoni Asili Utilization Apiary (MAUA) tayari kwa kuuzwa ndani na nje ya nchi.

Kikwete aiteka Karatu, Maelfu wafurika mkutano wake wa kampeni

Maelfu ya wananchi wa Jimbo la Karatu na vitongoji vyake wamefurika kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo jioni hii.

Mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa michezo Karatu mjini ulifurika wana CCM na wananchi waliokuwa na hamasa kubwa ya kumsikiliza Mheshimiwa Kikwete.

Umati huo kwa ujumla wake ulimueleza Mheshimiwa Kikwete kwamba wananchi wa Karatu wamechoshwa na sera za upinzani ambazo zimeshindwa kuleta maendeleo kwa miaka mingi.

Akiwauliza wananchi hao iwapo wako tayari kuipigia kura CCM na madiwani wake na mbunge, wananchi wao kwa ujumla wao wote walinyanyua mikono na kuonyesha ishara ya kuikubali CCM na kuwa wataipa kura zote.

Mkutano huo uliochangamka na uliokuwa na shamrashamra nyingi, ulihudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumai ambaye aliwasalimu wananchi na kuwaomba wachague CCm kwa maendeleo ya kweli.

Mkutano huu ni wa mwisho kwa siku ya leo ambapo Mheshimiwa Kikwete alianzia Kibaya na Matui Mkoani Manyara.

Baada ya Matui, msafara wa Mheshimiwa Kikwete ulielekea Olkesumet na Mang'ola, kabla ya kuingia hapa Karatu mkoani Arusha.

Oct 23, 2010

MWISHO MWAMPAMBA AKARIBISHWA NYUMBANI TANZANIA.

Mwisho Mwapamba akiwasili katika hafla hiyo huku akiwa ameongozana na baadhi ya wageni waalikwa akiingia kwenye Hoteli ya Continental jijini Dar es salaam ambapo hafla ya kumkaribisha mshiriki huyo wa Bigbrother Africa AllStars 2010 aliyerejea hivi karibuni kutoka Afrika Kusini alikokuwa akishiriki katika shindano hilo kwa miezi mitatu shindano hilo lililomalizika wiki iliyopita huku Mnigeria Uti akiibuka mshindi na kujinyakulia kitita cha Dola za Kimarekani laki mbili .
Ukiangalia picha hii watu wote wanaangalia upande mmoja, huu ulikuwa ni wakati wa kuwasili Mwisho Mwampamba katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na watu mbalimbali kwenye Hoteli ya Continental jijini Dar es salaam.
Wageni waalikwa mbalimbali wakipiga story huku wakipata kinywaji.
Vijana wa Joseph Kusaga kutoka Clouds Television kutoka kulia ni Katunda, Ray, Casto na Ezra nao walikuwepo katika kurekodi tukio zima la kmkaribisha Mwisho Mwampamba.
Mshindi wa BigBrother mwaka 2008 Richard akiwa na rafiki yake kushoto katika hafla hiyo.
Wadau kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakipozi kwa picha huku wakigonga bata zao katika hafla hiyo.
Wadau kutoka Multchoice Tanzania wakijimwaga katika hafla ya kumkaribisha Mwisho Mwampamba kwenye Hoteli ya Continentol jana usiku.

Oct 21, 2010

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete Ziarani Zanzibar

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na wanachama wa UWT Mkoa wa Mjini Magharibi (20-10-2010)wakai alipowasili na kuzungumza na wanachama wa UWT kwenye mkutano wa ndani wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu Okt.31 mwaka huu. Picha na Mwanakombo Jumaa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimnadi Mbunge wa jimbo la Makunduchi Samia Suluhu Hassan Mkoa wa Kusini Unguja (20-10-2010) wakati alipozungumza katika mikutano ya ndani ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu Oktoba 31 mwaka huu. Picha na Mwanakombo Jumaa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimnadi Mgombea Urais Dk.Jakaya Kikwete, Mgombea Urais wa Zanzaibar Dk. Ali Mohamed Sheni, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani katika Mkoa wa Mjini Magaharibi (20-1-2010 ) na kuwaombea kura katika Uchaguzi Mkuu ujao Okt.31, mwaka huu. (Picha na Mwanakombo Jumaa)
Wanawake wa Mkoa wa Mjini Magharibi. Unguja wakimshangiria Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati wa mkutano wa ndani wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu utakaofanyia Okt.31 mwaka huu. Picha na Mwanakombo Jumaa.

Oct 20, 2010

Wakenya walivyosherehekea kwa mara ya kwanza siku ya mashujaa

Rais Mwai Kibaki akiwasalimia wananchi wa Kenya waliojitokeza katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi kuhudhuria sherehe ya mashujaa. Kwa mara ya Kwanza wakenya wamesherehekea siku ya mashujaa waliopigania uhuru wa nchi hiyo. Miaka ya nyuma walikuwa wanasherehekea siku hiyo kumkumbuka rais wa kwanza wa Nchi hiyo hayati Jommo Kenyatta. (Picha na Anna Nkinda Nairobi)
Askari wa Jeshi la Kenya wakitoa salamu ya heshima kwa Rais Mwai Kibaki (hayupo pichani) wakati wa sherehe za mashujaa zilizofanyika leo katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi . Kwa mara ya Kwanza wakenya wamesherehekea siku ya mashujaa waliopigania uhuru wa nchi hiyo. Miaka ya nyuma walikuwa wanasherehekea siku hiyo kumkumbuka rais wa kwanza wa Nchi hiyo hayati Jommo Kenyatta.
Askari Polisi kikosi cha mbwa wakitoa salamu ya heshima kwa Rais Mwai Kibaki (hayupo pichani) wakati wa sherehe za mashujaa zilizofanyika leo katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi . Kwa mara ya Kwanza wakenya wamesherehekea siku ya mashujaa waliopigania uhuru wa nchi hiyo. Miaka ya nyuma walikuwa wanasherehekea siku hiyo kumkumbuka rais wa kwanza wa Nchi hiyo hayati Jommo Kenyatta.
Wapiganaji wa vita vya Maumau wakipita kwa heshima mbele ya Rais Mwai Kibaki (hayupo pichani) wakati wa sherehe za mashujaa zilizofanyika leo katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi . Kwa mara ya Kwanza wakenya wamesherehekea siku ya mashujaa waliopigania uhuru wa nchi hiyo. Miaka ya nyuma walikuwa wanasherehekea siku hiyo kumkumbuka rais wa kwanza wa Nchi hiyo hayati Jommo Kenyatta.
Wapiganaji wa vita vya Maumau wakipita kwa heshima mbele ya Rais Mwai Kibaki (hayupo pichani) wakati wa sherehe za mashujaa zilizofanyika leo katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi . Kwa mara ya Kwanza wakenya wamesherehekea siku ya mashujaa waliopigania uhuru wa nchi hiyo. Miaka ya nyuma walikuwa wanasherehekea siku hiyo kumkumbuka rais wa kwanza wa Nchi hiyo hayati Jommo Kenyatta.
Wanariadha wa Kenya ambao pia ni mashujaa walioshiriki michezo ya Jumuia ya Madola iliyomalizika hivi karibuni Nchini India na kuipatia nchi yao medali 32 ambazo 12 zilikuwa za dhahabu, 10 za Shaba na 10 za fedha wakipita kwa heshima mbele ya Rais Mwai Kibaki (hayupo pichani) wakati wa sherehe za mashujaa zilizofanyika leo katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi . Kwa mara ya Kwanza wakenya wamesherehekea siku ya mashujaa waliopigania uhuru wa nchi hiyo. Miaka ya nyuma walikuwa wanasherehekea siku hiyo kumkumbuka rais wa kwanza wa Nchi hiyo hayati Jommo Kenyatta.
Wananchi wa Kenya wakiwa wamejitokeza kwa wingi kuhudhuria siku ya mashujaa iliyofanyika leo katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi. Kwa mara ya Kwanza wakenya wamesherehekea siku ya mashujaa waliopigania uhuru wa nchi yao. Miaka ya nyuma walikuwa wanasherehekea siku hiyo kumkumbuka rais wa kwanza wa Nchi hiyo hayati Jommo Kenyatta.
(kwa msaada wa blog jirani)

MWISHO MWAMPAMBA AREJEA NA KUPOKELEWA NA BABA YAKE!

Mwisho Mwampamba akipokea shada la maua kutoka kwa ndugu zake mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere jioni ya leo akitokea Afrika kusini kwa ndege ya shirika la ndege la SAA ambako alishiriki shindano la BigBrother Africa na kushika nafasi ya tatu huku mshiriki Uti kutoka Nigeria akijinyakulia kitita cha Dola laki mbili za Kimarekani.
Mwisho kesho anatarajiwa kutembelea vyombo mbalimbali vya habari na kueleza mambo mbalimbali yaliyojiri kwa muda wote wa miezi mitatu walipokuwa kwenye jumba la Bigbrother na washiriki wenzake na keshokutwa atazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam katika picha kushoto ni baba yake mzee Mwampamba.
Mwisho Mwampamba akisindikizwa na ndugu zake pamoja na walinzi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere jioni ya leo akitokea nchini Afrika Kusini alikoshiriki katika shindano la BigBrother Africa Allstars na kushika nafasi ya tatu.
Mwisho mara baada ya kpokelewa akiwa katika usafiri aina ya Lemousine huku akiwa mwenye furaha.
Meneja Masoko wa Multchoice Furaha Samalu kulia akiwa katika pilika za mapokezi na Meneja Utawala wa Kampuni hiyo Tike Mwakitwange.
Mzee Mwampamba kulia ambaye ni baba yake na Mwisho akiwa na baadi ya watoto na ndugu na jamaa wakimsubiri Mwisho huku wakiwa wameshikilia maua.
Anna Kulia na Teddy kutoka Multchoice nao walijumuika katika mapokezi hayo.
Wafanyakazi wa kampuni ya Multchoice wakiwa kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere wakati walipokwenda kumpokea mshiriki wa shindano la Bigbrother All Stars 2010 lililomalizika jumapoili iliyopita huko Afrika Kusini.
(full shangwe)

SERIKALI YAIKEMEA TAMWA YAITAKA KUZINGATIA MASHARTI YA USAJILI!

Ismail Ngayonga na Magreth Kinabo

MAELEZO

Dar-Es-Salaam

SERIKALI imekitaka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kuzingatia masharti ya usajili waliopewa na malengo waliyojipangia pasipo kuingilia masuala ya kisiasa nchini, ikiwemo kuzingatia suala la utawala bora.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar-Es-Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Seth Kahumanda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamko (TAMWA) juu ya taarifa ya vyombo vya ulinzi na usalama lilivyotolewa hivi karibuni na Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania( JWTZ ) Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo, utafiti wa taasisi ya Synovate pamoja na REDET.

Kamuhanda alisema kuwa Serikali inashangazwa na Kauli ya Mkurugenzi wa TAMWA, Analilea Nkya kwa kuwa imekwenda kinyume na majukumu ya taasisi hiyo, ambayo ni pamoja na kusaidia waandishi wanawake kujiendeleza kitaaluma ili kushika hatamu ya uongozi katika vyombo vya habari, kubadilisha mfumo wa habari hasi za wanawake na kuwasaidia wanawake Watanzania kujiletea maendeleo.

Aliongeza kuwa TAMWA ni chama cha kitaaluma kama vilivyo vyama vingine, na iwapo kinahitaji kubadili malengo yake kuwa ya 0kisiasa basi hakina budi kuangalia mustakabali wa chama chao na mwelekeo wao na kufuata utaratibu kwa mujibu wa sheria .

“Matamko ya Mkurugenzi wa TAMWA yamevuka mipaka na kwenda nje ya malengo ya TAMWA. TAMWA inatakiwa kuheshimu masharti ya usajili wao na kuyatekeleza,” alisema Katibu Mkuu huyo huku akisisitiza kwamba chama hicho pia kinatakiwa kuheshimu masuala ya utawala bora uliopo nchini kwa kuwa suala la kuheshimu misingi ya utawala bora si la Serikali pekee.

Kwa mujibu wa Kamuhanda alisema kuwa chama hicho bado kinakabiliwa na changamoto mbalimbali za utekelezaji wa malengo yake ikiwemo kuwaendeleza waandishi wa habari wanawake kwa ajili ya kuwapatia ujuzi wa kutosha utakaowawezesha kushika nafasi za uongozi katika vyombo vya habari na sehemu nyinginezo za maeneo ya kazi.

Aidha Kamuhanda aliongeza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na chama hicho, katika malengo yao waliojiwekea.

Akizungumzia kuhusu mwenendo wa vyombo vya habari juu ya mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31,mwaka huu, Kahumanda alivishukuru baadhi ya vyombo vya habari na wahariri wake kwa kukemea matendo na kauli zinazoashiria kuhatarisha uvunjifu wa amani nchini.

“ Vyombo vya habari vinafanyakazi nzuri katika kuhabarisha wananchi juu ya mchakato wa Uchaguzi Mkuu baadhi yake vimepinga na kukemea waziwazi juu ya vitendo vinavyoashria uvunjifu wa amani kwa mfano kwa kuandika tahariri ninavipongeza kwa kuwa vimeonyesha ujasiri na ninaomba viendelee na msimamo huo kwa sababu amani ndio hazina kubwa ya nchi yetu,” alisisitiza Kamuhanda.

Awali akimkaribisha Katibu Mkuu ambaye alikuwa kwenye ziara ya kuitembelea Idara ya Habari(MAELEZO), Mkurugenzi wa Idara hiyo, Clement Mshana alisema ofisi zaidi zinahitajika kwa ajili ya kuhifadhi picha, machapisho mbalimbali na habari, hotuba za viongozi pamoja na vipindi mbalimbali ambavyo ni vya radio na televisheni ili viweze kutumika katika sehemu za baadae endapo janga la moto likitokea.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa idara hiyo inaratibu shughuli za tovuti ya wananchi ambapo mpaka sasa wananchi kadhaa wwaliokuwa na kero zao zimewezwa kutatuliwa na kupatiwa majibu kutoka mamlaka husika.

NGWE YA LALA SALAMA:KAMPENI ZA MNYIKA UBUNGO KATA YA SINZA MPAKA BAA!

Mgombea Ubunge jimbo la Ubungo kwa kupitia CHADEMA Ndugu John Mnyika akiwahutubia wakazi wa Sinza Palestina jijini Dar ves salaam katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika Jumapili iliyopita John Mnyika anagombea ubunge katika jimbo la Ubungo.
Mnyika akiwa katika gari kwenye msafara wake wakati alipopita katika mitaa mbalimbali ya Sinza na kusalimiana na wakazi wa Sinza.
Hapa akisalimiana na watu mbalimbali wakati alipokatiza katika moja ya baa zinazouza pombe huko Sinza.

MISS PROGRESS INTERNATIONAL KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA MAUAJI YA MAALBINO



Katibu Mtendaji wa BASATA Bw.Materego akisisitiza jambo kwenye Jukwaa la Sanaa ambapo alimpongeza Julieth kwa mpango wake wa kupambana na mauaji dhidi ya maalbino.
Mdau akichangia mada kwenye Jukwaa la Sanaa.Alimshauri Julieth kutokutumbukia kwenye skendo ambazo zimekuwa zikiwakumba baadhi ya warembo nchini.
Sehemu ya wadau wa Jukwaa la Sanaa wakimsikiliza Miss Progress International Julieth William (Hayuko pichani)

****************** ******************* *******************
Na Alistide Kwizela

Mshindi wa Shindano la Urembo la Progress International Julieth William amesema kwamba waandaaji wa shindano hilo lililofanyika nchini Italia hivi karibuni na kushirikisha warembo zaidi ya 50 kutoka mataifa mbalimbali wamemtengea kitita cha Euro 20,000 sawa na shilingi milioni 40 za kitanzania kwa ajili ya kupambana na mauaji dhidi ya walemavu wa ngozi (maalbino)

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa Jumatatu hii,Julieth alisema kwamba, fedha hizo amezipata kufuatia kuandika andiko la mradi (proposal) la jinsi ya kupambana na mauaji ya walemavu wa ngozi ambalo lilimpa asilimia 50 za ushindi kwenye shindano hilo.

Alisema kwamba, anasikitishwa na kuumizwa na mauaji dhidi ya binadamu wasio na hatia na kusisitiza kwamba,lazima watanzania wabadilike na kujua kwamba utajiri au mafanikio katika shughuli zao hayapatikani kutokana na viungo vya binadamu bali juhudi katika kazi na kujituma.

Alisema kwamba, mradi wake huo ambao atauendesha kwa kushirikiana na wanaharakati wengine utajikita kwenye maeneo ya kanda ya ziwa ambapo atakuwa akitoa elimu kwa umma,uhamasishaji wa jamii dhidi ya vitendo hivyo, kuunda Kamati ndogondogo chini ya walemavu wa ngozi zitakazokuwa zikifanya kazi ya kuielimisha jamii na mambo mengine mengi.

Aliongeza kwamba,ameshaanza mazungumzo na serikali ili kuona ni kwa jinsi gani atashirikiana nayo katika kufanikisha mradi huo ambao alisema kwa kuanzia utalenga maeneo yaliyoathirika zaidi ambayo ni ya Mikoa ya Mwanza na Shinyanga.

Kuhusu ushindi wake kwenye Shindano hilo la Miss Progress International ambapo aliwabwaga warembo zaidi ya 50 kutoka nchi mbalimbali, alisema ulitokana na yeye kutokukata tamaa,kujenga utamaduni wa kutafuta fursa na kuzitumia ipasavyo,kujituma na kujiamini.

Aliwaasa warembo kutokubweteka na kukata tamaa bali kujenga utamaduni wa kujiamini,kusaka fursa mpya na kuzitumia ipasavyo, kuwa mfano katika jamii kwa kuwa na maadili bora na zaidi kujihusisha na masuala mbalimabali ya kijamii.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alimpongeza Julieth William kwa ushindi wake zaidi wazo lake la kushirikiki vita dhidi ya mauaji ya walemavu wa ngozi na kumueleza kwamba BASATA iko pamoja naye kwani ni mlezi wake.

Alisema kwamba, warembo hawana budi kujifunza kutoka kwenye mafanikio ya Julieth kwani kwa muda mrefu Tanzania pamoja na kupeleka warembo kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa wamekuwa hawafanyi vizuri sana ingawa alisema wamekuwa wakiitangaza nchi kwa kiwango kikubwa.

Wachangiaji wengi kwenye Jukwaa la Sanaa walimpongeza Julieth na kumtakia kila la kheri kwenye mradi wake huo ingawa pia hawakusita kumuonya dhidi ya tabia zisizofaa ambazo zimekuwa zikioneshwa na warembo mara wanapopata mafanikio.

Swahili Fashion Week yazinduliwa rasmi leo



Mbunifu wa Mavazi na Muandaaji wa onyesho la mavazi la Swahili Fashion Week,Mustafa Hassanali akifafanua jambo mbele ya wandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na tamasha hilo katika mkutano na wanahabari hao uliofanyika leo katika hoteli ya Southen Sun jijini Dar.


Muwakilishi wa Hoteli ya Southen Sun,Bi. Judith Muyo akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu onyesho la mavazi la Swahili Fashion Week,wengini ni Mustafa Hassanali (katikati),Mratibu wa Mitindo,Bw. Washington (kulia),Afisa habari wa Mustafa Hassanali,Saphia Ngalapi (pili kushoto) na mwisho kabisa ni Alex Galinoma kutoka EATV.


Kwa mara ya tatu sasa Swahili Fashion Week itafanyika Karimjee Hall kuanzi tarehe 4 hadi 6 November 2010, Dar Es Salaam , Tanzania .


Swahili Fashion Week itawaleta pamoja wabunifu wa mavazi 24 kutoka nchi zinazoongea lugha ya Kiswahili ili kuweza kuonyesha ubunifu wao katika kubuni mavazi ya aina mbalimbali kwa kutumia aina mbalimbali za malighafi.


Wabunifu watakaoonesha mavazi katika Swahili Fashion Week kwa mwaka huu ni pamoja na Ailinda Sawe, Manju Msita, Kemi Kalikawe, Christine Mhando, Shellina Ibrahim, Farha Naaz Sultan, Gabriel Mollel, Robi Morro, Asia Idarous, Zamda George, Khadija Mwanamboka, Jamilla Vera Swai and Made by Afrika. wabunifu kutoka Kenya ni Sonu Sharma, Moo Cow, KiKoromeo, John Kavike na Kooroo, na kutoka Uganda ni mbunifu Stella Atal.


“Pamoja na maonyesho ya mavazi, mwaka huu Swahili Fashion Week itakwenda sambamba na tamasha la maonyesho ya bidhaa mbalimbali zenye asili ya mswahili kutoka mwambao wa Afrika mashariki”. Alisema Mustafa Hassanali muaandaaji y tukio la Swahili Fashion Week.


“Tunafungua milango zaidi kwa ajili ya watazamaji wapya wa Swahili Fashion Week, amboa watapata fursa ya kununua bidhaa mbalimbali. Tamasha hili ambalo linazileta pamoja bidhaa mbalimbali za sanaa na utamaduni wa mswahili, pia litahamasisha ubunifu zaidi katika bidhaa zinazokwenda sambamba na maisha halisi ya jamii ya watu wanaoongea lugha ya Kiswahili kwa kukutana pamoja na kubadilisha mawazo na kujifunza uzoefu mpya katika masuala yanayohusiana na sanaa kwa ujumla.” Aliaongeza Hassanali.


Pamoja na maonyesho, pia kutakuwepo aina tofauti za burudani kutoka kwa vikundi


Mbalimbali vya muziki, uchoraji wa hina, usukaji mikeka, sambamba na semina za aina tofauti zitakazo washirikisha wabunifu wa mavazi.


Aidha Swahili fashion Week imeandaa aina tofauti za zawadi zitakazotolewa mwaka huu kwa lengo la kutambua na kuthamini vipaji vya aina mbalimbali vitakavyooneshwa, ikiwa ni pamoja na zawadi ya mwaka kwa mbunifu anaechipukia.


Swahili fashion week 2010 imedhaminiwa na Home of Swahili Fashion week Southern Sun, Origin Africa, USAID Compete, EATV, East Africa Radio, Malaria Haikubaliki, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) Ultimate Security, Monier 2000, Colour Print ltd, Global Outdoor Ltd, Amarula, Vayle Springs Ltd, ZG Films, Darling Hair, Danish make up designs, Nipashe, Bilicanas, Perfect Machinery LTD, 1 & 1 internet solutions, Sengi Tours, Ifashion na 361 Degrees.

Oct 19, 2010

YOU ARE RESPONSIBLE FOR YOUR OWN LIFE "PIPI"

She loves life...nobody made the happiness she has,she is responsible for her own life.
The fact that she turned 18 this year....made her feel excited because it would be her first time to vote!!and now she is getting more and more excited about that day, the 31st of October.....

PLEASE TUMIA KURA YAKO PIA TAREHE 31 MWEZI WA KUMI, SIO UKAE UNALALAMIKIA SERIKALI.....

KIDUM, NONINI AND MATONYA LIVE@CLUB VOLTS LONDON FRI 22ND OCT

JUNGLE DREAM / BONGO UK PRESENTS
EAST AFRICAN ARTISTS WITH SWAGGAEST AND FINEST ARTISTS FROM EAST AFRICA..

FEATURING: KIDUM, NONINI, MATONYA

PERFORMANCES FROM UGANDAN UK BASED ARTISTS....ITS KENYA, UGANDA, TANZANIA, BURUNDI, RWANDA....
ON FRIDAY 22 OCTOBER
AT CLUB VOLTS
169-171 FORE STREET EDMONTON, LONDON, N18 2XB

FRO MROE INFO:
07944456643 ED K EDRIS
07533512670 VICTOR

MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE HONORED IN WASHINGTON DC.

The 3rd Annual Celebration in Remembrance of the Life and Work of The Father of the Tanzanian Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere was held at the Howard University Towers Auditorium on October 16th 2010.
This event is hosted annually by the Julius K. Nyerere Commemoration, Inc. of Washington DC. JKNC, Inc. is founded and largely sponsored by an African American couple; Ndugu and Mrs. Rick Tingling-Clemmons, whose love for Mwalimu and admiration for his works and philosophy inspired them to organize this worthy event in his name. The theme this year is in concurrence with Mwalimu's core values… "Fighting Poverty, Ignorance and Disease".
Rick and Mama Michele Tingling
H. E., Ambassador Mwanaidi Maajar - third from right; with the event organizers, together with Mr. Suleiman Saleh; Minister Plenipotentiary Political affairs, Tanzania Embassy - second from left, Ms. Khadija Mwanamboka of Tanzania Mitindo House - 3rd from left and Ms. Belinda Mlingo the Mistress of ceremony and JKNC Inc. partner - second from right.

DR. GHALIB BILAL KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI KILIMANJARO.

Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, DK. Mohamed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Kata za Bomambuzi na Pasua wakati alipofanya mkutano wa kampeni katika Wilaya ya Moshi mjini Mkoa wa Kilimanjaro jana okt 17. Picha na Muhidin Sufiani
-Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombhea ubunge wa Jimbo la Moshi Vijijini, Cyril Chami, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyiika leo Okt 18 kwenye uwanja wa Kijiji cha Chekereni Mkoa wa Kilimanjaro. Pichha na Muhidin Sufiani
Mmoja wa wanachama wa chama cha mapinduzi akishangilia huku wenzake wakimuangalia wakati wa mkutano wa Kampeni wa Dr. Ghalib Bilal.
Wanachama na mashabiki wa CCM wa Mtaa wa Sokoni Kata ya Bomambuzi na Pasua, wakimsikiliza mgombea Mwenza wa urais wa CCM. Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipofanya mkutano wa kampeni jana Okt 17 katika uwanja wa Sokoni Pasua Wilaya ya Moshi Mjini Mkoa wa Kilimanjaro na kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo hilo, Justine Salakana. Picha na Muhidin Sufiani

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA