Oct 24, 2010

TIMOTHY ABEL MDINKA"ASALI YA ITIGI NDIYO BORA ZAIDI DUNIANI"

Mzee Abel Mdinka kulia akiwa ameongozana na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo Mijini. Kapteni John Chiligati wakati alipotembelea Shamba la Nyuki la MAUA lililopo kijiji cha Mwanzi Manyoni hivi karibuni kulia nyuma ni Timothy Abel Mdinka Mkurugenzi Mtendaji wa MAUA.
Katika pitapita yangu mkoani Singida nilikutana na Mkurugenzi wa Manyoni Asili Utilization Apiary (MAUA) Bw. Timothy Abel Mdinka ambaye anamiliki shamba kubwa la nyuki mkoani huo akishirikiana na baba yake mzee Abel Mdinka akanisimulia ni jinsi gani walifanya na kuamua kuanzisha shamba hilo kubwa.
Timoty alianza kwa kusema Manyoni Asili Utilization Apiary MAUA, ni Shamba la ufugaji nyuki ambalo lipo nje kidogo ya mji wa Manyoni, lina ukubwa wa ekari 216 ambayo inajumuisha banuai ya pekee duniani , banuai yenye uoto wa asili wa ITIGI THICKETS hupatikana sehemu mbili tu katika uso wa dunia nayo ni Manyoni na Zambia. Uoto huu wa asili unaotengeneza maua ya pekee unawezesha nyuki kupata asali yenye ubora wa hali ya juu na pekee kabisa duniani, mpaka sasa asali ya Itigi ndiyo asali bora zaidi kupita zote na ilipata ushindi wa kishindo katika maonyesho ya asali yaliyofanyika mwaka jana pale Mnazi mmoja.
Nia na madhumuni ya kuanzisha mradi huu ni 1)MAUA tunataka kutunza msitu huu wa pekee duniani 2)MAUA tunataka Kuwa mfano bora na wakuigwa na jamii inayotuzunguka katika utaunzaji wa mazingira na kufuga nyuki 3) MAUA tunataka kutumia maili asili ya pekee duniani tuliyopewa na Mungu katika kupunguza umasikini na kutunza mazingira .4) MAUA tunataka kufanya mradi wa kufuga nyuki uwe mradi mbadala wa kiuchumi ambao utasababisha watu waache kuuza mkaa na na wafuge nyuki ambayo ni sehemu ya kutunza mazingira. 5) MAUA tunataka kuitangaza Manyoni kitaifa na kimataifa ili tuweze kufungua soko la asali na bidhaa zake.
Mradi huu ulianza mwaka 2006 chini ya uongozi wa Mzee Abel Mdinka na Kijana wake Timothy Mdinka, uamuzi huu ulitokana na hali halisi ambayo mzee mdinka amakuwa akiiona ikiendelea kutokana na jinsi ambavyo misitu inakatwa kwa ajili ya maendeleo ya binadamu na kuanzisha mashamba pamoja na ufugaji mifugo usiozingatia utunzaji wa mazingira.
Safari ya kutembelea shamba hilo ilikuwa ni kubwa kwakuwa eneo la shamba ni kubwa sana kama unavyoona mizinga ya nyuki ikiwa imepangwa.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo Mijini. Kapteni John Chiligati akionyesha jinsi ya kutumia mizinga ya nyuki aliyoitoa kwa kikundi cha wanawake cha Upendo kwa ajili ya kufugia nyuki ili kuongeza uzalishaji wa asali na kuongeza kipato chao kiuchumi.
Hii ndiyo asali ambayo tayari imeshaandaliwa na Kampuni ya Manyoni Asili Utilization Apiary (MAUA) tayari kwa kuuzwa ndani na nje ya nchi.

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA