Oct 13, 2010

ZIARA YA MAMA SALMA KIKWETE,MEATU,BARIADI NA MASWA MKOANI SHINYANGA.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwanadi wagombea wa CCM jimbo la Bairadi Magharibi Andrew Chenge (kushoto) na Mgombea Bariadi Mashariki Martine Makondo wakati alipofanya ziara na kuongea na wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika kuwahamasisha na kuwaelezea juu ya umuhimu wa kupiga kura ili wajitokeze kwa wingi katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu nchini kote (Picha zote na Mwanakombo Jumaa wa Maelezo Dar es salaam)
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanachama wa UWT jimbo la Maswa mkoani Shinyanga pamoja na kuwaombea kura za Rais , Wabunge na Madiwani wa CCM ili waweze kupata kura kwa wingi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 31 mwaka huu.
Nimevutiwa na uzalendo wa mwanafunzi huyu wa shule ya msingi jimbo la Meatu ambaye sikuweza kumpata jina lake,kwani nilikuwa katika msafara ila jicho lilivutiwa naye jinsi alivyopata hamasa na kuvaa kichwani mwake.kama anvyoonekana akitoka shuleni.
Wanachama wa UWT Jimbo la Maswa na Kisesa wakimsikiliza Mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika mkutano wa ndani wa kampeni na kuwanadi wagombea wa CCM ili waweze kushinda wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu ujao Oktoba 31 mwaka huu. Picha zote na Mwanakombo Jumaa.
Wanachama wa UWT jimbo la Bariadi Mashariki na Magharibi wakimshangiria Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) alipokutana nao kwenye mkutano wa ndani kuhusu umuhimu wa kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 31 mwaka huu.

TAARIFA YA LADY JAYDEE KWA VYOMBO VYA HABARI , KUHUSIANA NA UBALOZI WA WANAWAKE WENYE UGONJWA WA FISTULA KWA KUSHIRIKIANA NA HOSPITALI YA CCBRT

Asubuhi ya leo katika mkutano na waandishi wa habari, CCBRT walitangaza kushirikiana na Lady JayDee na Watanzania wengine wote pande mbali mbali za nchi wanaofahamu wagonjwa wa Fistula au hata wagonjwa wenyewe kujitokeza ili kusaidiwa kutatua tatizo hilo.

Meza kuu ni CEO wa CCBRT Bw.Erwin Telemans, Lady JayDee pamoja na Mkurugenzi wa Programs za jamii Bi.Brenda Msangi

HABARINI ZA JIONI NA ASANTENI SANA KWA VYOMBO VYA HABARI KUITIKIA WITO HUU

KAMA MWANAMUZIKI WA TANZANIA, NASHUKURU KUWA JAMII YA WATANZANIA WENZANGU WANAPOKEA VIZURI KAZI YANGU YA SANAA YA MUZIKI.

KWA JINSI HIYO BASI……, NA MIMI NINALO JUKUMU LA KURUDI KWA JAMII YANGU NA KUSHIRIKIANA NAO KATIKA HARAKATI ZA KUJIKWAMUA KUTOKA KATIKA MATATIZO MBALIMBALI KAMA VILE MAGONJWA NA UMASIKINI.

NINAYO FURAHA KUWAFAHAMISHA KUWA, MIMI KAMA MSANII NINAE ANGALIWA NA KUSIKILIZWA NA JAMII YA WATU WENGI PANDE MBALI MBALI ZA TANZANIA.

LEO HII NIMEUNGANA NA HOSPITALI YA CCBRT KUWA SHUJAA WA WANAWAKE WANAOSUMBULIWA NA FISTULA.

UAMUZI HUU UMEKUJA BAADA YA CCBRT KUNIALIKA KUTEMBELEA WODI MBALIMBALI ZA WAGONJWA ZILIZOPO HOPITALINI HAPA.

LAKINI BINAFSI NILIGUSWA ZAIDI NA WANAWAKE WANAOSUMBULIWA NA UGONJWA WA FISTULA, UKIZINGATIA PIA MIMI NI MWANAMKE NIKAKUBALI KUUNGANA NA CCBRT ILI KUSAIDIA KWA HALI NA MALI KUOKOA MAISHA YA WANAWAKE WALIO WENGI..

TANGU NIZALIWE MPAKA NAKUWA MKUBWA NA KUFIKIA HATUA NILIOPO HIVI SASA, NAKIRI SIKUWAHI KUSIKIA WALA KUONA MGONJWA WA FISTULA. MPAKA NILIPOTEMBELEA HOSPITALI YA CCBRT

NIMESIKITISHWA ZAIDI BAADA YA KUELEZWA KUWA WANAWAKE WENGI WENYE UGONJWA HUU HUSHINDWA KUFANYA KAZI WAKATI MWINGINE HATA KUTENGWA AU KUJITENGA NA JAMII ZAO WANAMOISHI KUTOKANA NA KUWA WANAVUJA HAJA NDOGO AU HAJA KUBWA KILA MARA BILA WAO WENYEWE KUPENDA WALA KUJIJUA. KWAKUWA WANAKUWA WANASHINDWA KUJIZUIA.

HIVYO KUPELEKEA WANAWAKE HAO WENYE FISTULA KUENDELEA KUISHI MAISHA DUNI YA UPWEKE NA KUENDELEA KUWA MASKINI

LABDA NIONGELEE KWA KIFUPI KUHUSIANA NA FISTULA.

NI UGONJWA UNAOWAPATA WASICHANA NA WANAWAKE WAKATI WA KUJIFUNGUA NA HII HUTOKANA NA KUSHINDWA KUFIKA VITUO VYA AFYA VYENYE HUDUMA YA UZAZI.

FISTULA NI UGONJWA UNAOZUILIKA NA UNATIBIKA.

HAKUNA MWANAMKE ANAETAKIWA KUISHI NA FISTULA HASA UKIZINGATIA CCBRT INATOA MATIBABU, USAIFIRI, CHAKULA NA MALAZI BURE KWA WAGONJWA WOTE WANAOSUMBULIWA NA FISTULA.

JUKUMU LANGU KUBWA KATIKA UBALOZI HUU NI KUSIMAMA NA KUTUMIA SAUTI YANGU, NA NAFASI NILIONAYO KATIKA JAMII KAMA MWANAMUZIKI KUTOA WITO KWA WAGONJWA WENYE FISTULA NA HATA WALE WANAJAMII WENGINE WOTE WANAOFAHAMU WAGONJWA HAO, WAJE CCBRT KUPATA MATIBABU NA HUDUMA ZOTE BURE.

NITAFANYA HAYO POPOTE NITAKAPOPATA NAFASI YA KUONGEA NA JAMII INAYONIZUNGUKA, AMA IWE KATIKA MAONYESHO YANGU AU MAHOJIANO NA VYOMBO VYA HABARI.

NITAFANYA HIVYO PIA KATIKA MITANDAO YA KIJAMIII, NINAYOHUSIKA NAYO KAMA BLOGS NA FACEBOOK NA HATA KATIKA MATANGAZO YA TV, RADIO NA VIPEPERUSHI.

ILIMRADI TU UJUMBE UWAFIKIE WANAWAKE WENYE FISTULA WAJE KUTIBIWA BURE CCBRT.

NDUGU ZANGU WAANDISHI WA HABARI, NAOMBA MJIUNGE NAMI KUWA SHUJAA WA WANAWAKE WENYE FISTULA


ASANTENI SANA
LADY JAYDEE a.k.a KOMANDOO

VODACOM MWANZA CYCLE CHALLENGE KUTIMUA VUMBI MWEZI UJAO MKOANI MWANZA!!

Meneja Udhamini wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa akionyesha nembo ya Mashindano ya baiskeli ya Vodacom Mwanza Cycle Challenge yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Mwanza Mwezi ujao wanaoshuhdia katikati ni Mkuu wa Udhamini Vodacom Tanzania George Rwehumbiza na kulia ni Nazir Manji Mwenyekiti wa Chama cha Baiskeli CHABATA.
Mkuu wa Udhamini Vodacom Tanzania Bw. George Rwehumbiza akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati alipotangaza rasmi kufanyika kwa mashindano ya Baiskeli yanayojulikana kama Vodacom Mwanza Cycle Challenge yanayotarajiwa kufanyika tarehe 12 na 13 mwezi ujao mkoani Mwanza. Akielezea zaidi George Rwehumbiza amesema mashindano hayo yatakuwa katika mbio za kilomita 196 kwa wanaume, kilomita 80 kwa wanawake na mbio mbio hizo pia zitawahusisha walemavu ambapo zitafanyika mbio za kilomita 15 kwa walemavu wanaume na kilomita 10 kwa walemavi wanawake. Ameongeza kuwa zawadi zimeboreshwa zaidi kwa mwaka huu na zitatangazwa hapo baadae mara baada ya mambo yote kukamilika. Amefafanua kwa mba mashindano ya Vodacom Mwanza Cycle Challenge yanaandaliwa na kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania kwa miaka 5 sasa na kwa mwaka huu yanadhaminiwa pia na kampuni za Alphatel, TBL, Knight Support na SBC. Vodacom Tanzania imekuwa ikidhamini michezo mbalimbali kama vile Soka, Riadha, Kuogelea, Mashindano ya Boti, Mashindano ya Mbuzi, Vodacom Miss Tanzania, Tenisi michezo mingine mini, mwingine aliyepo kwenye picha ni Rukia Mtingwa Meneja Udhamini Vodacom Tanzania.

Oct 12, 2010

KATIBU MKUU SAYANSI NA TEKNOLOJIA AZINDUA HUDUMA YA MALIPO YA KABLA YA (TIGO PRE PAID BLACKBERRY)

Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Dr. Patrick James Makungu amezindua huduma mpya ya Tigo Pre Paid Blackberry leo kwenye uzinduzi uliofanyika kwenye hotelia ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam.
Akisoma hotuba yake katibu mkuu huyo amesema"Ninayo furaha kubwa kuwa nanyi mchana huu wa leo ambapo Tigo mnazindua huduma yenu kabambe ya malipo ya kabla ya mtandao wa intanet ya backberry kupitia mtandao wa Tigo – Tigo Pre paid blackberry Kwa niaba ya serikali kupitia wizara mawasiliano sayansi na teknolojia kwanza niwapongeze kwa hatua hii nzuri mliofikia ya kuamua kuleta huduma hii ya blackberry malipo ya kabla ambayo kama mlivyosema mmeitikia ombi toka kwa wateja mnaowahudumia Pili ninawapongeza kwa kuweka vifurushi vya viwango vya chini zaidi na nafuu kuliko mtandao wowote nchini katika huduma hii ya backberry malipo ya kabla
Zuri zaidio ni kwamba nyie mmeweka kiwango cha chini kabisa cha kulipia shilingi elfu saba tu kwa siku saba na mteja akafurahia huduma ya intaneti! Hongereni kwa hilo Hayo yote ni mafanikio na ndio maana hata mlitunukiwa ubora wa huduma za mawasiliano nchini na wataalamu wanaofanya utafiti kwenye zaidi ya nchi 80 “Su

BAYPORT YAKARABATI SHULE KIGOMA KWA SHILINGI MILIONI 20

Bayport Financial Services imetumia shilingi milioni 20 kukarabati shule ya msingi Airport Mkoani kigoma. Akizungumza Bw Ngula Cheyo Meneja Masoko na Mahusuiano ya Jamii katika ofisi zao Mako Makuu jijini Dar es Salaam, alisema tarehe 8 Oktoba 2010, Bayport ilifanya sherehe ya uzinduzi katika shule ya Msingi Airport Kigoma kuzinduza rasmi Shule hiyo.

Aliongeza kwakusema , kila mwaka chini ya Huduma ya Jamii kupitia mradi wa “Bayport Change a Life”, Bayport hutoa msaada chini ya huduma hii wa zaidi ya shilingi milioni 50 kwa jamii nchi nzima. Misaada hii imetolewa kwa waathirika wa majanga, watoto yatima, mipango ya vijiji kama vile uchimbaji wa visima vya maji safi na salama, na kuimarisha jamii kielimu kwa kutoa udhamini kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu au ukarabati wa shule kama Shule ya Msingi Airport Kigoma.

Ngula Cheyo alisema kampuni hii imetoa shilingi milioni 20 kwa ajili ya ukarabati wa shule, ambayo ni mchango mkubwa wa Huduma za Kijamii kufanywa na taasisi yoyote za kifedha au kampuni yoyote binafsi katika shule moja Nchini Tanzania. Alieleza kuwa ukarabati huu ulikuwa wa ujenzi kamili wa ofisi mbili mpya za Utawala, ambayo moja kwa ajili ya Mwalimu Mkuu na nyingine ikiwa ofisi ya Waalimu, pia utengenezaji wa madawati 160, ambayo ni madawati 40 kwa kila darasa kuanzia darasa la kwanza mpaka la nne na ukarabati wa sakafu zote nje na ndani na upigaji rangi wa shule nzima.

Wakuu wa idara kutoka Bayport Makao Makuu waliohudhuria sherehe hii ni Dk Ken Kwaku Mwenyekiti wa bodi wa kampuni, Ibrahim Kaduma Mkurugenzi wa bodi, Etienne Coetzer Afisa Mtendaji Mkuu, John Mbaga Afisa Mkuu wa Uendeshaji, na Ngula Cheyo Meneja Masoko na Mahusuiano ya Jamii. Bw. Ibrahim Kaduma aliongea kwa niaba ya kampuni katika sherehe hiyo

.

Ngula Cheyo alisema shule hiyo ilitakiwa kuzinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa Kigoma Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia ambaye alikuwa ndio mgeni rasmi, lakini kutokana na shughuli za kimkoa ilishindikana kuhudhuria kwake katika uzinduzi huo na kuwakilishwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. John Mongela.

Wakuu wa Idara kutoka Bayport baadaye walialikwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ili kupewa shukrani za kipekee kutoka kwa Mkuu wa Mkoa kwa mchango wa shilingi milioni 20 ya ukarabati wa Shule ya Msingi Airport Kigoma.

Bw. Cheyo alisema, Bw. Ibrahim Kaduma ambaye aliongea kwa niaba ya kampuni alisema ahadi yetu kwa Tanzania imeonyeshwa hapa leo, huu mchango wa shilingi milioni 20 kwa ajili ya elimu ni ukweli usio na pingamizi kwamba Bayport ni kampuni imara na ipo hapa kubaki.

Katika miezi ijayo Bayport itafungua tawi jipya wilayani Kasulu katika Mkoa wa Kigoma. Bayport Tanzania imekua katika shughuli hii ya utoaji mikopo nchini kwa zaidi ya miaka minne na nusu. Kampuni inaendelea kukua zaidi Vijijini na Mijini na sasa tuna matawi 40 katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Kampuni inaamini kuwa na matawi karibu na makazi ya wateja wetu na wao kupata huduma toka kwa mwakilishi wa Bayport ambaye ni mwanajumuiya na si tuu mteja kuweza kupata mtaji kwa haraka bali inamhakikishia faraja na imani kwamba kampuni yetu iko tayari kusikiliza mahitaji ya mteja hata kwa lugha asilia ikibidi, Alisema Bw. Cheyo

Taasisi ya Kifedha ya Bayport ni kikundi cha Pan-Afrika inayojihusisha na utoaji wa mikopo ambayo haina dhamana au amana kwa wafanyakazi walioajiriwa, ambao kulingana na kipato chao Benki za kibiashara hushindwa kuwapatia mitaji. Taasisi ya Bayport imeanzishwa mwaka 2002, na Makao yake makuu yako Mauritius.

Mafanikio ya shughuli zake za utoaji mikopo zimepanua wigo katika nchi sita, kutoka Ghana katika nchi za Afrika Magharibi, Uganda na Tanzania katika nchi za Afrika Mashariki, kupitia Zambia, Botswana hadi Afrika Kusini. Kundi la Bayport limetoa huduma kwa zaidi ya wateja 300,000 kupitia matawi yake 235 na zaidi ya wafanyakazi 2,500.

SERIKALI YASEMA NYIMBO ZA TAIFA KUIMBWA NA BRASS BAND.

NA MAGRETH KINABO- MAELEZO

SERIKALI imeiagiza Shirikisho ya Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) kuhakikisha kuwa kuanzia sasa kila mchezo wa kimataifa unaofanyika hapa nchini ambao masharti yake ni kuimbwa nyimbo za Taifa kuwa zitaimbwa kwa ‘Brass ban d’ kama ilivyokuwa inafanyika katika miaka ya nyuma.

Kauli hiyo ilitolewa jana (leo) na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Kapteni Mstaafu George Mkuchika katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Seth Kamuhanda wakati akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu tukio la kutoimbwa nyimbo za taifa za Morocco na Tanzania kabla ya mchezo wa kimataifa baina ya nchi hizo mbili uliofanyika Oktoba 9,mwaka huu kuanza.

Aliongeza kuwa hali hiyo ilisababisha adha kubwa kwa Rais Jakaya Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi, washabiki, wapenzi wa soka, wageni na umma wa Tanzania kwa ujumla.

“Waziri ameielekeza TFF kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kufanya uzembe na kulitia aibu kubwa taifa letu,” alisema Kamuhanda.

Aidha Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa uamuzi huo unalenga kuhakikisha kwamba aibu iliyotokea wakati wa mchezo huo, kuwa tukio la kutoimbwa kwa nyimbo za taifa halitokei tena

.

Akizungumzia kuhusu mitambo ya kuc hezesha CD iliyopo kwenye Uwa nja wa Taifa, Katibu Mkuu huyo alisema ni mizuri, safi na ni ya kisasa hivyo haina tatizo na watu wa kuiendesha wapo.

Katibu Mkuu huyo, Kamuhanda alisema jukumu la kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo ni la TFF wenyewe, hivyo wizara inaweza kushirikishwa kwa kutoa maelekezo na kuongeza kuwa wizara ndiyo imeelekezaTFF kufanya uchunguzi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Michezo, Leonard Thadeo, alisema wenye ujukumu la kufanya maandalizi ya kutosha kuhusu kupatikana kwa CD au kanda za nyimbo za taifa za timu husika ni TFF kama endapo timu inayokuja nyimbo yake haipo basi TFF huwasiliana nayo ilikuipata nyimbo hiyo.

Wasanii wa Kiume wadhalilishaji wa wenzao wa Kike

Wasanii wa kiume hususan wa muziki wa dansi ikiwa ni pamoja na wapenzi wa muziki huo wametajwa kuwa chanzo cha kuwadhalilisha wasanii wa kike hali ambayo imekuwa ikisababisha waonekane chini pia wasio na maadili ndani ya jamii. Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa Jumatatu hii,Muimbaji mahili wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’,Luiza Mbutu alisema kwamba hali imekuwa mbaya kiasi kwamba wasanii wa kike hususan wanenguaji wamejikuta wakifanya mambo kinyume cha maadili ili kukidhi matakwa ya wasanii wa kiume na baadhi ya wapenzi wa muziki wa dansi. Akitoa mfano wa udhalilishaji huo, Luiza Mbutu alizungumzia tabia chafu ya (wapenzi wa muziki wa dansi) ‘mapedeshee’ kuwatuza fedha wanenguaji wa kike wawapo kwenye maonyesho kwa kuwawekea fedha kwenye matiti yao au makalio hali ambayo imekuwa ni ya kidhalilishaji kwa kiwango cha juu. “Wanenguaji wa kiume wamekuwa wakituzwa fedha kwa kupewa mikononi au mifukoni lakini wale wa kike wamekuwa wakiwekewa kwenye matiti na makalio kitu ambacho kimekuwa ni cha kiudhalilishaji sana” alilalamika Luiza Mbutu. Alitaja pia tabia ya wanamuziki wa kiume kwenye bendi kuponda mawazo ya wanamuziki wa kike hasa pale wanapokuwa na wazo la kutunga nyimbo hali ambayo imekuwa ikisababisha wao (wanaume) wawe wakipitisha nyimbo zao tu na kuwaacha wanawake nyuma kwenye suala la utunzi wa nyimbo. Aidha, alilalamikia baadhi ya wazazi ambao wamekuwa wakiwakataza watoto wao wa kike kushiriki kwenye shughuli za sanaa hivyo kuwafanya wawe wakitoroka usiku wa manane hivyo kushindwa kurudi majumbani baada ya kuomba hifadhi kwa wanaume hivyo kuishia kupata mimba zisizo tarajiwa na watoto wa mtaani. Kuhusu hili la kuwadhalilisha wasanii wa kike, wachangiaji wengi kwenye jukwaa walisema kwamba, rushwa za ngono zimekuwa zikisikika sana miongoni mwa wasanii wa kike na mara nyingi kimekuwa ni kikwazo kwao kupata mafanikio ya kisanaa.Walisema kwamba, kila wanapohojiwa wasanii wa kike lazima walalamikie rushwa za ngono wanazoombwa na wasanii waliokwishapata majina au wakuzaji sanaa (mapromota).

Oct 11, 2010

MWENYEKITI TUME YA UCHAGUZI (NEC) AWATAKA VIONGOZI WA VYAMA KUHAMASISHA AMANI KATIKA UCHAGUZI MKUU!!

Na Bakari Kimwanga TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imevitaka vyama vya siasa nchini kuzingatia Amani na Utulivu katika kipindi chote cha kuelekea uchaguzi Mkuu Octoba 31, mwaka huu. Hayo yamesemwa leo katika ufunguzi wa mkutano baina ya vyama vya siasa na NEC na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Lewis Makame,uliofanyika Paradise Hoteli Jijini Dar es Salaam na kuwataka viongozi hao kutambua wajibu wao wa kuelekea uchaguzi mkuu. Aidha alisema umefika wakati kwa viongozi wa vyama vya siasa kuhamasisha wananchi kupitia mikutano ya kampeni umuhimu wa amani na kuhakikisha wanaweka mawakala katika vituo vya uchaguzi ili kuepuka malalamiko. "Sasa umefika wakati kwa vyama vya siasa kutambua wajibu wao ni vema mkahubiri amani na utulivu na kuhakikisha mnaweka mawakala mnaowaamini katika vituo vya kupigia kura, tunajua tunachangamoto ya kupokea malalamiko toka kwa vyama vya siasa kuhusu mwenendo wa uchaguzi na tunayashughulikia kwa wakati" alisema Jaji Makame. Hata hivyo Jaji Makame, alisema hivi sasa NEC, imeshafanya maandalizi ya kutosha na kusambaza vifaa vya uchaguzi katika majimbop yote nchini.
Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Lewis Makame, Mjumbe wa tume Omar Makungu Makamu Mwenyekiti, Prof. Amon Chalila Mjumbe na Mary Longway Mjumbe.
Wawakilishi wa vyama vya siasa wakiwa katika majadiliano hayo.
Baadhi wa wawakilishi wa vyama vya siasa wakifuatilia majadiliano hayo katika yao na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Waangalizi wa kimataifa walikuwepo pia katika mkutano huo ili kuangalia mambo yanavyokwenda kulia ni Tania Marques na Frida Lyaruu kutoka kitengo cha sheria Jumuiya ya Ulaya.
Wawakilishi mbalimbali wa vyama vya siasa wakiwa katika mkutano huo.
Waandishi wa habari wakiwa makini na kazi yao wakati wa mkutano wa wawakilishi wa vyama vya siasa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi unaofanyika katika hoteli ya City Paradise jijini Dar es salaam.

VODACOM TANZANIA YAKABIDHI MADARASA SHULE YA SEKONDARI ILULA.

Mkurugenzi wa mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom(Vodacom Foundation)Mwamvita Makamba akikata utepe ikiwa ni inshara ya kukabidhi madarasa mawili yenye thamani ya shilingi Miliopni 30 katika shule ya Sekondari ya Ilula wilaya ya kilolo Mkoani Iringa,na wapili kutoka kushoto ni Afisa Elimu wa Sekondari wilaya ya kilolo Theresa Zenda na watatu ni Mwalim Mkuu wa shule hiyo Damas Mgimwa,Mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom(Vodacom Foundation)Mwamvita Makamba (kushoto)akiteta jambo na Meneja wa mfuko huo Yessaya Mwakifulefule wakati walipokuwa wakikabidhi madarasa mawili yenye thamani ya shilingi Miliopni 30 katika shule ya Sekondari ya Ilula wilaya ya kilolo Mkoani Iringa,Mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom(Vodacom Foundation)Mwamvita Makamba(kushoto)akibadilishana mawazo na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ilula wilayani kilolo mkoa wa Iringa mara baada ya kukabidhi madarasa mawili yenye thamani ya shilingi Miliopni 30 katika shule hiyo,Mwishoni mwa wiki.
.Haya ndiyo madarasa yaliyojengwa na Vodacom Foundation

MSEMAJI WA TFF FROLIAN KAIJAGE APIGWA CHINI!!

Aliyekuwa msemaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF Frolian Kaijage kushoto akiongea na Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari TASWA Juma Pinto hivi karibuni kabla ya kupigwa chini na TFF.
Shirikisho la soka nchini TFF limemsimamisha kazi msemaji wa Shirikisho hilo TFF FROLINAN KAIJAGE baada ya kushindwa kupiga nyimbo za taifa wakati wa mchezo wa kufuzu fainali za mataifa la Mataifa ya afrika kati ya morocco na Taifa Stars ya Tanzania.
Kabla ya kuanza kwa mchezo huo ambapo rais kikwete alikuwa mgeni rasmi baada ya kukagua timu Rais alisubiri kwa muda ili nyimbo za mataifa yote mawili kupigwa kama ilivyo kawaida, lakini hakuna kilichosikika zaidi mashabiki wa timu ya Taifa Stars ambao walianza kuimba wimbo huo wakisikika "mungu ibariki yanga".
Mpaka sasa bado haijafahamika kwanini nyimbo hizo zilishindwa kupigwa na kufuatia kitendo hicho TFF imeamua kumsimamisha kazi msemaji wa huyo wa TFF FROLIAN KAIJAGE mpaka hapo uchunguzi dhidi yake utakapokamilika juu ya sakata hilo.
Rais wa TFF RODGER TENGA amesema kwa kushirikiana na wizara ya Habari Utamadunia na Michezo wanaunda kamati ambayo itachunguza chanzo cha tatizo hilo huku KAIJAGE akiwa nje mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika.
Lakini katika hatua nyingine RODGER TENGA amesema ndani ya mwezi mmoja TFF inatarajia kutangaza nafasi mbili ya katibu wa TFF na msemaji wa TFF ili kuziba nafasi hizo haraka iwezekanavyo. Source Janejohn5.blog

Oct 10, 2010

JAKAYA KIKWETE AITIKISA SONGEA MJINI

Jakaya Kikwete Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM akimnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Songea Mjini BW. Emmanuel Nchimbi.
Dr. Emmanuel Nchimbi amemhakikishia Jakaya Kikwete kuwa kura zote za watu wenye akili timamu Songea mjini ni zake.
Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu nchini kote.
( Picha Freddy Maro na Muhidin Michuzi)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiingia katika uwanja wa Majimaji mjini Songea akishangiliwa na umati mkubwa wa wakazi wa mji huo jana jioni.
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wakazi wa mji wa Songea muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Songea jana jioni
Dogo Ditto akifanya vitu vyake uwanja wa majimaji leo
Diamond akidondosha almasi ya sauti uwanja wa Majimaji
Hafsa Kazinja akimwaga Presha uwanja wa MajiMaji leo.
Dr. Emmanuel Nchimbi akisindikizwa kuhutubia uwanja wa Majimaji Songea leo.
Maelfu ya wana Songea wakimsikiliza JK uwanja wa Majimaji leo
maelfu ya wana Songea wakimsikiliza Jakaya uwanja wa Majimaji leo
Sehemu ya umati mkubwa wa wakazi wa mjini Songea wakimshangilia Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akiingia katika uwanja wa michezo wa Majimaji ambapo aliwahutubia katika mkutano mkubwa wa kampeni.

SYNOVATE YASEMA JAKAYA KIKWETE ANAONGOZA KWA ASILIMIA 61 KURA ZA MAONI!!


Meneja Mkazi wa Synovate, Aggrey Oriwo (kati) akiongea na wanahabari leo. Kushoto ni Meneja Huduma Jane Meela na kulia ni Bw. Ernest.
Ikiwa ni takribani siku tatu zimepita tangu REDET kutoa matokeo ya utafiti ya uchaguzi nafasi ya Urais kuwa Raisi wa sasa, Jakaya Kikwete ndiye anayeongoza katika kura hizo, Kampuni nyingine ya kimataifa ya utafiti ya SYNOVATE wametoa matokeo ya utafiti wao kuhusu nafasi ya uraisi ambao imeonesha kuwa iwapo uchanguzi ungefanyika leo, mgombea uras wa Chama Cha Mapinduzi, DK. Jakaya Mrisho Kikwete angepata asilimia 61 ya kura zote. Dk. Wilbroad Slaa wa CHADEMA yeye angeshika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 16 na kufatiwa na Prof. Ibrahim Lipumba wa CUF ambaye angepata asilimia 5. Utafiti huo umeonesha pia kuwa kuna asilimia 13 ya waliohojiwa ambao hawakuweka wazi maoni yao na ambao kama watapiga kura leo, JK angeweza kupata asilimia 70, Dk Slaa asilimia 18 na Lipumba asilimia 6. "Waliobana maoni yao katika swali hili ni wengi sana asiilimia 13% ya wahojiwa wote. Ikiwa watapiga kura ilivyodhihirika hapa basi 70% watampigia Jakaya Kikwete,Wilbroad Slaa 18%, Lipumba 6% wengine 6%," ilismea sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa mchana huu na Meneja wa Synovate Tanzania, Aggrey Oriwo, mbele ya wanahabari ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es salaam.
credit source: http://www.wavuti.com/4/post/2010/10/synovate-urais-tz-2010.html?utm_source=feedburner&utm_medium=email&utm_campaign=Feed%3A+wavuti+%28Wavuti%29#ixzz11zRwfkjK

Ridhiwani ndani ya Bagamoyo!!

Pikipiki zikiongoza mapokezi ya msafara wa Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Barza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete ulipowasili, Bagamoyo jana, kwa ajili ya mikutano ya kampeni za kuweka mikakati ya ushindi wa kishindo kwa CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao.(PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Barza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete akivishwa skafu na vijana,alipowasili, Bagamoyo jana, kwa ajili ya mikutano ya kampeni ya kuweka mikakati ya ushindi wa kishindo kwa CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao.(PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

Mama Singano Aagwa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania!!

Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ambaye pia ni Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania Jaji Profesa Ibrahim Juma akimkabidhi zawadi ya Jokofu Bi. Philipino Singano baada ya kustaafu utumishi wa umma aliotumikia zaidi ya miaka thelathini katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za Tume Dar es Salaam
Mama Singano akiwa na waliokuwa watumishi wenzake mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake
Jaji Profesa Juma akitoa nasaha kwa mama Singano
Baadhi ya watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria wakigonganisha bilauri wakati wa kumuaga mama Singano.
Picha zote na Ofisa Habari wa Tume Munir Shemweta

SIKU TAIFA STARS ILIPOPIGWA NA MOROCCO!!

Mshambuliaji wa Morocco, Chamakh Marouane ambaye anaichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza akiipangua ngome ya Stars wakati wa mchezo wa kufuzu Fainali za Afrika uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Hekaheka langoni pa Morocco
Timu ya Taifa ya Morocco imeweza kujipatia pointi muhimu na goli la ugenini baada ya kuifunga Taifa Stars bao 1-0 katika mchezo wao uliopita katika Uwanja wa Taifa jijini Dar. Alikuwa mshambuliaji Mounir El-Hamdaou wa Morocco aliyefunga bao hilo pekee la mchezo kwa shuti kali toka mguu wa kushoto, lililomshinda mlinda mlango Juma Kaseja, dakika mbili tu kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza. Hii ilikuwa ni mwendelezo wa ratiba ya mechi za kufuzu kucheza fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika ambapo katika mechi iliyotangulia iliyochezwa nchini Algeria hapo Septemba 3, 2010, Tanzania walipata pointi muhimu ya ugenini japo walitoka sare ya bao 1 - 1 dhidi ya wenyeji wao. Tanzania imepangwa kundi moja la D, na timu za Algeria, Morocco na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Mgeni rasmi katika mechi hiyo alikuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mdau mkubwa wa michezo, Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alisitisha kampeni za uchaguzi mkuu ili kuhudhuria mechi hiyo. credit source: http://www.wavuti.com

Oct 9, 2010

MATUKIO MBALIMBALI YA KUSAINI MIKATABA YA MSAADA JIJINI WASHINGTON DC LEO!!

Bw. John Murray McIntire akitoa ufafanuzi kuhusu misaada iliyotolewa na Benki ya Dunia tarehe 8/10/2010.
Mhe. Mustafa Haidi Mkulo, Waziri wa fedha na Uchumi akibadilishana mikataba aliyosaini na Bw. John Murray McIntire wa Benki ya Dunia.
Mhe. Mustafa Haidi Mkulo ambaye ni Waziri wa fedha na Uchumi na Bw. John Murray McIntire kwa pamoja wakisaini mikataba miwili ya mikopo yenye thamani ya kiasi cha shillingi bilioni 397.5.
Mhe. Mustafa Haidi Mkulo, Waziri wa fedha na Uchumi akishukuru kwa kufanikiwa kupata msaada huo wa kiasicha shilingi 397.5 kwa kipindi hiki kifupi alichokua hapa mjini Washington DC.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA