Oct 13, 2010

TAARIFA YA LADY JAYDEE KWA VYOMBO VYA HABARI , KUHUSIANA NA UBALOZI WA WANAWAKE WENYE UGONJWA WA FISTULA KWA KUSHIRIKIANA NA HOSPITALI YA CCBRT

Asubuhi ya leo katika mkutano na waandishi wa habari, CCBRT walitangaza kushirikiana na Lady JayDee na Watanzania wengine wote pande mbali mbali za nchi wanaofahamu wagonjwa wa Fistula au hata wagonjwa wenyewe kujitokeza ili kusaidiwa kutatua tatizo hilo.

Meza kuu ni CEO wa CCBRT Bw.Erwin Telemans, Lady JayDee pamoja na Mkurugenzi wa Programs za jamii Bi.Brenda Msangi

HABARINI ZA JIONI NA ASANTENI SANA KWA VYOMBO VYA HABARI KUITIKIA WITO HUU

KAMA MWANAMUZIKI WA TANZANIA, NASHUKURU KUWA JAMII YA WATANZANIA WENZANGU WANAPOKEA VIZURI KAZI YANGU YA SANAA YA MUZIKI.

KWA JINSI HIYO BASI……, NA MIMI NINALO JUKUMU LA KURUDI KWA JAMII YANGU NA KUSHIRIKIANA NAO KATIKA HARAKATI ZA KUJIKWAMUA KUTOKA KATIKA MATATIZO MBALIMBALI KAMA VILE MAGONJWA NA UMASIKINI.

NINAYO FURAHA KUWAFAHAMISHA KUWA, MIMI KAMA MSANII NINAE ANGALIWA NA KUSIKILIZWA NA JAMII YA WATU WENGI PANDE MBALI MBALI ZA TANZANIA.

LEO HII NIMEUNGANA NA HOSPITALI YA CCBRT KUWA SHUJAA WA WANAWAKE WANAOSUMBULIWA NA FISTULA.

UAMUZI HUU UMEKUJA BAADA YA CCBRT KUNIALIKA KUTEMBELEA WODI MBALIMBALI ZA WAGONJWA ZILIZOPO HOPITALINI HAPA.

LAKINI BINAFSI NILIGUSWA ZAIDI NA WANAWAKE WANAOSUMBULIWA NA UGONJWA WA FISTULA, UKIZINGATIA PIA MIMI NI MWANAMKE NIKAKUBALI KUUNGANA NA CCBRT ILI KUSAIDIA KWA HALI NA MALI KUOKOA MAISHA YA WANAWAKE WALIO WENGI..

TANGU NIZALIWE MPAKA NAKUWA MKUBWA NA KUFIKIA HATUA NILIOPO HIVI SASA, NAKIRI SIKUWAHI KUSIKIA WALA KUONA MGONJWA WA FISTULA. MPAKA NILIPOTEMBELEA HOSPITALI YA CCBRT

NIMESIKITISHWA ZAIDI BAADA YA KUELEZWA KUWA WANAWAKE WENGI WENYE UGONJWA HUU HUSHINDWA KUFANYA KAZI WAKATI MWINGINE HATA KUTENGWA AU KUJITENGA NA JAMII ZAO WANAMOISHI KUTOKANA NA KUWA WANAVUJA HAJA NDOGO AU HAJA KUBWA KILA MARA BILA WAO WENYEWE KUPENDA WALA KUJIJUA. KWAKUWA WANAKUWA WANASHINDWA KUJIZUIA.

HIVYO KUPELEKEA WANAWAKE HAO WENYE FISTULA KUENDELEA KUISHI MAISHA DUNI YA UPWEKE NA KUENDELEA KUWA MASKINI

LABDA NIONGELEE KWA KIFUPI KUHUSIANA NA FISTULA.

NI UGONJWA UNAOWAPATA WASICHANA NA WANAWAKE WAKATI WA KUJIFUNGUA NA HII HUTOKANA NA KUSHINDWA KUFIKA VITUO VYA AFYA VYENYE HUDUMA YA UZAZI.

FISTULA NI UGONJWA UNAOZUILIKA NA UNATIBIKA.

HAKUNA MWANAMKE ANAETAKIWA KUISHI NA FISTULA HASA UKIZINGATIA CCBRT INATOA MATIBABU, USAIFIRI, CHAKULA NA MALAZI BURE KWA WAGONJWA WOTE WANAOSUMBULIWA NA FISTULA.

JUKUMU LANGU KUBWA KATIKA UBALOZI HUU NI KUSIMAMA NA KUTUMIA SAUTI YANGU, NA NAFASI NILIONAYO KATIKA JAMII KAMA MWANAMUZIKI KUTOA WITO KWA WAGONJWA WENYE FISTULA NA HATA WALE WANAJAMII WENGINE WOTE WANAOFAHAMU WAGONJWA HAO, WAJE CCBRT KUPATA MATIBABU NA HUDUMA ZOTE BURE.

NITAFANYA HAYO POPOTE NITAKAPOPATA NAFASI YA KUONGEA NA JAMII INAYONIZUNGUKA, AMA IWE KATIKA MAONYESHO YANGU AU MAHOJIANO NA VYOMBO VYA HABARI.

NITAFANYA HIVYO PIA KATIKA MITANDAO YA KIJAMIII, NINAYOHUSIKA NAYO KAMA BLOGS NA FACEBOOK NA HATA KATIKA MATANGAZO YA TV, RADIO NA VIPEPERUSHI.

ILIMRADI TU UJUMBE UWAFIKIE WANAWAKE WENYE FISTULA WAJE KUTIBIWA BURE CCBRT.

NDUGU ZANGU WAANDISHI WA HABARI, NAOMBA MJIUNGE NAMI KUWA SHUJAA WA WANAWAKE WENYE FISTULA


ASANTENI SANA
LADY JAYDEE a.k.a KOMANDOO

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA